Sababu za kupinga Bob Sambeke sio bilionea

chimbuvu,kama mimi nimeshinda bahati nasibu ya nyumba ya millioni 200,zikija kuthamanishwa mali zangu je nyumba yangu hiyo thamani yake itakuwa ni zero shilling?
wewe chimbuvu ukiamua tu kuniuzia lile vogue lako kwa millioni 5 tu,zinapothamanishwa mali zangu hiyo vogue unadhani itaelezwa thamani yake ni 5m?

ukinielewa hapa utajifunza kutizama thamani ya ndege zake na sio bei aliyonunulia,pia mawalla ametoa eneo kwa ajili ya hospitali la thamani ya millioni 500,unadhani mawalla alinunua eneo hilo kwa millioni 500?hata ukijumlisha na gharama za kuliendeleza?

TAFAKARI
 
Maada hii ni tamu kweli kiukweli mimi ni mchunguzi wa mambo sana lakini huyu jamaa hana pesa ya kuitwa bilionea alikuwa na hela ya kuishi na kufanya mambo yake yeye na familia yake hata sehemu alizoishi ni za kawaida ila pia alipataje hilo ndio swali gumu
 
mfano mmojawapo ni dalali wa viwanja anayejulikana kama Simba alikopa fedha akaweka nyumba anayoisha rehani siku ya siku aliposhindwa kulipa nyumba ikachukuliwa siku hizi anaishi Mwanama nyumba ya kupanga ya vyumba viwili,fikiria huyu katoka kwenye nyumba yake self contained,car park,gati kubwa na makorokoro kibao leo anakichukuliaje kifo cha Babu !

Mkuu Ngongo, asante kwa data, hizi hazina walakini, simba namfahamu sana hata nyumba yake iliyokuwa kule Njiro kwa msola, chini ya hadware ya jamaa flani anaitwa MRIMBA, naifahamu, jamaa kweli alivuma ghafla, mara tukasikia nyumba yake imeuzwa, ila jamaa ni mbishi yuko town bado!
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi, punguza vuta pumzi, na utulizane. Unao uhuru wa kupinga, maana tunajadiliana hapa. Sijabatisha. Duka lililo karibu na soko la Moshi ni la marehemu Mzee Sembeke (Baba yake Babu). Mzee Sambeke naye alikuwa na vijisenti kiasi wakati wa uhai wake. Na kama umenisoma vizuri, Babu hakuwa mtu kutegemea Baba au mama. Alikuwa anapambana kivyake, kuanzia miaka hiyo ya 80s.

Kwao wapi, Karanga? Mambo ya Karanga ni ya zamani, Babu alikuwa mara nyingi Arusha. Karanga anakaa mama yake na kaburi la Mzee Sambeke.

Pia soma post No 15.

Babu hela ilikuwepo, tena miiingi sana. Swali linatakiwa alizipataje?
Mkuu pale karanga ameangusha bonge la nyumba ila amepangishia wazungu na yeye akahamia AR.
 
Ile mall yake ya Rose Garden anashindwa kuijenga, eti mwenye Rose Garden anamroga usiku na mchana

Chezea Assey weye!!! Masharti yake hapandi gari ni baiskeli tu!!! Ha ha ha!!! Simo mimi!!! Ni mwisho wa habari!
 
All in all hata Bob Sambeke at al wangekuwa na utajiri wa trillions but hauna mashiko kwa kuwa umepatikana kihalifu. Watafaidika wale waliokopeshwa maana ndiyo zimeingia mitini kabisa!! Sasa wanagonga glass!!
 
Mkuu hao waliokopeshwa kama waliweka assets rehani,basi documents bado ziko kwenye miliki ya marehemu.Usidhani kwamba hakuwa na familia na watu wake.
 
prince-of-brunei-private-jet_600x450.jpg

vijay-mallya-the-liquor-mogul-who-also-owns-kingfisher-airlines-rides-this-boeing-727-he-has-been-known-to-use-his-jet-as-an-office-and-a-home-as-well-as-for-transportation.jpg

net-jets-ad-300.jpg

indian_billionaires_mukesh_600x450.jpg
 
All in all hata Bob Sambeke at al wangekuwa na utajiri wa trillions but hauna mashiko kwa kuwa umepatikana kihalifu. Watafaidika wale waliokopeshwa maana ndiyo zimeingia mitini kabisa!! Sasa wanagonga glass!!

Babu, pamoja na kwamba hakusoma saaaana, lakini alikuwa makini kwenye biashara. Kuna baadhi ya mali zitapotea lakini nyingi zitapatikana, na kama kuna mtu anataka kujidai mjanja basi inabidi awe makini.
 
Duh' ma billionaire magumashi.... na ndio maana hata vifo vyao vimekaa kiutatautata..

Copy: Chimbuvu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hao waliokopeshwa kama waliweka assets rehani,basi documents bado ziko kwenye miliki ya marehemu.Usidhani kwamba hakuwa na familia na watu wake.
Mkuu jmushi1, wachaga wengi mna sifa ya kuweka mambo sirisiri sana hasa kama ni ya kifisadi au yale ya utajiri wa giza kama wa akina Sambeke. Sambeke hakuwa na mke rasmi, ambaye tunategemea wakati mwingine ndiye anakuwa mtu wako wa karibu katika mambo yako. Sambeke pia kwa taarifa zisizo rasmi haelewani sana na ndugu zake wengine. Sina hakika kama kila deal zake ikiwemo mikataba ya mikopo ilikuwa wazi kwa ndugu na marafiki zake. Likewise kwa Nyaga jua hakuwa na uhusiano mzuri na familia yake karibu wote. Na mali zake zote hadi hela hakuna mwenye uhakika zilipo kwa 100%. Kwa mantiki hii ni lazima mali nyingi za wawili hawa (Nyaga na Sambeke) zitapotea. Kumbuka hata ndugu hawezi kuwa na uchungu sana na mali zako ambazo hakushiriki kuzalisha. Sana sana watapigania zile mali wanazoziona tu na zile wasizoziona au zenye ugumu kuzifahamu basi zitabaki sintofamu kwa maisha yote. I tell you kuna watu wanafurahia vifo hivyo maana wanajua kuwa deal zao na marehemu hao zipo to their advantage.

Jamani hata uwe na utajiri au mambo ya giza kiasi gani bora uoe tu. Ukiogopa kuoa descent lady ambaye hatakubaliana na deal zako basi tafuta hata mwanamke jambazi kama wewe!!!! Si tunasikia ujambazi mkubwa na akina mama wamo!! Tafuta basi hata mmoja uoe japo nayo ni hatari kubwa maana wote mnaweza kula shaba na watoto wakabaki yatima.
 
Babu, pamoja na kwamba hakusoma saaaana, lakini alikuwa makini kwenye biashara. Kuna baadhi ya mali zitapotea lakini nyingi zitapatikana, na kama kuna mtu anataka kujidai mjanja basi inabidi awe makini.

Suala la kuwa makini ni muhimu sana maana jua Bob alikuwa na ring lake kubwa sana ambalo huwa ukikosea mmoja wao unaipata fresh. Kwa mantiki hiyo kama kuna mali ambayo one of his ring anajua ilipo basi mwenye nayo ni lazima aisalimishe kabla hawajamtia shaba. Ila pia inategemea na usafi wa hao ring wake maana nao wanaweza zichukua na kukaa kimya nazo tu!! Si unajua kunguru wanaofanana wanaruka pamoja? Zulumati kwa zulumati.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu Spike Lee hawa jamaa wanamitandao yao sijui tusema ni mitandao ya kihalifu au nakosa neno sahihi la kiswahili.Ni hivi usifikiri hata mara moja Babu akikudai fedha zake atakupitisha kwenye mikono ya dola la hasha atapamaba na wewe binafsi au genge lake.Ndiyo maana nakwambia leo ukienda Njiro,Kimandolu,Baraa,Mitaa ya mjini kati na Sakina nyumba,magari na viwanja alizofanikiwa kuzichukua kupitia mikopo yake utashangaa ni kiasi gani serekali ilikuwa ikipoteza mapato yake.Vuta subira kidogo mtu mwenye uwezo wa kumkopesha Sunda unamweka daraja lipi ?,ngoja kidogo ni kwambie umewahi kujiuliza Sunda ana miliki asset za aina gani ?.Mtu mwenye uwezo wa kutoa mkopo wa tsh 10,000,000,000/= halafu serekali haina habari zake halafu leo unashangaa wanahabari wanamwita bilionea!.

Kifupi sana kuna baadhi ya banks za hapa Arusha na Moshi sipendi kuzitaja ulikuwa ukiomba mkopo na wakiona unaweza kuwasumbua wanakuelekeza kwa Babu Sambeke.Kama hiyo haitoshi pia alikuwa akiulizwa kama mkopaji alikuwa akidaiwa kabla hazijamkopesha sasa nadhani umeelwa maana ya mtandao pia nadhani umeelewa Babu alikuwa na uwezo kiasi gani.
Mkuu salute kwako ,
Nadhani wengi ambao walikuwa hawajamjua vyema Babu wanachanganya sana habari zake . Babu alivuma sana kipindi cha mtandao wa uwizi wa magari kutoka Kenya na kusini mwa Africa ,walikuwa wengi kina marehemu Nyaki, Oraa na wengine wengi waliotangulia mbele ya haki . Ukweli hawa mabwana mtandao wao ulikuwa mpaka ndani ya system ndio maana walifanikiwa sana. Miaka ya mwishoni mwa miaka ya 1990 Mambo yalibadilika biashara ile ikadhibitiwa kwa kiwango stahiki, ikapungua hivyo hawa jamaa wakabadili biashara ,wengine wakafungua magereji Arusha na Moshi na wengine wakamalizwa .

Babu amekoswa koswa sana ,na umahiri wake wa kukwepa na kushinda majaribu ndio uliomfanya akubalike na makundi mengine yaliyojitokeza kuefanya biashara zisizoeleweka.

Babu hakuwa bilionea hata siku moja ,Babu alikuwa middleman mzuri kwa maana wapo watu kwenye system walikuwa wanasafisha fedha chafu kupitia watu kama kina Babu . System ya utawala wa chama chetu wasingemwacha kama hakukua na watu kwenye system waliokuwa wanamtumia. Mifano ipo ya walioadhibiwa kutokana na kujiona wao ni zaidi ya system ya chama chetu. Nadhani unakumbuka mchezo wa cheusi chekundu maeneo ya kuelekea njoro kabla ya relini pale Moshi,sasa Babu alikuwa ni sawa na wale wachezeshaji kwani wasimamizi wa ule mchezo walikuwa wapo pembeni kumlinda mchezeshaji .Huo mchezo wa kukopesha na ku-grab ulikuwa ni mtandao mkubwa kuliko Babu ,Babu alikuwa anatangulizwa front coz alikuwa middleman .That issue ilikuwa kubwa zaidi ya kujua chanzo cha kifo cha Nyaga.

Moshi ni mji uliobahatika kuwa na middleman wengi ambao walijitahidi kwa nguvu zao kufikia level fulani kisha wabadhilifu wa mali za umma kupitia mfumo mbovu wa chama chetu kuwatumia . Hawa middleman baadhi yao baada ya kuwa mawakala wa fedha chafu wakajiona wao ni matajiri kuliko wenye mpini .Hili lipo wazi matajiri wa Moshi system ya utawala inapobadilika wengi wao ulikuwa ndio mwisho wao,na wanaporomoka kwa kasi ya concord -supersonic jet.

Utakumbuka era ya Mahita na Chicco ,wale waliokuwa karibu nao unawaona leo ? Sina haja ya kuwataja .

So kusema Babu alikuwa bilionea ni upotoshaji wa hali ya juu ,hakuwahi hata kumfikia Buni wa mailisita ambaye naye ni middleman wa aina yake .
 
Kuna watu wapo vizuri kujiadvertise na jamaa yaelekea alikuwa mtu wa advertisement sana
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Ni kweli kumekuwa na mtindo wa kuwakweza baadhi ya wafanyabiashara wa kawaida kabisa na kuwaita mabilionea.Mfano mzuri ni huyu Babu Sambeke.Marehemu alikuwa anafanya biashara kubwa ya kukopesha watu fedha binafsi nawajua baadhi ya wafanyabiashara wakubwa waliokopa fedha kwake 1.Ove huyu ni mfanyabiashara ya wa magari na pia anajishughulisha na uchinjaji wa magari kwaajili ya kuuza spares (us 450,000/=) 2. Sunda mfanyabiashara na mchimbaji wa madini ya Tanzanite (Tsh 2 bilioni) 3.Mmiliki wa Snow Crest kiasi hakijulikani. 4 Wachimbaji wa wengi wa Tanzanite wanadaiwa kiasi kikubwa cha fedha walichokopa kwaajili ya kuendesha mashimo ya mawe.

Bado kuna wafanyabiashara wengi wadogo wadogo walioporwa nyumba na magari kupitia mikopo ya Babu,mfano mmojawapo ni dalali wa viwanja anayejulikana kama Simba alikopa fedha akaweka nyumba anayoisha rehani siku ya siku aliposhindwa kulipa nyumba ikachukuliwa siku hizi anaishi Mwanama nyumba ya kupanga ya vyumba viwili,fikiria huyu katoka kwenye nyumba yake self contained,car park,gati kubwa na makorokoro kibao leo anakichukuliaje kifo cha Babu !

Babu Sambeke ni mfanyabishara mkubwa ingawa biashara yake haijulikana rasmi na serekali huyu jamaa ni bilionea usiangalie kigezo cha kumiliki ndege ukadhani wanahabari wamekurupuka la hashaa jamaa alikuwa akimiliki biashara kubwa sana yenye kumuingizia fedha nyingi pasipo kulipa kodi ya serekali.Inashangaza sana jambo kama hili linatendeka wazi wazi huku serekali ikikubali kuibiwa mapato yake kupitia ukwepaji wa kodi mkubwa.Nina hakika kufuatia kifo chake fedha zake nyingi zitapotea (kufa kufaana).

Mwisho serekali ijipange vizuri ihakikishe inapanue uwogo wa walipa kodi wake.Wafanyabiashara wakubwa aina ya Babu ni wengi lakini utashangaa serekali haina taarifa zao za mapato na matumizi.

Marehemu Wakili Nyaga huyu ni bilionea kwa vigezo vyote ukitaka kujua uwezo aliokuwa nao nenda Mawala estate ni zaidi ya eka 200 4 kilometa from city center kaweka miundo mbinu yote kuanzia barabara za lami,mtandao wa maji na umeme.Isitoshe Mawalla alikuwa na connection za matajiri wakubwa wa dunia kama Paul Tudor.Pia ana miliki estate huko South Afrika na Zimbabwe usishangae kwenye mazishi yake mawaziri walikuwa wanapigana vikumbo.

maelezo yako yanaridhisha, asante kwa ufafanuzi
 
Mkuu jmushi1, wachaga wengi mna sifa ya kuweka mambo sirisiri sana hasa kama ni ya kifisadi au yale ya utajiri wa giza kama wa akina Sambeke. Sambeke hakuwa na mke rasmi, ambaye tunategemea wakati mwingine ndiye anakuwa mtu wako wa karibu katika mambo yako. Sambeke pia kwa taarifa zisizo rasmi haelewani sana na ndugu zake wengine. Sina hakika kama kila deal zake ikiwemo mikataba ya mikopo ilikuwa wazi kwa ndugu na marafiki zake. Likewise kwa Nyaga jua hakuwa na uhusiano mzuri na familia yake karibu wote. Na mali zake zote hadi hela hakuna mwenye uhakika zilipo kwa 100%. Kwa mantiki hii ni lazima mali nyingi za wawili hawa (Nyaga na Sambeke) zitapotea. Kumbuka hata ndugu hawezi kuwa na uchungu sana na mali zako ambazo hakushiriki kuzalisha. Sana sana watapigania zile mali wanazoziona tu na zile wasizoziona au zenye ugumu kuzifahamu basi zitabaki sintofamu kwa maisha yote. I tell you kuna watu wanafurahia vifo hivyo maana wanajua kuwa deal zao na marehemu hao zipo to their advantage.

Jamani hata uwe na utajiri au mambo ya giza kiasi gani bora uoe tu. Ukiogopa kuoa descent lady ambaye hatakubaliana na deal zako basi tafuta hata mwanamke jambazi kama wewe!!!! Si tunasikia ujambazi mkubwa na akina mama wamo!! Tafuta basi hata mmoja uoe japo nayo ni hatari kubwa maana wote mnaweza kula shaba na watoto wakabaki yatima.

kweli kuoa muhimu, kuna umuhimu wake kwakweli
 
Sambeke hakuwa na mke rasmi, ambaye tunategemea wakati mwingine ndiye anakuwa mtu wako wa karibu katika mambo yako. .

Babu Sambeke alikuwa na mtazamo wa kipekee kuhusu ndoa! Alikuwa anasema wazi kabisa "siwezi kukaa na mwanamke mpaka anizeekee nikiwa namuona kwa macho"!

Hata hivyo ukiangalia watu wa mishemishe hawajakaa kifamilia sana kwa maana ya kuoa. Pengine wanahofia wajanja wanaweza kuchungulia kwenye mambo yao kupitia 'mama watoto'.
 
Back
Top Bottom