Sababu 6 Kwanini Rais Magufuli Hana Sababu ya Kuhofia Ripoti ya CAG; Itapelekwa Bungeni kama Kawaida

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
1065521

Na. M. M. Mwanakijiji
Rais Magufuli hana sababu ya kuhofia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Kinyume na hisia na maneno ya watu mbalimbali wanaotaka tuamini kuwa kuna hofu hiyo, Rais Magufuli ataacha ripoti hiyo iwekwe hadharani. Kuna sababu nyingi za kwanini ninaamini Rais Magufuli hatozuia ripoti hiyo au kusababisha isisomwe. Naomba hapa nidokeze sababu saba za kwanini Rais Magufuli hatozuia na wala hana sababu ya kuhofia mjadala wa ripoti za CAG Bungeni au mahali pengine.
  • Hayuko tayari kusababisha mgogoro wa Kikatiba usio wa kilazima
  • Cheo cha Rais, nafasi, madaraka na haki zake viko ndani ya Katiba. Bunge, Spika, haki, wajibu na madaraka yake vimo ndani ya Katiba. Cheo cha CAG, kazi na wajibu wake navyo vimo ndani ya Katiba. Hivyo hivi vyote japo ni tofauti tofauti bado vyote ni vyeo vya Kikatiba. Hata hivyo, CAG yuko chini ya Rais (Executive branch) wakati Spika yuko kwenye mhimili wa Utungaji wa sheria Bunge. Vyombo vyote hivi vinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka ya madaraka yao. Kutokana na hili Magufuli hana sababu ya msingi ya kusababisha mgogoro wa Kikatiba kwa kufanya chochote ambacho kiko nje kabisa ya madaraka na haki zake. Hivyo, ripoti ya CAG itapelekwa Bungeni kama inavyotakiwa; hakuna kuvunjwa Bunge wala nini. Spika anaweza asimpende Profesa Assad lakini hawezi kuzuia kazi ya CAG isifanye kazi.

  • Tayari ameshaacha ripoti za CAG kusomwa na kujadiliwa hadharani huko nyuma; hana sababu ya kuzuia sasa.
  • Ripoti za CAG zimekuwa zikitolewa na zimekuwa zikionesha kinachoendelea – kwa uzuri na kwa ubaya. Hakuzuia ripoti zilizopita sioni kwanini aamue sasa kuwa zisiwepo. Kama angetaka kutumia Bunge kuzuia ripoti za CAG angeweza kwani chama chake kinaongoza serikali zote mbili na zina wingi wa kutosha kufanya mabadiliko ya Katiba hata kufuta cheo cha CAG (chini ya Ibara ya 100). Kwa vile hakuna “movement” au mwelekeo wa kufanya jambo hili ni wazi hakuna sababu kubwa ya kuzuia ripoti za CAG kupelekwa, kujadiliwa au kuwekwa kadharani kwani Katiba imeweka mfumo wa kuziweka hadharani hata kama Rais atashindwa.

  • Kama Mtendaji Mkuu wa Serikali (CEO) ripoti za CAG zinamueleza kwa kina kinachofanyika ndani.
  • Rais Magufuli ndiye Afisa Mtendaji Mkuu wa serikali. Kama kiongozi mkuu wa serikali ambaye amekuwa akichukua hatua mbalimbali na kusimamia mambo mbalimbali yanahusisha mabilioni ya fedha ana maslahi makubwa ya kutaka kujua fedha inaingiaje na inatumikaje. Yeye ndiye anapaswa kujua fedha za walipa kodi zinaenda wapi, kwa vipi, kwa nani, na kwanini. Ripoti za CAG basi zinampa nafasi ya kujua mwanya wa ufujaji wa fedha za umma uko wapi, na hatua gani zichukuliwe. Ripoti za CAG basi ni kama taarifa ya madaktari bingwa ambao wanaeleza hali ya mgonjwa kwa kina na nini kinatakiwa kifanywe. Kuzuia, kukataa au kwa namna yeyote kuficha ripoti hizo hakutamsaidia yeye wala serikali itakuwa ni kama yule “mficha maradhi”. Kwa karidi anavyopenda ukweli sidhani kama haupendwi ukweli ukisemwa kuhusu serikali yake. Alitaka waandishi wa gazeti la Chama chake wajilipue kufichua uuzwaji wa mtambo wa kuchapa magazeti sasa kwanini leo aogope kujilipua kwa CAG? Huku ni kutokumuelewa Magufuli.

  • Magufuli halazimiki kuchagua upande kati ya CAG na Bunge; anatakiwa kutimiza wajibu wake tu wa Kikatiba.
  • Kama nilivyosema hapo juu vyeo vyote vya Rais, Spika na CAG ni vya Kikatiba ni wazi kuwa mtu yeyote makini ataelewa kuwa Magufuli halazimiki kuchagua upande kati ya malumbano na mgongano wa Prof. Assad na Spika Ndugai. Binafsi naamini ya Ndugai na Assad ni mambo binafsi kuliko ya kitaasisi. Na katika hili nakubaliana kabisa na wale wanaoona Ndugai anatumia madaraka yake kama Spika vibaya. Ndugai hana uamuzi wa kutopokea ripoti ya CAG; hana uamuzi wa kukataa kuijadili kwa sababu hampendi Assad? Na hana namna ya kutaka kuweka matakwa kwenye ripoti ya CAG ambayo hayajawekwa Kikatiba. Akitaka kufanya hivyo anapaswa kuzungumza na chama chake na wabadili Katiba kama nilivyosema hapo juu. Nje ya hapo, inabidi ajikaze kiume na kuukubali ukweli ulivyo. Hoja ya “udhaifu” siyo sababu ya msingi ya kuvuruga utaratibu wa Kikatiba; angetafuta kisingizio kingine kinachoweza kuonekana kinakubalika. Magufuli halazimi kuchagua upande kwani upande wake ulishaguliwa na Katiba. Anatakiwa kuufuata tu.

  • Profesa Assad anaweza bado kuweka hadharani ripoti hizo hata kama Rais na Spika hawako tayari kuzijadili.
  • Hadi hivi sasa ripoti ya CAG inaweza kuwekwa hadharani na Ofisi ya CAG kwani kazi yake yeye ilikuwa ni kuifikisha kwa Rais na Rais anatakiwa kuifikisha Bungeni. Kama Rais hatofanya hivyo – kitu ambacho sioni uwezekano wake kwa sababu za hapo juu; CAG ataipeleka ripoti hiyo yeye mwenyewe kwa Spika au Naibu wake (chini ya Ibara ya 143:4). Tukumbuke kuwa Katiba hailazimishi ripoti za CAG kujadiliwa; ni Kikwete ndiye aliyeanzisha utaratibu huu na kufungua kilichokuwa kinajulikana gizani. Mwenye kubeba lawama katika sakata hili hadi hivi sasa ni Ndugai na washauri wake. Bahati mbaya sote tunajua kuwa kuna wakati kutokana na wingi wao wabunge wa CCM wanafuata ‘party line’ hata kama jambo haliko sawa.

  • Mwanasheria Mkuu (AG) anatakiwa kubeba lawama kubwa zaidi
  • Kwa kushindwa kutoa ushauri sahihi kuhusiana na uamuzi wa Bunge kukataa kufanya kazi na “CAG” iwe kwa jina lake au cheo chake AG amewaweka vibaya Rais na Spika. Hili jambo lilitakiwa kutolewa ushauri mara moja na AG kwa kuweza kuona tatizo la Kikatiba na kiutendaji. Na kama alifanya hivyo na kupuuzwa basi alitakiwa ajiuzulu na kama hakufanya hivyo wakati anajua jambo sahihi lilikuwa ni lipi anapaswa kujiuzulu vile vile. Nje ya hapo, ni muhimu kuonekana amefanya jambo sahihi na liwe somo huko mbeleni.

Kutokana na sababu hizi sita ni wazi kuwa sioni sababu za msingi kwanini watu wanahofia sana na kuanza kudhania kila jambo baya kuwa Magufuli anahofia au ataficha ripoti za CAG. Hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo. Watanzania waondoe hofu ya hii migongano ya kawaida ya kikatiba kwani ni muhimu kwa demokrasia. Na watu wasihofu sana kiasi cha kuona kama mbingu inaanguka; kesho bado itakuwepo na jua bado litachomoza. Kwa maoni yangu ya kawaida basi sioni ni kwa namna gani Ripoti ya CAG imtishe Rais Magufuli kiasi cha watu kudhania mambo mengi. Watu wasije kuwa kama Chicken Little au "The Boy who Cried Wolf". Hili nalo litapita.
 
Hii Report ya wakati huu imegusa Manunuzi ya Ndege zetu ambazo ndiyo kilele cha uzalendo.

Mpaka sasa CAG kakataa kubadili wording kwenye Key Significant Weaknesses ambazo ziko related na manunuzi ya ndege za ATCL.

Hapo ndipo matishio yote yalipoanzia.

Unaambiwa shughuli kubwa ipo Kwenye gharama Za Ujenzi wa Majengo ya Makao Makuu ya Dodoma Na Taratibu Za tender kwa jumla

Namaanisha taratibu zote zimefuatwa Na Hakuna Ubadhirifu hahahah
 
Rekebisha heading yako. Sema, "ushauri kwa mh Rais kwa nn anapaswa kuwasilisha ripoti ya CAG bungeni".
Kama hahofii mbona katuma watu wake wa usalama wamwambie Prof. Assad ajiuzulu?! Sisi CAG akishurika au kuuwawa tuna nyie mnaotisha watu kila siku..
 
Umeandika vizuriiiii , tena sana, lakini Jiwe being a renowned dictator anaweza kuamua kufanya lolote in a lawlessness shithole country like ours!
Idd Amin alitawala Uganda kwa miaka 7 bila bunge... Dikiteita katili kuliko wote waliowahi tokea Africa!
 
Unaambiwa shughuli kubwa ipo Kwenye gharama Za Ujenzi wa Majengo ya Makao Makuu ya Dodoma Na Taratibu Za tender kwa jumla

Namaanisha taratibu zote zimefuatwa Na Hakuna Ubadhirifu hahahah
1. Matibabu ya Ndugai India - gharama sake kufuru tofauti na hata ya Nyerere St. Thomas
2. Ununuzi wa madege ni pasua Moyo
3. Maujenzi kibao na utaratibu wa ma tender ovyo kweli hata ujenzi wa Dodoma

Cha muhimu wasimdhuru CAG wetu maana wamemtishia sana na kumtaka ajiuzulu..
 
... kingine Rais ana kinga ya Kikatiba; hashtakiki kokote, na yeyote, wakati wowote hata baada ya kuachia madaraka. Mtu wa aina hii hata afanye madudu ya aina gani, kitu ambacho naamini Mh. wetu hawezi kufanya, hana sababu ya kuhofia chochote. Hivyo, ni rai yetu sote tumwombe Mh. Rais aiwasilishe ripoti ya CAG mbele ya Bunge ili, pamoja na mambo mengine, la muhimu zaidi iwe Public Document; umma upate wasaa adhimu wa kuisoma na kuijadili ili kujua matumizi ya resources za nchi yao.
 
Hili picha la kihindi mnaleta lakini ni john pombe asiemtaka assad , sababu Asad haelekezwi kwa remote na hata hili la kumtisha hadharani na peke yake ndio kwanza amekuwa strong. Magu akijerekbisha na swala la kujufanya perfect atakuwa raisi mzuri sana lkn ndio hvo
 
Na. M. M. Mwanakijiji
Rais Magufuli hana sababu ya kuhofia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Kinyume na hisia na maneno ya watu mbalimbali wanaotaka tuamini kuwa kuna hofu hiyo, Rais Magufuli ataacha ripoti hiyo iwekwe hadharani. Kuna sababu nyingi za kwanini ninaamini Rais Magufuli hatozuia ripoti hiyo au kusababisha isisomwe. Naomba hapa nidokeze sababu saba za kwanini Rais Magufuli hatozuia na wala hana sababu ya kuhofia mjadala wa ripoti za CAG Bungeni au mahali pengine.
  • Hayuko tayari kusababisha mgogoro wa Kikatiba usio wa kilazima
  • Cheo cha Rais, nafasi, madaraka na haki zake viko ndani ya Katiba. Bunge, Spika, haki, wajibu na madaraka yake vimo ndani ya Katiba. Cheo cha CAG, kazi na wajibu wake navyo vimo ndani ya Katiba. Hivyo hivi vyote japo ni tofauti tofauti bado vyote ni vyeo vya Kikatiba. Hata hivyo, CAG yuko chini ya Rais (Executive branch) wakati Spika yuko kwenye mhimili wa Utungaji wa sheria Bunge. Vyombo vyote hivi vinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka ya madaraka yao. Kutokana na hili Magufuli hana sababu ya msingi ya kusababisha mgogoro wa Kikatiba kwa kufanya chochote ambacho kiko nje kabisa ya madaraka na haki zake. Hivyo, ripoti ya CAG itapelekwa Bungeni kama inavyotakiwa; hakuna kuvunjwa Bunge wala nini. Spika anaweza asimpende Profesa Assad lakini hawezi kuzuia kazi ya CAG isifanye kazi.

  • Tayari ameshaacha ripoti za CAG kusomwa na kujadiliwa hadharani huko nyuma; hana sababu ya kuzuia sasa.
  • Ripoti za CAG zimekuwa zikitolewa na zimekuwa zikionesha kinachoendelea – kwa uzuri na kwa ubaya. Hakuzuia ripoti zilizopita sioni kwanini aamue sasa kuwa zisiwepo. Kama angetaka kutumia Bunge kuzuia ripoti za CAG angeweza kwani chama chake kinaongoza serikali zote mbili na zina wingi wa kutosha kufanya mabadiliko ya Katiba hata kufuta cheo cha CAG (chini ya Ibara ya 100). Kwa vile hakuna “movement” au mwelekeo wa kufanya jambo hili ni wazi hakuna sababu kubwa ya kuzuia ripoti za CAG kupelekwa, kujadiliwa au kuwekwa kadharani kwani Katiba imeweka mfumo wa kuziweka hadharani hata kama Rais atashindwa.

  • Kama Mtendaji Mkuu wa Serikali (CEO) ripoti za CAG zinamueleza kwa kina kinachofanyika ndani.
  • Rais Magufuli ndiye Afisa Mtendaji Mkuu wa serikali. Kama kiongozi mkuu wa serikali ambaye amekuwa akichukua hatua mbalimbali na kusimamia mambo mbalimbali yanahusisha mabilioni ya fedha ana maslahi makubwa ya kutaka kujua fedha inaingiaje na inatumikaje. Yeye ndiye anapaswa kujua fedha za walipa kodi zinaenda wapi, kwa vipi, kwa nani, na kwanini. Ripoti za CAG basi zinampa nafasi ya kujua mwanya wa ufujaji wa fedha za umma uko wapi, na hatua gani zichukuliwe. Ripoti za CAG basi ni kama taarifa ya madaktari bingwa ambao wanaeleza hali ya mgonjwa kwa kina na nini kinatakiwa kifanywe. Kuzuia, kukataa au kwa namna yeyote kuficha ripoti hizo hakutamsaidia yeye wala serikali itakuwa ni kama yule “mficha maradhi”. Kwa karidi anavyopenda ukweli sidhani kama haupendwi ukweli ukisemwa kuhusu serikali yake. Alitaka waandishi wa gazeti la Chama chake wajilipue kufichua uuzwaji wa mtambo wa kuchapa magazeti sasa kwanini leo aogope kujilipua kwa CAG? Huku ni kutokumuelewa Magufuli.

  • Magufuli halazimiki kuchagua upande kati ya CAG na Bunge; anatakiwa kutimiza wajibu wake tu wa Kikatiba.
  • Kama nilivyosema hapo juu vyeo vyote vya Rais, Spika na CAG ni vya Kikatiba ni wazi kuwa mtu yeyote makini ataelewa kuwa Magufuli halazimiki kuchagua upande kati ya malumbano na mgongano wa Prof. Assad na Spika Ndugai. Binafsi naamini ya Ndugai na Assad ni mambo binafsi kuliko ya kitaasisi. Na katika hili nakubaliana kabisa na wale wanaoona Ndugai anatumia madaraka yake kama Spika vibaya. Ndugai hana uamuzi wa kutopokea ripoti ya CAG; hana uamuzi wa kukataa kuijadili kwa sababu hampendi Assad? Na hana namna ya kutaka kuweka matakwa kwenye ripoti ya CAG ambayo hayajawekwa Kikatiba. Akitaka kufanya hivyo anapaswa kuzungumza na chama chake na wabadili Katiba kama nilivyosema hapo juu. Nje ya hapo, inabidi ajikaze kiume na kuukubali ukweli ulivyo. Hoja ya “udhaifu” siyo sababu ya msingi ya kuvuruga utaratibu wa Kikatiba; angetafuta kisingizio kingine kinachoweza kuonekana kinakubalika. Magufuli halazimi kuchagua upande kwani upande wake ulishaguliwa na Katiba. Anatakiwa kuufuata tu.

  • Profesa Assad anaweza bado kuweka hadharani ripoti hizo hata kama Rais na Spika hawako tayari kuzijadili.
  • Hadi hivi sasa ripoti ya CAG inaweza kuwekwa hadharani na Ofisi ya CAG kwani kazi yake yeye ilikuwa ni kuifikisha kwa Rais na Rais anatakiwa kuifikisha Bungeni. Kama Rais hatofanya hivyo – kitu ambacho sioni uwezekano wake kwa sababu za hapo juu; CAG ataipeleka ripoti hiyo yeye mwenyewe kwa Spika au Naibu wake (chini ya Ibara ya 143:4). Tukumbuke kuwa Katiba hailazimishi ripoti za CAG kujadiliwa; ni Kikwete ndiye aliyeanzisha utaratibu huu na kufungua kilichokuwa kinajulikana gizani. Mwenye kubeba lawama katika sakata hili hadi hivi sasa ni Ndugai na washauri wake. Bahati mbaya sote tunajua kuwa kuna wakati kutokana na wingi wao wabunge wa CCM wanafuata ‘party line’ hata kama jambo haliko sawa.

  • Mwanasheria Mkuu (AG) anatakiwa kubeba lawama kubwa zaidi
  • Kwa kushindwa kutoa ushauri sahihi kuhusiana na uamuzi wa Bunge kukataa kufanya kazi na “CAG” iwe kwa jina lake au cheo chake AG amewaweka vibaya Rais na Spika. Hili jambo lilitakiwa kutolewa ushauri mara moja na AG kwa kuweza kuona tatizo la Kikatiba na kiutendaji. Na kama alifanya hivyo na kupuuzwa basi alitakiwa ajiuzulu na kama hakufanya hivyo wakati anajua jambo sahihi lilikuwa ni lipi anapaswa kujiuzulu vile vile. Nje ya hapo, ni muhimu kuonekana amefanya jambo sahihi na liwe somo huko mbeleni.

Kutokana na sababu hizi sita ni wazi kuwa sioni sababu za msingi kwanini watu wanahofia sana na kuanza kudhania kila jambo baya kuwa Magufuli anahofia au ataficha ripoti za CAG. Hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo. Watanzania waondoe hofu ya hii migongano ya kawaida ya kikatiba kwani ni muhimu kwa demokrasia. Na watu wasihofu sana kiasi cha kuona kama mbingu inaanguka; kesho bado itakuwepo na jua bado litachomoza. Kwa maoni yangu ya kawaida basi sioni ni kwa namna gani Ripoti ya CAG imtishe Rais Magufuli kiasi cha watu kudhania mambo mengi. Watu wasije kuwa kama Chicken Little au "The Boy who Cried Wolf". Hili nalo litapita.
1: upotevu wa trilion 1.5 pia zipo bilion zingine kibao hazijulikani zilipo 2: Ununuzi wa ndege kuna ufisadi mkubwa 3: ujenzi wa Chato Airport upo ufisadi wa kutosha 4: ofisi ya Bunge upo ufisadi wa kutisha 5: zipo trilion kibao zimepotea ktk mazingira ya kutatanisha
 
Mkuu una roho ngumu kama ngozi ya kiboko! Katiba! Does the incumbent know there is a constitution? Au katiba ni kichwa chake?

I doubt whether it is you who wrote these rubbish, uko mbali sisi tulio humu tunapambana na hali zetu knowing there isn't a constitution here anymore!
 
Back
Top Bottom