Safari ya Makamba Wizara ya Nishati, Rushwa, Kuachia ngazi na Mengineyo toka 2010

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2010, January Makamba alipata nafasi ya kuhudumu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati nyeti ya Nishati na Madini ikiwa ni Wiki chache tu tangu kuingia kwake bungeni. Ilikuwaje akaaminiwa katika nafasi hiyo? Na nini kilipelekea kamati hiyo kuvunjwa mara tu baada ya yeye (Makamba) kuachia Uenyekiti? Na nini hasa alikiandika katika kitabu chake Mazungumzo na January Makamba (Maswali na Majibu 40) hasa katika sekta hii ya Nishati anayoiongoza sasa?

Hili ni andiko linalonukuu simulizi ya January Makamba kutoka kwenye kitabu hicho.

“Nilivyoingia Bungeni, nilipewa fomu za kuchagua Kamati ambayo ningependa kupangwa. Chaguo langu la kwanza lilikuwa ni Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Ilipotoka orodha ya Wajumbe wa Kamati nikaona jina langu kwenye Kamati ya Nishati na Madini. Kusema kweli, nikiwa kama mbunge wa mara ya kwanza, changamoto zilizokuwa zimezigubika sekta hizi miaka ile zilinitia hofu kidogo.

Baada ya kutafakari na kushauriana na marafiki zangu bungeni, nikaona kuwa nikielekeza nguvu zangu na ari yangu katika Kamati hii, nitaweza kufanya mabadiliko makubwa katika sekta na kuwapunguzia kero wananchi wengi. Nikaamua kugombea Uenyekiti wa Kamati.

Hakukuwa na muda wa kampeni kwa sababu majina ya Kamati yametangazwa leo, uchaguzi kesho yake. Tukaingia ukumbini. Kwa nafasi ya Uenyekiti, nikaweka jina langu mbele, na Mheshimiwa Festus Limbu, Mbunge wa Magu, naye akaweka jina lake. Tukajieleza. Kura zikapigwa. Nikapata kura 19, Mheshimiwa Limbu kura 6. Baada ya siku chache tu kama mbunge, nikakabidhiwa dhamana hiyo nzito.”

“Kwa kutambua umuhimu wa dhamana tuliyokabidhiwa, tulijipanga kuwa wakali sana katika kuisimamia Serikali. Kama Mwenyekiti, nilijitahidi sana kuweka nidhamu na umakini katika utendaji wa kazi zetu. Tulikuwa tunapata taarifa kwamba Serikali a Taasisi zilizokuwa zinakuja mbele ya Kamati yetu zilikuwa zinajiandaa vyema kwa sababu walikuwa wanajua kwamba tulikuwa hatuna
mchezo.

Kuhusu umeme, tulifanikiwa kuishauri Serikali mambo mengi ya msingi, ikiwemo kuachanaa mitambo ghali ya kukodisha na kupanga fedha zaidi kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini. Kuna nyakati katika kujadili Bajeti ya Wizara, tulihamisha fedha kutoka mafungu yasiyo na tija na kupeleka kwenye miradi ya meme vijijini. Tulilazimisha ratiba ya uhakika ya kumalizika kwa mgao wa Umeme, tuliibua maeneo yaliyokuwa na ufisadi ikiwemo kwenye suala la ununuzi wa mafuta ya mitambo ya dharura, tulihoji kuhusu gharama kubwa za kesi za Tanesco.

Tulishirikisha wadau wote wa umeme, ikiwemo wenye viwanda, katika kazi zetu. Tulifanya mihadhara a midahalo mbalimbali katika kuisaidia nchi kupata suluhu ya tatizo hilo. Tuliwezesha kusimamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ili Serikali ilete Bungeni Mpango wa Dharura wa kulinusuru taifa na mgao wa umeme.

Kuhusu sekta ndogo ya mafuta, tullingilia kati wakati nchi imeingia kwenye hatihati ya kusimama kabisa wakati wa mgogoro wa waagiza mafuta a Serikali kuhusu upangaji bei. Moja ya siku ninazojivunia katika muda wangu kwenye siasa ni pale nilipoleta hoja Bungeni ili Bunge lisimamishe shughuli zake zote na tujadili na kupata majawabu ya dharura ya mafuta nchini.

Bunge lilikubali na Serikali ikalazimika kuchukua hatua za dharura kuokoa hali ile. Baadae tulisimamia Serikali kuanzisha mfumo mpya wa ununuzi wa mafuta wa pamoja, yaani Bulk Procurement System. Vilevile, tulifanva vikao a Chama cha Wamiliki wa magari ya mizigo na kusikia kilo chao kuhusu tatizo la uchakachuaji wa mafuta na tukapendekeza njia muafaka zilizomaliza tatizo hilo kabisa.

Kuhusu gesi, kabla Kamati yetu haijaundwa, hapajawahi kuwa na mjadala Bungeni kuhusu masuala ya gesi. Niliunda Kamati Ndogo ya Kamati yangu ili kulichunguza kwa kina suala la gesi. Kamati ile ilifanya kazi zuri na kwa kweli napendekeza watu waitafute ile ripoti a kizalendo na kuisoma. Ripoti ile ilijadiliwa Bungeni na maazimio yenye maslahi kwa nchi kupitishwa. Ripoti ile ilitikisa Bunge. Yapo baadhi ya masuala ya ulaghai wa wazi uliofanywa na baadhi ya makampuni ya gesi na tukapendekeza mikataba ivunjwe, watu hao wakamatwe, na warudishe pesa.

Vilevile mapendekezo ya ripoti hii kwa sehemu kubwa ndio yametengeneza rasimu ya Sera mpya ya gesi. Nakumbuka tulisimamisha ugawaji wa vitalu vipya wa gesi mpaka sheria mpya ya gesi ipitishwe. Bahati mbaya, sheria hiyo mpaka leo hi haijapitishwa. Natumaini itapitishwa karibuni.

Kama Kamati tulipata changamoto nyingi mara kwa mara. Sekta ya Nishati ni nyeti na kuna watu wengi wenye maslahi makubwa katika sekta hi. Sekta hii inahusisha fedha nyingi na kumekuwa na historia ya rushwa na ubadhirifu. Kazi kubwa tuliyofanya ni kuhakikisha wajumbe wote tunasimama pamoja na kuepuka ushawishi unaoweza kutupeleka pabaya. Katika kipindi changu tulifanikiwa kwa kiasi fulani. Binafsi nilipata changamoto kubwa za kuchafuliwa. linakosa transfoma. T

ano, kudhibiti hujuma na rushwa kwenye sekta ya nishati, ikiwemo mikataba mibovu isiyo na maslahi kwa taifa. Na mwisho tukamilishe haraka ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara ili tuzalishe umeme wa gesi na kuondokana na umeme wa kukodi wa kuzalishwa kwa mafuta. Binafsi nafarijika, na naamini pia wenzangu tuliokuwa nao kwenye Kamati wanafarijika, kwamba udhibiti wa sekta hi na mapendekezo yetu ndio yalianzisha kwa uhalisia mapinduzi chanya katika sekta hii.

Kamati yetu iliweka msukumo mkubwa kwa serikali kulishirikisha bunge katika mikataba yote, mikubwa na midogo, ya nishati na madini, hasa umeme na gesi, ili kupunguza mianya ya taifa letu kudhulumiwa na wawekezaji wa ndani na nje. Mpango-Mkakati Mpya wa Mageuzi kwenye Sekta ya Umeme kwa kiasi kikubwa umezingatia tuliyoyapendekeza.

Pia, tulihakikisha walau tunayabainisha matatizo yaliyokuwepo kwenye sekta ndogo ya mafuta, ikiwemo suala nyeti la upangaji bei katika soko ambao hauakisi uhalisia wa bei ya Dunia kupitia mdhibiti wetu, EWURA. Vilevile, tulisimama kidete kuhakikisha kwamba wachimbaji wadogo wa madini wanawezeshwa ipasavyo. Tuliilazimisha Serikali kupanga fedha nyingi zaidi kwa ajili hiyo. Nafarijika kwamba utaratibu huo umeeendelezwa hadi sasa.

Miaka 11 Baadaye Makamba amekabidhiwa rungu Wizara ya Nishati, ngoja tuone matokeo

january-yusuf-makamba.jpeg
 
Februari hawezi kutuaminisha uzalendo wake tofauti na tunavyomfahamu tangu akiwa anakula meza kuu.

Matumizi ya media yapunguzwe watu wanataka vitendo bana.
 
Bado tunauhitaji UPEO MKUBWA alionao kaka mkubwa Komredi January Makamba.

Taifa linamhitaji sana tu.

Yeye ni HAZINA.

#SiempreJMT
 
Ngoja tuone ana nini cha kutupa hapo Nishati
Baada ya yote kupita, nina imani kubwa mno kuwa mh.J.Makamba atafanya kazi kwa weledi zaidi ya kipondi cha nyuma.....ili tu "awaprove wrong" baadhi ya WANAOMKOSOA.

TAIFA LINAUHITAJI SANA WELEDI WAKE

#SiempreJMT
#NchiKwanza
 
Akiwekwa mbali na keki ya taifa anaanzisha visa, anadhani hii nchi ni ya ukoo wao lazima awe kiongozi, wale wajumbe wa bodi ya Tanesco aliowateua ameonesha dhahiri nature yake, kuweka marafiki zake ili awe huru kufanya apendavyo bila kupata pingamizi toka kwa members wa bodi.
 
Ukimuona amekaa, unaweza kudanganyika kwamba juu kuna kitu, lakini ukweli ni mtupu! Huyu si ndiye miaka ya kugombea alikuwa anaombewa pesa za kampeni na dada yake kwa mahawala zake? Yaani dada anaomba pesa kwa mzungu anayejivunia kula uroda naye ili kaka apate pesa za kampeni, na kuahidi kurudisha fadhira! Siyo huyu? RUBBISH!
 
Ukimuona amekaa, unaweza kudanganyika kwamba juu kuna kitu, lakini ukweli ni mtupu! Huyu si ndiye miaka ya kugombea alikuwa anaombewa pesa za kampeni na dada yake kwa mahawala zake? Yaani dada anaomba pesa kwa mzungu anayejivunia kula uroda naye ili kaka apate pesa za kampeni, na kuahidi kurudisha fadhira! Siyo huyu????? RUBBISH!
Hafai. Hizo pesa dada mtu alizirudishaje kama sio kwa kutupiga watanzania kwenye ofisi ya umma aliyokabidhiwa?
 
Ukimuona amekaa, unaweza kudanganyika kwamba juu kuna kitu, lakini ukweli ni mtupu! Huyu si ndiye miaka ya kugombea alikuwa anaombewa pesa za kampeni na dada yake kwa mahawala zake? Yaani dada anaomba pesa kwa mzungu anayejivunia kula uroda naye ili kaka apate pesa za kampeni, na kuahidi kurudisha fadhira! Siyo huyu? RUBBISH!
Mkuu hebu shusha pumzi 🤣

Wanasiasa huwa wanakusanya fedha za kampeni kutoka vyanzo mbalimbali.

Sina uhakika na usemacho ila hata kama ni kweli je fedha zote alizonuia kukusanya ilikuwa zitoke kwa huyo SHEMEJI yake?

Je, mashemeji hawatakiwi kuchangia?
Kuna kipengele hicho?!!

Na kama haitakiwi fedha kutoka kwa wasio watanzania kuepusha KUWATUMIA WANASIASA je ni kiasi gani alikitoa huyo mzungu, una ushahidi alitoa?
 
Baada ya yote kupita.....nina imani kubwa mno kuwa mh.J.Makamba atafanya kazi kwa weledi zaidi ya kipondi cha nyuma.....ili tu "awaprove wrong" baadhi ya WANAOMKOSOA.......

TAIFA LINAUHITAJI SANA WELEDI WAKE

#SiempreJMT
#NchiKwanza
Nishati ni Wizara ya kisayansi. Makosa ni kuendelea kuweka watu ambao hata hawafahamu formula ya kutafuta energy ya starch.
 
Mkuu hebu shusha pumzi 🤣

Wanasiasa huwa wanakusanya fedha za kampeni kutoka vyanzo mbalimbali.....

Sina uhakika na usemacho ila hata kama ni kweli je fedha zote alizonuia kukusanya ilikuwa zitoke kwa huyo SHEMEJI yake ?!!!

Je mashemeji hawatakiwi kuchangia?!!!
Kuna kipengele hicho?!!

Na kama haitakiwi fedha kutoka kwa wasio watanzania kuepusha KUWATUMIA WANASIASA je ni kiasi gani alikitoa huyo mzungu.....una ushahidi alitoa?!!!!
Tatizo siyo Shemeji au nyumba ndogo. Tatizo ni kile anachoahidiwa shemeji pindi Januari akipita.
 
Binafsi nadhani tumwamini sehemu nyeti kama hizi hawezi kuwa peke yake kuna macho yanamtazama

Wakati6 wowote akienenda isivyotakiwa hatua zitachukuliwa

Sio mgeni serikalini kwahiyo anajitambua tumpe muda tuone
 
Back
Top Bottom