Watu walikufa kwa sababu ya uzembe, wangeweza kuokolewa katika ajali ya ndege

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,011
4,165
Ndege ya Precision air iliyoanguka katika Ziwa Victoria Bukoba, Tanzania, November 6, 2022

Ndege ya Precision air iliyoanguka katika Ziwa Victoria Bukoba, Tanzania, November 6, 2022
Ripoti ya awali kuhusu uchunguzi unaoendelea kuhusu ajali ya ndege ya Precision nchini Tanzania inasema kwamba Maisha ya watu yangeokolewa endapo maafisa wa uokoaji wangeajibika kwa muda unaofaa.

Licha ya serikali kusema kwamba mawasiliano kati ya rubani na usimamizi wa uwanja wa ndege yalionyesha kwamba ndege ilikumbwa na usumbufu wa kutua kwa karibu dakika 20, hakuna hatua yoyote ilipangwa kuchukuliwa hata baada ya ndege kuanguka.
Watu 19 walifariki Novemba 6, wakati ndege ya precision yenye watu 43 ilipoanguka katika ziwa Victoria, Bukoba.

Wavuvi wanaotumia boti ndogo ndio waliokuwa wa kwanza kufika kwenye ndege hiyo na kusaidia kuokoa watu 24.

Ripoti inayodaiwa kuwa ya awali kuhusu uchunguzi huo, imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kulingana na ripoti hiyo, kuna vifaa vya uokoaji kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba, lakini wahusika hawakufika kusaidia katika uokoaji.

Polisi wa uokoaji walikosa oxygen, mafuta, walifika saa 5 baada ya ajali kutokea

Polisi wa kupiga doria baharini hawakupata taarifa kuhusu ajali hiyo, na walipopewa taarifa, walifika eneo la ajali saa tano baadaye bila ya Oxygen. Isitoshe boti la uokoaji halikuwa na mafuta ya kutosha kufanikisha shughuli hiyo.

Na baada ya ripoti kuenea kwenye mitandao ya kijamii, waziri wa habari, sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa ametetea serikali akisisitiza kwamba kwamba ilichukua kila hatua kuokoa Maisha, ikijiondolea lawama kwamba hali ya hewa ilibadilika ghafla na kwamba ndege ilizunguka kwa dakika 20 kabla ya kuanguka na kwamba zipo kanuni za kimataifa kuhusu uokoaji ambazo lazima zizingatiwe wakati wa ajali ya ndege.
21E393C0-73D8-4482-B3D6-C84371B32BBA.jpeg

Waziri Mbarawa alisema; “Wananchi hawa waliendelea na jitihada za kufungua mlango kwa nje, hali iliyompa ujasiri muhudumu wa ndege na abiria kuufungua mlango baada ya kuona nje ya ndege kuna msaada,” amesema Profesa Mbarawa.

“Nikweli kuwa mlango wa ndege iliyopta ajali ulifunguliwa na mhudumu wa ndege kwa msaada wa abiria. Hata hivyo, kama ripoti ya uchunguzi ilivyosema, wananchi waliokuwa wanafanya kazi shughuli za uvuvi, Jirani na eneo la ajali walifika eneo la ajali dakika 5 baada ya ndege kuanguka. Wananchi hao waliendelea na juhudi za kufungua mlango kwa nje. Hali hiyo ilisaidia kumpa ujasiri mhudumu wa ndege na abiria ndani ya ndege kufungua mlango huo baada ya kuona nje ya ndege kuwa kuna msaada ambao unaweza kuwasaidia.”

Serikali ya Tanzania imefutilia mbali ripoti inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Serikali inasisitiza kwamba hakuna mtu mwingine ana haki ya kutoa ripoti ya uchunguzi pasipo serikali.

Akizungumzia kuchelewa kwa vyombo vya uokozi, Profesa Mbarawa amesema katika ajali zinazotokea majini ipo miongozo na taratibu za kimataifa kuhusu uendeshaji wa mchakato huo na inayongozwa na mkataba wa kimataifa wa namna ya utafutaji na uokoaji majini wa mwaka 1974 ambao Tanzania imeridhia.

“Mkataba huu umetoa mwongozo kwamba, pale inapotokea ajali katika maji ya ziwa au bahari, inamtaka mtu au kikundi cha watu waliopo karibu na eneo la ajali kuwajibika na uokozi na kutoa taarifa kwa vyombo husika.

“Watu hawa wanawajibika kuendelea na uokozi hata pale inapotokea vyombo vya uokoaji vinavyofika katika eneo la ajali, huu ndio mwongozo sahihi unaotolewa na unaendana na utamaduni wetu kwamba, inapotokea ajali watu walio karibu husaidia kuwakoa manusura,”
amesema.

Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, wavuvi walioshiriki katika mchakato wa uokozi kwenye ajali hiyo ya ndege, walitimiza wajibu wa kizalendo na suala hilo linakubalika kimataifa.

Kuhusu Majaliwa (Jackson) kuwa shujaa, Profesa Mbarawa amesema “katika ripoti haikutaja mtu jina, bali imewatambua wavuvi hata mhuhudumu imesema muhudumu wa ndege haikutaja jina. Nimekuja hapa kuripoti kile kilichosemwa na kwenye ripoti.”

Itakumbukwa kuwa Majaliwa ni miongoni mwa vijana waliowaokoa abiria wa ajali ya ndege hiyo.
139E95A5-9600-4020-8A74-045A4CAFF638.jpeg

8108E092-BD92-406E-BE49-A68BAB161814.jpeg
 
Back
Top Bottom