Safari ya Spika Sitta Urambo baada ya NEC August 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya Spika Sitta Urambo baada ya NEC August 2009

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zyansiku, Aug 20, 2009.

 1. Z

  Zyansiku Member

  #1
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika kile kinachoonekana kutofautiana na maamuzi ya NEC, baadhi ya wapambe wa Mh SS wanaoshi katika jimbo la Urambo wanafanya maandalizi makubwa ya kumpokea Mh SS kwa maandamano makubwa ikiwa ni pamoja na kukodi piki piki zote za kibiashara katika mji wa urambo, aidha mapokezi hayo ya aina yake yatafanyika katika kijiji cha Ndorobo nje kidogo ya mji wa Urambo na kwa kiasi kikubwa maandalizi yote yamekamilika chini ya uongozi wa Bwana Welly aliyekuwa katibu uchumi na fedha wilaya ya urambo na Katibu mhamasishaji wa vijana mkoa wa Tabora kwa mwaka 2003-2004.

  Wakati huo huo taarifa nilizopata muda si mrefu kutoka kwa wadau wa siasa wa mji wa Tabora

  Ni kwamba maandalizi kama hayo pioa yanafanyika Tabora mjini chini ya katibu wa siasa na uenezi wa CCM wa Tabora mjini bwana Rashid Ramadhani Tall. kila la kheri Spika tunakusubiri kwa hamu Tabora na mapokezi ya nguvu!
   
  Last edited by a moderator: Aug 22, 2009
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  tehe tehe tehe mitanzania bana.......sijui niipe jina gani.....
   
 3. B

  Bwassa Member

  #3
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Jamani,

  Mzee huyu wa Urambo anapokelewa kwa shangwe, kwa kitu gani hasa? Huyu si ametuhumiwa waziwazi ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama chake cha CCM kuwa, kwa vitendo vyake, anakisaliti chama hicho na akanusurika kung'olewa baada ya kuomba radhi? Sasa ndiyo anazidi kujichimbia kaburi la kisiasa. Si aliwahi kushindwa huyu Urambo mwaka 1995? Sasa, tangu 2005, amekuwa akijaribu kujijenga upya kisiasa, kuchukua ajenda ya "Ufisadi" imsaidie (kwa kushirikiana na timu yake ya Wabunge, wenye gele na usongo na UWAZIRI, inayoitwa "First Eleven": akina Dk. Mwakyembe, Ole Sendeka, Lucas Selelii, Anne Kilango,Stella Manyanya, Betrice Shelukindo n.k. anaowapangilia Bungeni). Lakini kumbe, kwa vile zote hizo ni hila, sasa ameshitukiwa na Chama chake. Hii kwamba anapokewa kwa shangwe ni propaganda tu za kujaribu kumvika nguo!

  LAKINI, kama nilivyowahi kueleza hapo awali, mahali pengine humu katika JF, tatizo la mzee huyu la fitina na usaliti wa kisiasa, halikuanza leo! Katika miaka ya mwanzoni ya 1990, akiwa Waziri wa Sheria (na baadaye akaondolewa, baada ya kushindwa Ubunge wa Urambo), alishiriki "kiujanjaujanja" katika hoja ya kutaka kuleta Serikali ya Tanganyika katika mfumo wa Muungano, ili uwe wa Serikali Tatu badala ya Mbili.
  Katika kitabu chake, UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA. Uk. wa 20 hadi Uk. 27, Mwalimu Nyerere alimsema vibaya sana Sitta, kwa kupeleka mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM, Dodoma, "TAARIFA YA SERIKALI JUU YA AZIMIO LA BUNGE KUHUSU HAJA YA KUUNDA SERIKALI YA TANGANYIKA NDANI YA MUUNDO WA MUUNGANO". Mwalimu Nyerere alisema, kuhusu taarifa hiyo, katika kijitabu hicho: "Taarifa yenyewe ni ndefu, maana ina maelezo mengi ya mapambo tu, au ya kiinimacho(Uk. 20)...Baadaye, baada ya kikao, nilimtafuta Ndugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki (Uk. 27)...". Huyo ndiyo Spika Sitta, mbele ya macho na fikra za Mwalimu Nyerere! Hivi ni mpiganaji kweli wa vita dhidi ya "Ufisadi", au ni msaliti tu wa Chama chake? Wana-CCM na msio wana-CCM na ni Watanzania tu wenye nia njema, pimeni!

  Bwassa
   
 4. l

  libidozy Member

  #4
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  6 hana lolote ni zezeta wa kisiasa tuuu,wacha aandamane aone kilichomtoa kanga manyoya!Injii hii bwana,achana nayo.
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,106
  Trophy Points: 280
  karibuni wabaya wa Sitta, hapa linapendwa Taifa siyo chama na kuchukiwa mafisadi. wote.
   
 6. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamaa yangu mmoja ananikumbusha kuwa aliyekubali kufa kwa ajili ya watu alikuwa yesu peke sijui kama sita ataweza kuvaa viatu vya yesu, any way lets wait and see!
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nazidi kushangaaa.......hapa cha kufurahia ni nini sasa? Huyo six, maandamano au ufujaji wa pesa kwa kukodi mapikipiki ambapo zingeweza kutumika kwa masuala mengine ya maendeleo ya wananchi? Embu tuamke wa TZ siyo kushabikia kila jambo.........
   
 8. nkawa

  nkawa Senior Member

  #8
  Aug 20, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani acheni wivu, c wananchi wake wa Urambo wanamwamini bado? Mbona bwana Chenge nae alipokelewa kwa mbwembwe kipindi kileeee.......
   
 9. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sitaa badoo anatapatapaa..amue mojaa..uspikaa sio mama yake, ccm sio mama yakee..
   
 10. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2009
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyu Bwana Welly naona anataka kujipalia mkaa. Kuna wakati yeye na Brother wake waliwahi kutishwa kuwa sio raia baada ya kutoonyesha mapenzi mema kwa sisiemu. Kwa vile ameamua kusigana na NECK ambayo inabeba HEAD(Fisadis) ya sisiemu basi awe tayari kwa Mapambano from RA et al.
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Mkuu nakitafuta hicho kitabu kwa udi na uvumba!!! Unaweza kunipatia mkuu???
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Oh My Gosh!!!

  Mzee sitta, kama unasoma humu jamvini... achana kabisa na huo upuzi wa maandamano!!!! fanya kazi yako na usiendeleze huu ujinga wa kupokelewa kwa vifijo wakati kazi bado ngumu.

  Tumeshaona ya CHENGE, LOWASA sasa naona na wewe unaingia chunguni

  WAKATI UMEFIKA TU-ADDRESS DEVELOPMENT ISSUES NA KUACHA WAFU WAZIKE WAFU WAO
   
 13. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2009
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sio wananchi wote wana mwamini. Nenda pale Kalemela na Ussoke sehemu ambazo zilikuwa moja ya ngome zake utapata habari kamili. Magazeti yamefanikiwa kwa kiasi fulani kumchafua. Hasa issue ya Kodi ya nyumba na kupenda vimwana(japo hili ni personal).
   
 14. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Saaaaafi sana! Na wale vibaraka wa mafisadi mliotumwa kmpiga vita Mh. Sitta karibuni uwanjani mmwage sumu zenu, hazisaidii. Wanananchi wameamua. Si afadhali kumpokea Sitta kwa vifijo kuliko yale ya Fisadi Chenge??? Nitacheka pale atajitokeza kibaraka wa mafisadi hapa na kusema hastahili mapokezi!!!! Kwani yale ya Chenge alistahili??? Sitta amefanya kazi, je Chenge alifanya nini?? Ningeweza ningeshiriki kabisan ili kumuunga mkono shujaa pekee katika historia ya maspika wa bunge letu ambao aliruhusu demokrasia ya mawazo Bungeni. Bunge ni chombo cha Wananchi!! Si mali ya NEC!!!
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Bila shaka atapata muda wa kuyahutubia maandamano hayo. Atasema alichoambiwa kwenye vikao hivi "vizito" vya chama chake na huenda akaenda mbali zaidi ya hapo.....
   
 16. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2009
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni kweli ni vizuri CREDIT iende pale inapostahili. Lakini wasiwasi wangu ni juu ya organizer wa mapokezi bwana Welly, sidhani kama ana ujasiri wa kusimama akitishwa kidogo tu. Manake historia ya huko nyuma inamhukumu. Yalifaa yaandaliwe na mtu mwenye wasifu uliojengeka ndani ya jamii lakini sio huyu ambaye wasifu wake unamfanya kuwa mwepesi kwenye jamii.
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mugo sina habari za huyu Welly, ila kama si nzuri katika jamii, naomba mtu wa karibu na spika au kamati ya maandalizi wafanye mabadiliko haraka sana. Anatakiwa mtu credible kwa jamii ajitose kuyaandaa. Asante mkuu kwa hint na kama nilivyosema walioko humu wawasiliane haraka na waandaaji warekebishe. Pia dondosha kidogo ya Welly hapa ili isije ikawa atatuchafulia hali ya hewa hasa ukizingangatia kampeni za 2010 zimeshaanza.
   
 19. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ni upuuzi mtupu...
   
 20. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ama kweli mafisadi wako kila mahali. Hata kwenye JF kibao.Tanzania kazi tunayo. sasa nyinyi mnaomshambulia spika mnatofauti na waliokuwa ndani ya NEC? Kuna msemo wengi wape lakini kwa hili mmegonga mwamba. Hata zito alimshambulia karamagi ,akasimamishwa lakini baadaye mnajua kilichomkuta mwana Kara..kwenye Richmond .hakuna tofauti.
   
Loading...