Sababu ya kusafirisha mafuta kutoka Uganda kupitia Bomba mpaka Tanga

maramojatu

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
1,170
1,535
Za weekend wanaJF,
Nimekuwa nikifikiria sababu inayotumiwa na nchi za Afrika kusafirisha mafuta kupeleka nchi za mbali bila kupata majibu.
Nilitegemea mafuta ya Uganda na Tanzania tungeya-,process hapa kwetu Africa sababu sisi ni watumiaji wa bidhaa hii muhimu halafu ndio tuuze nje. Lakini kinyume chake tunawauzia wenzetu mafuta ghafi halafu baadae watuuzie petrol na dizeli etc.
Hebu wanauchumi mtuelezee kwa lugha rahisi sababu ya kupeleka mafuta nje wakati mahitaji yetu ni makubwa.
Asanteni
 
Gharama ya kujenga kiwanda cha kuchakata hayo mafuta ni kubwa sana, na kiasi cha mafuta yaliyopo hapo Uganda hayataweza rudisha faida endapo yatasafishiwa hapo hapo Uganda,

Hope umenielewa japo mm sio mchumi,
Dangote anajenga chake kwa Dollar 12B, sawa na bajet ya mwaka mzima pale uganda na chenji unapata
 
Haya tunayoyatumia humu nchini yanafika bandarini yakiwa yamesafishwa?
 
Nadhani hoja yako ni sawa na kwa nini mkulima auze mahindi badala ya unga!
Lakini mkulima anauza mahindi baada ya kutoa yanayomtosha kula. Lakini mafuta tunayauza hata kabla ya kutoa tunayotakiwa kutumia kwanza. Shida ni nini hapo?
 
Lakini mkulima anauza mahindi baada ya kutoa yanayomtosha kula. Lakini mafuta tunayauza hata kabla ya kutoa tunayotakiwa kutumia kwanza. Shida ni nini hapo?
Uko sahihi sana! Kosa lililofanywa na hasa Tanzania ni kutokukiendeleza kiwanda cha kusafisha mafuta cha Aggip. Kiwanda kile angalau kingeweza kusafisha mafuta ya kutoshekeza Uganda na Tanzania!
 
Uliza kwanza kwa nini gas ilitoka mtwara kuja dar wakati kuna bandari mtwara. Jibu ni ufisadi tu.

Kwani gesi inayokuja Dar ni kwa sababu ya kuhitaji kusafirishwa kupitia bandari ya Dar?

Gesi inayotumika Dar ni kwa matumizi ya uzalishaji umeme, viwanda na makazi (kwa asimilia kidogo)...

Mtwara sijui Lindi huko plan ilikuwa ni kujenga LNG plant, yaani kiwanda cha kuikandamiza gesi ili iwe kimiminika kinachoweza bebeka na kuuzwa ughaibuni...
 
Back
Top Bottom