Ruvuma: Viongozi wa Dini CPCT watakiwa kutangaza amani na umuhimu wa kufuata Sheria za Nchi kwa waumini wao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Viongozi wa Dini zote Mkoani Ruvuma wanatakiwa kuwa mstari wa mbele Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutangaza umuhimu wa amani na kusaidia kutoa elimu kwenye maeneo tofauti tofauti ya nyumba za ibada kupitia mahubiri yao ili wananchi waweze kufuta sheria za Nchi na kuepukana na vitendo vya uhalifu.
332b1117-2efd-4840-841d-91fcb1400420.jpeg

57fa1e8d-c20a-4af8-bb53-f408b2cbe7d5.jpeg

Akizungumza mbele ya Baraza la Maaskofu Wapentekoste Mkoa wa Ruvuma (COUNCIL OF PENTECOSTAL CHURCH OF TANZANIA - CPCT) lililofanyika katika Ukumbi wa Herritage Cotage Msamala Wilaya ya Songea, Oktoba 12, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi wa Poliis (ACP) Marco G. Chilya akiwa Mgeni rasmi amesema "Viongozi wa dini ni nguzo muhimu sana katika kujenga tabia njema za watu , maadili ya jamii na kuandaa taifa la kesho kielimu na kiimani.

5d85723d-c530-483a-97e2-01e07b6e167f.jpeg








Ameongeza "Hivyo, kwa kutambua umuhimu huo tunawaomba sana ninyi viongozi wa dini mkawe mstari wa mbele katika kukemea mambo yote ambayo ni kinyume na sheria za nchi , Maadili ya jamii na Sheria za Mungu kwani watu wasipokuwa na hofu ya Mungu hupelekea ongezeko la Wahalifu na uvunjifu wa Sheria za Nchi na amri za Mungu , kama vitabu vya dini vinavyo elekeza."

Sanjari na hilo, Kamanda Chilya (ACP) ameto wito kwa kuliomba Baraza hilo la CPCT kuwa chachu ya kumuandaa na kumlea mwanadamu kuwa Raia mwema na mwenye hofu ya mungu , na pia iwapo mahubiri yatakwenda Sambamba na Matendo mema kwa kuwa matendo huleta mabadiliko ya haraka kuliko maneno matupu," alisema Kamanda Chilya.
174fa44c-74ea-4905-857a-937073ee5609.jpeg

87664176-43b6-4bad-ab93-11294926da37.jpeg
Kwa upande wa mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu CPCT Mkoa wa Ruvuma Mh, Askofu Edward Njiku ameshukuru uongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa umoja, mshikamano na utendaji wao wa kazi Kwa kuhakikisha jamii inakuwa salama na kuweza kuwachukulia hatua wale wote wanyelengo la kupotea amani Kwa wananchi na kuahidi kutangaza umuhimu wa amani Kwa waumini sambambana umuhimu wa kufuata sheria za Nchi na sio kujichukulia Sheria Mkononi

Chanzo: Dawati la habari Ruvuma
 
Back
Top Bottom