Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.
Mkuu, wala huna haja ya kumchukia Mungu. Ngoja nijaribu kujibu hoja zako kulingana na mie nilivyoelekezwa. Angalia kama ninachosema kina make sense.
1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe Jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)
Si kweli kwamba Mungu ameandaa jehanamu. Jehanamu ni sehemu ya fundisho la kidini la uongo sana. Kwenye Biblia ukweli uko wazi, kwamba Mungu atahukumu kwa kifo watu wanaotenda dhambi - kama alivyofanya wakati wa Sodoma na Ghomora na ghalika. Kwani waliohukumiwa wakati huo wako sehemu fulani jehanamu? Yeye amesema wazi - mshahara wa dhambi ni mauti. Hajawahi kusema mshahara wa dhambi ni moto wa milele. Kwanza unawezaje kumchoma mtu kwa umilele? Yaani aungue milele asife - labda huo moto hauunguzi basi. Lakini hakuna kitu kama hicho.
2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?
Kitendo cha shetani Mungu hakukipanga wala kuruhusu. Japo Mungu aliweka mti wa matunda kwa ajili ya kujaribu utii wa Adamu, hakutarajia kwamba Adamu angekula lile tunda kupitia kushawishiwa na Ibilisi. Na pia jambo la msingi sana wewe kuelewa, ni kwamba Mungu ana uwezo wa kuelewa kila kitu hata kitakachotokea kesho au muda mrefu ujao - lakini mara nyingine anaamua kutoangalia nini kitatokea mbele ili aone mambo yanavyotokea katika "real time".
Kumbuka pia Mungu alimuuliza Adamu - "nani amekuambia uko uchi, umekula tunda nililosema usile?" Ndipo Adam na Eva wakampa taarifa ya kilichotokea. Asingewauliza yale maswali kama alijua kimefanyika kitu alichopanga. Na hakujua kwamba Adam na Eva wangeshindwa jaribu dogo la tunda - kwa sababu hakutaka kuangalia matokeo yatakuwaje, kama watakula au la. Ukweli ni kwamba alikuwa amewapa jaribu dogo sana ili kupima uaminifu wao kwake. Adamu na Eva walikuwa na maelfu ya matunda na vyakula vingine, sio kuwa walikula kwa sababu ya njaa ya kukosa kitu cha kula. Waliamua kutokutii amri ya Mungu kwa utashi, wakitaka kuwa sawa na Mungu, kama Ibilisi alivyowadanganya.
Matokeo ya sisi kuteseka kutokana na dhambi ya Adamu ni kweli yapo. Lakini hiyo ni sehemu ya shutuma ya Ibilisi kwamba sisi binadamu tunamwabudu pale tu anapokuwa ametupa raha na starehe - kama kusema anatuhonga ili tumtii. Kwa hiyo Mungu ameachia mambo yalivyo sasa ili kujibu shutuma za shetani - kama ilivyokuwa katika episode ya Ayubu. Ila alisema wazi, muda wa kutosha utakapopita kumwonyesha Ibilisi kwamba wanadamu wapo watakaomtii Mungu katika generation zote na hali zote, basi ataleta hukumu. Suala ni sisi kuvumilia hadi siku atakaposema sasa inatosha!
3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? Au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?
Hata siku moja Mungu hajasema tusipomtii atatuchoma moto. Kumbuka Ibilisi alimwambia Mungu tunamtii kwa kuwa anatuhonga na hali nzuri, na Mungu akaonyesha si kweli. Sasa unafikiri ingekuwa kweli Mungu anatishia kutuchoma moto ili tumwabudu - si ndio shetani angetoa shutuma mbaya hata zaidi dhidi ya Mungu kwamba watu hawa wanakutii kwa sababu umetishia kuwachoma moto? Kumbuka mshahara wa dhambi ni mauti - na wa utii kwa Mungu unaleta uzima wa milele. Hivyo maandiko yanasema wazi - mbele yetu tuna uchaguzi - uzima wa milele au mauti. Usipotii Mungu ni kwamba utakufa, period. Eidha ukifa sasa hutafufuliwa tena (unakuwa umeshapata mshahara wako) au ukiwa hai siku ya kiama utakufa siku hiyo, Period.
4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way he is and we have to live with it.
Bado jibu ni lile lile - Mungu hana mpango wa kuchoma moto wa milele watu wasiomtii. Atawaangamiza kwa kifo kama alivyofanya wakati wa Sodoma na Gomora na Gharika, watakufa wasiwepo tena.
5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.
Kweli, Mungu ana hekima sana kuliko wanadamu. Hatuwezi hata kujilinganisha naye kwa mbali sana. Kwa hiyo una mwanzo mzuri, unaonyesha unyenyekevu tayari. Basi jaribu kuwa mnyenyekevu hata zaidi, na utaona ni jinsi gani kwa maelezo yaliyopo chini.
6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mimi nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.
Ni baraka kuzaliwa - kumbuka maandiko yanasema watoto ni zawadi toka kwa Mungu. Sasa je, unalaani zawadi ambayo Mungu aliwapa wazazi wako na huenda wakaifurahia sana? Na kumbuka Mungu ana kusudi moja kwa kila mwanadamu anaezaliwa - kwamba maisha yake yatumike kujibu shutuma za shetani kwamba wanadamu hawawezi kuwa watiifu kwa Mungu, na kwamba Shetani ana uwezo wa kumfanya kila mwanadamu anaezaliwa amtukane Mungu, kwa matendo au maneno. Sasa suala ni wewe unataka usimamie wapi katika hili suala - je utakuwa kati ya watu wachache ambao watamjibu shetani kwamba wapo watu kama wewe ambao come rain come sunshine watakuwa upande wa Mungu? Kumbuka Mungu anataka kumjibu Ibilisi kwamba katika kila generation ya wanadamu, watakuwapo ambao wataonyesha wako upande wa Mungu, hata kama ni angalau mmoja tu. Haitatokea wasiwepo kabisa, Labda wewe pia ulizaliwa kwa ajili ya hilo - uweze kuonyesha kwamba tuhuma za shetani dhidi ya Mungu ni za uongo kwa kuwa wewe pamoja na kuzaliwa katika generation iliyojaa maovu na mateso, bado unasimama upande wa Mungu.
Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa nitakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo.
Mkuu, nimejifunza mambo mengi sana kwa sababu niliamua kuwa open minded na kufanya discussion nyingi sana na Mashahidi wa Yehova. Hayo mambo niliyokutajia hapo juu wao watakuonyesha hata maandiko ili kukuthibitishia. Ushauri wangu kwako ni kwamba watafute ufanye nao discussion. Wala hawatakutoza fedha. Fanya hivyo, ukiona wanakupa majibu ya kuridhisha, japo siku ya kwanza tu, basi kubali kufanya discussion zaidi pamoja nao. Huenda ukapata majibu kwa maswali yote yanayokusumbua.
Wengi wanawadharau na kuwakebehi Mashahidi wa Yehova bila kujua wana ufahamu wa juu sana juu ya mambo ya Biblia. Ila inahitaji unyenyekevu sana kuwa tayari kuwasikiliza na kujadiliana nao haya mambo. Mkumbuke Naamani. Unyenyekevu ulimsaidia sana.
Kuna uzi humu ndani juu yao hata ilibidi nitoe post kuwaeleza watu ukweli. Angalia
Mahakama Urusi yapiga marufuku Mashahidi wa Yehova