Je, inaweza kuwa Rushwa yenye Maslahi kwa Umma?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,032
3,913
Habari za wakti huu?

Moja kati ya changamoto tunazokabiliana nazo kama TAIFA ni Tatizo au KERO ya RUSHWA hasa zile RUSHWA kubwa kubwa. Katika Pitapita mitandaoni na tafakari zangu nikakutana aina fulani ya Wala Rushwa ambao kwao wameamua kufanya jambo la kipekee.

Jambo hili linaweza kuwa na ukakasi wa kisheria na hata kijamii lakini kwa kiwango fulani linaonekana kufanya kazi vizuri sana. Kuna watu kutokana nafasi zao nyeti hujikuta Rushwa zikiwafuata kwa Lazima hata kama hawazitaki. Hii ni kutokana ama na nafasi zao za kiushawishi au nafasi za wale ambao wanataka kuwa RUSHWA.

Basi kwa kuwa Rushwa ni Adui wa Haki na Rushwa ipo basi watu hawa huwa wanakuwa na Orodha ya NGOs, Charities na TRUSTS ambazo ama wana maslahi nazo au wanapenda kazi zao wanazofanya kwa kiwango fulani zinawapa jukwaa mfano kuwaalika kwenye matukio yao na kuwapa majukwaa ya kufanya shughuli za kijamii na kutengeneza PUBLIC images zao.

Sasa hawa watu huwa unapotaka kuwapa HONGO huwa wanakupa maelekezo ukafanye DONATION yako kwenye Taasisi husika, mfano NGO, Foundation etc ili wao waangalie namna ambavyo wanaweza kukufanyia favours fulani.

Kwa kawaida wanakwambia kwamba mchango unaweza kuutoa kwa jina lako au la kampuni na baada ya kutoa unamjulisha na yeye akithibitisha kwamba kweli mchango umefika basi anakupa ile favour yako au kukamilisha jambo lako.

Hii inafanyika sana huko Duniani na mara nyingine muhongwaji huwa ana namna ambavy anapata faida na donations hizo.

Swali la kujiuliza je Mbinu hii ni mbinu nzuri na, je unafakiri hilolinaweza kuwa linafanyika hapa TANZANIA?

Tujadili pia na namna ambavyo tunaweza kupambana na rushwa katika jamii zetu.
 
Taja NGO moja ambayo imepokea fedha za namna hiyo ili mjadala huu uwe halisi.
 
Yes mtoa hoja hili linawezekana ,ILA nafsi ya mpokeaji ina play big part, kipindi cha awamu ya kwanza,kuna waziri alipelekwa nje kusaini mkataba wa pesa nyingi, na akapewa 10%yake binafsi (rushwa),aliporudi nchini akaisalimisha kwa president Nyerere (elewa tiss yake ilikua sharp sana na walikuwa very respected SIO uchafu huu wa sasa),Mwalimu alimwelewa waziri wake na ile pesa ikatumika kwa training ya pilot's wetu, yes Tanzania bila rushwa iliwezekana,hadi leo Botswana traffic officer's almost corruptions ni zeros
 
Mpokeaji na mtoa rushwa ni maadui wakubwa wa jamii na Mungu.
Hakuna aina ya rushwa sio laana
 
Back
Top Bottom