Rushwa Tanzania: Ni Kwa sababu ya njaa au tabia

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Rushwa! Ni msamiati unaofahamika sana Tanzania. Si matajiri wala maskini, wote wameathiriwa na Rushwa, kama wahanga au wanufaika.

Rushwa! Rushwa Tanzania! Kila Kona ni rushwa. Huenda hata kwenye dini nako kuna rushwa!

Inashangaza na kusukitisha! Hata watoto wanajua rushwa.

Kwa nini rushwa? Ni kwa sababu ya njaa au tabia?

Rushwa humfanya mnufaika kuwa na moyo wa "korosho". Hajali ni kiwangi gani mwathirika anaumia. Muhimu ni lengo lake ovu kutimia. Utamkuta askari wa usalama barabarani, tena aliye nadhifu, anakubali kuhongwa 1,000/= na dereva ambaye kwa mwonekano wake wa kimpauko ni dhahiri kuwa ni choka mbaya. Lakini trafiki anachukua elfu moja yake bila huruma.

Rushwa, imewafanya waliopewa dhamana kujisahau kuwa wao nao ni binadamu.

Ni kwa sababu ya rushwa, inavyosemekana, ukiwa na hela Tanzania, kila kitu kitawezekana. Hata kisicho haki yako kitakuwa haki yako.

Rushwa imeumiza wengi. Yumki, kuna hata waliopoteza maisha kwa sababu ya rushwa.

Kama si mtoa rushwa Tanzania, unaweza ukakosa haki zako zilizo halali.

Miaka ya nyuma, baada ya kuhitimu kidato cha Sita, nilifanya kwanza kazi mahali fulani kabla ya kuacha kwa ajili ya kuenedelea na masomo ya Chuo.

Tulipofunga Chuo likizo ndefu, nilirejea Arusha kwa mapumziko na kufuatilia stahiki zangu NSSF.

Miezi mitatu ilikatika nikiwa ninapangiwa bila kuwepo dalili ya kuweza kulipwa. Kila nikienda, napangiwa siku nyingine ya kurudi. Nilikuwa nikiambiwa sijui faili langu halionekani, mara faili langu mpaka lirejeshwe toka makao makuu ya NSSF, Dar ES Salaam, na majibu mengineyo ambayo yalinifanya niwatilie mashaka.

Kwa kuhofia kuwa nitajikuta ninarejea chuoni kabla sijalipwa stahiki zangu, niliamua kwenda kulalamika kwa mmoja wa "wakubwa" hapo NSSF. Ni sahihi nikisema hakunisikiliza kwa sababu aliishia kunijibu "mbovu"

Niliendelea kwenda NSSF kama walivyokuwa wakiniambia, huku kukiwa hakuna matumaini ya kuweza kulipwa kabla ya kurudi chuoni. Ningelipwaje kama hata faili lilikuwa halionekani?

Siku moja nikiwa hapo NSSF, nilikutana na classmate wangu wa primary, naye akiwa anafuatilia malipo yake. Alinishangaza aliponiambia kuwa alianza mchakato wiki hiyo na siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kulipwa. Nilishangaa!!!

Nilipomdadisi, aliniambia kuwa aliamua kuharakisha kwa kumwahidi mtoa "Afisa" ten percent.

Siku hiyo kabla ya kurudi nyumbani, nilijikuta na mimi ninamropokea Afisa husika kuwa siku nikifanikiwa kupata malipo yangu, "ningemjali"

Maajabu! Faili halikuweza kujificha tena!

Maajabu! Kesho yake na mimi nilikuwa miongoni mwa waliolipwa.

Rushwa, ipo kwa "wanene" na watu wa kawaida! Tatizo ni njaa au tabia?
 
Vyote kwa pamoja.

Na mazoea pia mkuu mtu unaenda ofisi fulani kufuata stahiki zako kama wewe ivo, unamkuta huyo afisa anakunywa supu, pembeni ana pepsi big huku kashanunua korosho za 5000 kwenye foleni anazo hapo.
Na bado kahawa ya ofisi inamsubiri lakini bado ataitaka hiyo elfu 5 au 10 yako wewe ambae kimuonekano tu umeitamani ile supu.
 
Ndio maana Mwenyezi Mungu hii kitu rushwa aliilaani kabisa na kusema wala rushwa kiama chao ni lile ziwa liwakalo moto.
Kwa mantiki hiyi naona watu wa 'chama flani cha siasa' uelekeo wao ni lile ziwa liwakalo moto!
 
Binafsi nadhan tatizo la rushwa na ufisadi kuna ma role model ambao na wengine huishi humo na wengine huamua kula rushwa au kufanya ufisadi! NB; Naamin mfano wa vita dhidi ya rushwa na ufisadi uanzie ngaz za juu za utawala kwa vitendo, naamin watanzania wakiona viongoz wakishughulikiwa effectively wataelewa sasa hapa kimenuka!!
 
Kabisa, mbona magufuli alijaribu na mabadiliko yalianza kuonekana
 
Ofcz, kwa upande wake alijaribu at least kdg kukawa na woga. But JPM kama kwel alihitaji Taifa liwe la kizalendo alipaswa aikite katiba mpya yenye makali haswa kwa wabadhirifu na mafisad!!
 
Vyote kwa pamoja.

Na mazoea pia mkuu mtu unaenda ofisi fulani kufuata stahiki zako kama wewe ivo, unamkuta huyo afisa anakunywa supu, pembeni ana pepsi big huku kashanunua korosho za 5000 kwenye foleni anazo hapo.
Na bado kahawa ya ofisi inamsubiri lakini bado ataitaka hiyo elfu 5 au 10 yako wewe ambae kimuonekano tu umeitamani ile supu.
Pia hata sisi Kama jamii tushajenga mazoea ili uhudumiwe ni lazima mkono uwe mwepesi kidogo,hakuna akatae pesa hata Kama ni elf 5 yeye analipwa milion.
Sisi pia tunawalazimisha kuwapa kosa lao ni kupokea
 
Rushwa! Ni msamiati unaofahamika sana Tanzania. Si matajiri wala maskini, wote wameathiriwa na Rushwa, kama wahanga au wanufaika.

Rushwa! Rushwa Tanzania! Kila Kona ni rushwa. Huenda hata kwenye dini nako kuna rushwa!

Inashangaza na kusukitisha! Hata watoto wanajua rushwa.

Kwa nini rushwa? Ni kwa sababu ya njaa au tabia?

Rushwa humfanya mnufaika kuwa na moyo wa "korosho". Hajali ni kiwangi gani mwathirika anaumia. Muhimu ni lengo lake ovu kutimia. Utamkuta askari wa usalama barabarani, tena aliye nadhifu, anakubali kuhongwa 1,000/= na dereva ambaye kwa mwonekano wake wa kimpauko ni dhahiri kuwa ni choka mbaya. Lakini trafiki anachukua elfu moja yake bila huruma.

Rushwa, imewafanya waliopewa dhamana kujisahau kuwa wao nao ni binadamu.

Ni kwa sababu ya rushwa, inavyosemekana, ukiwa na hela Tanzania, kila kitu kitawezekana. Hata kisicho haki yako kitakuwa haki yako.

Rushwa imeumiza wengi. Yumki, kuna hata waliopoteza maisha kwa sababu ya rushwa.

Kama si mtoa rushwa Tanzania, unaweza ukakosa haki zako zilizo halali.

Miaka ya nyuma, baada ya kuhitimu kidato cha Sita, nilifanya kwanza kazi mahali fulani kabla ya kuacha kwa ajili ya kuenedelea na masomo ya Chuo.

Tulipofunga Chuo likizo ndefu, nilirejea Arusha kwa mapumziko na kufuatilia stahiki zangu NSSF.

Miezi mitatu ilikatika nikiwa ninapangiwa bila kuwepo dalili ya kuweza kulipwa. Kila nikienda, napangiwa siku nyingine ya kurudi. Nilikuwa nikiambiwa sijui faili langu halionekani, mara faili langu mpaka lirejeshwe toka makao makuu ya NSSF, Dar ES Salaam, na majibu mengineyo ambayo yalinifanya niwatilie mashaka.

Kwa kuhofia kuwa nitajikuta ninarejea chuoni kabla sijalipwa stahiki zangu, niliamua kwenda kulalamika kwa mmoja wa "wakubwa" hapo NSSF. Ni sahihi nikisema hakunisikiliza kwa sababu aliishia kunijibu "mbovu"

Niliendelea kwenda NSSF kama walivyokuwa wakiniambia, huku kukiwa hakuna matumaini ya kuweza kulipwa kabla ya kurudi chuoni. Ningelipwaje kama hata faili lilikuwa halionekani?

Siku moja nikiwa hapo NSSF, nilikutana na classmate wangu wa primary, naye akiwa anafuatilia malipo yake. Alinishangaza aliponiambia kuwa alianza mchakato wiki hiyo na siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kulipwa. Nilishangaa!!!

Nilipomdadisi, aliniambia kuwa aliamua kuharakisha kwa kumwahidi mtoa "Afisa" ten percent.

Siku hiyo kabla ya kurudi nyumbani, nilijikuta na mimi ninamropokea Afisa husika kuwa siku nikifanikiwa kupata malipo yangu, "ningemjali"

Maajabu! Faili halikuweza kujificha tena!

Maajabu! Kesho yake na mimi nilikuwa miongoni mwa waliolipwa.

Rushwa, ipo kwa "wanene" na watu wa kawaida! Tatizo ni njaa au tabia?
Ni tabia iliyo lelewa hivyo imesha komaa
 
Imeandikwa rushwa hupofusha fikra za wenye akili. Ndio maana trafiki nadhifu anachukua pesa kwa Konda choka mbaya
 
Back
Top Bottom