SoC01 Safari ya miaka 7 katika uraibu wa filamu za ngono

Stories of Change - 2021 Competition

longi mapexa

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
3,197
3,994
Habari Natumaini upo na Uzima.

Basi tumshukuru Mungu kwa hilo. Lakini kama Pia haupo sawa amini kwamba wakati wako Utafika tu.

Bila kupoteza wakati acha nikushirikishe mkasa huu ulionipata na namna nilifanikiwa kujitoa Katika Uraibu wa Machapisho, Picha na Video za Ngono kwa Miaka 7.

Nikiwa na umri mdogo tu wa kati ya 14 au 15 nilijikuta kwa mara ya kwanza natazama picha ya mwanamke akiwa Uchi kabisa. Hii ni baada kupekua simu ya Kaka yangu aliyokuwa kaiweka katika chaji japo Akili yangu ilibadilika nikapatwa na mshangao uliochanganyikana na uwoga kwa haraka nilirudisha simu kisha nikaendelea na mambo mengine.

Ajabu ni kuwa picha ile ilizidi kujirudia kichwani mwangu zaidi na zaidi. Hali hii ilinipelekea kutamani kuziona tena.
Wakati mwingine ulipofika nikajaribu bahati yangu Na kwa hakika nilifanikiwa. Tofauti na wakati uliopita, sikutazama moja tu bali nilikutana na nyingine nyingi sana. Huu ukawa mwanzo wa mimi kupenda picha za wanawake walio uchi kila wakati nikipata nafasi nikawa nazitazama.

Miezi michache mbele nilifanikiwa kumiliki simu najua utashanga. Sikununua nilipewa palepale nyumbani nadiriki kusema kwamba kwa hili familia ilikosea sana. Japo Simu haikua simu janja ila ilikuwa na sehemu ya Intaneti nafkiri kasi ya mtandao ilikuwa ni 2G Hapa nilianza kutumia Google kusearch maneno yoyote yenye kuashiria habari za ngono.

Nayo Google ikanipatia kila nililolitafuta Ikiwa ni pamoja na Simulizi za ngono, Picha na sasa nikaanza hata kupakua video japo ilichukuwa muda mrefu kulingana na kasi ya mtandao.

Wakati wa usiku ndio niliutumia kwani hakukuwa na yeyote wakunishika wala kuniona. Sikupenda usingizi tena nilipenda kutazama ngono kila wakati.

Hii ilifanya wakati mwingine hata mama kukaribia kunikamata. Nakumbuka Mama yangu aliwahi kukuta picha niliyochora kwa penseli japo picha ile ilikuwa ni Ya Ngono kwa asilimia zote. Nilizikana sana ila nafahamu mama alijua tu mwanae nshaharibikiwa.

Shuleni matokeo yakaanza kuporomoka. Nilazima ingekuwa hivyo kwani usiku wote nilikesha mitandaoni. Wakati wa kuamka mimi ndo naanza kulala.

Najivunia kwamba Nikipindi hicho hicho ndicho ambacho nilibahatika kujiunga pia na JamiiForums.

Nilifanya mtihani wa kidato cha nne kinyume na matarajio ya familia nilifanya vibaya sana japo nilifanikiwa pia kwenda kidato cha tano. Lakini nililaumiwa sana kwa kufanya uzembe nilifahamu wapi chanzo cha tatizo lilipo hivyo nilijiapiza kubadilika.

Maisha ya High school Yalinisaidia kupunguza uraibu kwani sikuweza tena kupata simu... Tatizo ni kwamba zile picha nilizozitazama bado zilikuwa zimehifadhiwa kichwani zikijirudia hata kwa njia ya ndoto.

Mfumo wa maisha yangu Ya uraibu ulikuwa ukiendelea pindi napokuwa likizo kwa kuhakikisha kuwa nakata kiu ya uteja wangu.

Miaka ikasogea nikamaliza Kidato cha sita Namshkuru Mungu matokeo yalikuwa mazuri hii ikafanya hata nyumbani wanipumzishe kunisemaa.

Nilipata nafasi ya kujiunga na chuo fulani maarufu hapa Dar es Salaam kwa Kozi ya miaka mitatu. Nikamiliki simu janja Yenye kasi ya 4G Hapa nilibadilika nakujikita rasmi kwenye Uraibu nikawa Porn hunter natazama napakua nahifadhi hata nikaamua kujiunga kwenye porn sites mbalimbali Nilifahamu Porn Stars wengi Hata wakitumika kwenye Memes ilikua rahisi kwangu kuwafahamu.

Sio Tanzania tu bali duniani Kote.
Nilianza kuchagua mpaka aina ya video hatari kubwa ni kuwa kila siku nilikesha kutafuta video za kusisimua zaidi kwani ilifika hatua nikawa sisisimuki kwa baadhi ya video. Mpaka muda huo sikuwa nimewahi kushiriki tendo lenyewe kwa uhalisia.

Maisha ya uhuru chuoni nilijikuta katika uhusiano na binti fulani. Lakini kwa bahati mbaya haukudumu. Sikuwa na tabia za kupendeza nilitaka kuishi na binti yule kama Pornstars wafanyavyo katika videos nilichojali ni ngono hakuna mazungumzo hakuna kubembeleza nilichotaka ni kufanya ngono kadri muda unavyoruhusu Hostel Chuo Barabarani popote kila nikimtazama naona ngono tu. Maskini binti yule hakuyaweza hayo.

Sikujali sana kuhusu mahusiano kwani wapenzi wangu wako kwenye simu nawaona mda wowote nikiwahitaji na wanafanya kile nachotegemea kuona wakifanya. Sikufahamu kwamba nimepoteza Ufahamu wa kawaida.

Miezi ikazidi kusonga lakini tofauti na vijana wengine mimi sikuwa natesekea mahusiano, Sikupenda habari za mapenzi nilikuwa bingwa wa majibu machafu. Kwanini nikasumbuane na wasichana ambao hawafanani na wanawake waliopo kwatika simu yangu.

Kiukweli sikuwa na heshima kwa wadada niliwafokea sikutaka wanizoee wengine niliwaona kabisa wakiumia lakini ningefanyaje?

Kuna wakati Ndani yangu nilihisi nina hatia. Ukweli sikuwa najiamini hivyo nilifanya yote hayo kukinga ukosoaji ni vipi wakigundua tabia yangu ya sirini?

Kila nikiwa kanisani mahubiri yalinichoma. Ajabu wakati wote baada ya kutazama videos nilijiapiza kutokuziangalia tena nikaweka mpaka nadhiri mbele za Bwana Nikaandika tarehe na kuzisaini kabisa kwa vitabu nikajaribu mpaka kufunga na maombi lakini wapi. Niliishia kuteleza na kurudia uteja wangu tena kwa kasi zaidi Kwanini?

Kwa sababu Video na picha za ngono ni tofauti na vilevi ama madwa ya kulevya ambavyo vinahitaji Fedha pia Upatkanaji wake ni mgumu pamoja na Usiri. Ukilewa kila mtu atafahamu. Ila kwa upande wa Porn materials unazipata kwa urahisi bila mtu kufahamu tena kwa uhakika kabisaa. Mtandao unaweza kuwa chini lakini kwenye Pornsites unaperuzi bila shida kabisa.

Namshukuru Mungu mimi ninapenda kujisomea vitabu kupitia hapa nilianza kusoma namna ya kujikwamua kwani Hatia ilinizidia. Njia nilizozipata kupitia vitabu nilianza kuzitumia japo kila wakati nilianguka, Sikukata tamaa kwani niliona nikiwa napunguza kasi ya kutazama mitandao hiyo.

Baada ya muda niliingia katika uhusiano mwingine sijui ilikuaje lakini moyo ulikuwa dhaifu kwa binti yule nilimpenda. Muda mwingi nikatumia kumuona kama malaika wakuniondoa katika janga lile aliweza vumilia ujinga wangu wote hata nikaona napaswa kubadilika.

Ni kweli nilijikuta napunguza muda wa kupita kwenye Porn webs mpaka atleast mara moja kwa Wiki hapa ilikua ni kipindi ambacho yeye anakuwa hayupo na mimi.

Taratiibu nikawa na imarika nikiteleza basi inakuwa ni bahati mbaya tu umepita mtandaoni unakutana nazo(Hii mpaka sasa ni changamoto)

Nilimaliza Chuo lakini uhusiano ukiwa imara sana nampenda Sana binti huyu Siwafikirii tena Pornstars. Kwa sasa Nafikiria namna gani nitaokoa vijana wenzangu.

Ikiwezekana Siku moja nitoke hadharani nishuhudie ili walio dhaifu wapate nguvu kupitia mimi.

Kiukweli madhara ya machapisho Video na picha za ngono naziona mpaka sasa japo nimestaafu kabisa lakini picha zile bado zipo kichwani hata baadhi ya mambo nayoyapenda kitandani ni matokeo ya janga lile.

Kwa sasa nimejitengenezea mpango wa kusafisha mawazo yangu kama ikiwezekana nizisahau kabisa.

Nimalize kwa kusema Kuwa huru kutoka kwenye uraibu wa picha video na machapisho ya Ngono inawezekana.

Chukua hatua madhubuti kwani Ubongo wako ni muhimu sana kwa kuwa huo ndio unaokufanya uwe Wewe. Wewe ni matokeo ya ubongo wako.

Kuna msemo unasema " Kila mtu ana majitu makubwa mawili moja baya moja zuri na siku zote huwa yana pigana Je! wewe unadhani ni yupi atakayeshinda? Atakayeshinda ni yule unaye mlisha" Mungu akubariki!

Njia Nilizotumia.
♡ Nimekuwa nikitafuta maarifa zaidi kuhusu imani yangu na uhusiano na Mungu.
♡ Nimetoa kipaumbele sana kwenye mambo mengine nayopenda tofauti na kazi Kama kupiga Gitaa na Kuchora.
♡ Kwa namna yoyote nimekuwa nikikwepa kukaa mwenyewe kwa muda mrefu.
♡ Kila mara nina utaratibu wa kupitia mabandiko yanayohusu madhara ya Video picha na mabandiko ya ngono ( ukitaka kuua mbwa mpe jina baya ).
♡ Nimemshirikisha mwenza wangu changamoto hii hivyo amekuwa masaada kwangu.
♡ Nimetengeneza ratiba inayoeleweka isiyotoa nafasi ya kuingiza wazo la kutazama Porn sites
kila napofikiria kufanya hivyo nabadili haraka wazo hilo.
♡ Mwisho nilipakuwa App fulani inayofungia picha video ama tangazo lolote la ngono kunifikia.
♡ Simu siweki password ama pattern yeyote akiingia kwa simu yuko huru hii inakuwa kama ulinzi kwamba ukikutwa na porn video ni aibu na sipo tayari kuaibika.

Kila la Kheri.
 
Ni uraibu mbaya kwa kweli, wenzetu wametutengeneza na sisi tukatengenezeka haswaaa hata huku mitaani hali n mbaya kwasababu ya hizi video zmechangia kwa kiasi Fulani na wengi wa watu tz ni wajinga Sasa kutoka huko inawawia vigumu sana,tuwe viongozi wa familia,ndugu,jamaa na marafiki ktk kupambana na huu uraibu kwani wengi wanaumia...
 
Kama litazungumzwa hadharani pengine itasaidia kupunguza. Tofauti na sasa ambapo imekuwa siri yenye aibu ndani yake.
 
The easiest way kuachana na hayo mambo na mengine yote yanayohusiana nayo ni kuhamia rohoni, shika neno, kama ni mkristu soma biblia, kadri utakavyozidi kumkaribisha roho wa Mungu ndani yako ndivyo atakavyomuondoa shetani anayeishi ndani yako anayekufanya upende mambo yake.

Siku zote mambo ya mwilini hayamalizwi na mwili, mambo ya mwilini humalizwa kwa kuhamia rohoni, kwani ukiendekeza hiyo tabia mwisho wa dhambi ni mauti, kupenda ngono kutakufanya utake kutembea na mwanamke/ume wa kila aina mwishowe magonjwa yatakupata ufe.
 
TUBU narudia tena TUBU leo leo kakaangu kesho ni majaaliwa ya Muumbaji tu mimi Namuomba Mungu akufanyie wepesi usiyarudie tena matapishi yako.
Kutubu peke yake hakutoshi, atatubu lakini aendelee na hiyo tabia, kuna maandiko kwenye biblia yanasema "roho I radhi, bali mwili ni dhaifu", hapa hata akitubu bado uwezekano wa kurudia ni dhambi ni mkubwa.

Muhimu aanze taratibu kuacha kuangalia hayo mambo kwenye simu, n.k huku akisoma biblia kila siku, akijenga hiyo tabia taratibu ataanza kuipenda biblia zaidi ya vyote, ajitahidi kika siku asome hata page moja ya kitabu chochote, baada ya hapo atembee huku akitafakari kile alichosoma.

Mambo kama kufanya mazoezi hayaondoi hiyo hali moja kwa moja, ukishafanya zoezi mwili utachoka na kutotaka hayo mambo, lakini utakaporudia kwenye hali yako ya kawaida utaanza kuyakumbuka tena, mambo ya mwilini yanamalizwa kwa kuhamia rohoni, sio na mambo ya mwilini tena( mazoezi).
 
Kutubu peke yake hakutoshi, atat toubu lakini aendelee na hiyo tabia, kuna maandiko kwenye biblia yanasema roho I radhi, bali mwili ni dhaifu, hapa hata akitubu bado uwezekano wa kurudia ni dhambi ni mkubwa.

Muhimu aanze taratibu kuacha kuangalia hayo mambo kwenye simu, n.k huku akisoma biblia kila siku, akijenga hiyo tabia taratibu ataanza kuipenda biblia zaidi ya vyote, ajitahidi kika siku asome hata page moja ya kitabu chochote, baada ya hapo atembee huku akitafakari kile alichosoma.

Mambo kama kufanya mazoezi hayaondoi hiyo hali moja kwa moja, ukishafanya zoezi mwili utachoka na kutotaka hayo mambo, lakini utakaporudia kwenye hali yako ya kawaida utaanza kuyakumbuka tena, mambo ya mwilini yanamalizwa kwa kuhamia rohoni, sio na mambo ya mwilini tena( mazoezi).
Umesoma Uzi wote?

Mimi nimemuambia afanye Toba kwasababu Yawezekana hajawai kutubu kwa kitendo cha kujichua.

Wewe unakuja kumuelekeza mbinu za kuacha na kukosoa mikakati yake na wakati kaandika kaacha, ni wazi umekurupuka kunijibu (NAFAHAMU HILI nilishakutambua rohoni mpendwa, Karibu), na pia si ajabu wewe na mwandishi ni Mudi na Mwamedi (majina tofauti mtu yuleyule).

Nisamehe Kama nimekukwaza, leo intelejensia ya kiroho ipo kwa kiwango kikubwa Sana.. nisamehe pia kama nimekujibu vibaya.

Asante
 
Hili jukwaa lipo kwa ajili ya mafundisho, lugha niliyoitumia hapo inawahusu wengine wenye tabia kama zake ambao bado hawajaacha (ujue kujiongeza), na mojawapo ya sababu wanazotumia kama kinga ni kufanya mazoezi ambazo nimemwambia yeye alieandika na wengine wanaoamini hilo mazoezi pekee hayatoshi, muhimu ajielekeze kiroho zaidi.

Nimekujibu kwasababu hujatoa jibu kamili, kutubu/ toba ni maandalizi, yeyote kabla hajatubu lazima aseme na roho yake, awe tayari kutubu na aache moja kwa moja.

Kumwambia mtu atubu wakati haijui kesho yake ni kukurupuka, tena asieijua hata maana ya kutubu kama mleta mada ni kukurupuka zaidi, narudia tena; "roho I radhi mwili u dhaifu" (hili unalijua ndio maana umemuombea asirudie), nakuwekea maandiko ya biblia uelewe vizuri.

Amekuuliza toba ni nini hujamjibu (comment # 7), kumbe hata kutubu hakujui wewe umemuandikia tu atubu, hapo sijui kati yangu mimi na wewe nani amekurupuka, jibu unalo.

Habari ya mudi na mwamedi sijakuelewa, ila kama huyo roho wako ndie kakuelekeza hongera, siku hizi kila mtu anajidai na "roho wake" kwani wale wenye roho wa kweli huwa hawajisifu, Yesu Kristo amekataza hilo.
 
Hili jukwaa lipo kwa ajili ya mafundisho, lugha niliyoitumia hapo inawahusu wengine wenye tabia kama zake ambao bado hawajaacha (ujue kujiongeza), na mojawapo ya sababu wanazotumia kama kinga ni kufanya mazoezi ambazo nimemwambia yeye alieandika na wengine wanaoamini hilo mazoezi pekee hayatoshi, muhimu ajielekeze kiroho zaidi.

Nimekujibu kwasababu hujatoa jibu kamili, kutubu/ toba ni maandalizi, yeyote kabla hajatubu lazima aseme na roho yake, awe tayari kutubu na aache moja kwa moja.

Kumwambia mtu atubu wakati haijui kesho yake ni kukurupuka, tena asieijua hata maana ya kutubu ni kukurupuka zaidi, narudia tena; "roho I radhi mwili u dhaifu" (hili unalijua ndio maana umemuombea asirudie), nakuwekea maandiko ya biblia uelewe vizuri.

Amekuuliza toba ni nini hujamjibu (comment # 7), kumbe hata kutubu hakujui wewe umemuandikia tu atubu, hapo sijui kati yangu mimi na wewe nani amekurupuka, jibu unalo.

Habari ya mudi na mwamedi sijakuelewa, ila kama huyo roho wako ndie kakuelekeza hongera, siku hizi kila mtu anajidai na "roho wake" kwani wale wenye roho wa kweli huwa hawajisifu, Yesu Kristo amekataza hilo.
Hahahaha, hizi kurupuka kurupuuu zitawavunja magoti nyie akina anko JeiJei.. Leo intelejensia ya kiroho imetamalaki Sana ndani yangu na ndio maana nikakuomba na msamaha, lakini kwasababu unataka basi tutajifunza kwa faida ya wengi.

Haya nieleze huo mstari wa Yesu kukataza
 
Hope umeelewa nilichoandika ndio maana hujauliza juu ya maelezo yangu kwako yaliyohusu mada husika, habari ya msamaha wako kwangu kama ulidhani sitakuelewesha zaidi ili uelewe vizuri pole, am much more wider in context than you.

Unachotaka kuhusu mstari fungulia thread yake tusiharibu mantiki ya huu uzi, halafu huyo roho wako anaonekana anapenda taarabu!. Mtumaini Mungu vyema uache mipasho, sio kubeba jina tu.

Hav a gud evening.
 
Back
Top Bottom