Mkuu salute kwako ,
Nadhani wengi ambao walikuwa hawajamjua vyema Babu wanachanganya sana habari zake . Babu alivuma sana kipindi cha mtandao wa uwizi wa magari kutoka Kenya na kusini mwa Africa ,walikuwa wengi kina marehemu Nyaki, Oraa na wengine wengi waliotangulia mbele ya haki . Ukweli hawa mabwana mtandao wao ulikuwa mpaka ndani ya system ndio maana walifanikiwa sana. Miaka ya mwishoni mwa miaka ya 1990 Mambo yalibadilika biashara ile ikadhibitiwa kwa kiwango stahiki, ikapungua hivyo hawa jamaa wakabadili biashara ,wengine wakafungua magereji Arusha na Moshi na wengine wakamalizwa .
Babu amekoswa koswa sana ,na umahiri wake wa kukwepa na kushinda majaribu ndio uliomfanya akubalike na makundi mengine yaliyojitokeza kuefanya biashara zisizoeleweka.
Babu hakuwa bilionea hata siku moja ,Babu alikuwa middleman mzuri kwa maana wapo watu kwenye system walikuwa wanasafisha fedha chafu kupitia watu kama kina Babu . System ya utawala wa chama chetu wasingemwacha kama hakukua na watu kwenye system waliokuwa wanamtumia. Mifano ipo ya walioadhibiwa kutokana na kujiona wao ni zaidi ya system ya chama chetu. Nadhani unakumbuka mchezo wa cheusi chekundu maeneo ya kuelekea njoro kabla ya relini pale Moshi,sasa Babu alikuwa ni sawa na wale wachezeshaji kwani wasimamizi wa ule mchezo walikuwa wapo pembeni kumlinda mchezeshaji .Huo mchezo wa kukopesha na ku-grab ulikuwa ni mtandao mkubwa kuliko Babu ,Babu alikuwa anatangulizwa front coz alikuwa middleman .That issue ilikuwa kubwa zaidi ya kujua chanzo cha kifo cha Nyaga.
Moshi ni mji uliobahatika kuwa na middleman wengi ambao walijitahidi kwa nguvu zao kufikia level fulani kisha wabadhilifu wa mali za umma kupitia mfumo mbovu wa chama chetu kuwatumia . Hawa middleman baadhi yao baada ya kuwa mawakala wa fedha chafu wakajiona wao ni matajiri kuliko wenye mpini .Hili lipo wazi matajiri wa Moshi system ya utawala inapobadilika wengi wao ulikuwa ndio mwisho wao,na wanaporomoka kwa kasi ya concord -supersonic jet.
Utakumbuka era ya Mahita na Chicco ,wale waliokuwa karibu nao unawaona leo ? Sina haja ya kuwataja .
So kusema Babu alikuwa bilionea ni upotoshaji wa hali ya juu ,hakuwahi hata kumfikia Buni wa mailisita ambaye naye ni middleman wa aina yake .