Safi sana wabunge wa UKAWA

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,683
149,887
Leo hii tena wametoka mara tu baada ya dua ya kuliombea Bunge kukamilika.Haina haja ya kuongozwa na mtu msie na imani nae.Walizani posho ndio zingewarudisha Bungeni.

Mbunge mzalendo hawezi kuweka mbele posho kuliko maslahi ya anaowawakilisha.

Wabunge wa UKAWA hawawezi kuishi kwa posho bali kwa kila neno la kizalendo la kuwaunga mkono.

UKAWA mnavaa viatu vya mzee Mandela ambae alivumilia mengi ila mpaka leo hii dunia nzima inamuheshimu.

Pambanane mkitambua the end justifies the means.
 
Wabunge wa upinzani almaarufu UKAWA waendelea kususia vikao vya bunge wakiongozwa na kiongozi wao Mh. Mbowe.

Inasikitisha sana kwa wapiga kura wetu wito wangu wakae meza moja ya mazungumzo kumaliza mgogoro huu.
 
Hahahaha.... Sasa bunge lenyewe bado siku kadhaa tu liishe... Mwisho siku UKAWA ndio watakao kuwa wamepotza...

Na kama hawajui basi ccm ndio wanapenda hivyo ilivyo sasa....
 
Nimewaona, wametoka kama mashujaa wakiacha sura za mawaziri na wabunge wa ccm zikiwa zimetahayari.

Habari toka Dodoma zinasema wabunge wa CCM nao wanahoji sababu ya naibu spika kutokutoa nafasi kwa wenyeviti ni nini? Sasa kwa nini walichagua hao wenyeviti?
Ni wazi kuwa kweli bunge linaongozwa na mtu mwingine nje ya bunge.

Nao sasa wamechoka kuburuzwa wanawataka wenzao wajadiliane na kupingana kwa hoja sio kutumika kusema ndio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom