Safari yangu ya kumuona Maxence, nimejifunza mengi gerezani

Mimi pia nimepata nafasi ya kumuona swahiba wangu Melo leo hii.

At least gereza la Keko hali siyo mbaya kuliko segerea, keko unapata nafasi ya kuongea na mahubusu face to face ikibidi zaidi mnaongea wawili tu.

Tupo pamoja na mkuu wetu wa JF.
Da hata wewe mkuu? Inatia moyo kuwa wamoja katika mambo yasiyo ya kiitikadi
 
Mwenyezi Mungu ambariki Maxcence pamoja na wale wote waliotuwakilisha kwa kumtembelea pale gereza la Keko. Wengine tuko nje ya Dar.
 
Magereza zetu nyingi, hali sio mbaya kama za Kenya, Uganda, au nchi nyingi za Africa... kwa hili tuwape pongezi serikali yetu kuwajali mahabusu na wafungwa...

Max atatoka tu, ni haki yake kupata dhamana, serikali na mahakama hazijakataa dhamana yake..
 
Haijawa mwiba kwakua hata hao watawala wanataka kuwepo kwa huduma bora kwa mteja na hayo magereza yako chini ya Serikali ambayo inaongozwa na hao watawala unaowasingizia mambo ambayo hayana nyuma wala mbele.
Umeandika NiNi hapo? Watawala wanataka huduma bora kwa mteja yupi? Watawala hao Ni akina nani? Polisi? Mahakama? Magereza? Au mtu fulani anayeamua tu kumtesa mtu mwingine kwa hayo mambo yasiyo na mbele wala nyuma?
 
Habari wakuu, mie ni miongoni mwa tuliojaaliwa kumtembelea ndugu yetu Maxence Melo gereza la Keko. Nikiri sijawahi kufika gerezani ama kwa kushikwa ama kwenda kumtembelea mtu hivyo pamoja na kumuona Max nmejifunza hali ilivyo kwenye Magereza yetu japo sio kwa undani.

Nilifika wakanikagua na kisha nikaingia ndani, ukiingia na simu unaiacha kwa mlinzi ikiwa na ID. Ukifika unachukua namba na namba ilipofika nikaitwa ndani. Alietusindikiza akaishia mlangoni na ndani unasema jina. Nilichokiona pale chini watu wa magereza wanawajua sana watu wao na ni marafiki(Sijui watu wasipokuwepo).

Nilivyotaja jina, yule jamaa wa magereza akasema 'Huyu mtu kavunja rekodi leo' hivyo hongera kwetu sote tulioenda kisha akamuita mtu akanisindikiza juu na kuitiwa Maxence. Nilifika kwa Maxence nikamsalimu na kwa ujumla alikuwa na bashasha. Akasema anategemea kutoka lakini hata asipotoka kwa kuwa mambo yako sawa kwetu hata akilia sikukuu gerezani hewala.

Tukaongea mambo mawili matatu na miongoni mwa wachangiaji wa mawili matatu walikua watu wa magereza na nilienda na vitu kadhaa, akachukua kadhaa na vilivyobaki akasema nimpe jamaa aliempokea gerezani(Alikua sehemu ya chini) kwani yeye tayari ana vingi sana.

Wakati nasubiri kumuona Maxence nilipata nafasi ya kuongea na watu kadhaa ambao wameenda kuwaona na kuwapa chochote kitu ndugu zao, nilisikia hadithi kadhaa zilizopelekea watu kuwekwa ndani(Wote bado mahabusu). Najua ni stori za upande mmoja ila kuna watu wamekaa four good years bila hukumu, hebu fikiria kesi ikaisha halafu hana hatia!

Poleni kwa kuwachosha, ni mara yangu ya kwanza wakuu na nahisi washkaji wanaishi peace sana tofauti na tunavyosikia pia pongezi sana kwa askari wa magereza kama jinsi nilivyowaona leo ndio wako hivyo siku zote(Kuanzia mapokezi mpaka ndani).

NB: Gerezani sio kuzuri na anaenda yeyote, mahakama ziongezewe uwezo wa kusikiliza kesi ili wasiohusika waondoke, kumuweka mtu miaka minne bila hukumu kwangu ni zaidi ya hukumu kwani hasira ya mtu kunisingizia na kunisababishia maumivu naijua mwenyewe.

[HASHTAG]#Kesho[/HASHTAG] ntakuwa mahakamani
Magereza hawana shida,hawa polisi ndio kikwazo!Ungeenda kumuona akiwa kituo cha polisi!
 
Jamani wanaume wa Dar na wanawake kwa ujumla,tujitokeze mahakamani kwa wingi ili hii habari izidi kuvuma!

[HASHTAG]#freemaxmelo[/HASHTAG]
 
Natamani hata kulia basi tu
7e6b4a5eb5220acf106caf95fdba9e27.jpg
Bora wewe unayetamani,mimi kila nikiona picha za huyu mtu naliaaaa.
Hastahili haya jamani,he is too kind.
Dah
 
-Ningemshauri tu Maxence Melo vyakula, matunda au vinywaji anavyopelekewa asitumie mpaka kwa mtu maalum anaemhudumia. Sio wote watu wazuri
-Kuhusu kucheleweshwa kesi kusikilizwa mahakamani ni tatizo kubwa sana.
-Pongezi kwa wote mliofika kumfariji Maxence Melo.
 
Ndipo tuliposema, ahimidiwe bwana Mungu wa majeshi na sifa zote ziwe juu yake.

Max atatoka kwa kuwa Mungu yu upande wetu
 
Back
Top Bottom