Nigeria: Wafungwa 4,068 walioshindwa kulipa faini waachiwa huru

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Serikali ya Nigeria imetangaza kuwaachia huru zaidi ya Wafungwa 4000 walioshindwa kulipa faini mbalimbali ikiwa ni mpango wa kupunguza msongamano gerezani

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nigeria, Olubunmi Tunji-Ojo amesema jumla ya Wafungwa kabla ya msamaha huo ni 80,804 katika magereza 253.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa (UN) ulisema Nigeria inawafungwa na mahabusu mara mbili ya uwezo wa magereza yaliyopo ambapo Watu wengi wanawekwa ndani Miaka kadhaa kusubiri hukumu.


#####

Nigeria frees 4,000 inmates jailed over fines


The Nigerian government has announced that more than 4,000 prisoners have been released to ease overcrowding in jails.

Interior Minister Olubunmi Tunji-Ojo said those freed were inmates who had been in custody for not paying fines.

He said it was part of an initiative by President Bola Tinubu which included introducing more non-custodial sentences.

The United Nations has said that Nigeria's prisons are currently operating at more than twice their total capacity.

Suspects often have to wait years in detention before being tried.

Source:BBC


Rais Tinubu aachilia huru maelfu ya wafungwa Nigeria kukabiliana na msongamano gerezani


Maelfu ya wafungwa kote nchini Nigeria wameachiliwa kutoka gerezani katika juhudi za kukabiliana na msongamano wa watu, waziri wa mambo ya ndani Olubunmi Tunji-Ojo alisema Jumamosi kwenye mtandao wa kijamii.

Maelfu ya wafungwa kote nchini Nigeria wameachiliwa kutoka gerezani katika juhudi za kukabiliana na msongamano wa watu, waziri wa mambo ya ndani Olubunmi Tunji-Ojo alisema Jumamosi kwenye mtandao wa kijamii.

Hatua hiyo ni sehemu ya harakati za Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu, ambaye alichaguliwa mapema mwaka huu, kupunguza msongamano katika magereza ya Nigeria yenye idadi kubwa ya watu.

Jana, tulitangaza kuachiliwa kwa wafungwa 4,068 kati ya 80,804 katika jela zetu 253 kote nchini kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kulipa faini, Olubunmi Tunji-Ojo aliandika katika taarifa yake kwenye mtandao wa X.

Alitoa tangazo hilo baada ya kuitembelea jela ya Kuje karibu na mji mkuu Abuja.

Chanzo: VOA
 
Back
Top Bottom