Sababu kuu zenye Mantiki zilizowafanya na zinazowafanya Wayahudi wengi Wasimuamini Yesu Kristo

Kwako mtoa maada, andiko lako ni zuri sana lakini naomba nikuambie kuwa dhambi kuu ya Wana Israel ni kutokuamini bila kuona au kusikia.Yani myahudi hawezi kuamini hivi hivi bila kuona au kusikia yeye mwenyewe.
Lakini pia unaitaji kuoata neema ya ajabu ili uweze kumwelewa Yesu Kristo na Mungu pia.maana mawaze yake ( Mungu) si kama mawazo ya wanadamu!
Ikumbukwe kuwa wayahudi walikataa uongozi wa kimungu wakataka waongozwe na mfalme wa kidunia kama mataifa mengine.soma kitabu Cha Nabii Samwel.....Mungu anamwambia : hawajakukataa wewe Bali wamenikataa mimi .Hii ni baada ya kuwa Wana Israel walimwomba Nabii Samwel awachagulie mfalme wa kuwangoza ,jambo hili likawa baya machoni pa Nabii Samwel .

Kwa hiyo Wayahudi mpaka sasa wanateseka Kwa sababu ya ubishi wao,kutokuamini,kukataa Mungu asiwaongoze Bali kutaka mfalme wa kidunia mwanadamu kama wao awaongoze.
Ndiyo maana kuzaliwa Kwa Yesu Kwa njia ya miujiza Yani bila baba wa kidunia wanamwona kama kamuungu Fulani hivi,au mwongo kabisa ( Yani mariamu mwongo,au Yusufu mwongo).Walitegemea azaliwe kibinadamu kabisa halafu ndani yake awe nabuwezo wa ajabu ,mfalme mwenye nguvu amabaye ataweza kupigana na maadui wote wa taifa la Israel na kuwaletea amani.

Sasa hawakuelewa hili:

1.masihi ambaye atazaliwa kama wao ( wanadamu) Hataishi milele.Hata kama atawaletea amani ,lakini ingekuwa amani ya kitambo tu maana huyu masihi mwenye asili ya kibinadamu sharti atakufa,na akishakufa nguvu ya utawala wake lazima ipotee.

2.Yesu Kristo ni masihi wa kweli ,mfalme wa kweli aletaye amani ya kweli .
Ili uweze kuelewana na maelezo yangu kwanza unatakiwa uamini kuwa Yesu alizaliwa,akafa ,akafufuka na akapaabinguni!! Kama huelewani na maneno haya itakuwa vigumu kuamini kwamba Yesu Kristo ni masihi wa kweli.
Yesu Kristo ndiye masihi wa kweli,mfalme wa ajabu Kwa sababu yeye alikuwepo,yupo na atakuwepo.Yani anao uwezo juu ya uzima na mauti.Alifufuka kutoka Kwa wafu .kule kuzimu Kwa siku tatu alikuwa na kazi maalumu ya kupambana na yule Joka aitwaye ibilisi na kumnyang'anya funguo za mamlaka.ndiyo maana huwa na mwita komandoo wa vita,jemadari asiyeshindwa .Ibilis mwenyewe alishangaa kumuona amemfuata mpaka kuzimu.Hahhaaaaa.vita ile ikuwa Tamu sana aisee.

Ufalme wa Mungu ,ufalme wa Yesu siyo ufalme wa kidunia Yani kwamba kuwepo na kundi la kijeshi au uwezo wa kijeshi wa kupambana na maadui.Hapana.kwanza ufalme wa unatakiwa ujue kwamba hapa duniani tuna wafalme wakuu wa wili amabao wanamungombania mwanadamu .Kila mfalme ana lengo lake

Kuna wafalme wa wili.Ibilisi ambaye ni shetani ,na Yesu Kristo akimwakilisha Mungu .Kila mfalme utamjua Kwa matendo yake.Wafalme Hawa wa wili utawala wao unaanzia katika ukimwengu wa roho.Yani kwenye moyo wako na akili zako .Wana drive binadamu from the heart and your mind. Kwa hiyo tunachokiona kikifanyika hapa duniani kimeanzia katika ulimwengu wa roho.yani mipango imeanzia kwenye moyo wako na kwenye akili zako.

Wafalme hao wawili ni maadui kweli kweli.uadui wao ukianzia mbinguni Tena sehemu takatifu.

Mfalme ibilisi anataka watu wamuasi Mungu kama yeye alivyomwasi Mungu.Yesu Kristo anataka watu wamtii Mungu .

Mfalme ibilisi yeye ufalme wake ni WA kuchukiana,kuuana,kuibiana,kulawitiana,Yani Kila aina ya maovu. mfano wa ufame wake ni huu.Ukitaka utajiri ibilisi anakuambua nitakupa lakini uzini na mama Yako,umtoe kafara mama ,baba au mtoto wako,umfanye msukule nduguyo.Mungu na Yesu Kristo ufalme wao ni WA amani.yani upendano wa ndugu .mfano wa ufalme wa kimungu au wa Yesu Kristo ni huu: ukitaka utajiri anakuambia nitakupa lakini Fanya kazi Kwa bidii,nenda kanisani,toa sadaka,wasaidie wajane na yatima ,kuwa na amani na watu wote .

Nitaendelea badaye ngoja niende kusali kwanza
Ila kumbuka hadi wewe kutafsiliwa maneno ya Mungu ujue kumepita LUGHA nyingi

Je kama lugha nyingine wameEdit maneno?
 
Kumbe yesu ni mungu Isaya 9:6 ndio mana mtu akishikwa na pepo ukimwambia kwa Jina la yesu pepo toka linatoka hapo hapo
 
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani.

Leo Taikon atajadili sababu zinazopelekea wayahudi wengi kutokumuamini Yesu Kristo Kama Masihi wao na waulimwengu.

Andiko hili lijadiliwe Kwa Hoja zisizo na mihemko ya kidini. Kama unajijua Akili yako imefungwa fungwa hii mada haitakuhusu.

Hivi uliwahi kujiuliza ni Kwa nini Wayahudi hawamuamini Yesu Kristo? Yaani Kwa nini wamuamini Musa, Daudi, yona, Daniel, Isaya, Ezra, Joshua, n.k lakini Kwa nini hawataki kumuamini Yesu Kristo?

Embu nawe Fikiria hapo. Kumbuka hata huyo Yesu naye NI Myahudi.

Je, ni Yesu pekeake aliyekataliwa na Wayahudi au kuna manabii Masihi wengine waliokataliwa n mayahudi?
Ikiwa wapo je nini sababu ya wao kukataliwa? Nisirefushe andiko.

Twende sasa!

Wayahudi wanasababu kadhaa za kutokumzingatia Yesu kama Masihi au Nabii aliyetabiriwa katika maandiko kaa sababu kuu zifuatazo;

1. Yesu Mnazareth Hakutimiza Unabii hivyo anakosa vigezo vya kuwa Masihi mtabiriwa.
Hapa kuna mambo ambayo Masihi aliyetabiriwa alipaswa kuyatimiza Siku atakapokuja. Mambo hayo ni pamoja na;

a). KUSHUSHA UTAWALA WA MUNGU NA KUKOMBOA WANADAMU
Masihi aliyetabiriwa moja ya majukumu yake akija ni kukomboa Wanadamu na kushusha utawala wa Mungu. Wayahudi hawamuamini Yesu Wa Nazareth Kwa sababu hakutimiza Jambo Hilo. Hakuushusha utawala wa Mungu na wala hakumkomboa Mwanadamu.

Hii ni Kwa sababu mpaka hapa tunapozungumza Bado Dunia haijakombolewa, madhambi ni mengi, na utawala wa Shetani ndio umetamalaki.

Soma utabiri wa Isaya juu ya Masihi atakayekuja kisha linganisha, je Yesu Mnazareth analingana na utabiri huo;

Isaya 9:6
6 . Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto wa kiume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

Ukichambua Unabii huo sentensi Kwa sentensi, je Yesu Mnazareth anatimiza Unabii huo. Embu tuone, "Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;"
Je Yesu alikuwa na uwezo wa kifalme began mwake? Je alitimiza vigezo vya kuitwa Mfalme? Labda Kwa vile hapa Tanzania kizazi cha sasa hakijaongozwa na wafalme. Lakini tunaweza kuchukulia mfano WA mamlaka ya Rais.

Je Yesu Mnazareth alikuwa anauwezo wa kirais, yaani mamlaka kama tuyaonayo Kwa Rais? Zingatia Mfalme ni zaidi ya Rais Kwa mambo mengi.

Ukisoma maandiko Yesu hakuwa na uwezo wowote wa Kifalme, alikuwa ni nabii kama walivyomanabii wengine.
Hivyo Sifa hii hakuwa nayo.
"Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani
"

Je, Yesu Mnazareth alitimiza Unabii wa kuwa na Sifa ya kuitwa Mungu mwenye nguvu? Je Yesu alileta Amani? Maana Unabii unasema ataitwa Mfalme wa Amani.

Je ni kweli Yesu alileta Amani Duniani? Jibu ni Hapana, Yesu Mnazareth hakuleta Amani. Msikilize Yesu mwenyewe;

Mathayo 10:34 BHN​

“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.​

Yesu hakuleta Amani Duniani isipokuwa Upanga. Hivyo anakosa kigezo cha Nabii aliyetabiriwa na manabii wa zamani.

Kwa tuliosoma Histori ya Ulimwengu. Ukristo ndio dini pekee iliyoua Watu wengi Duniani katika kuueneza.
Watu wengi wameuawa Kwa sababu ya Kristo au Kwa jina la Kristo. Hivyo hakuwa Mfalme wa Amani Bali alikuwa Mfalme wa machafuko.

Ukombozi uliolengwa na manabii waliotabiri Ujio wa Masihi ulikuwa ukombozi wa Kimwili. Lakini Yesu hakuja kukomboa yeyote Kimwili. Hiyo ni hoja inayofuata baadaye

b) MASIHI LAZIMA AZALIWE KATIKA UKOO WA DAUDI LAKINI YESU HAKUZALIWA KATIKA UKOO WA DAUDI.

Wayahudi wanamkataa Yesu Kwa sababu yupo Kinyume na Unabii wa Masihi aliyetabiriwa. Ndio maana wao wanamsubiri huyo Masihi Kwa jinsi vitabu vyao vinavyoeleza.

Maandiko yanaonyesha kuwa Yesu hakuwa Uzao wa DAUDI. Hii ni Kutokana na sababu zifuatazo;

I) Yesu alizaliwa pasipo na Baba.
Maandiko yanaeleza kuwa Yesu alizaliwa Kwa Njia ya Roho mtakatifu. Hana Baba wa kibinadamu. Jambo ambalo linampotezea Sifa ya kuwa Masihi aliyetabiriwa.

Wayahudi wanaeleza kuwa Masihi aliyetabiriwa angezaliwa kikawaida kama binadamu wengine tena angetoka katika Uzao WA Daudi. Yaani Baba yake lazima awe katika ukoo wa Daudi (Daudi mtoto wa Year).

Mwanzo 49:10 BHN​

“Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda, wala bakora ya utawala miguuni pake, mpaka atakapofika yule ambaye ni yake; ambaye mataifa yatamtii.​

Soma Unabii wa Isaya;
ISAYA 11
1 Kutatokea chipukizi katika kisiki cha Yese,
tawi litachipua mizizini mwake.
2Roho ya Mwenyezi-Mungu itakaa kwake,
roho ya hekima na maarifa,
roho ya shauri jema na nguvu,
roho ya ujuzi na ya kumcha Mwenyezi-Mungu.
3Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.
Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,
wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.
4 Atawapatia haki watu maskini,
atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.
Kwa neno lake ataiadhibu dunia,
kwa tamko lake atawaua waovu.
5 Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga,
uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.
6 Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo,
chui watapumzika pamoja na mwanambuzi.
Ndama na wanasimba watakula pamoja,
na mtoto mdogo atawaongoza.
7Ngombe na dubu watakula pamoja,
ndama wao watapumzika pamoja;
na simba atakula majani kama ng'ombe.
8Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyoka
mtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu.
9 Katika mlima mtakatifu wa Mungu
hakutakuwa na madhara wala uharibifu.
Maana kumjua Mwenyezi-Mungu kutaenea pote nchini,
kama vile maji yajaavyo baharini.
10 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka.
11Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani


Unabii huu unaeleza Sifa za Masihi atakayekuja, yaani sharti atokee Katika ukoo wa Daudi. Jambo ambalo Yesu Mnazareth maandiko yanaeleza kuwa hajatokea kwani hakuwa na Baba.

Hata Mariam mamaye Yesu angetokea ukoo wa Daudi bado isingemsaidia lolote Yesu kwani kiunabii au kimaandiko Uzao unatoka Kwa Baba.

Hoja hii inaungwa mkono na Wayahudi wengi na kufikia hitimisho kuwa Yesu sio Masihi aliyetabiriwa. Yesu hakuwa na Baba, huyo Yusufu ambaye ukoo wake umetajwa kwenye Biblia hakuwa Baba mzazi wa Yesu. Ndio maana alitaka kumkimbia Mariam.

Wayahudi wanadai kuwa Masihi angezaliwa kikawaida, Kwa kuwa Na Baba mzazi na Mama mzazi na sio kutumia njia ya miungu kutunga mimba. Jambo ambalo Wayahudi wanaliita ni dhana ya upagani wa Kirumi.

C) MASIHI LAZIMA AWARUDISHE WAYAHUDI WOTE WALIOTAWANYIKA DUNIANI WARUDI ISRAEL.
Yesu Mnazareth hakutimiza hilo. Wayahudi walichukuliwa uhamishoni huku na Huko. Na wapo wengine waliobakizwa Uyahudini.

Masihi aliyetabiriwa moja y majukumu yake ilikuwa kuwakusanya na kuwarejesha waisrael wote waliotawanyika warudi nyumbani Yesu hakufanya hilo. Hivyo anakosa Sifa za kinabii za Masihi aliyetabiriwa

ISAYA 11:
10 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka.
11. Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani.


Yesu Mnazareth hakumrejesha hata myahudi mmoja Israel. Hivyo anakosa Sifa za kinabii za Masihi.

Wakristo wanadai Yesu Mnazareth atatimiza hayo kwenye Ujio wa Pili Wakati upande Kwa Wayahudi na vyanzo vya Kiyahudi vinaonyesha kuwa MASIHI atatimiza utume wake Moja Kwa Moja. Katika Biblia hasa ya Unabii wa Masihi aliyetabiriwa hakuna dhana "Masihi Kurudi/kuja Mara yapili.

d) MASIHI ATAKUJA KUKOMESHA MAGONJWA, VITA, TAABU, NJAA N.K
Masihi aliyetabiriwa na manabii moja ya Kazi yake akija atakomesha magonjwa, Vita, Taabu, njaa na majanga mengine. Lakini Yesu Mnazareth hakukomesha chochote Kati ya hivyo kwani mpaka hivi leo, Mambo hayo yapo.
Hivyo anakosa Sifa za Masihi aliyetabiriwa.

Hoja ya kusema kuwa Yesu Mnazareth alikuja Kwa mambo ya ufalme wa Kiroho inazidi kumuondoa Yesu kwenye Sifa za Masihi aliyetabiriwa.

Labda tuseme, Yule Aliyetabiriwa na Yesu Mnazareth kuwa atakuja ambaye Wakristo wanamuita Roho mtakatifu ndiye Masihi ambaye kwa HAKIKA bado hajaja.

E) Masihi hataleta mambo ya utatu mtakatifu ambayo Kwa Torati ni Shirki, ibada za Sanamu.
Masihi ataleta ufalme wa Mungu, Haki yake, na utawala wake. Ataleta Amani Duniani. Hatakuwa sehemu ya Mungu, Ila atakuwa ni sehemu ya Uzao wa DAUDI. Utatu mtakatifu pekee yake unamuondoa Yesu Mnazareth katika Sifa za Masihi aliyetabiriwa na vitabu vya Kale.

Hao ni Wayahudi wanavyomchukulia Myahudi mwenzao yaani Yesu Kristo.

Maswali ambayo tunatakiwa tujiulize;

1. Ikiwa Yesu alitoka mbinguni, Kwa nini hakuandaa makao ya Watu wake Kabla hajaja Duniani kuwakomboa?
Badala yake Akaja Duniani kwanza ndipo akaenda kuandaa Makao. Hii maana yake ni nini?

Mungu aliumba makazi, Dunia ndipo akaumba MTU. Nuhu alijenga Safina ndipo akawakomboa Watu wake. Iweje Yesu aanze na ukombozi kwanz alafu ndio akaandae Makao?

2. Je Yesu na Ukristo, Yesu kama mwenye uwezo na Nabii. Kabla hajaja hakuona hatari ya Ujio wake kuwa mamilioni ya Watu watauawa kisa jina lake.

Yaani watalazimishwa kukubali jina lake kilazima hata kama hawataki? Kwa maana mpaka sasa jina la Yesu ndio linashikilia nafasi ya Kwanza Kwa Watu kuuawa ili tuu Watu waupokee Ukristo au waukatae Ukristo.

3. Iweje Yesu Mnazareth alishindwa kutimiza kazi yake Kwa miaka 33 aliyokaa Duniani mpaka awape majukumu Wanafunzi wake?

Je, hakuona kuwa kuna upotoshaji ungeweza kujitokeza Wakati ambapo hatokuwepo?
Ikiwa alilisha Watu zaidi ya elfu tano Kwa mikate mifano na samaki Wawili, akafufua Watu, na miujiza mingine, kumaanisha alikuwa na uwezo.

Ni kipi alishindwa kuhakikisha kila binadamu anayezaliwa automatically, amjue Mungu na habari zake pasipo kufundishwa na yeyote, ili kuepusha kile kiitwacho uongo na habari zake kuingiziwa hadithi za Uongo. Huo ungekuwa muujiza mzuri na wala asingewapa Wanafunzi wake kazi ya Kutangaza habari zake na habari za Mungu.

4. Yesu aliwaagiza Wanafunzi wake kuhubiri Injili. Je hakujua kuwa Miaka na miaka itapita, Vizazi na Vizazi vitapita.

Je, Vizazi ambavyo havikuwepo Wakati wake(Wakati WA Yesu) Sisi tukiwa miongoni mwa Vizazi hivyo, tunapata mamlaka ipi na uthibitisho upi kuwa Injili tuliyonayo ndio Ile aliyoitoa Yesu? Je, tutatumia kipimo kipi kuthibitisha ukweli WA kile tukisemacho?

5. Ikiwa lengo la Kufa Kwa Kristo ni kuwakomboa wanadamu na kuifia dhambi. Je kama dhambi ilikomeshwa na Kifo cha Yesu, ni kwanini Watu wanaendelea kutenda dhambi?

6. Swali la mwisho, ni Jambo Gani linalopelekea Wakristo kuamini Yesu Mnazareth ndiye Kristo/Masihi ilhali hajatimiza robo tatu ya Masihi aliyetabiriwa na manabii?

Kwa mfano, swali alilouliza Yohana Mbatizaji kuwatuma Wanafunzi wake wakamuulize Yesu kuhusu, Je Ni yeye Masihi au wamsubiri mwingine na jibu la Yesu kuwa viwete wanapona, vipofu wanatembea, viziwi wanasikia, na wafu wanafufuliwa. Je hiyo ndio ilikuwa misheni kuu ya Yesu?

Vipi kuhusu kuwarejesha Wayahudi Israel, vipi kuhusu yeye kuwa Mfalme na kuleta Amani na Haki Duniani, vipi kuhusu kuadhibu na kuhukumu?

7. Je Yesu anapowaambia Wanafunzi wake kuwa atarudi tena, je anaongea hayo Kwa kutimiza Unabii upi wa Masihi?

Maana hakuna sehemu Huko Nyuma ambayo ilitabiriwa ataondoka kisha atarudi tena. Ikiwa ndiye aliyetabiriwa, hiyo dhana aliitolea wapi?

Karibuni kwenye mjadala.
Mihemko hapa haitakuwa sehemu yake.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Swali namba tatu napingana nalo, nikimaanisha kuwa kristo alitimiza hilo.
Hata sasa watu wanazaliwa wanamjua Mungu, wala haihitaji kufundishwa ili umjue Mungu bali Mungu yupo kwenye dhamiri zetu wenyewe toka ukiwa kichanga.
Thibitisha kwa namna ipi
 
Umedadavua vyema Kwa kutumia akili za kibinadamu.

Hata hivyo HEKIMA Yako na ya wayahudi kibinadamu haitoshi kufungua codes za kinabii bila Mungu mwenyewe kukusaidia.

Baada ya wayahudi kumkataa Yesu Kwa ujinga wao, Mungu amejichagulia Taifa la AGANO ambalo atajidhihirisha Kwa Dunia kabla ya Yesu kuja kutawala Duniani Kwa miaka ELFU kama mtawala. Na Taifa Hilo ni TANZANIA.

Ameshazaliwa huyo Masih Jadal au Mpinga kristo ambaye atakuwa na sifa zote ambazo wayahudi walizitaka na watamuamini, Atakuwa mfalme na ataziunganisha Dini zote, na wataabudu ktk siku moja isipokuwa TANZANIA.

Atakuwa na nguvu ya kifalme na kusaidia kuunganisha mifumo yote ya nchi na kutumia Sarafu moja. Ataabudiwa wakidhani ni masihi kumbe ni mwana wa Ibilisi na shetani. Atakuwa akipata nguvu Kutoka pale vaticanoni.

Mungu tayari analitengeneza Taifa hili Ili kuandaa wamwaminio YESU kuwa salama dhidi ya utawala ujao wa mnyama.

ANGALIZO: HEKIMA ya Mungu ni Upumbavu Kwa WANADAMU, and vice versa is true.

Amen
 
Umedadavua vyema Kwa kutumia akili za kibinadamu.

Hata hivyo HEKIMA Yako na ya wayahudi kibinadamu haitoshi kufungua codes za kinabii bila Mungu mwenyewe kukusaidia.

Baada ya wayahudi kumkataa Yesu Kwa ujinga wao, Mungu amejichagulia Taifa la AGANO ambalo atajidhihirisha Kwa Dunia kabla ya Yesu kuja kutawala Duniani Kwa miaka ELFU kama mtawala. Na Taifa Hilo ni TANZANIA.

Ameshazaliwa huyo Masih Jadal au Mpinga kristo ambaye atakuwa na sifa zote ambazo wayahudi walizitaka na watamuamini, Atakuwa mfalme na ataziunganisha Dini zote, na wataabudu ktk siku moja isipokuwa TANZANIA.

Atakuwa na nguvu ya kifalme na kusaidia kuunganisha mifumo yote ya nchi na kutumia Sarafu moja. Ataabudiwa wakidhani ni masihi kumbe ni mwana wa Ibilisi na shetani. Atakuwa akipata nguvu Kutoka pale vaticanoni.

Mungu tayari analitengeneza Taifa hili Ili kuandaa wamwaminio YESU kuwa salama dhidi ya utawala ujao wa mnyama.

ANGALIZO: HEKIMA ya Mungu ni Upumbavu Kwa WANADAMU, and vice versa is true.

Amen
Kuna mvurugiko mkubwa ndani ya fuvu lako
 
Tukumbuke kuwa Yesu Kristo hakupendwa kabisa na; Mafarisayo na Waandishi ambao ndio wakuu wa mabaraza na Makuhani wakuu!
Hawa ndio walieneza dhana hii, ILA Yesu alifanya yote kama unabii ulivyonena na kutabiri.
 
Tukumbuke kuwa Yesu Kristo hakupendwa kabisa na; Mafarisayo na Waandishi ambao ndio wakuu wa mabaraza na Makuhani wakuu!
Hawa ndio walieneza dhana hii, ILA Yesu alifanya yote kama unabii ulivyonena na kutabiri.
Hao waandishi ndio wameandika biblia

Hapo imekaaje mkuu?
 
Katafute hiki kitabu cha Dr Myles Munroe utajibiwa maswali yako yote uliyo yauliza hapa.
images%20(12).jpg
 
Katafute hiki kitabu cha Dr Myles Munroe utajibiwa maswali yako yote uliyo yauliza hapa.View attachment 2577111
Dr Myles Munroe alikuwa mwalimu makini aliekamilika,,alikuwa smart,,muadilifu na mkweli.Ni moja ya watu ambao humaliza bando langu kwenye internet.Mungu ampumzishe mahali pema peponi na mwanga wa milele amwangazie. He was intelegent blackman of his kind.
Huu uzi nimeupitia ila una alama za mtu asie mkristo/mwamini na ndio maana niliupuuza ila na mimi nitajaribu kuweka maneno ili watu wasioijua biblia kiundani wapate ilim.
 
Back
Top Bottom