Mfumo Baguzi wa Ajira za Umma Unazalisha Mitume na Manabii Wengi Tanzania

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Mustakabali wa ajira JMT unapaswa kuwa agenda ya kitaifa ili kuutafutia muafaka wake.

Kwenye nchi ambayo uchumi ni labour intensive (uzalishaji unaotegemea watu zaidi ya teknolojia) ni aibu kuwa na jeshi kubwa la wasio na ajira rasmi (ajira za kola nyeupe).

Hali hii inakaribisha ufisadi na rushwa ili kupata fursa ya ajira, ni uponyaji wa tatizo unaozaa tatizo lingine gumu na sugu (kununua ajira kunazaa rushwa).

Hali hii inadhalilisha wanawake kuliko wanaume katika kupigania fursa adimu; kupitia rushwa ya ngono.

Hali hii inabomoa utangamano wa kitaifa na kuzaa madaraja ya kimaisha miongoni mwa jamii.

Asilimia kubwa ya Mitume na Manabii tulio nao ni wasomi wazuri waliokosa ajira rasmi (ajira za kola nyeupe)

Kwenye Huduma wanakuwa matajiri wakubwa kwa muda mfupi hadi kujutia walioajiriwa. Mapato yao hayana ukaguzi wa ndani na nje wa mali, fedha na madeni.

Vyanzo vya mapato ya Mitume na Manabii:-

1. Sadaka na matoleo mengine.

2. Wahisani wa ndani na nje.

3. Marafiki wa ndani na nje.

4. Mauzo ya bidhaa za kiimani kama maji, mafuta, udongo, chumvi, vitambaa, bangili, vitabu, keki, matunda nk.

5. Fedha za mafisadi zinazotunzwa kwa Mitume na Manabii badala ya offshore; ambazo watumishi hawa wa Mungu wanakatiwa % fulani kama malipo ya kazi ya kutunza ela za mafisadi kwenye akaunti zao.

Wasomi waliokosa ajira nchini kwao wamekuwa wakimiminika muongo mmoja uliopita JMT kuja kufungua Huduma kufuatia Watz wengi sana (wakiwemo waliokosa ajira) kuwa wepesi mno na wenye kiu na uchu mkali sana wa kutafuta na kuamini Injili.

Tujisahihishe na kujipanga upya kama taifa.
 
Back
Top Bottom