SoC01 Safari ya miaka 7 katika uraibu wa filamu za ngono

Stories of Change - 2021 Competition

longi mapexa

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
3,197
3,994
Habari Natumaini upo na Uzima.

Basi tumshukuru Mungu kwa hilo. Lakini kama Pia haupo sawa amini kwamba wakati wako Utafika tu.

Bila kupoteza wakati acha nikushirikishe mkasa huu ulionipata na namna nilifanikiwa kujitoa Katika Uraibu wa Machapisho, Picha na Video za Ngono kwa Miaka 7.

Nikiwa na umri mdogo tu wa kati ya 14 au 15 nilijikuta kwa mara ya kwanza natazama picha ya mwanamke akiwa Uchi kabisa. Hii ni baada kupekua simu ya Kaka yangu aliyokuwa kaiweka katika chaji japo Akili yangu ilibadilika nikapatwa na mshangao uliochanganyikana na uwoga kwa haraka nilirudisha simu kisha nikaendelea na mambo mengine.

Ajabu ni kuwa picha ile ilizidi kujirudia kichwani mwangu zaidi na zaidi. Hali hii ilinipelekea kutamani kuziona tena.
Wakati mwingine ulipofika nikajaribu bahati yangu Na kwa hakika nilifanikiwa. Tofauti na wakati uliopita, sikutazama moja tu bali nilikutana na nyingine nyingi sana. Huu ukawa mwanzo wa mimi kupenda picha za wanawake walio uchi kila wakati nikipata nafasi nikawa nazitazama.


Miezi michache mbele nilifanikiwa kumiliki simu najua utashanga. Sikununua nilipewa palepale nyumbani nadiriki kusema kwamba kwa hili familia ilikosea sana. Japo Simu haikua simu janja ila ilikuwa na sehemu ya Intaneti nafkiri kasi ya mtandao ilikuwa ni 2G Hapa nilianza kutumia Google kusearch maneno yoyote yenye kuashiria habari za ngono.

Nayo Google ikanipatia kila nililolitafuta Ikiwa ni pamoja na Simulizi za ngono, Picha na sasa nikaanza hata kupakua video japo ilichukuwa muda mrefu kulingana na kasi ya mtandao.

Wakati wa usiku ndio niliutumia kwani hakukuwa na yeyote wakunishika wala kuniona. Sikupenda usingizi tena nilipenda kutazama ngono kila wakati.

Hii ilifanya wakati mwingine hata mama kukaribia kunikamata. Nakumbuka Mama yangu aliwahi kukuta picha niliyochora kwa penseli japo picha ile ilikuwa ni Ya Ngono kwa asilimia zote. Nilizikana sana ila nafahamu mama alijua tu mwanae nshaharibikiwa.

Shuleni matokeo yakaanza kuporomoka. Nilazima ingekuwa hivyo kwani usiku wote nilikesha mitandaoni. Wakati wa kuamka mimi ndo naanza kulala.

Najivunia kwamba Nikipindi hicho hicho ndicho ambacho nilibahatika kujiunga pia na JamiiForums.

Nilifanya mtihani wa kidato cha nne kinyume na matarajio ya familia nilifanya vibaya sana japo nilifanikiwa pia kwenda kidato cha tano. Lakini nililaumiwa sana kwa kufanya uzembe nilifahamu wapi chanzo cha tatizo lilipo hivyo nilijiapiza kubadilika.

Maisha ya High school Yalinisaidia kupunguza uraibu kwani sikuweza tena kupata simu... Tatizo ni kwamba zile picha nilizozitazama bado zilikuwa zimehifadhiwa kichwani zikijirudia hata kwa njia ya ndoto.

Mfumo wa maisha yangu Ya uraibu ulikuwa ukiendelea pindi napokuwa likizo kwa kuhakikisha kuwa nakata kiu ya uteja wangu.

Miaka ikasogea nikamaliza Kidato cha sita Namshkuru Mungu matokeo yalikuwa mazuri hii ikafanya hata nyumbani wanipumzishe kunisemaa.

Nilipata nafasi ya kujiunga na chuo fulani maarufu hapa Dar es Salaam kwa Kozi ya miaka mitatu. Nikamiliki simu janja Yenye kasi ya 4G Hapa nilibadilika nakujikita rasmi kwenye Uraibu nikawa Porn hunter natazama napakua nahifadhi hata nikaamua kujiunga kwenye porn sites mbalimbali Nilifahamu Porn Stars wengi Hata wakitumika kwenye Memes ilikua rahisi kwangu kuwafahamu.

Sio Tanzania tu bali duniani Kote.
Nilianza kuchagua mpaka aina ya video hatari kubwa ni kuwa kila siku nilikesha kutafuta video za kusisimua zaidi kwani ilifika hatua nikawa sisisimuki kwa baadhi ya video. Mpaka muda huo sikuwa nimewahi kushiriki tendo lenyewe kwa uhalisia.

Maisha ya uhuru chuoni nilijikuta katika uhusiano na binti fulani. Lakini kwa bahati mbaya haukudumu. Sikuwa na tabia za kupendeza nilitaka kuishi na binti yule kama Pornstars wafanyavyo katika videos nilichojali ni ngono hakuna mazungumzo hakuna kubembeleza nilichotaka ni kufanya ngono kadri muda unavyoruhusu Hostel Chuo Barabarani popote kila nikimtazama naona ngono tu. Maskini binti yule hakuyaweza hayo.

Sikujali sana kuhusu mahusiano kwani wapenzi wangu wako kwenye simu nawaona mda wowote nikiwahitaji na wanafanya kile nachotegemea kuona wakifanya. Sikufahamu kwamba nimepoteza Ufahamu wa kawaida.

Miezi ikazidi kusonga lakini tofauti na vijana wengine mimi sikuwa natesekea mahusiano, Sikupenda habari za mapenzi nilikuwa bingwa wa majibu machafu. Kwanini nikasumbuane na wasichana ambao hawafanani na wanawake waliopo kwatika simu yangu.

Kiukweli sikuwa na heshima kwa wadada niliwafokea sikutaka wanizoee wengine niliwaona kabisa wakiumia lakini ningefanyaje?

Kuna wakati Ndani yangu nilihisi nina hatia. Ukweli sikuwa najiamini hivyo nilifanya yote hayo kukinga ukosoaji ni vipi wakigundua tabia yangu ya sirini?

Kila nikiwa kanisani mahubiri yalinichoma. Ajabu wakati wote baada ya kutazama videos nilijiapiza kutokuziangalia tena nikaweka mpaka nadhiri mbele za Bwana Nikaandika tarehe na kuzisaini kabisa kwa vitabu nikajaribu mpaka kufunga na maombi lakini wapi. Niliishia kuteleza na kurudia uteja wangu tena kwa kasi zaidi Kwanini?

Kwa sababu Video na picha za ngono ni tofauti na vilevi ama madwa ya kulevya ambavyo vinahitaji Fedha pia Upatkanaji wake ni mgumu pamoja na Usiri. Ukilewa kila mtu atafahamu. Ila kwa upande wa Porn materials unazipata kwa urahisi bila mtu kufahamu tena kwa uhakika kabisaa. Mtandao unaweza kuwa chini lakini kwenye Pornsites unaperuzi bila shida kabisa.

Namshukuru Mungu mimi ninapenda kujisomea vitabu kupitia hapa nilianza kusoma namna ya kujikwamua kwani Hatia ilinizidia. Njia nilizozipata kupitia vitabu nilianza kuzitumia japo kila wakati nilianguka, Sikukata tamaa kwani niliona nikiwa napunguza kasi ya kutazama mitandao hiyo.

Baada ya muda niliingia katika uhusiano mwingine sijui ilikuaje lakini moyo ulikuwa dhaifu kwa binti yule nilimpenda. Muda mwingi nikatumia kumuona kama malaika wakuniondoa katika janga lile aliweza vumilia ujinga wangu wote hata nikaona napaswa kubadilika.

Ni kweli nilijikuta napunguza muda wa kupita kwenye Porn webs mpaka atleast mara moja kwa Wiki hapa ilikua ni kipindi ambacho yeye anakuwa hayupo na mimi.

Taratiibu nikawa na imarika nikiteleza basi inakuwa ni bahati mbaya tu umepita mtandaoni unakutana nazo(Hii mpaka sasa ni changamoto)

Nilimaliza Chuo lakini uhusiano ukiwa imara sana nampenda Sana binti huyu Siwafikirii tena Pornstars. Kwa sasa Nafikiria namna gani nitaokoa vijana wenzangu.

Ikiwezekana Siku moja nitoke hadharani nishuhudie ili walio dhaifu wapate nguvu kupitia mimi.

Kiukweli madhara ya machapisho Video na picha za ngono naziona mpaka sasa japo nimestaafu kabisa lakini picha zile bado zipo kichwani hata baadhi ya mambo nayoyapenda kitandani ni matokeo ya janga lile.

Kwa sasa nimejitengenezea mpango wa kusafisha mawazo yangu kama ikiwezekana nizisahau kabisa.

Nimalize kwa kusema Kuwa huru kutoka kwenye uraibu wa picha video na machapisho ya Ngono inawezekana.

Chukua hatua madhubuti kwani Ubongo wako ni muhimu sana kwa kuwa huo ndio unaokufanya uwe Wewe. Wewe ni matokeo ya ubongo wako.

Kuna msemo unasema " Kila mtu ana majitu makubwa mawili moja baya moja zuri na siku zote huwa yana pigana Je! wewe unadhani ni yupi atakayeshinda? Atakayeshinda ni yule unaye mlisha" Mungu akubariki!

Njia Nilizotumia.
♡ Nimekuwa nikitafuta maarifa zaidi kuhusu imani yangu na uhusiano na Mungu.
♡ Nimetoa kipaumbele sana kwenye mambo mengine nayopenda tofauti na kazi Kama kupiga Gitaa na Kuchora.
♡ Kwa namna yoyote nimekuwa nikikwepa kukaa mwenyewe kwa muda mrefu.
♡ Kila mara nina utaratibu wa kupitia mabandiko yanayohusu madhara ya Video picha na mabandiko ya ngono ( ukitaka kuua mbwa mpe jina baya ).
♡ Nimemshirikisha mwenza wangu changamoto hii hivyo amekuwa masaada kwangu.
♡ Nimetengeneza ratiba inayoeleweka isiyotoa nafasi ya kuingiza wazo la kutazama Porn sites
kila napofikiria kufanya hivyo nabadili haraka wazo hilo.
♡ Mwisho nilipakuwa App fulani inayofungia picha video ama tangazo lolote la ngono kunifikia.
♡ Simu siweki password ama pattern yeyote akiingia kwa simu yuko huru hii inakuwa kama ulinzi kwamba ukikutwa na porn video ni aibu na sipo tayari kuaibika.

Kila la Kheri.
 
Kama fikra zangu zitakuwa sahihi kuhusu ulicholenga kukimaanisha hapa basi utakuwa huonyeshi tabia za kumpendeza kristo.
Fikra zako ziko sahihi, Mimi simpendezi Mungu wala Kristo.

Ila wewe, kiboboso, na denooJ..
"One people, different identity (color)"..

Ulichokielewa ndicho sahihi..
 
Fikra zako ziko sahihi, Mimi simpendezi Mungu wala Kristo.

Ila wewe, kiboboso, na denooJ..
"One people, different identity (color)"..

Ulichokielewa ndicho sahihi..

Mathayo 7:3-4 BHN​

Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
 

Mathayo 7:3-4 BHN​

Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
Asante mtumishi.
 
Hahahaha.

Sijataka kuuliza kwasababu nafahamu unadandia kitu usichokifahamu, kiufupi wewe ni mdananda wa imani, kaa chini ujifunze taratibu na kanuni mbalimbali za mambo ya imani (Sio mambo ya dini, maana wengi mnadhani kuwahi kanisani au kuswali swala tano ndo kuiva kiimani).

Wagalatia 6:3 NEN​

Kama mtu yeyote akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe sivyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe.
 
Jaman website ya ku download hii makitu naata wapi?maana vpn haikubali kudownload
 

Mathayo 7:3-4 BHN​

Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
Nimependa ulichofanya hapa, natumai wewe atakuelewa, kwangu aliamua kuleta ubishi wa kitoto nikaona bora nimuache ili huu uzi usiharibike na kupoteza mantiki yake.
 

Wagalatia 6:3 NEN​

Kama mtu yeyote akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe sivyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe.
Asante sana, nimemuimbia mpaka nikachoka ila nilivyojua ni aina gani ya mtu ninaehangaika nae na maandiko yananiambia nini kumhusu nikaona bora niachane nae, bado hajajitambua, hasa Mathayo 7:6.

Nikuongezee na baadhi ya maandiko yanayokataza watu wa Mungu kujikweza, Mathayo 23:12, Luka 14:11, na Luka 18:14 yeyote ajikwezaye atadhiliwa, na yule ajidhiliye atakwezwa.

Tusichoke kujinyenyekeza mbele zake.
 
Mna akili kweli?? Mmeharibu Uzi wa mwenzenu mpaka unakosa wachangiaji. Mnajihisi ni wakristo ila hamjui chochote upumbavu na ujinga umewajaa
Uko sahihi unachosema, na kama nisingekuwa makini basi naamini huu uzi ungezidi kuharibika, but nilivyotambua aina ya mtu niliyekuwa nikidhani namuelewesha kumbe yeye anapendelea ubishi nikaona bora nimuache, Waefeso 5:4, sorry for that.
 
Hahahahah

Sisi wengine Kwa Mungu hatuiigizi wajomba, yeye aliye juu ndiye aonaye ni namna gani nafsi zetu zimemgeukia na Kumtegemea yeye.

Unaweza ukajitutumua sana kwa kuja na ngozi mbalimbali, lakini ukweli unaujua.. Hakuna njia ya mkato kwa Mungu ni kujitoa haswa kuyafuata yaliyo maelekezo yake.
 
Kuna mtu mmoja alikua anajitekenya afu anacheka mwenyewe. Wenzake wakamwuliza kwanini? Akawajibu "Naigiza furaha, na Mimi nionekane mtu mwenye kufurahi"

Kwa Mungu hakuna maigizo.

Ayubu 28:20-24
"Basi hekima yatoka wapi?
Na mahali pa ufahamu ni wapi?
Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai,
Na kusitirika na ndege wa angani.
Uharibifu na Mauti husema,
Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.
Mungu ndiye aijuaye njia yake,
Naye anajua mahali pake.
Maana anatazama hata miisho ya nchi,
Na kuona chini ya mbingu nzima."
 
Daaaah ukiwauliza watu wengi wanasema hawaangalii kabsa ila katka takwimu hizo website za porn znaongozwa kwa kutazamwa mara nyingi
 
Back
Top Bottom