Safari yangu ya kumuona Maxence, nimejifunza mengi gerezani

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,153
2,000
Habari wakuu,

Mimi ni miongoni mwa tuliojaaliwa kumtembelea ndugu yetu Maxence Melo gereza la Keko. Nikiri sijawahi kufika gerezani ama kwa kushikwa ama kwenda kumtembelea mtu hivyo pamoja na kumuona Max nmejifunza hali ilivyo kwenye Magereza yetu japo sio kwa undani.

Nilifika wakanikagua na kisha nikaingia ndani, ukiingia na simu unaiacha kwa mlinzi ikiwa na ID. Ukifika unachukua namba na namba ilipofika nikaitwa ndani. Alietusindikiza akaishia mlangoni na ndani unasema jina. Nilichokiona pale chini watu wa magereza wanawajua sana watu wao na ni marafiki(Sijui watu wasipokuwepo).

Nilivyotaja jina, yule jamaa wa magereza akasema 'Huyu mtu kavunja rekodi leo' hivyo hongera kwetu sote tulioenda kisha akamuita mtu akanisindikiza juu na kuitiwa Maxence. Nilifika kwa Maxence nikamsalimu na kwa ujumla alikuwa na bashasha. Akasema anategemea kutoka lakini hata asipotoka kwa kuwa mambo yako sawa kwetu hata akilia sikukuu gerezani hewala.

Tukaongea mambo mawili matatu na miongoni mwa wachangiaji wa mawili matatu walikua watu wa magereza na nilienda na vitu kadhaa, akachukua kadhaa na vilivyobaki akasema nimpe jamaa aliempokea gerezani(Alikua sehemu ya chini) kwani yeye tayari ana vingi sana.

Wakati nasubiri kumuona Maxence nilipata nafasi ya kuongea na watu kadhaa ambao wameenda kuwaona na kuwapa chochote kitu ndugu zao, nilisikia hadithi kadhaa zilizopelekea watu kuwekwa ndani(Wote bado mahabusu). Najua ni stori za upande mmoja ila kuna watu wamekaa four good years bila hukumu, hebu fikiria kesi ikaisha halafu hana hatia!

Poleni kwa kuwachosha, ni mara yangu ya kwanza wakuu na nahisi washkaji wanaishi peace sana tofauti na tunavyosikia pia pongezi sana kwa askari wa magereza kama jinsi nilivyowaona leo ndio wako hivyo siku zote(Kuanzia mapokezi mpaka ndani).

NB: Gerezani sio kuzuri na anaenda yeyote, mahakama ziongezewe uwezo wa kusikiliza kesi ili wasiohusika waondoke, kumuweka mtu miaka minne bila hukumu kwangu ni zaidi ya hukumu kwani hasira ya mtu kunisingizia na kunisababishia maumivu naijua mwenyewe.

[HASHTAG]#Kesho[/HASHTAG] ntakuwa mahakamani
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,290
2,000
Mimi pia nimepata nafasi ya kumuona swahiba wangu Melo leo hii.

At least gereza la Keko hali siyo mbaya kuliko segerea, keko unapata nafasi ya kuongea na mahubusu face to face ikibidi zaidi mnaongea wawili tu.

Tupo pamoja na mkuu wetu wa JF.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom