Rushwa Bungeni.. it has come to my attention... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa Bungeni.. it has come to my attention...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 1, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Habari toka kwa ka'nzi' ni kuwa mshiko wa nguvu umekuwa ukitembezwa kwa muda sasa kuwalainisha watendaji mbalimbali serikali na Bungeni ili kuhakikisha kuwa mabadiliko ya haraka hayatokei Tanroads. Kama wachunguzi wetu walivyoliibua suala la ATCL ambalo nalo hadi leo bado linabebwa, Tanroads vile vile hakutafanyika mabadiliko wakati wowote karibuni. Sababu kubwa ambayo imehakikishiwa ni mlolongo wa zawadi na vituliza midomo (kama vuvuzela) ambavyo baadhi ya wanasiawa wamepatiwa au kujipatia.

  Hivi sasa inaonekana mlolongo huu umefika hadi Majumba yote mawili makuu! Watu wamekatiwa fedha taslimu na wengine vitu mbalimbali huku wengine wakiahidiwa zaidi huko mbele ya safari.

  Ka nzi kanadokeza kuwa katika hili msaidizi mmoja wa Rais yuko karibu kwa namna ya kutisha na mambo yanayoendelea aidha kwa baraka za huyo Rais au akimwacha gizani lakini akilitumia jina lake (Rais). Hadi hivi sasa kwa uhakika ni kuwa licha ya kelele nyingi kwenye magazeti kuhusu Tanroads na ushahidi wote wa kubebwa na kukiukwa kwa taratibu mbalimbali Bw. Mrema hang'oki na watu wajifunze kuishi hivyo hivyo naye. Kama ilivyokuwa vigumu kumng'oa Mataka pale ATCL ni vigumu kumng'oa Mrema Tanroads bila ya kumtafutia mahali pengine pa "kuchumia" taifa. Ni ugumu ule ule ulioko Bandari kama ulivyokuwepo TAnesco.

  habari kwa ufupi ndiyo hiyo, mkitaka kwa urefu.. subirini turudi mitamboni siku chache zijazo.
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umemsahau Mheshimiwa Mbunge pale TAKUKURU
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, hivi ndivyo tunavyoishi na bongo yetu, siku zote kelele za mlango, haziwezi kumyima mwenye nyumba usingizi, tena haswa katika kipindi hiki cha nipe nikupe, nilinde nikulinde, nibebe unibebe, watu kama hawa lazima waendelee kuwepo mpaka upepo utakapomaliza kuvuma.

  Miongoni mwa maeneo ambayo mimi binafsi namkubali JK, ni uwezo wake wa kutia pamba masikioni, hasikii la muadhini wala mnadi swala. Hii ni streghth kwenye anga za msimamo, ndio maana hata kilio cha wafanyakazi kuhusu maslahi duni, hasikii kitu na kuzima tishio la mgoma kwa ahadi kuwa hata wagome miaka 8, kima cha chini cha 315,000 halipi ng'o!
   
 4. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Aminia mkuu, naona wameamua saa na hakuna wa kuwaambia kitu wale wapinga ufisadi wamefyata pyuuuuu!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Rushwa iliyotembea na wale ambao tukiwaandika kuwa ndio wamepokea, wengine majina yao yatawaliza watu au kuwafanya wasikitike. Huu mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kuondolewa kwa makubaliano mezani. Ni wakubomolewa tu.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi who is this Mrema wa Tanroads, ina maana huyu jamaa ana influence kiasi hiki? Mbona alikuwa hajulikani kabla ya kuingia hapo Tanroads? How is this impossible that the guy is so important mpaka inamuhusisha na mkuu wa nchi? Is Tz really serious?
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mnamwonea tu Mrema wa watu. Watendaji Wakuu wa Taasisi za UMMA walioteuliwa na wanaoishi kama yeye wako wengi tu. Wengine wana miaka zaidi ya 20 kwenye nafasi hizo. Mfano yule TPDC, DAWASA,.....Sasa hivi yule wa NSSF, SUMATRA, EWURA,....., ndivyo wanavyoishi na wanasiasa wetu waliowateua na wabunge wetu.
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  nchi inaendeshwa na ujamaa na KUJITEGEMEA ....kwa hiyo tusihangae sana. kila mtu anajitegemea kiupande wake huku taifa linayoyoma....
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  mmmh hawa wawili wameingia chomboni hivi karibuni; tena huyo wa EWURA I can vouch for him!
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huyu wa SUMATRA alikuwa astaafu. Imekuwaje? Masebu wa EWURA anajua sana kuishi na wanasiasa wetu na njaa na tamaa zao zisizo na kikomo tangu akiwa NHC.
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu suala ni moja tu, weka mambo hadharani tuwaeleze ukweli. Hakuna haja ya kuwasetiri wasaliti!!
  Kweli kua uyaone, kuna wakati huwa natamani kurudi katika utoto nisiyaone na kuyajua haya!!
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wa DAWASA tayari kishang'olewa
   
 13. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwanakijiji, kwa Tanzania ya leo, hii si habari. Tell the people something they dont know.
   
 14. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hapa umenikumbusha mwalimu wangu wa kiswahili kuhusu methali/nahau:"KELELE ZA CHURA HAZIZUII NG'OMBE KUNYWA MAJI'.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, kumbe hili la mfumo wa kifisadi ambao hauwezi kuondolewa kwa makubaliano ya mezani unalijua?!
  Pia kumbe unajua njia pekee ni kubomolewa tuu kwa mfumo huu?!, Nyie na CCJ yenu, mezani mlikuwa mnaenda kufanya nini kabla ya kuishia kulia lia?.

  Wenzenu CUF Zanzibar hili waliliona na waliamua 2010 basi, wakaamua hawajiandikishi na kuahidi kura hawapigi!. Wenye nchi hili wakaliona na kitisho kilicho mbele yao, wakamkubalia Karume awashike mkono, wakakubali yaishe, na yanaisha.

  Sisi huku bara, kama mfumo ni wa kubomolewa, hao waboaji wenyewe ndio kina nani?. Zitto, Slaa na wengineo, wanajaribu, laki peke yao hawawezi, kuunganisha nguvu agaist common enemy ndio hivyo hatuaminiani, take this bitter pill and I beg you just swallow it because its a fact, hao wakombozi bado hatunao!

  2010 IS THE SAME! ni CCM tena na ni JK kwa kishindo!.
   
 16. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  1.Hivi marafariki wa Rais ni kina nani?

  2.Mie nimeshangaa sana,hadi yule kijana na yeye ni mmoja wao ..
   
 17. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  [QUOTE=MzeeMwanakijiji;973703]Rushwa iliyotembea na wale ambao tukiwaandika kuwa ndio wamepokea, wengine majina yao yatawaliza watu au kuwafanya wasikitike. Huu mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kuondolewa kwa makubaliano mezani. Ni wakubomolewa tu.[/QUOTE]

  Mkuu hapo huna sababu ya kumumunya maneno. Kama wao wamemwaga mboga wewe mwaga ugali. Chumvi chumvi tu!
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Aliyeng'olewa ni wa DAWASCO ambaye hakuonyesha "ushirikiano" wa kutosha na wanasiasa wetu.
   
 19. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Solution ni nini????
   
 20. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Solution ni kuukubali mfumo wa rushwa na kuuhalalisha. Watanzania wote tukiwa walarushwa basi rushwa itakosa mvuto na kufa kifo cha mende. Uadilifu sasa utachukua nafasi yake.

  Hebu fikiria tu scenario ambapo kila mtanzania ni mlarushwa. Fikiria nchi ambamo wanunuzi wote wanatembea na pesa feki na wauzaji wote wanauza bidhaa feki. Patakuaje hapo?
   
Loading...