Naona CCM hiko kwenye matatizo makubwa , kama kile kilichoandikwa hapo juu ni cha kweli. Na inaonyesha dhahiri ya kuwa CCM ina tatizo kubwa la uongozi kwani message wanazotoa viongozi wa nafasi za juu zinapingana. Hili sio jambo zuri kwa chama ambacho kinataka kuendelea kuongoza. Wapinzani nafasi mliyokuwa mkiiomba, sasa mmeipata.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba JK amekaa kimya kabisa na hasemi chochote. Kitendo cha kukubali kuunga kamati ndogo ni kutaka kukwepa kufanya maamuzi mazito ambayo ni kazi ya kiongozi wa juu.
Jana Makamba anasema mafisadi wabebeshwe mizigo yao na siyo kukibebesha chama. Sasa kama NEC yote inatetea mafisadi na CC yote inatetea mafisadi kwanini tusikibebeshe chama sifa ya ufisadi. Kama chama kinataka kujipambanua na mafisadi, kinatakiwa kuchukua hatua ya ama kuwafukuza mafisadi ama kuwaunga mkono wabunge wote wanaopinga ufisadi kwa nguvu zote.
CCM itashindwa kusimama kwenye majukwaa ikifika 2010 kama itakuwa bado inaendelea kuwakumbatia mafisadi, mbaya zaidi timing ya hili tukio ni mbaya sana, angalau ingekuwa ni miaka 2 kabla ya uchaguzi wadanganyika wengi wangesahau, lakini wakisema wamtose Sitta mwezi Novemba, basi watakuwa wanajiweka mahali pabaya zaidi na itawawia ugumu kujitetea.
The bottom line ni kwamba uongozi wote wa juu wa CCM ni ama mafisadi au umewekwa na mafisadi ili kulinda maslahi ya mafisadi. Kwa mwendo huo CCM haiwezi kujipambanua na ufisadi. Njia pekee kuwatosa hao jamaa ama wawabebe lakini wa-risk kupoteza majimbo mengi.
Ngoja tusubiri Mzee Mwinyi na Kamati yake ndogo watakuja na kipi kipya na pia kikao cha Bunge cha Novemba kitatoa mwelekeo.