Hujaona hapo juu kuwa kanuni ni mipaka ya Mungu pia? Nimekwambia Mungu hawezi kusema "uongo", hawezi kutenda bila " haki". Kanuni za Uungu zina mfanya asiweze kufanya hayo, kwahiyo yuko chini ya kanuni pia. Nimekwambia hakuna kitu kiishicho pasi na kanuni.
Nimejaribu kutoa mifano mingi ili unielewe, kwamba Mungu hakuuumba huu ulimwengu wenye hizi changamoto. Aliouunda yeye ulikuwa ni bora sana, ila ilinilazimu waifuate kanuni za uumbaji ndo auumbe, hizo kanuni zilitakiwa zitiishwe hili kile bora kiendelee.
Mfano, chakula, binadamu alivyoumbwa, kikanuni alitakiwa awe wanakula mbogamboga, nafaka na matunda tu. Hadi leo awezaye kuishi hivyo atabarikiwa na maisha marefu yenye afya tele. Alae nyama atapungukiwa baadhi ya vitu bora ktk ubinadamu wake, mfano afya bora, kuwa na asira nk. Chanzo, ni kutokuzitii kanuni.