BIGstallion
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 6,324
- 7,919
Where will he come from?......well if he exist then hope he has good excuse for his unnecessary, weak and destructive existence.
Duh mkuu umekata tamaa kiaina na Maisha nn,..!?
Where will he come from?......well if he exist then hope he has good excuse for his unnecessary, weak and destructive existence.
Ni vigumu kuthibitisha uwepo wa mungu na ni vigumu zaidi kudhitisha hayupo.Thibitisha kwamba yupo
Ndiyo! kama watu wakiacha kumwabudu Mungu, kizazi kitakachofuata hakitakuwa na uelewa wowote kuhusu Mungu.Uwepo wa Mungu unatokana na masimulizi ya dini ambayo hayana uthibitisho.Tofauti na dini za watu Mungu hana namna nyingine ya kujidhihirisha kwa watu wasiomjua.So Mungu anatutegemea sisi ili yeye awepo?
Nikate tamaa kwa sababu zipi? bado naendelea kufurahia maisha to the fullest level.Duh mkuu umekata tamaa kiaina na Maisha nn,..!?
Watu hawakuumbwa na Mungu maana Mungu hayupo.Kabla ya kutuumba palikua na watu?? Je aliishije?
Nikate tamaa kwa sababu zipi? bado naendelea kufurahia maisha to the fullest level.
The Universal and Personal Aspect of GodKuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.
1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)
2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?
3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?
4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way He is and we have to live with it.
5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.
6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mm nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.
Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa ntakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo. So im just keeping it real.
Kwa kuwa nyie mnaenda kwenye ibada ili mpate comfort ndio umeona tusioamini uwepo wa Mungu wala kujihangaisha naye tupo frustrated?.........Hivi kuna watu wanaishi maisha ya furaha kuliko wapagani na Atheists?Frustration zako zipo complicated mbaya,
Hallow pole na kile kinachokusibu moyoni, ila nina wasiawsi sana kama kweli unamchukia Mungu. Unaweza ukawa unampenda Mungu pasipo wewe mwenyewe kuwa unajua kuwa unampenda. Itakuwa unampenda Mungu iwapo:Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.
1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)
2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?
3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?
4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way He is and we have to live with it.
5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.
6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mm nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.
Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa ntakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo. So im just keeping it real.
Unaweza ukaongea au kuelezaje pale Musa alipomtokea YESU walipopanda mlimani na wanafunzi wake!? Musa na Elia,,muelezee zaidi Musa maana alikufa na MUNGU akamzika?Je YESU alikuwa na maana gani kumwambia yule mwizi pale msalabani kwamba leo nitakuwa na wewe mbinguni??? Je YESU atakaporudi mara ya pili na wafu kutoka makaburini na kupaa nae watakuwa ni wafu wapi hao?? Ile habari ya YESU kuelezea maskini na tajiri kufa na maskini kwenda kwa Ibrahim na tajiri kwenda penye shida unaielewaje??? Au ni fiction????Mkuu Loeb, ukweli ni kwamba, kulingana na Biblia, hakuna maisha baada ya kifo (ukiondoa ufufuo). Zipo sehemu kadhaa ndani ya Biblia zinaeleza hili wazi;
Kwa hiyo, kwa ujumla, mtu akifa anaenda kaburini, na kutegemea na uhusiano aliokuwa nao na Mungu kabla hajafa, anasubiri kufufuliwa au la. Akiwa kaburini, anakuwa hajui lolote linalooendelea, hana mawazo wala hisia, na hasikii raha wala taabu. Hivyo hata msemo watu waliozoea kusema kwamba "Mungu mweke mahali pema peponi" ni pure rubbish. Mtu akifa hahitaji kuwa pema wala pabaya kwa sababu hana hisia za kujua yuko pema au pabaya. Kumwambia Mungu mweke mahali pema peponi ni jambo lisilo na maana.
- Ukianza na kitabu cha Mwanzo, Mungu alisema wazi kwa Adamu kwamba angekufa na kurudi mavumbini alikotolewa. Kabla Adam hajaumbwa hakuwapo, na baada ya kufa asingekuwapo tena, angerudi kuwa vumbi (Mwanzo 3:19)
- Kitabu cha Muhubiri kinafafanua kwamba hakuna tofauti kati ya kifo cha mnyama kama panya, mbwa, ng'ombe, tembo, nk, na wanadamu. Kinasema wazi kwamba wote wanakufa sawa, wote wanarudi mavumbini. Na suala la kusema wanadamu wakifa roho inatoka inaenda mahali, nani amekueleza (Biblia inauliza sio mimi). Kwa hiyo inamaanisha kwamba kama utasema kuna mahali roho za watu zinaenda wanapokufa basi pia roho za paka na panya zinaenda huko - jambo ambalo halipo (Mhubiri 3:19-21)
- Kitabu cha Muhubiri kinazidi kusisitiza kwamba mtu anapokufa hawi tena na fahamu, hisia na mawazo yake hutoweka - hivyo hawezi kuhisi furaha au chuki, raha au taabu. Kumbuka watu wa mwili wa roho wana hisia, hivyo ikimaanisha ukifa wala hupati mwili wa roho (Mhubiri 9:5-6)
- Yesu alitamka wazi kwamba watu waliokufa wako kaburini, waliotenda wema kwa ufufuo wa uzima na waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu (kumbuka hakusema wako mahali wanaishi eidha kwa taabu au raha, alisema wako kaburini). Hivyo watu waliokufa wako kaburini - au kule walikoishia, baharini nk. (Yohana 5:28-29)
Jiulize swali - ikiwa ni kweli watu wema wakifa wanaenda sehemu fulani nzuri kama thawabu, sasa kuna haja gani ya kuwa na ufufuo? Je Mungu atafufua watu walio tayari katika sterehe ya milele kwa sababu walitenda mema? Kama watu wakifa wanapata mwili wa roho na kwenda kuteswa au kuishi milele - itamaanisha fundisho la ufufuo katika Biblia ni la uongo, kwa kuwa hakuna haja tena ya ufufuo!
Kwa hiyo Mkuu, mtu akifa hana tena hisia wala mawazo, inakuwa kama kulala usingizi fofofo bila hata kuota ndoto. Eidha subiri ufufuo, kama ulikuwa mtenda mema, au ndio hivyo, kwa heli ya mshahara wa dhambi - hutaishi tena!