Rushwa Bungeni.. it has come to my attention...

Mzee Mwanakijiji, kumbe hili la mfumo wa kifisadi ambao hauwezi kuondolewa kwa makubaliano ya mezani unalijua?!
Pia kumbe unajua njia pekee ni kubomolewa tuu kwa mfumo huu?!, Nyie na CCJ yenu, mezani mlikuwa mnaenda kufanya nini kabla ya kuishia kulia lia?.

Wenzenu CUF Zanzibar hili waliliona na waliamua 2010 basi, wakaamua hawajiandikishi na kuahidi kura hawapigi!. Wenye nchi hili wakaliona na kitisho kilicho mbele yao, wakamkubalia Karume awashike mkono, wakakubali yaishe, na yanaisha.

Sisi huku bara, kama mfumo ni wa kubomolewa, hao waboaji wenyewe ndio kina nani?. Zitto, Slaa na wengineo, wanajaribu, laki peke yao hawawezi, kuunganisha nguvu agaist common enemy ndio hivyo hatuaminiani, take this bitter pill and I beg you just swallow it because its a fact, hao wakombozi bado hatunao!

2010 IS THE SAME! ni CCM tena na ni JK kwa kishindo!.

Interesting.... what is the role and stance of Maalim Seif these days??!
 
Interesting.... what is the role and stance of Maalim Seif these days??!
Steve Dii, Maalim baada ya kulia lia kuwa ameputwa tonge mdomoni mara 3, kufuatia zoezi la uandikishaji, akasoma dalili za nyakati kwamba hawezi kushinda hata kwa dawa. Akaamua hakuna kulia lia wala kubembelezana tena, akayarudisha majeshi yake nyuma, wakasusia kujiandikisha na kuahidi kuwa hawapigi kura mwaka 2010, bora tuu sultan CCM andelee kutawala milele.

Wenye nchi hili wakaliona, sio kweli kuwa Karume ndio anampenda Seif ki hivyo kiasi cha kumkaribisha Ikulu, bali kitisho cha Zanzibar kuweza kusitawalike na kusikalike kama CUF watasusa jumla, kilionekana, hivyo wakatumwa wakamwite Seif, wao na Karume, walichokiongea wanakijua wao tuu, ila Seif amepata alichokitaka, sasa ametulia tuli.

Ndio maana mgombea wa CCM Zanzibar ni Dr. Shein, mtu asiye na mvuto, wala hauziki, lakini ndiye pekee anayeweza kufanya kazi chini ya Seif ama na Seif kwa vile yeye si yeye, yeye ni yes man hivyo jahazi litakwenda salama.

Sometimes politics is a game of give and take, win and loose or win win situation. Katika yote ni Seif ndie kalamba dume!.
 
TAKUKURU hawana habari au nao wamepozwa kidogo ili wafumbe midomo yao?hizi taasisi zimeanzishwa kwaajili gani sasa kama hazina meno ya kutosha.
 
Pasco,

Maono mazuri sana haya..... Yana mantiki
 
TAKUKURU hawana habari au nao wamepozwa kidogo ili wafumbe midomo yao?hizi taasisi zimeanzishwa kwaajili gani sasa kama hazina meno ya kutosha.

Zimeanzishwa ili wakubwa wazione na kutoa misaada. Si unajua tena sisi kazi yetu ni kulia lia tu!!!
Oooh masikini....oohh hatuwezi bila wawekezaji....etc.
 
Solution ni kuukubali mfumo wa rushwa na kuuhalalisha. Watanzania wote tukiwa walarushwa basi rushwa itakosa mvuto na kufa kifo cha mende. Uadilifu sasa utachukua nafasi yake.

Hebu fikiria tu scenario ambapo kila mtanzania ni mlarushwa. Fikiria nchi ambamo wanunuzi wote wanatembea na pesa feki na wauzaji wote wanauza bidhaa feki. Patakuaje hapo?

Solution yako kwa issue hii aaaaaaagh
 
Rushwa iliyotembea na wale ambao tukiwaandika kuwa ndio wamepokea, wengine majina yao yatawaliza watu au kuwafanya wasikitike. Huu mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kuondolewa kwa makubaliano mezani. Ni wakubomolewa tu.

Naanza kuhisi unako taka kwenda!
 
TAKUKURU hawana habari au nao wamepozwa kidogo ili wafumbe midomo yao?hizi taasisi zimeanzishwa kwaajili gani sasa kama hazina meno ya kutosha.

Mkuu hivi unafikiri Takukura wapo kwa ajiri ya kutokomeza rushwa? Hawa wapo kwa ajiri ya kuhalalisha rushwa. Haya yote huwa wana habari kabisa wakati mwingine wanakuwepo nakushiriki kikamilifu katika kuharalisha.

Hii ndiyo bongo. Wakikushinda ungana nao.
 
Huyu wa SUMATRA alikuwa astaafu. Imekuwaje? Masebu wa EWURA anajua sana kuishi na wanasiasa wetu na njaa na tamaa zao zisizo na kikomo tangu akiwa NHC.

Si wanasiasa tu, huyu ni class moja na EL, pamoja na Othman pale milambo secondary enzi hizo. Kumng'oa labda mkaazime winchi ya kuibulia meli zilizozama baharini.
 
Aliyeng'olewa ni wa DAWASCO ambaye hakuonyesha "ushirikiano" wa kutosha na wanasiasa wetu.

Nguzo yake alikuwa EL. Unakumbuka EL akiwa PM aliifukuza city water, akaunda DAWASCo bila hata kutangaza posts akamweka huyu?
kajamaa kalikuwa na kiburi kweli enzi za EL. Kwenye TV kalikuwa kanaongea kama ka-PM vile. gademu!!!!!!!!!!
 
Ni ngumu sana kudhibiti rushwa kwa wanasiasa wetu. Tena katika kipindi kama hiki ambacho kila senti inahitajika. Huyo Mrema na watu wake labda wameifanya "kishamba" tu. Wakuu wa Taasisi za UMMA wanaishi na wanasiasa wetu kwa njia hii.
 
Solution ni kuukubali mfumo wa rushwa na kuuhalalisha. Watanzania wote tukiwa walarushwa basi rushwa itakosa mvuto na kufa kifo cha mende. Uadilifu sasa utachukua nafasi yake.

Hebu fikiria tu scenario ambapo kila mtanzania ni mlarushwa. Fikiria nchi ambamo wanunuzi wote wanatembea na pesa feki na wauzaji wote wanauza bidhaa feki. Patakuaje hapo?

Man you made me lough. i remembered somalia risasi huuzwa sokoni kama nyanya kariakoo, na pesa inayotumika ni dola feki. you seem very desperate
 
Nguzo yake alikuwa EL. Unakumbuka EL akiwa PM aliifukuza city water, akaunda DAWASCo bila hata kutangaza posts akamweka huyu?
kajamaa kalikuwa na kiburi kweli enzi za EL. Kwenye TV kalikuwa kanaongea kama ka-PM vile. gademu!!!!!!!!!!
Wakati ule EL alikuwa waziri wa maji na mifugo. CityWater walionewa sana. Kamjamaa ni kweli kana kiburi. Kaliwavuruga sana wafanyakazi kaliowakuta pale. Kampuni haikutulia hadi kanaondoka.
 
Si wanasiasa tu, huyu ni class moja na EL, pamoja na Othman pale milambo secondary enzi hizo. Kumng'oa labda mkaazime winchi ya kuibulia meli zilizozama baharini.

..................pia kumbuka wakati ule Lowassa alipokuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Miji.................Masebu alikuwa nani.......Masebu ni mkono wa hilo wala sio siri EL...............
 
Habari toka kwa ka'nzi' ni kuwa mshiko wa nguvu umekuwa ukitembezwa kwa muda sasa kuwalainisha watendaji mbalimbali serikali na Bungeni ili kuhakikisha kuwa mabadiliko ya haraka hayatokei Tanroads. Kama wachunguzi wetu walivyoliibua suala la ATCL ambalo nalo hadi leo bado linabebwa, Tanroads vile vile hakutafanyika mabadiliko wakati wowote karibuni. Sababu kubwa ambayo imehakikishiwa ni mlolongo wa zawadi na vituliza midomo (kama vuvuzela) ambavyo baadhi ya wanasiawa wamepatiwa au kujipatia.

Hivi sasa inaonekana mlolongo huu umefika hadi Majumba yote mawili makuu! Watu wamekatiwa fedha taslimu na wengine vitu mbalimbali huku wengine wakiahidiwa zaidi huko mbele ya safari.

Ka nzi kanadokeza kuwa katika hili msaidizi mmoja wa Rais yuko karibu kwa namna ya kutisha na mambo yanayoendelea aidha kwa baraka za huyo Rais au akimwacha gizani lakini akilitumia jina lake (Rais). Hadi hivi sasa kwa uhakika ni kuwa licha ya kelele nyingi kwenye magazeti kuhusu Tanroads na ushahidi wote wa kubebwa na kukiukwa kwa taratibu mbalimbali Bw. Mrema hang'oki na watu wajifunze kuishi hivyo hivyo naye. Kama ilivyokuwa vigumu kumng'oa Mataka pale ATCL ni vigumu kumng'oa Mrema Tanroads bila ya kumtafutia mahali pengine pa "kuchumia" taifa. Ni ugumu ule ule ulioko Bandari kama ulivyokuwepo TAnesco.

habari kwa ufupi ndiyo hiyo, mkitaka kwa urefu.. subirini turudi mitamboni siku chache zijazo.

.....nina wasiwasi hata faili lake limepotea................maana...........kuna watu wamepewa ulaji sehemu nyingine kwa ajili ya kufunika mambo ya huyu bwana...............inaudhi sana
 
.....nina wasiwasi hata faili lake limepotea................maana...........kuna watu wamepewa ulaji sehemu nyingine kwa ajili ya kufunika mambo ya huyu bwana...............inaudhi sana

Mwaka wa uchaguzi huu jamani. Hamuwezi kuwaondolea Mrema wao hapo TANROADS ambako ndiko pesa inaweza kuvujia kirahisi na hasa baada ya kuimulika saana BOT.
 
TAKUKURU hawana habari au nao wamepozwa kidogo ili wafumbe midomo yao?hizi taasisi zimeanzishwa kwaajili gani sasa kama hazina meno ya kutosha.
Kwa taarifa yako TAKUKURU huwa wanashirikishwa kwenye madili makubwa makubwa, hujawahi kusikia mkuu wa kituo cha polisi anashiriki ujambazi yeye ndiye huwa anashauri leo msivamie Gongo la Mboto kuna doria kali kavamieni Tegeta na Takukuru hutoa ushauri kama huo, Bongo ndivyo ilivyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom