Mbunge Kainja na Wanawake wa UWT Wilaya ya Urambo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew leo tarehe 14 Julai, 2023 ameendelea na zoezi la Ugawaji wa fedha za miradi ambapo amefanikiwa kukutana na kuwakabidhi Wajumbe Wote wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka Kata 18 zilizopo Wilayani Urambo.​

Tukio la kukabidhi fedha kwa wanawake wa UWT liliambatana na Baraza la UWT lililofanyika Wilaya ya Urambo lilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo, Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Mbunge wa Jimbo la Urambo.

Aidha, Mbunge Mhe. Kainja alizungumza na kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani lakini vilevile alijikita sana kuwaelimisha wanawake wa UWT Urambo jinsi ya kuwa na nidhamu ya pesa ili waweze kukuza mitaji yao midogo.

Katika ziara yake, Mbunge Mhe. Kainja alifika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Kenani Kihongozi na kusaini kitabu cha wageni huku Mkuu wa Wilaya ya Urambo akiambatana na Mbunge katika Baraza la UWT.

WhatsApp Image 2023-07-14 at 18.16.05.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-14 at 17.48.51(17).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-14 at 17.48.51(16).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-14 at 17.48.51(15).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-14 at 17.48.51(9).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-14 at 17.48.51(11).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom