Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi,

Uendeshaji wa vyama vya siasa nchini, unaongozwa na sheria, taratibu na kanuni. Ikithibitika pasipo shaka kuwa chama fulani, kinakiuka sheria, taratibu na kanuni, kinapaswa kuwajibishwa, kuadhibiwa hata kufutwa, kutegemeana na tuhuma halisi!.

Miongoni mwa masharti ya usajili wa vyama vya siasa, ni kwa vyama hivyo, kuwasilisha katiba yake iliyopitishwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, ikithibitika pasipo shaka kuwa katiba ya CHADEMA iliyowasilishwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni Katiba "Fake" na sio ile katiba halisi ilipitishwa na Vikao Halali vya CHADEMA!, hili ni kosa kubwa linaweza kupelekea chama kufutwa!.

Tuhuma yenyewe ni hii na ilitolewa rasmi jana humu JF na mwana JF huyu.

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tenakatika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu balikwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.

Ahsanteni kwakunisoma!

Mara baada ya mwaJF huyu kuzishusha tuhuma hizi humu, uongozi wa CHADEMA umemsimamisha mmoja wa viongozi wake kwa kosa la kuutoa ukweli huu nje.

Maswali ambayo ni lazima CHADEMA wayajibu ni haya.

  • Jee ni kweli CHADEMA inaendeshwa kwa katiba fake na sio ile iliyopitishwa na vikao halali?
  • Jee ni nani alikinyofoa kipengele cha demokrasia ya ukomo wa uongozi ndani ya chama ili kutoa nafasi kwa uongozi wa kifalme na kisultani?
  • Ikithibitika kuna mtu alikinyofoa kipengele hicho kwa makusudi, atachukuliwa hatua gani?
  • Je ni nani alichomekea kipengele cha kumzuia mwanachama wa Chadema kutafuta haki yake mahakamani?.
  • Je mabadiliko ya "unyofoaji huo" yaliwasilishwa kwa Msajili wa Vyama?
  • Ikithibitika pasipo shaka kuwa CHADEMA walikiuka sheria taratibu na kanuni, jee watafanywa nini? (Masajili)
Baada ya kushushwa tuhuma nzito kama hizi, dawa sio kumsimamisha uongozi mtoa tuhuma, bali kutoa majibu ya kina kuhusiana na tuhuma hizi.

Namna rahisi ya kuthibitisha ni kupatikana kwa miniti za kikao kilichopitisha kunyofoa kipengele hicho cha ukomo wa uongozi na kuchomekea kipengele cha kuzuia wanachama wa Chadema kutafuta haki yao, mahakamani!.
Kisha zipatikane miniti za kikao chochote halali kilichopitisha unyofoaji huo!.

Kisha kwenda kwa Msajili kuthibitisha kama mabadiliko hayo yalifanyika kihalali.

Naandika haya nikiwa ni mwananchi tuu wa kawaida ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa, mwenye mamlaka kamili kuhoji jambo lolote kuhusu chama chochote, na sababu ni mimi pia ndiye ninayegharimia fedha za uendeshaji wa Chadema kupitia kodi yangu inayolipwa Chadema kama ruzuku!.

Pia naelewa fika kinachowakuta wakosoaji wowote wa chama "kitakatifu" humu jf, ila kwa vile hoja zangu ni za kweli, nasimama kwenye kweli, na ni ukweli tuu ndio utakao kiweka huru Chadema na sio timua timua au fukuza fukuza!.

Angalizo wa wapenzi wa Chadema, sijasema chama chenu kinafutwa, nimetoa angalizo tuu la tuhuma kwa chama chenu kuendeshwa kwa katiba feki!, tuhuma hizi zikithibitishwa, it's going to cost Chadema very dearly kwasababu Chadema hiyo katiba fake ya Chadema ya 2006 will be declared null and void, hivyo katiba ya Chadema kubaki ile ya 1992!.

Pasco.
Update 1. Majibu ya Katibu Mkuu wa Chadema.

WanaJF,
Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.

2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Tulichobishana Mimi na Msajili, na kwa maandishi, ni kuwa Msajili alit aka nimwasilishie nakala ya Katiba kwa Kiingereza. Nilimkatalia kwa msingi kuwa Katiba yetu ilipitishwa na Mkutano Mkuu kwa kiswahili na Mkutano Mkuu na hivyo siwezi Mimi kumpelekea kwa Kiingereza. Msajili alidai kuwa ni hitaji la kisheria. Nilimjibu kuwa sheria hiyo inapaswa kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, baadaye tulikubaliana kuwa nitengeneze " literal translation" lakini kwa mahitaji ya kisheria itatumika Katiba ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.

Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kaki kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.

Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.
Mkuu Dr. W. Slaa, kwanza, heshima yako!, maana ile kujibiwa tuu na mtu wa calibre yako pekee, ni heshima kwangu na kwa thread hii, hivyo majibu yako, nayaunganisha pale mbele ya thread as an authority.

Uwongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli. Sambamba na tuhuma hii, mtoa tuhuma pia ameweka tuhuma nyingine nyingi, zenye kuhitaji majibu ya kina kama haya uliyonijibu hapa.

Kwa majibu hayo, na kwa vile wewe ndio mtendaji mkuu wa Chama, ni uthibitisho pia kumbe ulikuwa huijui katiba ya Chadema kuwa ina kipengele cha ukomo wa uongozi!, kama KM hajui kipengele muhimu kama hiki, who will know?.

Kwa vile CCM ndicho chama tawala, Chadema kiko kwenye mizani ya tukiaminie mwaka 2015 au bora kuendelea na CCM tuliyoizoea!, hivyo haya makando kando yoyote kuihusu Chadema, lazima yajibiwe ipasavyo kama hivi ulivyofanya hapa.

Asante sana kwa hili.

Kwa vile maelezo haya yako ni ya upande mmoja, nasubiri verification ya data toka kwa msajili, then niufunge rasmi huu mjadala.

Nashukuru tena.

Pasco.
Update 2: Majibu ya Msemaji Mkuu wa Chadema, Mhe. JJ.Mnyika.

Pasco nimesoma mjadala ulioanzisha na majibu ya Dr Slaa. Kabla ya kusoma mjadala huu, niliitikia mwito wa Mtoi kwenye Jukwaa la Wanamabadiliko na nikaandika kwa kirefu kuhusu suala hili ambalo mimi nilishiriki kwa karibu sana nikiwa sehemu ya timu zote tatu zilizohusika na mchakato wa kukusanya maoni ya wanachama kwa ajili ya kuandika katiba, kanuni, itifaki na maadili ya chama pamoja na miongozo ya mabaraza ya chama. Naomba Mods muuweke waraka huo ambao nitawatumia kwa barua pepe au mnaweza kuuchukua kutoka huko. Nimekubaliana na katibu mkuu kuna marekebisho kwenye majibu yake ya awali, katiba ya mwaka 2004 iliondolewe katika orodha ya katiba alizozitaja. Suala la kwamba kuna kipengele kiliondolewa kinyemela halina ukweli, na kilichofanyika 2006 ni kuandika katiba upya kama ambavyo nimeeleza kwenye majibu hayo. Baada ya majibu hayo kusomwa, kama kuna masuala yanahitaji ufafanuzi wa kichama kuhusu suala hili la katiba na mengine au maoni yangu binafsi nitafanya hivyo leo kati ya saa 9 mpaka 10 Jioni. Niko kwenye kikao, baada ya hapo nitakuwa kwenye mkutano. Nikihitajika baadae nitarejea tena.

Nimeitika mwito, ni kweli nilikuwa mjumbe kwenye timu zilizohusika na kuandikwa kwa katiba mpya ya CHADEMA ya mwaka 2006, aidha nilikuwepo kwenye mkutano mkuu wa chama uliopitisha katiba mpya tarehe 13 Agosti 2006.

Madai ya kwamba "Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela"; hayana ukweli kwa kadiri ya ufahamu wangu.

Mosi, mwaka 2006 hatukufanya marekebisho ya katiba bali tuliandika upya katiba ya chama kutoka ile ya mwaka 2004. Waraka uliandikwa nchi nzima kwa wanachama kutoa maoni na kuwasilisha makao makuu kuanzia kwenye ngazi zao za chini za kikatiba.

Baada ya kukusanya maoni kulikuwa na timu tatu, timu moja ilihusu kuandika falsafa na itikadi ya chama ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Profesa Baregu na katibu wake nilikuwa mimi.

Sehemu hiyo ya katiba niliandika neno kwa neno mapendekezo ya awali kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa, tulifanya mapitio pamoja na Profesa Baregu na hatimaye ikaingia kwenye vikao vya kikatiba vya chama na kupitishwa.

Sehemu ya falsafa kwa sehemu kubwa tulinukuu kwenye katiba kama ilivyokuwa mwaka 2004, sehemu ya itikadi tuliandika upya kabisa haikuwepo katika katiba ya CHADEMA ya zamani.

Sehemu zingine katika katiba kwa sehemu kubwa kazi ya kuunganisha maoni mapya na kufanya pia rejea kwenye katiba ya zamani ilifanywa na timu ya watu watatu tukiongozwa na muasisi wa chama Mzee Victor Kimesera pamoja na Mkurugenzi Benson Kigaila na mimi.

Kulikuwa na timu nyingine ya kuandaa miongozo ya mabaraza ya chama: Baraza la Wazee, BAVICHA na BAWACHA ambao nao walifanya kazi kwa upande wao na nilishiriki katika kupendekeza mwelekeo na mapitio ya kulinganisha rasimu ya miongozo yao na rasimu ya katiba ya chama.

Kwa ninavyokumbuka hicho kinachoitwa "kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano" hakijawahi kuingizwa kwenye katiba mpya ya CHADEMA.

Baada ya timu zote kufanya kazi yake; rasimu ya katiba ilipita katika vikao vyote vya kikatiba yaani sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na hatimaye mkutano mkuu. Katika vikao vyote hivyo, iwapo kipengele hicho kingekuwa kimeondolewa ‘kinyemela' kama inavyodaiwa, mwandishi wa tuhuma hiyo angehoji toka Agosti 2006.

Aidha, baada ya katiba kupitishwa na kuanza kutumika kifungu hicho kingekuwa kimeondolewa kinyemela kati ya mwaka 2006 mpaka 2008 mtoa madai au mtu mwingine yeyote ndani ya chama angekuwa amehoji wakati wa matumizi. Kumekuwepo pia mchakato wa kufanya marejeo kwa ajili ya kushughulikia makosa ya uchapaji (errata) kwa nyakati mbalimbali, suala hili si kati ya mambo yaliyoibuliwa.

Mwaka 2009 CHADEMA kilifanya uchaguzi mkuu wakae mkuu nchi nzima ambapo vifungu vya masuala ya uchaguzi wa ndani ya chama vilifanyiwa rejea mara kwa mara. Mwandishi wa madai hayo alikuwepo wakati huo, suala hili la kwamba kuna kifungu kimeondolewa kinyemela sikulisikia likilalamikiwa kwenye vikao vyovyote vya kikatiba iwe ni sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu.

Kwa vyovyote vile kwa historia ya chama toka mwaka kilipoanzishwa mpaka wakati huo wa uchaguzi wapo viongozi ambao walikuwa wanagombea wakiwa na vipindi viwili wakati huo kwenye cheo kimoja cha ngazi moja; kifungu hicho kingekuwepo toka 2006 kingetumika kuwawekea mapingamizi. Na kama kingekuwa ‘kimeondolewa kinyemela' kungekuwa na malalamiko mengi kiko wapi kwa kuzingatia ‘joto' la uchaguzi wa wakati huo.

2010 mpaka 2013 madai hayo hayajawahi kutolewa kwenye kikao chochote cha kikatiba katika ngazi ya taifa kwa kuwa mimi ni mjumbe wa vikao vyote vya kitaifa ambavyo yeye amesema kwamba ni mjumbe.

Madai kama hayo yangetolewa na asiye mwanachama au walau mwanachama wa kawaida tungesema tu ni maoni ya kawaida yaheshimiwe na aelimishwe. Lakini madai kama hayo yakitolewa na kiongozi wa chama mwenye nafasi ya kuujua ukweli wote huo yanaacha maswali kuhusu dhamira yake. Naamini mamlaka zinazohusika za chama zitatumika katiba, kanuni, maadili na itifaki kuchunguza na kuchukua hatua kuanzia kwenye ngazi yao huko tukio lilipotokea.

Hata hivyo, kwa maoni binafsi (yasichukuliwe kuwa ni kauli ya nafasi ninazoshikilia kwenye chama), dhamira ya haya inajionyesha kwenye andiko lenyewe la muhusika kuanzia aya ya kwaza " Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari namadhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwawana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.

Mtoa madai anaendelea kuandika kwamba " Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu balikwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.

Anaendelea kuandika madai mengine mengi ya upotoshaji lakini mwishoni anamalizia kwa dhamira yake ile ile " Nitaendelea kuwadondolea ili muonekwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.". Kwa hiyo, dhamira yake ni uchaguzi na mabadiliko ya uongozi; dhamira yeyote njema ifuate mkondo wa katiba, kanuni, maadili na itifaki; kinyume chake ni ‘njama ovu' na ‘utovu wa maadili".

Nimekuwepo chaguzi mbili kuu za CHADEMA 2004 (nikiwa mtazamaji sio mwanachama) na 2009 nikiwa katikati ya chaguzi hizo kama kiongozi. Naamini uchaguzi huu wa chama ulioanza kuanzia mwaka huu 2013 utakamilika mwaka 2014 CHADEMA ikiendelea kusimamia dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.
Mjadala mwema. JJ
Asante sana Mkuu JJ. Mnyika, nitajitahidi kutembelea kule ili kujiridhisha, ila kwa vile mzizi wa fitna kwenye uzi huu ni katiba ya 2004, kama unayo, nitashukuru tukiipata, tukaufunga huu mjadala rasmi.

Kama unachosema wewe ndio right, kuwa ile katiba ya 2006 sio marekebisho ya katiba ya 2004, bali ni katiba mpya, hata kama ni kweli, katiba ya 2004 ilikuwa na kipengele tajwa, na katiba ya 2006 ikawa haina, then at this juncture,

Nkuwekea uthibitisho wa Katiba ya Chadema ya 2006, sio katiba mpya bali ni marekebisho ya katiba ya 2004 kama inavyoeleza katiba yenyewe
"HIVYO BASI,
Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 13/8/2006, Mjini Dar es Salaam tumeamua kuifanyia mabadiliko Katiba ya 2004 ya Chama chetu cha Siasa kinachoitwa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa FALSAFA yetu ya NGUVU NA MAMLAKA YA UMMA na Dira na Dhamira ya Chama kuanzia 2006 na kuendelea. Kuanzia sasa CHADEMA, kitaendeshwa kwa mujibu wa Katiba hii".

I put my hands down, mjadala umesitishwa kwa sababu wenye chama wanasema katiba ya 2006 katiba ni mpya, na kwa vile katiba yenyewe imeandikwa kufanyiwa mabadiliko, lakini haijasemwa popote kuwa ni katiba mpya, then its not ok kama haina kipengele hicho na hakuna any munutes, kipengele hicho, kilinyofokaje?.

Kipengele chenyewe ni hiki
Ukomo wa Uongozi Ulionyofolewa Kinyemela 2006.png



View attachment 233612View attachment 233613

Pasco.
Update 3 Final Update- Majibu ya Tundu Lissu, atoa siri ya jinsi kipengele hicho kilivyo yeyuka au kuyeyushwa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA
Wanabodi
Msingi Mkuu wa kazi ya uandishi wa habari ni ukweli, kuwa mkweli kuusema ukweli na kuandika ukweli!.

Sisi waandishi wa habari wa zamani tulifundishwa na waalimu wazungu, mimi mpaka leo mpaka kesho nakumbuka kauli ya Mwalimu wangu mzungu pale TSJ, a Canadian, Patrick Walsh akitufundisha kuwa kazi uandishi wa habari, "journalism is to tell nothing but the truth"

Hivyo mimi kama mwandishi wa habari, I have been telling the truth, writing the truth, until nilipogundua ukiwa mkweli mno , haswa kwa kuusema ukweli mchungu ambao watu hawapendi kusikia, utachukiwa and sometimes ni hatari hata kwako na kwa maisha yako.
Tumeyashuhudia kwa waandishi wakweli kama kuna Stan Katabalo, Ben Saanane, Azory Gwanda and the like!. Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Uandishi wa habari ni sawa na kazi ya siasa, siasa za ukweli wa kuleta maendeleo ya kweli ni siasa za kweli na wanasiasa wanaosema ukweli ndio wanasiasa wa ukweli wa kuleta maendeleo ya kweli. JPM alikuwa ni mmoja wao, Tundu Lissu pia yumo!.

Kuna wengi wanadhani kazi ya siasa na wanasiasa ni kazi ya kupiga bla bla, kuwadanganya wananchi kwa ahadi hewa kam kem zisizotekelezeka!.

Hivyo ndivyo walivyo wengi wa wanasiasa wetu wakiwemo baadhi ya viongozi wetu hadi wakuu, sio wakweli daima, ni watu wa blah blah nyingi!.

Ukimuondoa Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa ni mkweli daima, Rais Mwnyi yeye alikuwa ni mkimya sio mtu wa blah blah. Mkapa pia alikuwa mkweli, JK naomba nisimzungumzie ila JPM alikuwa ni mtu mkweli mwenye ukweli sometimes kupitiliza hivyo kumfanya achukiwe!.

Ni ukweli wa JPM ndio uliomfanya aweze kuyatenda yale aliyoyatenda. Kuna wakweli wa type fulani ambao wao ni "hapa kazi tuu", wakitaka jambo lao liwe na lifanyike kwa haraka, kama katiba, sheria, taratibu na kanuni, ni vikwazo, then wataziweka pembeni na kulifanya jambo lao, na ndio maana JPM alikanyaga katiba ili mambo yaende na kiukweli yalikwenda!. Watu tulinyooka!, nchi ilinyooka, mafisadi, wazembe, walarushwa walinyooka na vyama vilikaza kweli kweli!. Rais Magufuli ni Mkweli Daima!. Jee Tumuunge Mkono Rais Wetu Katika Kila Ukweli Wake, Hata Kama Uko Kinyume cha Katiba, Sera na Ilani?.

Mimi nimesoma sekondari Ilboru na Tundu Lissu, huyu jamaa Tundu Lissu ni mkweli na yuko bold tangu shuleni!. Kuna vitu vitatu Tundu Lissu anafanana sana na Magufuli, kimoja ni kwenye kuusema ukweli, Tundu Lissu ni mkweli kama JPM!, kwenye kuusema ukweli Lissu atausema no matter what!. Kitu cha pili ambacho Tundu Lissu ni kama Magufuli, naomba nisikitaje hapa kwasababu niliisha kitaja hapa, tena hicho cha pili Tundu Lissu ni zaidi ya Magufuli, hivyo hata ile 2020, mimi ni miongoni mwa tuliomchagiza Tundu Lissu agombee na Magufuli kwasababu Lissu ni zaidi ya Magufuli Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! ila kama mgombea wa CCM 2025, ni Mwanamke, simshauri Lissu kugombea!, maana kwa mwanamume jitu la miraba 4 kushindwa vibaya na mwanamke... itakuwa aibu!.

Jana nimetazama mahojiano ya Tundu Lissu kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV na kumsikiliza kwa makini Tundu Lissu, nikafarijika sana kwa jinsi Tundu Lissu alivyokuwa mkweli.

Mimi kama mwandishi mkweli kazi yangu ni kuuliza, hivyo hili ni bandiko la kuuliza, kumbe Tundu Lissu yuko kama JPM, kwa mambo matatu, JPM ni mtu mkweli. Na Tundu Lissu ni mtu mkweli. Jana meusema ukweli wa jinsi kipengele cha ukomo wa uongozi kilivyoyeyuka toka ndani ya katiba ya Chadema!. Kumbe kipengele hicho haikuyeyuka, kiliyeyushwa kwa kunyofolewa, kimya kimya na ku vanish into thin air!.

Kipengele hicho, nimekuwa nakiulizia sana kwa muda mrefu toka kwa viongozi wa Chadema, kuhusu kipengele hicho cha ukomo wa uongozi ndani ya katiba ya Chadema, kilitowekaje?, kiliondolewa au kiliyeyuka tuu chenyewe?

Hoja ya kunyofolewa kwa kipengele hicho, niliibua hapa Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Angalia nilichojibiwa na Dr. Slaa


Jibu la Dr. Slaa linaonyesha, licha ya huyu kuwa ni mtendaji mkuu wa Chadema, alipaswa kuijua katiba ya Chadema kinyume nyume!, lakini Dr. Slaa kumbe haijui katiba ya Chadema wala hajui uwepo wa kipengele hicho hivyo yeye akasema hakijawahi kuwepo!.

Mtu wa pili kulijibia hili ni J.J Mnyika, yeye alijibu

Jibu hili la Mnyika linaonyesha kipengele hicho hakikujadiliwa popote, hivyo kiliachwa kwa kuwa redundant.

Sasa jana ndio Tundu Lissu amefichua ukweli, kumbe kuna watu wakikijadili kipengele hicho kimya kimya bila Dr.Slaa na Mnyika kujua na kuamua kukinyofoa kimya kimya bila kuwasilishwa wala kujadiliwa!.
Kipengele chenyewe ni hiki View attachment 2845558

Kwa mujibu wa Tundu Lissu, sababu za kukiondoa ni changamoto ya kupata viongozi bora, kuwa kipindi cha miaka 10, hakitoshi kupika viongozi hivyo inapofika kipindi cha uchaguzi wa ndani, Chadema imekuwa ikipata changamoto ya kupata watu wa kujaza nafasi za viongozi waliotimiza umri wa miaka 10, hivyo wakaamua kukifuta kipengele hicho!.

Kiukweli kabisa kama chama hakina succession plan na hakuna grooming yoyote ya future leaders, na kipindi cha miaka 10 kinaonekana hakitoshi!, hii ni dalili ya incompetence ya aina fulani kwenye succession plan yao, na unaweza kukuta mpaka sasa ndani ya Chadema hakuna maandalizi yoyote ya succession plan ya Mwenyekiti wala hakuna grooming yoyote ya mtu yoyote wa kumpokea Mbowe uenyekiti!.

Lissu alipoulizwa kuhusu yeye kugombea urais 2025 alijibu kwanza katiba, alipobanwa sana akasema ndio atagombea!. That was a mistake!. Kwa vile Chadema bado hawajafanya kikao chochote cha kumteua mgombea wake wa urais wa 2025, hakuna ubaya wowote kwa mwana Chadema yeyote kuwa a wishful thinker kugombea urais 2025 lakini kutamka kwenye TV kuwa yes nitagombea wakati hakuna kikao chochote kilichomteua ni very dangerous!.

He who pays the piper, may call the tune!, whoever is paying the Chadema piper ndio may call the tune, nani agombee Chadema ili usimsumbue yule Malkia wetu, ikitokea sio Lissu, na huku Lissu ameisha tangaza kugombea, huko ndani kutakalika?.

Viongozi wasema ukweli wa type ya Lissu, ndio wanaolifaa taifa letu, na kwavile nilisema Lissu anafanana na Magufuli kwa mambo matatu, moja ni hili la ukweli, na hayo mawili yaliyobakia Lissu ni zaidi ya Magufuli, kama ikitokea Tundu Lissu akagombea tena urais na akachaguliwa kuwa rais wa JMT, then maendeleo ya Tanzania yatapaa maana Lissu ni zaidi ya Magufuli kwa hayo mengine mawili.

Hongera sana Tundu Lissu, jana umeongea vizuri kwenye ITV, hukutaja taja tena majina ya waliokushambulia.

Pia umesema dereva wao yuko Ubelgiji akihitajika kuhojiwa serikali inawaandikia serikali ya Belgium anarudishwa nchini kuhojiwa, kumbe Lissu hajui kuwa Tanzania hatuna mkataba wa extradition act na Belgium!.

Nimefurahi Lissu ameongea huku ametulia bila Jazba bila kutukana na au lugha ya maudhi.

Kilicho nifurahisha zaidi ni Tundu Lissu kuwa mkweli daima, keep on telling the truth and the truth will set you free!. Lissu akiendelea hivi, soon atakuwa like a real politician tena presidential material na sio mwanaharakati kama alivyo sasa!. Big up sana Bwana mdogo wangu wa Ilboru.

Paskali

Kitu kilichobakia kuufunga rasmi huu mjadala, ni kwa mimi kupita Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini, kukagua inventory ya Msajili wa vyama kuona hicho kilichofanyika mwaka 2006 kwa Chadema ni waliwasilisha katiba mpya ya Chadema, au waliwasilisha mabadiliko ya katiba?.
Paskali
 
Pasco nakujua wewe ni mtu wa kukurupuka mara nyingi hauko serious,

huwa unaendeshwa zaidi na matukio kuliko issues.

Katiba feki uijue wewe zaidi ya Msajili wa vyama.
 
CHADEMA isingekuwepo hadi leo hii kama CCM isingeruhusu "matukio", siyo maneno yangu haya ni maneno ya Mwigamba.

Ndiyo maana kukikosekana "tukio" CHADEMA wanalazimisha "matukio".

Hili la kuchakachua katiba yao hata kama mtu awe na akili mbovu kiasi gani ataona CHADEMA inamatatizo makubwa sana.
 
Pasco, nilijua lazima utajitokeza kwenye hili na hasa kutokana na mawasiliano yako na kiongozi aliyesimamishwa ili kupisha uchunguzi, huwezi kuchunguza mtu akiwa ameshikilia ofisi, sasa hapa una jaribu kuupindisha ukweli .

pili, ni kuwa Hiyo taarifa kuwa katiba ilibadilishwa ni uongo mtupu kwani hata katiba ya awali haikuwahi kuwa na kipengele cha ukomo wa uongozi, haya ni mambo ya kukariri , mwenye kupinga aweke ushahidi wake walau wa hicho kipengele cha katiba na kilikuwa kifungu gani na kilisomekaje , sio kuendeleza uongo na uzushi kama huu kwenye mitandao. wekeni hicho kifungu . Wenye katiba ya zamani, katiba ya Chadema ilibadilishwa mwaka 2006 , sasa leo ni mwaka 2013 why muda wote huo hapakuwa na haya?

Pasco, Mwigamba mwaka 2006 wakati katiba ya Chadema inabadilishwa hakuwa kwenye chama na hakuwa na nafasi yeyote ile, wakati huo alikuwa anafanya kazi UN ICTR , sasa leo naye unamtumia kama reference na kuhukumu bila kujipa muda wa kufanya hata utafiti kidogo tu? Hebu jaribu kuutafuta ukweli , hizi ni propaganda za kitoto kwani nyaraka zilizopitishwa na mkutano mkuu 2006 zipo na wajumbe wa mkutano mkuu waliobakia na nakala , wekeni hapa , ila sio kupiga makelele kama unavyofanya , ukweli uko mmoja tu na huwa haugawanyiki.
 
Pasco nakujua wewe ni mtu wa kukurupuka mara nyingi hauko serious,

huwa unaendeshwa zaidi na matukio kuliko issues.

Katiba feki uijue wewe zaidi ya Msajili wa vyama.

CHADEMA ndiyo inayoendeshwa kwa matukio na hii ni kwa mujibu wa Mwigamba.
 
Nafasi ya Uenyekiti wa Chama mbona inawatoa watu jasho namna hii?Huku ni kuzunguka tu.....Hebu nendeni straight kwenye point.

Nadhani ikithibitika hivyo basi ofisi ya msajili nayo itabidi kuwajibika.Ni kwanini isemwe kipindi hiki na si wakati wowote?

1. Katiba ilichakachuliwa au haikuchakachuliwa?

2. Unapouliza ni kwanini isemwe kipindi hiki, wewe ulitaka isemwe kipindi gani?
 
....

......Chadema purification .....2014 - 2015 !!!

....Kwanini isiwe Tundu Lissu au Mwingine?CHADEMA ni taasisi na kuna hazina ya Viongozi wenye misimamo na wasioyumbishwa.Sio chama cha mtu mmoja.Jitihada zenye hila zitashindwa vibaya sana.Trust me!
 
Pasco

Uko kwenye mlengo tata usiotimilika, tafsiri ya unachokiota ni kinyume chake
Mkuu Yericko Nyerere, mlengo tata usiotimilika, unapimika kwa specified time frame iliyowekwa, kama hiyo time haija lapse, huwezi sema usiotimilika, subiria time lapse ndipo ulizungumzie hili!.

Kuhusu ndoto, ni kweli, naweza kuwa naota ndoto mchana kweupe macho wazi na kidole kwenye keyboard, nayo pia ni ndoto!.
Pasco.
 
Nafasi ya Uenyekiti wa Chama mbona inawatoa watu jasho namna hii?Huku ni kuzunguka tu.....Hebu nendeni straight kwenye point.

Nadhani ikithibitika hivyo basi ofisi ya msajili nayo itabidi kuwajibika.Ni kwanini isemwe kipindi hiki na si wakati wowote?
​Ili kukata ngebe za baadhi ya wachangiaji wa mada hii ni vema kipengele hicho cha katiba kikawekwa hapa jamvini!
 
Pasco nakujua wewe ni mtu wa kukurupuka mara nyingi hauko serious,

huwa unaendeshwa zaidi na matukio kuliko issues.

Katiba feki uijue wewe zaidi ya Msajili wa vyama.
Mkuu Feedback, mimi ni ordinary mind, tunao discuss events, sio simple mind ku discuss people na bado sijawa great mind ku discuss ideas, hiki ninachikijadili humu ni "event" na jinsi Chadema inavyoweza futwa na sio "issues" ya Tuhuma za Katiba Fake!, hata tuhuma ni event tuu sio issue!.

Ila pia kama mwanahabari ripoter, events ni ndio kila kitu, issues ni kwa waandishi wa makala!.
Mimi ni reporter tuu, tena nimeuliza tuu na kutoa angalizo!.
Pasco.
 
Pasco, nilijua lazima utajitokeza kwenye hili na hasa kutokana na mawasiliano yako na kiongozi aliyesimamishwa ili kupisha uchunguzi, huwezi kuchunguza mtu akiwa ameshikilia ofisi, sasa hapa una jaribu kuupindisha ukweli ......

Aisee...kumbe Pasco wa JF naye ni mpiga ukombozi wa watanzania kufikia maendeleo yenye tija kwa raia wote. Yaani anatengeneza 'fitina' kwa viongozi wa vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom