Ruvuma: Akamatwa kwa tuhuma za kuwachinja watoto watatu wa mke mwenza kisa mke mdogo kupendwa zaidi

Ruvuma: Akamatwa kwa tuhuma za kuwachinja watoto watatu wa mke mwenza kisa mke mdogo kupendwa zaidi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia Wende Luchagula, Miaka 30, Kabila Msukuma, Mkazi wa Kijiji cha Milonji kwa kosa la mauaji baada ya kuwa chinja watoto wa mke mwenzake watatu mpaka kufa.

Tukio hilo limetokea Julai 12, 2025 majira ya saa nane mchana huko Kijiji cha Milonji, Kata ya Lusewa, Wilaya ya Namtumbo ambapo mtuhumiwa alivizia mume wake na mama mzazi wa watoto hao ambaye ni mke mdogo wakiwa wameenda mnadani kisha akatekeleza tukio hilo la kuwachinja watoto watatu kati yao wawili wakiwa mapacha ambao ni Lugola Lutelemula Samweli (6), Kulwa Lutelemula Samweli, Umri miezi 8 na Doto Lutelemula Samweli Umri Miezi 8, wote wakazi wa Kijiji cha Milonji chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi.
WhatsApp Image 2025-07-27 at 10.12.46_ead611be.jpg

WhatsApp Image 2025-07-27 at 10.12.45_a4a1eb68.jpg
Taarifa kamili ni kwamba, mume wa mtuhumiwa huyo alikuwa ameoa wake watatu lakini alikuwa akimpenda zaidi mke mdogo na Watoto wake kitendo ambacho mtuhumiwa hakukipenda ndipo akavizia mume wake na mama mzazi wa watoto hao ambaye ni mke mdogo wakiwa wameenda mnadani kisha akatekeleza tukio hilo la kikatili la kuwa chinja watoto hao mpaka kufa.

Miili ya marehemu imekabidhiwa kwa familia kwa ajili ya taratibu za mazishi. Mtuhumiwa amekamatwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia Leyson Pauli Mkinga (44) kwa kosa la mauaji ya Adamu Alto Mkinga Chengula (68) mkazi wa Kijiji cha Lihale – Mbinga kwa kumvunja shingo/kunyongwa hadi kufa.

Tukio hilo lilitokea Julai 7, 2025 majira ya saa mbili asubuhi huko Kijiji cha Lihale, Kata ya Mkako Wilaya ya Mbinga ambapo mtuhumiwa akiwa na mwenzake Dastan Mkinga, mkazi wa bombambili, mjukuu wa marehemu ambaye alikimbia baada ya kushirikiana kufanya tukio hilo walifika nyumbani kwa marehemu wakimtuhumu kuwa ni mchawi kisha kufanya tukio hilo la mauaji na kumuweka ndani ya zizi la mbuzi lililopo katika nyumba aliyokuwa akiishi marehemu na kutoroka kusikojulikana.

Baada ya kutokea tukio hilo Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa hao na ilipofika tarehe 24.07.2025 majira ya saa mbili asubuhi huko eneo la Ruhuwiko tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye ni Leyson Pauli Mkinga (44) na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa wa pili zinaendelea ili wote waweze kufikishwa mahakami kujibu tuhuma zao.

Sambamba na hilo pia Julai 20, 2025 majira ya saa mbili usiku huko barabara ya Tunduru - Songea katika kijiji cha Hulia, Kata ya Namwinyu, Tarafa ya Matemanga Wilaya ya Tunduru Gari lenye namba za usajili T.355 DLM Youtong mali ya Kampuni ya Selous Express inayomilikiwa na Omary Msigwa likitokea Songea kuelekea Dar - es - Salaam likiendeshwa na Hussein Omary Choka (53), mkazi wa Songea Matarawe likiwa na jumla ya Abiria Hamsini na Nne (54) liliwaka moto ambao ulioanzia kwenye tairi ya nyuma ya ndani ya difu na kupelekea gari lote pamoja na mizigo ya abiria kutekete, katika tukio hilo hakuna madhara yaliyotokea kwa abiria.

Chanzo cha moto huo kimesababishwa na kupasuka tairi la nyuma la ndani kwenye difu upande wa kulia na kuwaka moto na kusababisha moto kuenea kwa kasi na gari lote kushika moto.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa upande wa mafanikio yaliyopatikana kipindi cha Mwezi Julai 2025 kutokana na kufanya Doria, Misako na Operesheni maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma ya kuwasaka na kuwakamata wahalifu ambao wanajihusisha na matukio ya Uvunjaji na wizi wa mali za watu, limefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 40 pamoja na mali za wizi ambazo ni Televisheni 42, Pikipiki 05, Radio 10 na Solar Pannel 05 ambazo ziliibiwa maeneo katika maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma.

Vilevile katika Opereshini hiyo Julai 7, 2025 huko Kijiji cha Likuyusekamaganga, Wilaya ya Namtumbo Jeshi la Polisi kwa kushilikiana na Kikosi Kazi Maalum cha Kudhibiti Biashara Haramu ya Nyara za Serikali lilifanikiwa kumkamata Rajabu Ibrahimu Nihuka (53), mkazi wa Likuyesekamaganga akiwa na Vipande vya Vyuma 37, Fataki, Baruti njiti 33 na msumeno, alizokuwa akizitumia katika shughuli za uwindaji haramu akiwa amehifadhi kwenye chumba chake anacholala.

Operesheni zinaendelea kufanyika na Watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linatoa wito na kuwahasa wanandoa wote ambao wameridhia kuolewa kwenye ndoa ya zaidi ya mke mmoja kuhakikisha wanakuwa wavumilivu na kutokuwa na wivu wa kupindukia baina yao na pale inapotokea migogoro yoyote ndani ya ndoa zao nawashauri kutumia njia sahihi ya kutatua migogoro hiyo wao wenyenye au kuwashirikisha viongozi wa dini au wazee mashuhuri kusaidia kutatua migogoro hiyo kwa amani.

Pia Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wamiliki na madereva wa vyombo vya moto kuhakikisha wanakuwa na ukaguzi wa mara kwa mara katika vyombo vyao kabla ya kuanza safari na baada ya kumaliza safari pamoja na kufuata Sheria na kanuni za usalama Barabarani ili waweze kuepukana na ajali ambazo zinaweza kuepukika.

Aidha, katika kuelekea Uchaguzi Mkuu Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa uhuru, haki, amani na utulivu kwa kipindi cha kampeni, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi na wale watakaokiuka sheria tutahakikisha tunawashughulikia haraka iwezekanavyo.

Pia niendelee kuwakumbusha Wananchi na wakulima wote mkoani Ruvuma kujihadhari na matapeli ambao wameanza kuja mkoani kwetu kipindi hichi cha mavuno wakijifinya wanunuzi wa mazoa kisha kutapeli wananchi, niwatake kutokukubali kutapeliwa kwa namna yeyote ile na endapo mtabaini mtu au watu kufanya vitendo hivyo katika jamii zetu toeni taarifa za haraka kwa uongozi wa Serikali za mitaa/vijiji au Jeshi la Polisi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo ya sheria kwa hatua zaidi.

Pia soma > Aua watoto watatu wa mke mdogo kisa wanapendwa zaidi

r.jpg

rr.jpg

rrr.jpg
 
Mhhh mhhh mhhh imagine anaenda kufungwa kifungo cha maisha tu anakula bure gerezani
 
Back
Top Bottom