Saidia Mwana Halisi Saidia Said Kubenea

AHHH WELL....

MWKINGORELIST.jpg



RIP

419493476_0434c38db3.jpg
 
kwi kwi kwi ^ ^ ^ ^ ^ ^ ^^

Again!

nilidhani nilivyokuwa ignored last time ilikuwa for good?!
ohh jamani GT dont ignore me coz i will starve to death....lol

kwi kwi kwi kwi
 
Some of these kids in JF desperately need a father figure...so now they're latching on to JF ....this is pathetic...best option: PLACE THEM IN IGNORE LIST

exc1412098440_2.jpg
 
Mbona said hajaomba msaada? ama tu hoja huzaa hoja? Da !!! jamani haipendezi hata kidogo, kumshambulia na kumvunjia heshima ndugu yetu Kubenea, yeye ni mpiganaji tena mstari wa mbele, hata kama mweshimiwa kambuluza mahakamani, Mungu atamnusuru.
 
Michango ya kuchangia mwanahalisi imefikia wapi? Lunyungu uko wapi utupatie habari?
 
JF tuangalie Credibility yetu, Tusiwe tunakurupuka kurupuka.

Werevu watakuwa wamenielewa.
 
Nashukuru kwa michango ya mawazo yenu nyote mliochangia posively na negatively.Nichofikiri mimi ni kwamba hivi vita ya kifikra iliyoanzishwa dhidi ya ufisadi inaonyesha kuwa itakuwa ngumu kama vile ya Bush na igaidi.Ni bahati mbya sana mafisadi wana uwezo mkubwa kiasi cha kununua wajenda hoja wazuri.Sisi wanyonge ambao tumeguswa na ufisadi ambao naamini umegusa watu walio wengi.Maana kuna watu wamepoteza maisha yao kutokana na ndugu zetu wachache walioamua kuhujumu uchumi wetu na kufaidisha kikundi cha watu wachache.Naungana na wale wote wanaosema hapa tuwaandame political figures wanaoelewana na mafisadi bila kusubiri ushahidi wa kisheria kwa sababu utawala wa sheria upo kinadharia tu.Mnaonaje watu wamefanya uhalifu wa EPA wanakaa meza ya majadiliano na organs of state? Hiyo imetokea wapi kama si kugwaya kwa watawala wetu?Mwafrika wa kike endelea na mapambano hao wanaosubiri ushaidi wa kisheria waendelee kusubiri.Watu wa aina hiyo wapo hata Zimbabwe,watajitokeza siku ile watakapothibitisha Dictator Mugabe amekimbilia Indonesia.Ni katika hatua hiyo watajitokeza kuwa wapo pamoja na Tsivingirai wakiwemo na hao saa hizi wanajitia wapo na Mugabe.Culture of slence nad fear inawaumiza waafrika.
 
Mpoki asante sana .Nimeshangaa sana maana ya mada kubadilishwa na kuwa ni hate .Neno kuomba mchango ni la kistaraabu na tena la hiari .Was simple kukaa kimya na kuwaacha wenye nia aendelee na kama una hoja dhidi ya Kubenea fungua mada.Lately pamekuwa na uchafu wa watu kuharibu mada kwa matusi ama mada ndani ya mada .This is not JF ambayo nilianza nayo from day one .
 
JE NANI ANAHITAJI MSAADA KATI YA HAWA WAWILI:

SUED KUBENEA: Mhariri wa gazeti na mmoja kati ya watu wenye fedha Tanzania ambaye aliamua kuandika habari ambazo alijua fika kuwa angeshitakiwa.Na ALIPOMWAGIWA TINDIKALI KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA SERIKALI ILIMLIPIA TICKET NA MATIBABU INDIA...je huyu anastahili kupewa msaada
mmmmmmm.jpg



AU

SAMUEL NKYA: (pichani chini) anayehitaji kwenda india kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na matibabu katika uso wake ambao umeharibika. wanaoshuhudia ni wajumbe wa kamati ya kumsaidia mtoto samweli akatibiwe.

Sam5.jpg
 
Kila jambo lina wakati wake .Na ukileta issue ya Nkya am sure what watashiriki sambamba na issue ua Kubenea so no worries here .
 

interesting...

Interesting ? why is that ? Mapesa ya wizi ambayo Kubenea anayapigia kelele yangaliweza kutumika kirahisi kumsaidia huyu mtoto lakini sasa hayapo maana yameibwa .Unasemaje mkuu ? So kwa sasa mpiga mayowe anakabwa koo na tuna mgonjwa the same time tutajigawa tu .
 
Haya, Kubeana aendeleza mapambano....

Thursday, May 1, 2008
Tahariri dhidi ya Rostam
mwisho
Rostam, tukutane mahakamani


TUMESOMA katika vyombo vingine vya habari kwamba mfanyabiashara kizito na Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi, amefungua kesi dhidi ya gazeti hili-MwanaHALISI. Anataka gazeti hili limlipe Sh 3 bilioni kama fidia ya “kusafisha” jina lake. Hiyo ndiyo thamani yake.

Zaidi ya hayo, Rostam Azizi anaiomba mahakama iamuru habari zake wakati wa mwenendo wa kesi hiyo, zisiandikwe na gazeti hili. Wakati tunasubiri taarifa rasmi kuhusu kushitakiwa kwa gazeti hili, tunapenda kusisitiza kwamba kwetu, hiki ni kitisho kingine.

Anachojaribu kufanya Rostam Azizi, ni kufunga mdomo wa wananchi wanaommulika yeye kama mfanyabiashara na mwanasiasa, ambaye matendo yake yanagusa moja kwa moja maslahi ya wananchi wa Tanzania.

Ifahamike wazi kuwa Rostam naye ni mmiliki wa vyombo vya habari, vinavyofanya kazi kama inayofanywa na MwanaHALISI, ingawa kwa viwango na malengo tofauti.

Lengo la MwanaHALISI linafahamika. Gazeti hili ni mdomo wa wananchi maskini wa Tanzania. Ni kioo cha kuwamulika wote walio na dhamana katika jamii, wanaozitumia vizuri na vibaya – Rostam akiwamo. Ni kauli ya wanyonge wanaonyanyasika kutokana na uroho wa wakubwa na wafanyabiashara wasio waaminifu.

Inawezekana Rostam Azizi alidhani nasi tungeingizwa katika mkumbo wa vyombo vya habari vilivyoanzishwa au kununuliwa kwa ajili ya kulinda majina ya viongozi wa serikali ya awamu ya nne na maswahiba wao. Amekosea!

Kinachomsibu Rostam Azizi kimeshawasibu wengine pia walio katika mkondo mmoja naye. Kinafahamika. Faraja kubwa tuliyo nayo ni kwamba walau sasa jamii inaanza kuwajua watu wasiopendezwa na kazi yetu, wanaotutisha na kutudhulumu.

Kwa muda mrefu, baadhi ya wanasiasa walijifunika utukufu wa kisiasa ambao walidhani wangeendelea kuwa nao kwa sababu wanazozijua. Hawakutarajia kumulikwa na kukosolewa, kazi ambayo tumeifanya vema.

Kwa hatua hii ya sasa ya Rostam Azizi ni dhahiri hataki kukosolewa. Lakini hatutaki kuamini kwamba Rostam Azizi amesahau wasifu wake katika jamii ya Watanzania.

Na hatutaki kuamini kwamba hajui kuwa hata haya yaliyoandikwa juu yake anayolalamikia sasa ni matone tu katika bahari ya mengi ambayo sasa anajaribu kuyazuia kwa kitisho cha mahakama.

Rostam Azizi si maskini. Lakini hilo halikumzuia kuwadai maskini Sh bilioni tatu, ambazo kwake ni thamani ya jina lake. MwanaHALISI halina pesa ya kuwagawia matajiri.

Pesa kidogo inayopatikana ni kwa ajili ya kuwaunga mkono Watanzania wazalendo na maskini katika vita dhidi ya mafisadi kwa kutumia uhuru wao wa kuhabarishana na kuwasiliana.

Tunaamini kwamba vitisho hivi vya Rostam Azizi na ’amri’ anazoipa mahakama, havina nia njema kwa taifa, bali vina lengo la kuficha ukweli kwa umma kuhusu siasa na biashara zake.

Rostam Azizi anataka wananchi wafungwe mdomo, macho na masikio dhidi yake. Yeye ana pesa, na anadhani atazitumia pesa hizo hizo kutunyamazisha, na kuwadhulumu wananchi maskini tunaowatetea.

Tungependa kumweleza wazi wazi kwamba vitisho vyake havitawazuia wananchi kufikiri, kuchunguza, kusema na kujadili kuhusu ufisadi unaofanywa na vigogo na maswahiba wao.

Tuna hakika kwamba gazeti hili halijamkashifu Rostam Azizi, bali limeandika habari asizopenda zijulikane kwa umma. Tuna hakika kwamba shida ya Rostam Azizi – ambaye pia ni mmiliki wa magazeti - katika suala hili si pesa, kwani anazo nyingi kuliko hizi, bali anataka kulifilisi na kuliua gazeti hili.

Gazeti hili halipo tayari kuwasujudia mafisadi. Kama ambavyo tumekuwa tunafanya huko nyuma, licha ya vitisho kadhaa tunavyoendelea kukabiliana navyo, tutaendelea kuandika bila kumwonea, kumpendelea au kumwogopa mtu yeyote.

Tutasimamia ukweli na haki na tutafichua ufisadi kwa maslahi ya taifa. Katika hili, hatutarudi nyuma; na kama Rostam Azizi anataka kutupeleka mahakamani, atangulie tutamkuta huko; na asubiri matokeo.

Ends
 
Maneno haya ya Kubenea ni mazito sana halafu GT unasemaje kuhusu huyu jamaa ? Haya sasa kesha weka wazo msimamo wa gazeti hili na tunangoja kesi infunguliwe .Je kuna mtu ana taarifa za kesi ya hii kufunguliwa ? Rostam asipofanya kweli ataonekanaje kwenye jamii ?
 
Karamagi amewahi kukaririwa kuwa amewaomba wanasheria wake wamtake Slaa kumwomba Karamagi radhi na kulipa Sh billioni 10 kama fidia kwa kumchafulia jina. Slaa mpaka leo anasema hajaiona hiyo notice. Kwa maandishi hayo hapo juu, Kubenea & co inaonekana wanafahamu mengi sana kuhusu huyu bwana. Kama wanasema waliyokwisha andika ni sawa na matone tu, ni mjinga gani aliye tayari kuona bahari ya uovu wake ikianikwa ? Najaribu kutafuta gazeti la Mwanahalisi kwenye mtandao halipatikani. Laweza kuwa limeanza kuhujumiwa ?
 
Ndiyo maana nikamshangaa GT na kampeni zake , lakini pia nji haki yake ya kuto kubaliana na kila jambo.Kubena si mjinga kupokea pesa zao then aanze kuandika uchafu anajua mwisho wake ni mbaya .Nasema Kubenea ukipelekwa Mahakamani sisi tutauza hata viatu uendeshe kesi .Maneno ya hapo juu ni mazito na ujume fika kwa Serikali, Judge na Rostam mwenyewe .Ujumbe umesfika na hata GT kesha upata .
 
Tutasimamia ukweli na haki na tutafichua ufisadi kwa maslahi ya taifa. Katika hili, hatutarudi nyuma; na kama Rostam Azizi anataka kutupeleka mahakamani, atangulie tutamkuta huko; na asubiri matokeo.

Mkuu Kubenea,

Heshima mbele na safi sana, wananchi wengi tuko nyuma yako, huyu ni kukutana naye mahakamani tu, I love it!
 
Back
Top Bottom