Sadaka ya kweli ni ipi?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,216
SADAKA YA KWELI NI IPI?

Mtoto mmoja alikuwa amesimama, bila viatu, mbele ya duka la viatu akitetemeka kwa baridi. Mwanamke mmoja alikuja na kusema:

"Rafiki yangu, unatafuta nini hapa au umependezwa na dirisha la dukahilo?"

Akajibu, "Nimekuja hapa kumuomba Mungu anipe jozi ya viatu." Mwanamke huyo alimshika mkono na kuingia naye dukani na kumwomba muuzaji nusu dazeni ya soksi kwa ajili ya mtoto na jozi ya viatu.

Aliomba kama angeweza kumuazima beseni la maji na taulo na kumchukua mtoto huyo hadi nyuma ya duka.
Kwa upendo alianza kuosha miguu ya mtoto na kuikausha, kisha akavaa soksi na viatu vyake. Alimpapasa kijana kichwani na kusema: "Bila shaka rafiki unajisikia vizuri zaidi sasa!"

Mwanamke alipogeuka ili aondoke, yule mtoto, akiwa na furaha sana, akamshika mkono, akimtazama huku machozi yakimtoka, akamuuliza: "Wewe ni mke wa Mungu? Mwanamke akajibu: "Hapana, mimi ni mwanamke ambae ninatoa shukrani kwa kile alichonipa Mungu,"
 
Hizi tabia za wema wa Kimungu umekwisha kama sio kupungua. Na ndio maana maisha na ma Alaa yanatupata, tumekuwa wabinfsi Sana.
 
Back
Top Bottom