Hahahha Babu nawe bwana ah..... unanchosha sasa. Hivi kutokufanyia chochote ndio kufanyaje au kuna exclude nini? Sawa hujanikosea kwa maana ya kucheat au kunikera. But mfano ndo mie mama Havijawa, nyumba ya pili shogangu anamcheza ngoma mwanae Sheta, anakata sare. Mie mwanajamii, nashiriki kila shughuli mtaani (Isitoshwe mwanetu Havijawa karibia anavunja ungo na ataolewa soon) nakuomba mume wangu naomba hela nkakate sare, unaninyima kwa sababu tu kuwa wewe mambo ya mtaani huyapendelei (wewe unafikiria ni ya mtaani tu ila mie ni kama nainvest, ili name ikifika kwa mwanangu mama Sheta nae aniunge mkobno kwa kukata sare). Sasa sawa ntakuelewa, na sitakunyima ila ntakupa pungufu ya kiwango........cheza ukimaliza funika geukia upande wa pili. Sasa wewe ulishazoea Mama Havijawa mie ikifika muda huo ah mwanakwetu mizungu yote itajua kuwa binti yao anatekeleza jukumu lake sawasawa. Sasa nicheze chini ya kiwango kwa mechi mbili, tatu........hutoachia pesa za sare weye? huku ukisema mke Wangu kata kabisa na ya yule mwanae mwenye miaka 6 ili ikifika zamu yake uwe nayo?