Sakata la Bandari ya Dar es Salaam na uwekezaji wa DP World huu ndiyo mtazamo wangu

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,177
2,281
Kwa muda mrefu kumekuwa na mawazo mbalimbali kuhusu DP World kuwekeza ktk bandari ya Salama. Mimi binafsi Kuna vitu kadhaa nimevibaini ktk mjadala huu.

1) Wanaopinga ni km hawajui wanapinga nini na wanaounga mkono hawajui wanaounga nini.

2) Kitu kingine ni bendera fuata upepo. Baadhi ya Wanaopinga wanapelekwa na upepo wa watu wasiojua wanapinga nini na wanaounga mkono wanapelekwa na upepo wa watu wasiojua wanataka kuwekeza nini.

3) Mahaba niue. Baadhi ya wanaopinga wanapelekwa na mahaba niue ya Nchi Yao na baadhi ya wanaounga mkono huu uwekezaji wanapelekwa na mahaba ya ubinafsi.

4) Siasa kuingilia mambo nyeti. Suala hili limefanywa la kisiasa badala ya kuwa la kitaifa. Kuna wanasiasa wao walishakataa katakata kuwa wao pia hukosea. Kusema kuwa wamekosea kwao ni haramu. Hawa ndiyo huunga mkono hata masuala ya hovyo hovyo ili kuendelea kutetea matumbo Yao. Kuna wale wanasiasa wanaotaka kuchukulia suala hili km mtaji wa kujiongezea umaarufu. Hawa hata jambo likiwa zuri vipi lazima watie doa.

5) Ushaabiki usio na tija. Naweza kuita ushamba, ulimbukeni, uzwazwa, kujipendekeza, au umaskini wa fikira. Mtu hata km unajua jambo usijitie kimbelembele na kuona walioko nyuma yako ni wapumbavu. Watu wenye sifa km hizi siku zote ndiyo hufanya maamuzi ya hovyohovyo na mwishowe huangukia pua na kuabika. Kuna watu ktk hili suala wako tayari kuvua nguo na kuliunga mkopo kwa mbwembwe zote hata km wanajua halina manufaa kwa Taifa. Wao kutokana na tabia zao nilizotaja hapo juu hujiona wako sawa tu. Lakini pia ktk hili sakata Kuna watu wamekuwa washaabiki wa kupinga wakati hata mkataba wenyewe hawajauona. Wao fraha Yao ni kuona Kila jambo linalofanywa na mtu au taasisi fulani linakwama. Hawa wote kwa pamoja ndiyo nimesema awali kuwa wanapinga bila kujua wana pinga nini au kuunga mkono bila kujua wanaunga nini.

6) Historia. Sakata la Bandari ya Salama linachagizwa na historia ya uwekezaji ktk nchi hii. Tangu Tanganyika ipate Uhuru hadi leo hakuna eneo km Nchi imepiga hatua ktk uwekezaji hasa wa watu weupe. Kila uwekezaji umeangukia pua, mifano ipo mingi siyo ya kutaja. Mtanganyika halisi anajua ninachosema.

7) Udini. Suala la Bandari limeingiliwa na chembe chembe za udini. Kuna wanaodhani huyu kiongozi wa sasa kafanya hivi kwa sababu wanaokuja kuwekeza ni ndugu zake. Kwa mjibu wa dini ya Kiislam "ndugu yako ni Muislam mwenzio". Hivyo, wa upande wa pili wanaona km huyu anawagawia mali ndugu zake . Hivyo, wao kupinga ni lazima na wale Waislamu kuunga mkono ni lazima. Hapa haijalishi wanapinga ujinga au wanaounga mkono ujinga ilimradi tu waridhishe nafsi zao za udini.

8) Ukanda (Utanganyika na Uzanzibari). Kuna wanaona kwa vile kiongozi wa sasa anatoka visiwani na kukubali wawekezaji ktk bandari ya Salama ni kutojali rasilimali za Wabara (Watanganyika). Hapa ndiyo Kuna shida kubwa maana Wabara ni wengi hivyo wamekuwa na sauti kuu na kufanya kuchelewesha maamuzi.

NB: Tuachane na ujuaji kujiona mtu flani au kundi fulani ndiyo wenye haki ya kusema au kuamua juu ya mtu au kundi lingine. Wote ni Watanzania na wote wana haki ya kuhoji na kuhojiwa. Lakini pia Viongozi wako makini hawezi kurudia makosa ya nyuma.

Kazi iendellee.
 
Uwekezaji wa bandari una tija au hauna tija?,je' kama una tija uwe uwekezaji wa aina gani?

mimi nikajua utatiririka kwenye senstive content.
 
Back
Top Bottom