Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 15,037
- 16,031
[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana huo ni uongo kabisa manake JF Ina vitu vingi sana vya maana ambavyo havina mringo WA upande wowote ila watu kama ndiye unayeharibu JF kwa kufanya kila kitu Ni cha kisiasa wakati so kweli.Kuliko uandike vitu vya uongo kama hivi Ni busara kukaa kimya.Nilishasema Lumumba wengi wanafurahia sana hii hali.
Sikuzote yakisemwa yanayowaumbua inakuwa ni kuropoka, lakini yakisemwa yanayotukuza upumbavu wenu basi yanakuwa point.Povu!Lema si ametaka mwenyewe kwenda lupango au alitumwa aropoke?
Haijawa mwiba kwakua hata hao watawala wanataka kuwepo kwa huduma bora kwa mteja na hayo magereza yako chini ya Serikali ambayo inaongozwa na hao watawala unaowasingizia mambo ambayo hayana nyuma wala mbele.
Nmejikuta nacheka peke yanguKati yangu na wewe, kuna mmoja MWEHU.
Ni vema ale mwaka mpya pia baada ya ex mass ili atusimulie kwa uzuri
well analyzed story. highfiveHabari wakuu, mie ni miongoni mwa tuliojaaliwa kumtembelea ndugu yetu Maxence Melo gereza la Keko. Nikiri sijawahi kufika gerezani ama kwa kushikwa ama kwenda kumtembelea mtu hivyo pamoja na kumuona Max nmejifunza hali ilivyo kwenye Magereza yetu japo sio kwa undani.
Nilifika wakanikagua na kisha nikaingia ndani, ukiingia na simu unaiacha kwa mlinzi ikiwa na ID. Ukifika unachukua namba na namba ilipofika nikaitwa ndani. Alietusindikiza akaishia mlangoni na ndani unasema jina. Nilichokiona pale chini watu wa magereza wanawajua sana watu wao na ni marafiki(Sijui watu wasipokuwepo).
Nilivyotaja jina, yule jamaa wa magereza akasema 'Huyu mtu kavunja rekodi leo' hivyo hongera kwetu sote tulioenda kisha akamuita mtu akanisindikiza juu na kuitiwa Maxence. Nilifika kwa Maxence nikamsalimu na kwa ujumla alikuwa na bashasha. Akasema anategemea kutoka lakini hata asipotoka kwa kuwa mambo yako sawa kwetu hata akilia sikukuu gerezani hewala.
Tukaongea mambo mawili matatu na miongoni mwa wachangiaji wa mawili matatu walikua watu wa magereza na nilienda na vitu kadhaa, akachukua kadhaa na vilivyobaki akasema nimpe jamaa aliempokea gerezani(Alikua sehemu ya chini) kwani yeye tayari ana vingi sana.
Wakati nasubiri kumuona Maxence nilipata nafasi ya kuongea na watu kadhaa ambao wameenda kuwaona na kuwapa chochote kitu ndugu zao, nilisikia hadithi kadhaa zilizopelekea watu kuwekwa ndani(Wote bado mahabusu). Najua ni stori za upande mmoja ila kuna watu wamekaa four good years bila hukumu, hebu fikiria kesi ikaisha halafu hana hatia!
Poleni kwa kuwachosha, ni mara yangu ya kwanza wakuu na nahisi washkaji wanaishi peace sana tofauti na tunavyosikia pia pongezi sana kwa askari wa magereza kama jinsi nilivyowaona leo ndio wako hivyo siku zote(Kuanzia mapokezi mpaka ndani).
NB: Gerezani sio kuzuri na anaenda yeyote, mahakama ziongezewe uwezo wa kusikiliza kesi ili wasiohusika waondoke, kumuweka mtu miaka minne bila hukumu kwangu ni zaidi ya hukumu kwani hasira ya mtu kunisingizia na kunisababishia maumivu naijua mwenyewe.
[HASHTAG]#Kesho[/HASHTAG] ntakuwa mahakamani