Rwanda yapitisha mpango kujenga Kinu cha Nyuklia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,903
141,851
Haya maendeleo ya Ubungo fly over na SGR wapinzani kama Chadema wanalalamika eti wao wanataka maendeleo ya watu siyo vitu.

Rwanda imepitisha mpango wa ujenzi wa kinu cha nguvu za Nyuklia ili kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia na utabibu duniani, itasaidiwa na Urusi katika mpango wake huo.

Niko hapa Falcon najaribu kujiuliza tu mpango huo ungetangazwa na serikali ya CCM pale Ufipa pangekalika kweli?

Daudi Mchambuzi kama uko mitaa ya jirani karibu upate supu ya mbuzi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wajinga tu, maendeleo ya watu yanakujaje bila vitu kwanza? Utajenga nyumba ya kisasa mahali pasipokuwa na barabara, maji, shule?
Ukiugua utatibiwa vipi bila uwepo wa hospital au wao watatibiwa nje ya nchi na agakhan? Utanunuaje gari au pikipiki kama hakuna barabara.? Unajileteaje maendeleo bila nishati ya umeme?
 
Kinu cha nyuklia bongo mbona kipo!
Labda useme tu hicho cha rwanda kitakuwa kikubwa kushinda cha bongo.
 
[QUOTE="sheiza, post: 35729418, member: 27141 Unajileteaje maendeleo bila nishati ya umeme?[/QUOTE]

Ona mnavyojisahau. Kwani kule Mwalimu HEP wanajenga kiwanda cha konyagi ili mlevi wenu alewe kwa Bei nafuu?
 
Kwani Megastructures mlizopinga zisifanyike huzijui? Unajifanya JNHPP hujui kama ipo inakaribia kukamilika?
Kama hazigusi watu na haziangalii faida ya kiuchumi, Bali sifa,au ili aje akumbukwe, zisizo jali vipaumbele vya wananchi Bali watawala kutafutia sifa kupitia Kodi zetu ni badala ya kupeleka kwenye tija na ambazo si lazima Sana kwa Sasa ni lzm vipingwe.
 
Kwa hiyo mradi wa Sgr na JNHPP haitasaidia wananchi na hazitakuwa na faida kwa uchumi wa nchi?
 
Kwa hiyo mradi wa Sgr na JNHPP haitasaidia wananchi na hazitakuwa na faida kwa uchumi wa nchi?
Ungekuwa unajua uchumi ningekuelewesha,si kwamba sio muhimu sababu tayari mbadala upo yaani kuziboresha reli za zamani Kama ilivo sawa na kuziboresha dams zilizopo lengo kuu hizo pesa zikaguse maeneo yanayoweza chochea ukuaji wa uchumi ndani ya mda mfupi mfano miaka 4 tu hela yote iliyowekwa kwenye sgr, kwenye,bwawa,ikarudi Mara tatu tofauti na hio miradi ambayo yote tayari inayo mbadala wake,je kuna mizigo yeyeto imekwama kusafirishwa Hadi isubirie sgr?
 
Nawe ni mchumi mkuu?
 
Kwani Megastructures mlizopinga zisifanyike huzijui? Unajifanya JNHPP hujui kama ipo inakaribia kukamilika?
Mfano tungeweza kwenye kilimo tungeuwa mawe matatu kwa pamoja,kwanza kutatua shida ya ajira, kuongeza mauzo nje tukapata pesa nyingi badala ya kutegemea kukopa,tatu tungekuwa na ziada ya kutosha yaan malighafi na chakula cha kutosha.

Hizo megaprojects sio za kukamilika leo labda miaka 15 ijayo huku zikituachia ufukara wa kutosha Hadi tukamilishe kulipa madeni zimeshachakaa inabidi tukope tena kuzikarabati.

Kilimo kina ajira 80% machinga na bodaboda zimeongezeka sababu kilimo kimetupwa, sababu huwezi pata sifa au kukumbukwa kwa kuinua kilimo tofauti na ukijenga jengo,utakumbukwa kwamba jengo Hili lilijengwa na.. hata Kama halina faida kiuchumi
 
Back
Top Bottom