Hanzu Runi
Member
- Dec 28, 2014
- 49
- 34
Kwa hiyo wewe unachosema au unachodhani ni kipi?
Kwamba huyo balozi hajafa kwa kupigwa risasi, siyo?
Kwamba dunia nzima imedanganywa, siyo?
Miaka kadhaa imepita kipindi nilimualika jamaa nyumbani. Katika pitiapitia zake kwenye vitabu vyangu akakikuta kimoja kuhusu biashara ya utumwa. Ni moja kati ya vitabu vya kizamani, picha za kuchora, hata hivyo, zama za utumwa hususan Afrika Mashariki, teknolojia ya picha ilikuwa bado. Jamaa alikuja juu: "unaona njema za wazungu bwana! Wanataka kutuchonganisha na Waarabu, hivi huyo alichora picha hizi alikuwa wapi kama kweli kulikuwa na ukatili wa namna hii? Hawa jamaa wanataka tuuchukie Uislamu tu!"
Ilikuwa haijawahi kuingia akilini mwangu kumbe kwa mujibu wa Ngano za Njama (conspiracy theories) Utumwa haukuwepo kwani kusema ulikuwepo inapelekea maswali kuhusu kuingia kwa dini! Ghafla historia imegeuzwa vita vya kidini. Hayo hayo yalinikuta tena nilipowapeleka wanangu Makumbusho ya Utumwa, Bagamoyo. Mmoja wa wageni tuliyemkuta huko alininong'oneza: "kaka, unaona vita ya mzungu dhidi ya Uislam?"
Hivi ndivyo tulivyo, jambo kama hatulipendi na aidha linakinzana na imani tulizojenga, linatafutiwa sababu kwamba halikutokea. Mayahudi ninawasifu kwa msimamo thabiti walionao kuhusu gharika (Holocaust) waliyopitia na kupigania haki ya kihistoria kwamba kumbukumbu ya Shoal isifutike daima haswa katika zama juzi za Ngano za Njama. Wengine bado tunaamini kwamba kuzungumzia madhila ya historia ya Utumwa ni ngano dhidi ya dini fulani.
Kibaya zaidi, hata kumbukumbu za nyaraka ya biashara hii pale Jumba la Ajabu ziliuzwa kwa maafisa wa Ubalozi wa Oman kwa makasha ya tende. Ndiyo: tende! Kuondoa ushahidi katika kutengeneza Ngano za Njama. Ipo siku wanetu au vizazi vyao, wataambiwa kwamba Utumwa haukuwahi kutokea ni njama tu za kutuchonganisha na jamii za Maburushi na Waarabu wa Igunga, Mpanda mpaka Kipili, walishuka tu kwa kudra za Manaani kuleta neema ya Dín.