Russia Vs Ukraine hakuna mshindi wa Vita ila kwa Haraka Urusi amepoteza in reality

Ungeandika vita ya NATO na Russia sio Ukraine, Ukraine wanatumika tu kama uwanja ila kama wao hawana ubavu huo ni West na Russia, Mwisho wa siku walioumia ni Ukraine wameharibu maisha yao kwa maslahi ya wachache hasa UK wao nia yao kudhoofisha EU ili wao warudi juu na ushawishi kama walikuwa wanauchungua na EU wasingejitoa huko hawa UK ogopa sana wana fitna kama Simba na Yanga.
 
Hebu fafanua, mfano hii vita ya Ukraine inapochelewa kuisha Mtusi anaingiza vip pesa?
Bei ya mafuta na gesi zipo juu jamaa anapiga pesa
Bei za ngano zipo juu na unajua RUSSIA anauza sana ngano mashariki ya kati na afrika kwakiasi kikubwa
Jamaa kazorotesha usafirishaji wa mazao pale UKRAINE inamaana atakua anauza sana yeye nje kuliko UKRAINE ambae hana tena bahari yakusafirishia hayo mangano ngano nk
RUSSIA hakukurupuka aliposema anadeal zaidi na mashariki ya UKRAINE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.

USA Anza Lia pesa za msaada aliye tenga kwenye vita zinanza Kwisha na dalili ametuma 150 million msaada wa silaha ndio wa chini kabisa.

Mrusi wafilisi hao wajue vita so Lele mama
 
Bei ya mafuta na gesi zipo juu jamaa anapiga pesa
Bei za ngano zipo juu na unajua RUSSIA anauza sana ngano mashariki ya kati na afrika kwakiasi kikubwa
Jamaa kazorotesha usafirishaji wa mazao pale UKRAINE inamaana atakua anauza sana yeye nje kuliko UKRAINE ambae hana tena bahari yakusafirishia hayo mangano ngano nk
RUSSIA hakukurupuka aliposema anadeal zaidi na mashariki ya UKRAINE

Sent using Jamii Forums mobile app
Russia si kazuiliwa kuuza bidhaa zake nje, sasa anapigaje hela? Au me ndo sielewi
 
Bei ya mafuta na gesi zipo juu jamaa anapiga pesa
Bei za ngano zipo juu na unajua RUSSIA anauza sana ngano mashariki ya kati na afrika kwakiasi kikubwa
Jamaa kazorotesha usafirishaji wa mazao pale UKRAINE inamaana atakua anauza sana yeye nje kuliko UKRAINE ambae hana tena bahari yakusafirishia hayo mangano ngano nk
RUSSIA hakukurupuka aliposema anadeal zaidi na mashariki ya UKRAINE

Sent using Jamii Forums mobile app
mrusi anakula hasara kwa kuuza vitu kwa bei ya chini ila wanaonunua akina China na India ndo wanalamba dume
 
Twende kazi
IMG_20220531_151650.jpg
 
Habari za wakuu hapa ni vema uzi uachwe kuonesha nani kapoteza kwa namna tofaut tofauti,

Kuna Nyuzi nyingi Sana hapa ila huu utakuwa wa kitaalamu Na shuhuda nilizoshuhudiwa siyo kwa kusimuliwa

Wengi wameeleza chanzo cha Vita hii ila kwa hapa naonesha Matokea tu

1. Mpaka sasa week Jana natoka Moscow kulikuwa Na hali Ya sintofahamu juu Ya majenerali wanaokufa vitani,
Putin amepangua walinzi wake mara nne tokea vita imeanza, kutokana na kuhofia Usalama wake ,
2. Kuna Uhaba wa Bidhaa katika supermarkts na zimebaki zilizokaribia kuisha Muda wa matumizi,
3.mpaka tarehe 24/03/2022 warusi 1200 walikuwa wakipinga na kuandamana kukataa vita wamefungwa magerezani na watakuwa na kesi za kujibu

4. Wanajeshi wanaokufa ni wengi sana wa Urusi takriban wanajeshi 7000 wameuwawa kwa namba sahihi, Hii ni kwasababu wengi wao hawakuwa tayari na vita hii hawakupenda,

Ukawa mzozo mkubwa wa warusi kutengwa na Dunia

Waliosafiri Au waliobahatika Kusafiri wanaelewa hapa nikisema,

-Visa card yako haifanyi kazi,
-Hutaweza kulipa Au kulipwa na wadeni wako kwakuwa benki yako Iko disconnect
-hutapata visa Kwenda sehemu kadhaa Duniani hata Kama una maslahi huko
-Majumba Au mali ulizonazo zinawekwa rehani

Hayo ndo wanapitia warusi..

Suala la kutengwa Duniani kuhusu Biashara limemuumiza sana Urusi

1.Kuna nchi ambazo zilitaka kuonekana Neutral Kama India Lakin hakuna wakubishana na Dunia akaweza,

Natoa mfano tu

India na Marekani na Kwanini India hawezi poteza uchumi wake eti Kisa Ushikaji na Urusi

Watu wanadhani India ana uwezo wa kutenda Kunyume na USA.
Hebu tuangalie hapa.
Biashara kati ya India na Russia ni US$ 8 billion,
Kati ya hizo, india anaingiza US$ 2.6 wakati Russia anaingiza US$ 5.48 billion.

Biashara kati India na US ni US$ 113.391
Kati ya hizo, India anaingiza US$ 73 billion, wakati US wanaingiza over US$ 40 billion.

Yaani India abomoe uchumi wake kwa ajili ya Russia.
Kati the world largest trading partners 20 wa India duniani, Russia hayupo kabisa, halafu mnamuamini India akisema yeye hapangiwi cha kufanya...mnataka afee?.

Kabla ya kushabikia au kuyaamini maneno au taarifa zinazichapishwa. Huwa ninawafundisha watu kuwa siku zote kabla ya kuelezea maoni yao, au kuamua ku side na jambo, basi wawe wanaenda na facts zao, hata kama mhusika ndiyo anaongea, wewe just deal with the facts, the numbers, the data

Hivi India kujifaragua kwamba atanunua mafuta ya Urusi ni ya Muda tu!



Watu huwa wanaamini kuwa China na Marekani ni maadui. Siku zote nimekua nikisema China kamwe si aduiwa US. Wametuaminisha hivyo ila mimi nimegoma kuliamini hilo. Hao ni greatest partners na wanategemeana in so many ways baada ya US kuhamishia kule technolojia zake na viwanda vyake vingi kwa lengo la kupata cheap labours na masoko ambayo US asingeweza kukubalika.

Kwa kufanya hivyo aliondoa influence ya Russia kwa China. Mahusiano ya Russia na China yapo masikioni na kwa maneno zaidi, wakati mahusiano kati ya China na US ni ya dhahiri ingawa watu hawaoni, sababu ni ya kimkakati na kujizatiti zaidi. Hata ukiangalia among the Chinese wenyewe, wananchi wana prefer kuwa karibu zaidi na USA kuliko Russia.

Mwaka 2020 kulikua na Chinese 3.70+ milion wanaoishi USA, Wakati wachina waliokua wakiishi Russia mpaka mwaka 2021 walikua ni 39,000+ tu. Mind China na Russia anayesemekana kuwa greatest partner ni majirani wanao share border, inazidiwa hata na Japan ambaye ni taifa hasimu la Jadi la China lakini ndani ya Japan kuna Wachina 770,000+.

Hata Mongolia kuna Wachina wengi kuliko Russia, Mongolia kuna Wachina takribani 1.3 milion.
Hilo litakupa mwanga wa kujua kama kweli ni adui US na China ni maadui au laah.

Katika list ya Major trading Partner wa China Duniani, Marekani ni namba moja, halafu kuna European Eunion then kuna South Korea na Japan, wote hao ukiwataja unamtaja Marekani. US ndiye kampa mchongo China wa masoko hayo, ndiye aliyempa teknology, mitaji na viwanda na ndiye aliyewaambia jao wampokee.

Hata ukija kwenye mahusiano ya kijeshi, miongoni mwa partners watatu bora wa China, US ni mmoja wapo, ndiye anayempa technolojia za vifaa vya kijeshi na kubadilishana taarifa za kimafunzo na kimbinu...bado ni maadui kweli hao?

Uadui wa China na Marekani ni wa kutengenezwa tu.

USA siyo fala, hafanyi hizo investment ili kujiua, bali anajizatiti. They are there to stay, wamemtengeneza China ili kutoa sehemu ya wasiompenda kwenda ku ventilate ili wasije wakavimba wakapasuka wakakufa.

USA anawapenda sana mpaka anajitengenezea adui mdori ili tu watu wafurahi.

US anajua hapendwi na interests zake zinawindwa kote duniani, hivyo basi, kupitia mitaji, viwanda, technology etc alizompatia China anakua amezipaka rangi na logo ya China biashara na products zake ma hivyo kuweza kuuza Russia , Iran na sehemu zote ambazo mmarekani hakubaliki, amnako wanamuona China kama mkimbozi na mbadala wa Marekani. Wasilolijua ni kuwa US anamtumia China.

UN kwenye mzozo wa Ukraine wamepiga kura ya kuweka azimio la kuitenga Russia kuhusiana na kitendo chake cha kuivamia Ukraine, nchi 141 ziliunga mkono azimio hilo, nchi 35 hazijupiga kura kati ya nchi zilizopiga kura, nchi tano zilipiga kura kupinga hilo azimio na hovyo kuiunga mkono Russia, nchi hizo ni Russia yenyewe, Belarus, Syria, Eritrea and North Korea._* China ambaye anasemekana ndiye adui namba moja wa US na rafiki wa damu wa Russia hayupo hapo.

Watu wanatumia elimu zao, kufanya future predictions, innovations, management, productions, strategising and so so.. aisee, sisi ndiyo kwanza tunatumia vikao bungeni kuponda elimu na kuifubaza, pambavu zetu sisi.

Hivo China Kama ni mshkaji wa Russia asinge sita

Kuhusu kulipa Kwa Ruble Mafuta ya Urusi

Tukubali Urusi alikuwa Namba one kuuza Ulaya mafuta na gesi haina Ubishi ila kumbuka mwenye Reserve kubwa ya Mafuta Duniani ni Venezuela, na Iran Yuko miongoni mwa wenye reserves kubwa


Ally wa US Yaan UK Kalipa deni la $400M kwa IRAN na watu wake ma spy wawili wameachiwa sasa kinachofuata watamfungulia vikwazo na wanunue mafuta yake .....kuziba pengo la ya Rusia ....Marekani nae kamaliza vikwazo vya Venezuela ili akombe mafuta...

Boris wa UK alienda arabuni pamoja na kwamba mfalme kanyonga watu 81 Jumamosi Ya week kadhaa zilizopita LAKINI MAFUTA YANAFUTA DHAMBI HIYO NA LEO NAJUA MFALME ATAMWAMBIA PM KUWA HAKIKISHA CHELSEA ANAINUNUA MTOTO WA DADA YANGU...KESHAWEKA MEZANI £2.7B Sawa na $3.5B

Leo UMOJA wa Ulaya pamoja na G7 wamemwambia Urusi we can’t buy your gas by Ruble tutatumia Sarafu yetu Yaan hawataki madafu,

Italy na Spain leo wametia Saini kujenga Bomba Lao la Mafuta Kuacha kutegemea ya Urusi,

Ujerumani ambayo ilikuwa na mradi wa ujenzi wa Bomba na Urusi Kama Nordic 2 imesitishwa na pia hawatanunua gesi kwa Ruble hata Urusi wenyewe wamekubali,

Kuna Suala la Sarafu ya Ruble kupanda ni Kwa Muda tu Kwakuwa impact on currency changes have some factors moja ikiwa pegging Kama aliyo Fanya Urusi but won’t be in long run , ni kwakuwa wanunuzi wanatafta ufumbuzi wa mbadala

UPDATES

Kabla ya Mkutano wa Leo Rais Putin ameagiza Mtaalamu wa masuala ya the surgical treatment of oncological diseases," kumuondolea hofu dhidi ya Mambo kadhaa baada ya Afya yake kuwa na mzozo Kwa siku mbili mfululizo

Kyv independence na litivino wamereport hivo,

View attachment 2171628


Kuna mkutano wa maridhiano utaendelea punde kutoka pande mbili za Urusi na Ukraine,

Tokea awali Mkutano ulikuwa na mapendekezo haya kabla huko ulipofanyika Belarus

Kwanza PUTIN alikuwa kapendekeza Mkutano ufanyike Belarus kabisa, Zelensky akakataa maana anajua warusi ni mafia wa kuwekea watu Sumu , hata Roman juzi wamemuwekea,

Zelensky alisema siwezi enda kwa rafiki wa adui yangu hivo Mkutano ifanyike mpakani, Putin akakataa akampigia waziri Mkuu wa ISRAEL maana Warusi na Wa Ukraine wana muingiliano na wayahudi ndo maana wakaona ISRAEL anaweza facilitate Mazungumzo Hayo,

PM wa ISRAEL akasema basi wafnyie mpakani,

Mapendekezo ya Urusi yakawa

1. Zelensky aendelee kuwa Rais ila Yule Rais alopinduliwa mwaka 2014 Kwa maandamano akakimbilia Urusi awe waziri Mkuu ili kuleta hoja ya denazification!

2. Ukraine asijiunge NATO, EU wala asiwe na mahusiano ya Marekani

3. Urusi walisema watalipa fidia Zote kwa Ukraine,
4.Watambue DONBAS yaan Luhansk na Donestk Kama majimbo huru,

MAJIBU YA UKRAINE

1. Haitawezekana kupangiwa nani awe waziri Mkuu Kwa nchi yake

2. Suala la kutojiunga na EU halitawekaza na watajiunga ila Kwa NATO hapo watafikiria ili kulinda Neutrality

3. Kuhusu Donbas hawatakubali Ku acha hata inch moja ya mji kuchukuliwa,

KIKAO CHA UTURUKI URUSI WAKALEGEZA MASHARTI

1.Urusi ilisema in mutual trust wamesimamisha mapigano huko kuelekea Kiev, na maeneo mengine

2. Urusi wakasema Wanakubali UKRAINE ajiunge EU kuhusu NATO hapo hapana maana Kama UKRAINE atajiunga na NATO basi yake majimbo ya Donbas, Luhansk na Mauripol yajitawale kwakuwa yako mpakani kabisa,

3.Pia URUSI ILISEMA YUKO TAYARI KUKUBALI MSIMAMO WA UKRAINE JUU YA DONETSK, DONBAS, LUHANSK, ila CRIMEA HIYO HAPANA MAANA ISHAJITENGA NA UKRIANE SINCE 2014

4. Wazo la Kuijenga Ukraine , Ukraine wenyewe wamesema wana 35biln $ Kwa ajili ya Shughuli hiyo na wanazo tiyari watajenga wenyewe nadhani Hii ni michango ya Marekani na wengine,

UPDATES ZA SASA

KWA WASIOELEKWA GEOGRAFIE YA KYIV IMEZUNGUKWA NA IRIPIN NA BUCHA ndo Mlandizi na Msata Za mji wa Kyiv huko waJeshi wa Urusi walikuwa wameshapafikia Lakin wakazungukwa na majeshi ya UKRAINE na kuteka maeneo walipo ,


kwasasa kwenye Ramani hii ya satellite ya dakika nne zilizopita inaonesha majeshi ya Urusi Yameondoka Kwa wingi maeneo ya Iripin na Bucha baada ya kupata Upinzani mkubwa kutoka Kwa majeshi ya UKRAINE
Hii ni Ramani inayoonesha maeneo yaliyo kombolewa
Leo ni (blue) na jana (yellow).

Pia eneo la Chernihiv limekombolewa Rasmi.

View attachment 2171695


LEO 2/4/2022. CHERNOBYL UPDATES

BAADA YA NUCLEAR PLANT KUWA CHINI YA WARUSI KWA SIKU KADHAA NINI HADA KIMEENDELEA

1.Kwanz waliwalazimisha wafanyakazi wa Chernobyl kufanya kazi usiku na mchana isionekane wamekishika wakashindwa kukiendesha, na lengo la Urusi walitaka kuhadaa dunia kwamba lengo Lao si baya huku wakifanya kinyume , Mwandishi wa habari wa USA anaitwa Sarah Mor amefika hapo na kueleza hayo baada ya kuzuiliwa Kwa Muda neef kufika

Usiku wa kuamkia 29 kulionekana kuna leakage ya mionzi ya Urani (uranium) ikaonesha dalili zile zile za Mwaka 1986 kilipolipuka na kusababisha madhara, wakawa wanaanza kuona madhara kwenye Miili yao na wengine wakaacha kuona kwa mujibu wa mtaalamu wa mionzi Radiologist Medved akawashauri waache eneo huko liendeshwe na Wataalamu maana wanajeshi hao si wataalamu wakakaidi ila walivyoanza kupata madhara ndo wakaanza kuondoka wakiwa wanatelekezana pale

Leo hii tarehe 2 Bendera ya UKRAINE imepandishwa Rasmi



Ntaendelea Uzi usiungwe kwingine plz……

Mkuu kwa akili yako yote tangu uzaliwe??

Vita inapiganiwa Nyumbani kwako , ardhi yako, yanabomoka majengo yako, watu wako na miundo mbinu vinaharibika na wanajeshi wako wanakufa bado useme Russia ndo kapoteza??
mwenzetu una kichwa kweli??

haya angalia hesabu ndogo

Hasara ya Ukraine = Jeshi + Raia + Miundo mbinu + Mazao na mifugo + Miji na makazi + siraha + Uchumi

Hasara ya Russia = Jeshi + silaha

Russia mambo yakiwashinda wanarudi kwao. Ukraine kwao kumeharibika, na kila kitu kinaanza upya kifupi hawana option
 
Mkuu kwa akili yako yote tangu uzaliwe??

Vita inapiganiwa Nyumbani kwako , ardhi yako, yanabomoka majengo yako, watu wako na miundo mbinu vinaharibika na wanajeshi wako wanakufa bado useme Russia ndo kapoteza??
mwenzetu una kichwa kweli??

haya angalia hesabu ndogo

Hasara ya Ukraine = Jeshi + Raia + Miundo mbinu + Mazao na mifugo + Miji na makazi + siraha + Uchumi

Hasara ya Russia = Jeshi + silaha

Russia mambo yakiwashinda wanarudi kwao. Ukraine kwao kumeharibika, na kila kitu kinaanza upya kifupi hawana option
Uchumi ndio hasara kubwa, Russia uchumi wake hauwezi kuwa sawa Vita vikiisha.

Nchi yenyewe uchumi wake ni budget ya USA kwenye jeshi pekee kwa miaka mitatu

Nyongeza, Ukraine hana Cha kupoteza plus toka lini Russia akashindana na Ukraine.. Russia anataka kushindana na USA kitu ambacho hatokuja kuweza ikiwa uchumi wake utaendelea kushuka
 
Now ni ngapi haha
Mkuu, pesa iko string sana. Walichokifanya Russia ni kuishusha kidogo thamani kwa sababu kadri ilivyokuwa ikiimarika inakuwa mzigo mzito kwa serikali na wananchi. Kwa hiyo hapo ilipo iki vizuri sana. Jiulize ghafla tu ukiamka kesho ukuta usd 1 ñi sawa na Tshs 1000, unajua uchumi utayumba?

Swali ambalo nimeliina leo wachumi wengi huko majuu wanajadili: kwa nini benki za Russia hazifilisiki? Wenye uchumi imara mabenki yanakufa, wenye vikwazo kila kona benki zao ziko imara. Fuatilia PETRODOLLAR
 
Wadanganye hawahawa mashabiki maandazi ila sio watu wenye uwezo wa ku reason. Unasema Russia wamefiwa na wanajeshi 7000+, ila husemi Ukraine wamefiwa na wanajeshi wangapi? Unasema ndani ya urusi supermarket bidhaa zinaisha, Ukraine zipo?

Je urusi imezalisha wakimbizi wangapi? Ukraiane ni wangapi? Kichekesho ni hiki 'marekani wanaenda Venezuela kuvuna mafuta' je marekani wanamtambua rais wa Venezuela? Toka lini? Watafanya biashara na serikali wasioitambua?

Nenda kasome tena, itachukua miaka 8 kwa ulaya kupata mbadala wa ges ya urusi, haya sio maneno yangu ni wataalamu na wanasiasa wa ulaya wenyewe.
Marekani alitangaza kusitisha kuchukua mafuta nchini Urusi, kwa taarifa yako mpaka jana asubuh meli zao zilichukua mzigo.

Hao hao marekani wameondoa vikwazo kwenye mbolea kutoka urusi. Alafu wewe baada ya kula kachori unadanganya watu hapa. Semeni ukweli sio ushabiki

Jana Putin na scholz wa Germany wameongea kwa simu juu ya biashara ya gesi, wameelewana juu ya means of payments
Germany na Russia kila upande hunufaika na uwepo wa mwenzake. Ndiyo maana Germany hawana muda wa kukaza sana sababu wanajua itawaathiri wao pia.
 
Ni ngumu kumlaumu sana kwasasa kutokana na hari halisi ya Ukraine ilivyo na yeye ndiyo huiona "true colour ya Wagner" kwenye ardhi yake tofauti na media zilizo front line katika kupotosha.

Ingawa mapungufu yake nikwamba..tatizo lake hutaka kulifanya kuwa tatizo la ulimwengu mzima, ndiyo maana huenda mbali zaidi mpaka katika michezo hupenda kuliingiza tatizo lake.

Kila siku rais Mr. Sele analialia huko akiomba misaada na kuzishutumu jumuhiya mbalimbali hasa za ulaya kwa kuendelea kununua mafuta, gas na bidhaa zingine toka urusi kwa sababu pesa hizo au mabilioni hayo ndiyo yanayo enda isaidia urusi kuingamiza ukraine... na jana alikuwa akiongea moja kwa moja na bunge la uholanzi...
 
US anajua hapendwi na interests zake zinawindwa kote duniani, hivyo basi, kupitia mitaji, viwanda, technology etc alizompatia China anakua amezipaka rangi na logo ya China biashara na products zake ma hivyo kuweza kuuza Russia , Iran na sehemu zote ambazo mmarekani hakubaliki, amnako wanamuona China kama mkimbozi na mbadala wa Marekani. Wasilolijua ni kuwa US anamtumia China.
SI KWELI
 
Mkuu kwa akili yako yote tangu uzaliwe??

Vita inapiganiwa Nyumbani kwako , ardhi yako, yanabomoka majengo yako, watu wako na miundo mbinu vinaharibika na wanajeshi wako wanakufa bado useme Russia ndo kapoteza??
mwenzetu una kichwa kweli??

haya angalia hesabu ndogo

Hasara ya Ukraine = Jeshi + Raia + Miundo mbinu + Mazao na mifugo + Miji na makazi + siraha + Uchumi

Hasara ya Russia = Jeshi + silaha

Russia mambo yakiwashinda wanarudi kwao. Ukraine kwao kumeharibika, na kila kitu kinaanza upya kifupi hawana option
Good summary,Sasa Kuna warusi weusi wanakuja subiri
 
Back
Top Bottom