Safari za nje za Mhe. Rais Kikwete 2010 - 2015

Beling hiyo avata yako inaniletea shida kila ninapoiona,

anyway, lets get back to topic, jamaa mara ya mwisho nilisikia yupo DRC kaenda kutembelea mwana, nadhani akitoka atapitia kwa swaiba wake Mugabe baada ya hapo sijui,tena nasema sijui na sitaki kupigwa picha... lol Tz

Pole D5 itabidi nitafute nyingine kamanda...usipate shida tena:))
Back to topic,DRC ameshatoka utamuweza na naona nilimuandalia ratiba Jeykey kabla hajatua France,ha ha..Eniwei, Welcome to Paris Mr.President!..
 
Kwa muda mrefu sana kumekuwa na kilio au malalamiko ya baadhi ya watu kuhusiana na safari za JK nje ya nchi, hata wengine kudiriki kumuita yeye kwamba ni mtalii au hata Vasco da Gama. Wengine wamedai kwamba safari hizi ni kupoteza fedha na kwamba hazina tija kwa nchi yetu. Baadhi ya wanasiasa na hata wananchi wa kawaida wamekuwa wakisema kwamba alitakiwa abaki hapa hapa ili apate muda wa kutatua shida za wananchi badala ya "kuzurura". Mimi ninaomba kuingia kwenye mjadala huu kwa kujaribu kuunga mkono mantiki ya safari za JK na hata matunda yake pamoja na kwamba hili litanitia kwenye msukosuko wa vita vya maneno humu JF.

Mimi ninavyofikiri ni kwamba JK kama mkuu wa nchi amepewa dhamana ya kuongoza nchi hii na kuwakilisha maslahi ya watanzania kila wakati. Moja ya maslahi yetu ni kule kuitangaza nchi yetu huko nje na kujenga mahusiano mema ya kimataifa. Hili hufanyika katika namna tofauti, moja wapo ikiwepo hii ya kufanya ziara za ama kujitambulisha au kuingia katika ushirikiano wa kisiasa na kibiashara na mataifa rafiki, ikiwa pia na kutambua na kuzitumia fursa za kiuchumi katika mataifa anayoyatembelea. Ziko nyakati yeye hupewa mialiko inayomhitaji kuitekeleza, vinginevyo ataonekana ni kiongozi asiyejua reciprocity maana hata wale viongozi wanaotutembelea hawatakuwa na sababu ya kuikubali mialiko yetu. Kama kiongozi, yeye hupewa majukumu katika majukwaa mbalimbali anayohudhuria na baada ya hapo hutakiwa kuyatekeleza. Hili lilifanyika hata wakati wa baba wa taifa na hata enzi za mzee Mkapa. Leo hili linaonekana la ajabu. Shida zetu haziwezi kutatuliwa kwa kukaa tu ikulu na kusalimia wananchi. Hata hao viongozi walio kwenye misukosuko sasa hivi husafiri kwa nadra na bado matatizo ya watu wao yako pale pale. Waoneni Mugabe, Mubarak, Gadafi na hata Kibaki ambaye hata hapo Uganda huenda kwa nadra sana.

Mimi nafikiri tuangalie kwa undani hoja hizi tunazozitoa na hiyo inaweza kutufanya tuelewe chanzo cha matatizo yetu na hata suluhu ya matatizo hayo, na siyo kufikiria kwamba chanzo cha matatizo ni safari za nje au utatuzi wake ni kukaa hapa na kutazamana na wananchi wake.
 
juzi alikuwa safarini akaacha watu wanaomboleza, leo yuko france akitohuko anaenda sijui nchi ngani.. Mimi naona niuzaifu wawasaidizi wake kuna sehemu siyo lazima rais aende anaweza kwenda waziri wa wizara husika..hatutaki akae ikulu tunataka atembele wananchi wake ajione matatizo yaliyoko kama anavyofanya kipind cha kampeni vinginevyo nitaendelea kumuona mtalii
 
Mnamuonea bure. Ameshafanya ziara ya mikoa yote ya nchi hii, pengine kuliko rais yeyote aliyemtangulia. Kama safari za mikoani ni kujua shida za wananchi basi hakuna ambapo hajaenda na kwa hiyo anajua kila kitu sasa. Kazi ya utatuzi wa shida hizo si kama mnada wa mchikichini ambako watu hupiga kelele na kutangaza kinachofanyika. Ukiwa kiongozi unahemea kwa mikono yote miwili, mmoja katika vyanzo vya ndani na mwingine kwa marafiki wa nje. Mkuu anafanya ambacho kiongozi yeyeote muwajibikaji angefanya.
 
Mbopo,
Nafikiri umeanzisha topic nzuri. Wengi hatupingi kusafiri kwa rais. Lakini mpaka hivi leo, mwaka wake wa sita mamlakani, huwezi kutuambia kuwa safari za Kikwete zimesaidia nchi yetu kufahamika au kuongeza rate ya uwekezaji. Kabla ya kuanza safari hizo, Kenya na Uingereza zimekuwa zinaongoza katika uwekezaji nchini Tanzania. Hata hivi leo, hata baada yake kwenda Marekani mara kadhaa, uwekezaji wa Marekani Tanzania haujaongezeka kiasi kwamba tunaona kuna tofauti. Nasikia safari yake ya kwanza Marekani alikuja kukutana na Shaquille O'neal. Eti kuna ukweli katika madai hayo? By the way, mimi naamini kuwa uwekezaji Tanzania utaongezeka tu pale tutakaposhughulikia kikamilifu matatizo ya miundombinu, urasimu na umeme wa hakika. Bila kufanya homework yetu tutakuwa tunapiga dana dana tu.
 
Nakumbuka kuna wakati makala moja ilichapishwa katika gazeti mfu la Mjengwa (Kwanza Jamii) ikizungumzia jambo hili hili. Makala hiyo (unaweza kuisoma tena HAPA), ilizusha mambo mengi sana.

Kwangu mimi sina ugomvi na safari za rais na naamini kwamba anafanya hivyo kwa maslahi ya taifa. Na naamini kwamba safari hizi zimeshaleta faida kwa taifa letu. Pengine kinachogomba ni kutaka kujua faida ambazo zimepatikana kutokana na safari hizi. Viongozi kusafiri nje ni jambo la kawaida na kusema kweli si lazima kila safari inayofanyika waje watoe taarifa kuhusu mafanikio ya safari hiyo.

Pengine tatizo hapa ni kutokumwamini rais. Kuna watu ambao wanadhani kwamba raisi anakwenda huko nje kutembea tu. Pengine wakati umefika kwa watu wanaohusika huko Ikulu (akina Rweyemamu) kutoa taarifa kamili kuhusu mafanikio ambayo safari za rais zimeleta kama kweli kuna ulazima wa kufanya hivyo.

Hata kama akibakia hapa hapa, bila kuwa na mikakati sahihi ya kutatua matatizo yetu ni kazi bure tu.
 
Jasusi umetoa hoja nzuri sana, na hasa kuhusiana na mahitaji muhimu yanayoweza kuchochea uwekezaji. Hata hivyo, uwekezaji siyo matunda pekee au tija kwa safari zake. Kwa sasa watalii wa marekani wameongezeka sana na ndiyo wanaofanya idadi kubwa ya watalii wanaotembelea nchini sasa hivi na haya ni matunda ya kuitangaza nchi ambayo kwa kiasi kikubwa kumefanywa na yeye. Mimi nashawishika kwamba safari hizi zina matunda na yataendelea kuongezeka kadiri tutakavyojipa muda wa kutathmini kwa uyakinifu yale yaliyofanikiwa kutokana na safari hizi.
 
Kwa muda mrefu sana kumekuwa na kilio au malalamiko ya baadhi ya watu kuhusiana na safari za JK nje ya nchi, hata wengine kudiriki kumuita yeye kwamba ni mtalii au hata Vasco da Gama. Wengine wamedai kwamba safari hizi ni kupoteza fedha na kwamba hazina tija kwa nchi yetu. Baadhi ya wanasiasa na hata wananchi wa kawaida wamekuwa wakisema kwamba alitakiwa abaki hapa hapa ili apate muda wa kutatua shida za wananchi badala ya "kuzurura". Mimi ninaomba kuingia kwenye mjadala huu kwa kujaribu kuunga mkono mantiki ya safari za JK na hata matunda yake pamoja na kwamba hili litanitia kwenye msukosuko wa vita vya maneno humu JF.

Mimi ninavyofikiri ni kwamba JK kama mkuu wa nchi amepewa dhamana ya kuongoza nchi hii na kuwakilisha maslahi ya watanzania kila wakati. Moja ya maslahi yetu ni kule kuitangaza nchi yetu huko nje na kujenga mahusiano mema ya kimataifa. Hili hufanyika katika namna tofauti, moja wapo ikiwepo hii ya kufanya ziara za ama kujitambulisha au kuingia katika ushirikiano wa kisiasa na kibiashara na mataifa rafiki, ikiwa pia na kutambua na kuzitumia fursa za kiuchumi katika mataifa anayoyatembelea. Ziko nyakati yeye hupewa mialiko inayomhitaji kuitekeleza, vinginevyo ataonekana ni kiongozi asiyejua reciprocity maana hata wale viongozi wanaotutembelea hawatakuwa na sababu ya kuikubali mialiko yetu. Kama kiongozi, yeye hupewa majukumu katika majukwaa mbalimbali anayohudhuria na baada ya hapo hutakiwa kuyatekeleza. Hili lilifanyika hata wakati wa baba wa taifa na hata enzi za mzee Mkapa. Leo hili linaonekana la ajabu. Shida zetu haziwezi kutatuliwa kwa kukaa tu ikulu na kusalimia wananchi. Hata hao viongozi walio kwenye misukosuko sasa hivi husafiri kwa nadra na bado matatizo ya watu wao yako pale pale. Waoneni Mugabe, Mubarak, Gadafi na hata Kibaki ambaye hata hapo Uganda huenda kwa nadra sana.

Mimi nafikiri tuangalie kwa undani hoja hizi tunazozitoa na hiyo inaweza kutufanya tuelewe chanzo cha matatizo yetu na hata suluhu ya matatizo hayo, na siyo kufikiria kwamba chanzo cha matatizo ni safari za nje au utatuzi wake ni kukaa hapa na kutazamana na wananchi wake.

Mkuu,
Heshima yako!

Umeleta hoja nzuri sana kwa kujadiliwa nami naiunga mkono sana hasa kwenye bold nyekundu.Hapo kwenye bold nyeusi nitatofautiana nawe kwani ninaona kama ni hoja nyepesi mno kuhalalisha safari za kiongozi wa juu kabsa wa nchi.

Rais kama rais hapaswi kutumia muda mwingi angani akisafiri kwenda nchi za watu hasa pale ambapo ameshakaa madarakani muda wa kutosha.Sasa hivi ni kipindi cha pili, haihitaji sana kuendelea kujitambulisha au kuitangaza nchi yetu kama ulivyosema.

Kwa kifupi, pamoja na kuunga mkono hatua ya rais kusafiri kwa maslahi ya taifa, bado nashauri rais ashauriwe kuwa sensitive na sentiments za wananchi. Wananchi wako desperate katika kipindi hiki kigumu chenye shida za kila aina na ugumu wa maisha.Wananchi hawawezi kuona value inayoongezeka kwa rais kusafiri .Wananchoona au kuhisi ni gharama zinazoenda kumwezesha rais kusafiri.Wao wanahesabu hiyo gharama na kufikiria ni jinsi gani pesa hizo zingeweza kusaidia kupunguza matatizo na kero wanazozipata.

Kwamba raisi ana reciprocate mialiko ya wenzake siyo ishu kwa mlalahoi wala haiingii akilini.Wewe na mimi tunaweza kuelewa umuhimu wa rais kusafiri lakini bibi yangu kule kijijini hawezi kuelewa!
 
Nakumbuka kuna wakati makala moja ilichapishwa katika gazeti mfu la Mjengwa (Kwanza Jamii) ikizungumzia jambo hili hili. Makala hiyo (unaweza kuisoma tena HAPA), ilizusha mambo mengi sana.

Kwangu mimi sina ugomvi na safari za rais na naamini kwamba anafanya hivyo kwa maslahi ya taifa. Na naamini kwamba safari hizi zimeshaleta faida kwa taifa letu. Pengine kinachogomba ni kutaka kujua faida ambazo zimepatikana kutokana na safari hizi. Viongozi kusafiri nje ni jambo la kawaida na kusema kweli si lazima kila safari inayofanyika waje watoe taarifa kuhusu mafanikio ya safari hiyo.

Pengine tatizo hapa ni kutokumwamini rais. Kuna watu ambao wanadhani kwamba raisi anakwenda huko nje kutembea tu. Pengine wakati umefika kwa watu wanaohusika huko Ikulu (akina Rweyemamu) kutoa taarifa kamili kuhusu mafanikio ambayo safari za rais zimeleta kama kweli kuna ulazima wa kufanya hivyo.

Hata kama akibakia hapa hapa, bila kuwa na mikakati sahihi ya kutatua matatizo yetu ni kazi bure tu.

Hilo neno mkuu! Umeiweka vizuri sana!
 
Siungi mkono hoja, safari hizi zingekuwa na tija nadhani saa hizi uchumi wetu ungepaa kuliko awamu yoyote kwani JK amesafiri kuliko watangulizi wake wote.
 
Mimi nafikiri tuangalie kwa undani hoja hizi tunazozitoa na hiyo inaweza kutufanya tuelewe chanzo cha matatizo yetu na hata suluhu ya matatizo hayo, na siyo kufikiria kwamba chanzo cha matatizo ni safari za nje au utatuzi wake ni kukaa hapa na kutazamana na wananchi wake.

Na mimi siungi mkono hizo safari za Kiwete na hili ni suala la saikolojia tu. Ni kwamba wananchi tuna matatizo mengi na umasikini unaongezeka ha hatuoni faida ya hizo safari zake kwenye kuinua hali ya kimaisha wa watu wa chini. Vile vile, yeye Kiwete (kama alivyo Mwinyi) hana legacy yoyote ya kimataifa kama alivyokuwa Nyerere au Mkapa kwa hiyo asijisumbue. Akiondoka kwenye urais atasahaulika haraka kama alivyosahaulika Mwinyi. Tunajua tatizo kubwa tulilonalo nchini Tanzania ni UFISADI asitafute mchawi kwa kwenda nje na kutoa takwimu, nk. Kwa hiyo hizo fedha zinazotumika kwa ziara za nje zingetumika kwa mambo mengine nchini Tanzania na wakati huo huo angetulia nchini na kupambana na ufisadi.
 
Tatizo wa tanzania wengi tukiwa TZ, tunafikiri Ulaya au huku tunapo paita ng'ambo ni kila kitu. Sio kweli ndugu zangu. kiongozi mkubwa wa hizo nchi zetu akija ulaya hata anatembea na gari ya balozi tu! Nani atakaa anamuangalia hapo, hata unaweza usimuone kwenye taarifa yoyote ya habari. Tatizo wa Tanzania tunafikiri ulaya au marekani ni nusu mbinguni ambapo mtu akifika huko anarudi na kila kitu. Eti raisi anasema saa hii nilikua naongea na Obama. Huo ni usanii. Tengeneza nyumani kwako, kwa kile ulichopewa na Mwenyezu Mungu, na watu wote watapapenda hata watalii watakuja wenyewe!
 
Kuna wakati alikwenda unyamwezini akapiga picha na boys 2 men, swali ambalo sijalipatia jibu ni je, ni. Yeye alitaka kupiga nao picha au ni wao walitaka?
 
Kwa muda mrefu sana kumekuwa na kilio au malalamiko ya baadhi ya watu kuhusiana na safari za JK nje ya nchi, hata wengine kudiriki kumuita yeye kwamba ni mtalii au hata Vasco da Gama. Wengine wamedai kwamba safari hizi ni kupoteza fedha na kwamba hazina tija kwa nchi yetu. Baadhi ya wanasiasa na hata wananchi wa kawaida wamekuwa wakisema kwamba alitakiwa abaki hapa hapa ili apate muda wa kutatua shida za wananchi badala ya "kuzurura". Mimi ninaomba kuingia kwenye mjadala huu kwa kujaribu kuunga mkono mantiki ya safari za JK na hata matunda yake pamoja na kwamba hili litanitia kwenye msukosuko wa vita vya maneno humu JF.

Mimi ninavyofikiri ni kwamba JK kama mkuu wa nchi amepewa dhamana ya kuongoza nchi hii na kuwakilisha maslahi ya watanzania kila wakati. Moja ya maslahi yetu ni kule kuitangaza nchi yetu huko nje na kujenga mahusiano mema ya kimataifa. Hili hufanyika katika namna tofauti, moja wapo ikiwepo hii ya kufanya ziara za ama kujitambulisha au kuingia katika ushirikiano wa kisiasa na kibiashara na mataifa rafiki, ikiwa pia na kutambua na kuzitumia fursa za kiuchumi katika mataifa anayoyatembelea. Ziko nyakati yeye hupewa mialiko inayomhitaji kuitekeleza, vinginevyo ataonekana ni kiongozi asiyejua reciprocity maana hata wale viongozi wanaotutembelea hawatakuwa na sababu ya kuikubali mialiko yetu. Kama kiongozi, yeye hupewa majukumu katika majukwaa mbalimbali anayohudhuria na baada ya hapo hutakiwa kuyatekeleza. Hili lilifanyika hata wakati wa baba wa taifa na hata enzi za mzee Mkapa. Leo hili linaonekana la ajabu. Shida zetu haziwezi kutatuliwa kwa kukaa tu ikulu na kusalimia wananchi. Hata hao viongozi walio kwenye misukosuko sasa hivi husafiri kwa nadra na bado matatizo ya watu wao yako pale pale. Waoneni Mugabe, Mubarak, Gadafi na hata Kibaki ambaye hata hapo Uganda huenda kwa nadra sana.

Mimi nafikiri tuangalie kwa undani hoja hizi tunazozitoa na hiyo inaweza kutufanya tuelewe chanzo cha matatizo yetu na hata suluhu ya matatizo hayo, na siyo kufikiria kwamba chanzo cha matatizo ni safari za nje au utatuzi wake ni kukaa hapa na kutazamana na wananchi wake.

....nchi haikaliki,,,,,anazurura tu miaka mitano iende!!!!
 
hebu nijaribu kubenjua hili dungu na gololi ya kioo,issue ni safari au nani kasafiri, kuna hoja zingine zinaonyesha bado madhara ya chanjo hususan ya ndui bado zinasumbua kadamnasi ya walidanganyika, :hand:
 
Usimfananishe Kikwete na Kibaki. Kibaki hawezi kusafiri hovyo hovyo, anahofia akirudi atakuta Odinga keshachukua nchi, Kagame vilevile huwa hapendi kulala nje ya nyumbani kwake kwa sababu hizo hizo. Sasa JK wetu kila akisafiri akirudi anaikuta nchi kama alivyoiacha, nchi yetu ya amani bwana. JK anajiamini na anatuamini hatuwezi kumsaliti, mwacheni akabembee baba yetu..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom