Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja

Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja

Itakuitaji muda mrefu kufikiria na kuconnect dots membe na sofia wanachosema kina ukweli ndani yake. inawezekana wahisani wa nje wanapitia migongo ya wengine kusponsar vyama, na inawezekani hii imeanza muda mrefu.

Mzee Sabodo amekuwa akimwaga hela kwa CDM kwa muda mrefu na mara nyingi. Je wahisani wamepitia kwa sabodo kuipa nguvu cdm?

Naweza kusema hii ni moja wapo ya ushahidi wa cdm kupokea mkwanja toka nje

DSC09389.JPG

:msela::msela:

barabara afu tunaomba tupewe mapato na matumizi ya pesa za sabodo maana baadhi ya wanachama wa CDM niliongea nao wanalia njaa sana wakati viongozi wakuu wanakula peke yao
 
barabara afu tunaomba tupewe mapato na matumizi ya pesa za sabodo maana baadhi ya wanachama wa CDM niliongea nao wanalia njaa sana wakati viongozi wakuu wanakula peke yao

KAMA NISINGETUMIA BUSARA NINGESEMA HUJATUMIA BUSARA na ni mchochezi KUTAKA FEDHA ZA MSAADA WA KUIMARISHA CHAMA ZIFAIDIWE NA WANACHAMA.
 
''Kwa hiyo inawezekana hata
mfuko wa mama Salima Kikwete
uliosaidiwa na Sabodo ni kutoka
nje?''

Nafikiri kipindi kile baba wataifa alipo kuwa anahitaji viongozi wa kisiasa na asasi za kijamii kuainisha vyanzo vya mapato yao 'he was so right', kwa sasa kila mmoja atajaribu kupoint mistake za mwenzake ili aonekane mwema, kisa watu kama mimi hatujui yeye kama ni kibaraka au la.
 
Muwe mnaweka pia na vyanzo vyoote vya mapato kwa vyama vyote haswa ccm ili tuchangie vizuri..
btw picha haionekani..
hivi Gaddafi hajawahi kuimwagia CCM pesa through bernard membe mpaka membe akaamuliwa na Ghaddafi ajenge misikiti jimboni kwake?
 
No research no right to speak.Kwanini unataka kulazimisha assumptions kuwa facts?Umeandika mwenyewe kuwa "inawezekana",implying huna hakika...na pia iinachowezekana kinaweza pia kuwa hakiwezekani...lakini wakati huohuo unakurupuka kudai huu ndio ushahidi.

Mmerogwa na nani hadi kuwa vibaraka wa mafisadi?

Siamini kama w3w3 ni Alumni wa darasa la AS 102 la Dr. Fransic Lyimo pala UDSM.... Love you boy!
 
Itakuitaji muda mrefu kufikiria na kuconnect dots membe na sofia wanachosema kina ukweli ndani yake. inawezekana wahisani wa nje wanapitia migongo ya wengine kusponsar vyama, na inawezekani hii imeanza muda mrefu.

Mzee Sabodo amekuwa akimwaga hela kwa CDM kwa muda mrefu na mara nyingi. Je wahisani wamepitia kwa sabodo kuipa nguvu cdm?

Naweza kusema hii ni moja wapo ya ushahidi wa cdm kupokea mkwanja toka nje

DSC09389.JPG

:msela::msela:
amakweli JF imevamiwa na maharamia, hivi try to think a little huyu mzee Sabodo ni mtanzania au Mkenya, si mtanzania kuna ubaya gani akitoa msaada kwa CDM chama kinacho tetea maslai ya walalahoi, naomba ukiwa unapost article speak with authority wacha siasa za maji taka zisizo na tija. kama CDM inafadhiliwa na Balozi embu jaribu kutoa evidence sio unakuwa kama mamluki CCM i.e Chaka Chua Matokeo. nyinyi hiyo dhambi ya Ufisadi inawatafuna kama cancer hamjitambui, please try to think BIG.
 
Wewe hujui unachoongea, Membe ameongelea balozi na wahisani wa nje, sasa wewe unamuongelea Sabodo.....unamfaham vizuri Sabodo??

Leta evidence za mantiki, usikulupuke tu kuleta vipost vya hovyo...
 
barabara afu tunaomba tupewe mapato na matumizi ya pesa za sabodo maana baadhi ya wanachama wa CDM niliongea nao wanalia njaa sana wakati viongozi wakuu wanakula peke yao

acha umbea ndugu yangu, akina nani walikulilia wewe?? na wewe ni nani hata wakulilie???
 
porojo zao haziwezi kubadalisha ukweli unaweza kumdanganya mtu mmoja,watu wawili hata watu kumi lakini huwezi kuwadanganya watanzania wote ccm mwisho wenu umefika longolongo hatutaki tena
 
Sabodo alitoa mchango katika uchaguzi na siyo kuchangia kupinga malipo kwa dowans. Hakuna chama cha siasa hapa nchini ambacho kwa namna moja ama nyingine haipati misaada kutoka vyama rafiki au mashirika au watu binafsi. Hivyo sioni sababu ya watu kujadili sijui nani anapata hela wapi au kiasi gani, cha msingi kama nilivyomwelewa Mh. Mnyika ni kwamba kuna tuhuma kuwa chadema wanapewa pesa kutoka ubalozi fulani kufadhili uvurugaji wa nchi au nchi ionekane haitawaliki. Mimi nimefurahi sana kusikia kuwa chadema wanataka kwenda mahakamani na siyo kila siku lawama tu na kutaka serikali iende mahakamani nashauri wasichelewe waende mahakamani haraka sana ili tujue kile anachosema Rais ni kweli ama la kama ni kweli nini kifanyike? chadema kifutwe, kama la basi serikali ya ccm iondoke madarakani haraka sana. Tukumbuke kauli hiyo haijaanza kwa Membe na Simba tu bali Rais Kikwete alishawahi sema hivyo kuwa kuna balozi anachotaka yeye ni kuona ccm inaondoka madarakani.

Upande wangu sasa. Ni kweli kabisa kuna balozi hapa nchini ambaye anataka kuona ccm inaondoka madarakani na kinaingia chama anachokitaka yeye kwa maslahi ya nchi yake. Balozi huyo alifanya kazi ya ziada Zanzibar kuhakikisha kuwa cuf inaingia madarakani na aliweza kupanga hata safu ya mawaziri lakini alishindwa kucheza na system iliyopo mwisho karume akampasha maalimu kuwa nchi ni yao na si ya balozi huyo wanachotaka wenzetu ni mafuta. maalimu akakubali wakaleta serikali ya umoja wa kitaifa kitu ambacho kilimchukiza sana balozi huyo akiamini jk pamoja na taasisi fulanifulani walihusika kupanga huo mkakati. Nafurahi sana kwa kuwa waliyemtaka awe waziri wa uchumi hakupata uwaziri ila ni mwakilishi tu. Sasa wanahamia bara na gia ni ileile ya uchonganishi ili ifike mahali mtu wa ccm, cuf, tlp, nccr, nk asimwombe chumvi mtu wa chadema na hata kura zipigwe za chuki kama alisema karume.

mimi sitaki longolongo naweka mambo wazi kuwa balozi huyo ni balozi wa Denmark akisaidiwa na global platform na action aid. Hili hata management blog hii ya JF inalifahamu vyema. Ni kweli kuna matatizo mengi ya kiuongozi hapa nchini lakini isifike mahali tukagombanishwa na mataifa mengine kwa kutumia udhaifu wetu.

Nawasilisha.
 
HIzi za sabodo zilikuwa zinapitia mgongoni mwa mtu toka nje

Mtasema saaaaaaaana kwa kuwa mlikuwa mnataka vyama legelege... sasa mnachokiona ni kwamba Tanzania kipo chama ambacho kitaenda na nyie ng'adu kwa ng'adu mpaka uchaguzi unaofuata.

Sasa mnaona ile kauli ya kilaza wenu Kikwete ya kuwa vyama vya upinzani ni vya msimu ... mko karibu kuimeza na itawatokea puani.

Kama mnao ushahidi SI MSEME HADHARANI ni nchi gani na ni nani na ni kiasi gani??? Sisi kanyaga twende maana operation sangara PLUS imeanza sasa hivi mpaka 2015
 
Mfa maji haishi kubwabwaja, wamekosa swaga sasa wabwatuka tu! Siasa za FItina za miaka hatuzitak ktk kizazi chetu hiki!
 
barabara afu tunaomba tupewe mapato na matumizi ya pesa za sabodo maana baadhi ya wanachama wa CDM niliongea nao wanalia njaa sana wakati viongozi wakuu wanakula peke yao

We Kashaga wacha uchochezi, mtaje basi aliye kulilia njaa huyo!!! Hizo fedha za Sabodo zinawauma nini??????
 
Itakuitaji muda mrefu kufikiria na kuconnect dots membe na sofia wanachosema kina ukweli ndani yake. inawezekana wahisani wa nje wanapitia migongo ya wengine kusponsar vyama, na inawezekani hii imeanza muda mrefu.

Mzee Sabodo amekuwa akimwaga hela kwa CDM kwa muda mrefu na mara nyingi. Je wahisani wamepitia kwa sabodo kuipa nguvu cdm?

Naweza kusema hii ni moja wapo ya ushahidi wa cdm kupokea mkwanja toka nje

DSC09389.JPG

:msela::msela:

Saasa mnachotaka ni nyie tu ndio muwe na hela??? Nyie mbona mumeiba 40bl kwa kampeni kwa jina la kagoda??? Mumetumia zaidi ya 94bl kwa ajili ya kampeni ambazo leo mnalazimisha tulipe dowans kumbe mnataka kuziba mashimo.

Ok !!! wao wanadhaminiwa nje... je na nyie mnaochota HAZINA nani mbaya??? Maana zao wanazopata ni hela halali... je nyie wezi?? Waduanzi wakubwa nyie...
 
Back
Top Bottom