cherie neisha
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 3,873
- 20,705
Mungu anatupenda na alitupa akili tuitawale dunia,Alitupa freewill.
Binadamu akakata miti, kuchoma misitu,akaua wanyama,akajenga na kutawala.
Binadamu akatengeneza gari, ndege,treni,meli na bunduki.Akatengeneza ndege na nuclear bombs.Akaua na kutesa wenzake.
Binadamu akamtumia binadamu mwenzake katika majaribio ya magonjwa na madawa(rejea waisraeli walichofanyiwa na Nazi pamoja na the Tuskegee syphilis experiment huko US).
Binadamu akaona sayansi ndiyo kila kitu.
Binadamu akajaribu kujiumba.Binadamu katoa mimba.Kajibadilisha maumbile.Kafanya kila atakalo.
Binadamu kachoka sasa.Binadamu amefika stage anajiogopa.Anaitafuta Amani ya moyo.Sayansi haijampa majibu aliyokuwa Anataka.Anaitafuta Amani katika homosexuality labda.
Kaona kila juhudi aliyoifanya haijamletea chochote zaidi ya uharibifu aliokuwa anaukwepa.Binadamu Ana hasira.Mungu aliyemkana sikuzote leo ndo ameona aje kumtupia lawama.
Anaona akisema Mungu hayupo atakuwa amemkomoa Mungu.
All the best humanity.
Mimi simwoni mtu anayekataa uwepo wa Mungu mjinga,kila mtu na maamuzi yake na sababu zake binafsi za imani.Siforce tufanane.
Ila mimi naamini uwepo wa Mungu.Sayansi ndogo ninayoijua mimi haikunifanya kamwe kutoamini uwepo wa Mungu,sanasana imenizidishia Imani.