Rupia ya kijerumani

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
Nimekuwa nikisikia muda mrefu kama simulizi hivi, kwamba rupia ya kijerumani ukiipata unatajirika!! Binafsi sielewi ni kwa namna gani hadi juzi hapa nimekutana na mtu mmoja ambaye tunafahamiana naye na ni mfanyabiashara akadai yeye ana taarifa kuhusu rupia ambayo iko sehemu, ila kwa maelezo yake ni kwamba rupia hiyo wajerumani ndio huwa wanatafuta na kwamba ukiwapatia wanatengeneza pesa za kutosha kutokana na rupia hiyo.

Na sababu iliyopelekea mtu huyo kunifuata ilikuwa kuniuliza kama nina fahamiana na mjerumani yeyote, kwani inasemekana kila mjerumani ni mjuzi wa utaalamu huu wa kutengeneza utajiri kwa njia ya rupia.

Kwa imani inaelezwa kwamba: Kama zoezi likienda vizuri huwa zinapatikana pesa za kutosha na hivyo watu wote ambao walihusika kwa namna moja au nyingine na upatikanaji wa rupia hiyo hupata mgao na kuwa matajiri. Kwa hivyo ninachopenda kufahamu kutoka kwa wana JF ambao wamewahi kusikia story kama hii wanijuze kuhusu mbivu na mbichi kuhusiana na nadharia hii.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
39,851
Likes
12,507
Points
280

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
39,851 12,507 280
Kwa kadiri ninavyofahamu, sarafu za zamani zinakusanywa na watu fulani wenye hobby hii.Kuna watu wanalipa hela nzuri tu kwa sarafu za zamani zinazoweza kutahiniwa uhalisi.
Na thamani inaongezeka kadiri sarafu zinavyokuwa za zamani, si ajabu ukipata sarafu za enzi ya utawala wa Ming utaweza kupata malaki kama si mamilioni ya dola.Haya hayaishii kwenye sarafu tu, watu wanauza mpaka vinyago vya kale, wanajeshi wa Kimarekani waliiba sana artifacts za Babeli kutoka makumbusho za Iraki.

Hizi habari nyingine zinazoelekea kwenye ushirikina ni tetesi zisizo na msingi.

Kwamba kila mjerumani ni mtaalamu wa kutengeneza utajiri kwa rupia inachekesha.
 
Heshima mkuu,
Kwa maelezo yako hayo ina maana kwamba issue ni kuwa sarafu ya zamani lakini inasemekana wanunuzi wa rupia huwa wana vifaa maalumu vya kupimia na kama rupia husika ilishawahi kufanyiwa mambo wanakwambia kabisa kwamba hii imeshatumika!!
 
Inawezekana kabisa kwamba vifaa hivyo vinapima authenticity na age ya rupia hizo, kama inaonekana feki au si ya zamani sana unaambiwa hii haina thamani.

Sasa wengine tuliozoea kuambiwa gari la msalaba mwekundu ni la nyonya damu tunaona kitu kinachokuwa lost in translation, kwamba zinatumiwa katika shughuli.

Hamna shughuli yoyote hapo.

Unaweza kuona hata online hizi habari kwenye sites kama hii hapa

http://www.zoomcoin.com/insiders-top-picks/?gclid=CNPgp6eX3J8CFQmdnAod4jZbGw
 
Injinia

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
850
Likes
4
Points
0

Injinia

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
850 4 0
Wajinga ndio waliwao.

Man, one is able to use a computer to access JF but is still bound by baseless myths!!

Rupia ya kiJerumani haina chochote cha ajabu zaidi ya sarafu yeyote ya zamani, kama alivyokueleza Kiranga, ni kwamba tu hizi sarafu za zamani ni "collectors' items" kama zilivyo stempu nk
 
alibaba

Senior Member
Joined
Jun 24, 2009
Messages
185
Likes
3
Points
0

alibaba

Senior Member
Joined Jun 24, 2009
185 3 0
Inawezekana kabisa kwamba vifaa hivyo vinapima authenticity na age ya rupia hizo, kama inaonekana feki au si ya zamani sana unaambiwa hii haina thamani.

Sasa wengine tuliozoea kuambiwa gari la msalaba mwekundu ni la nyonya damu tunaona kitu kinachokuwa lost in translation, kwamba zinatumiwa katika shughuli.

Hamna shughuli yoyote hapo.

Unaweza kuona hata online hizi habari kwenye sites kama hii hapa

http://www.zoomcoin.com/insiders-top-picks/?gclid=CNPgp6eX3J8CFQmdnAod4jZbGw
Karinga,
Asante kwa maelezo mazuri, pia kati ya haya kuna mapokezi ya hadithi simulizi abazo huzuka na kupotea kati ya kizazi na kizazi. (the so called Legend) Hii hadithi ya Rupia ni moja wapo kuna wakati ilizushwa ya Noti ya sh 100 yenye picha ya Mmasai. Naamini ziko nyingi nyuingine.
 
Sugar wa Ukweli

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Messages
373
Likes
3
Points
0

Sugar wa Ukweli

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2009
373 3 0
Mie kwa uelewa wangu hadithi juu ya rupia zilikuwa zinahusishwa na utapeli,watu wanakuletea deal kuna rupia inatafutwa kwa thamani yoyote,halafu hao hao WANAKUZUNGUKA unakuletea rupia unainunua kwa hela nyingi,ukisha inunua tu mnunuzi anayeyuka!!!!,inakuwa imekula kwako.upo hapo?
 
drphone

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2009
Messages
3,561
Likes
35
Points
145

drphone

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2009
3,561 35 145
kwakweli ni utapeli mtupu kwani maelezo yake ni hayo hayo ila atawalokuwa nazo akuna aliyepata hizo pesa zaidi ya maneno na ushirikina mtupu
 
ELNIN0

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
3,837
Likes
288
Points
180

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
3,837 288 180
Kwa kadiri ninavyofahamu, sarafu za zamani zinakusanywa na watu fulani wenye hobby hii.Kuna watu wanalipa hela nzuri tu kwa sarafu za zamani zinazoweza kutahiniwa uhalisi.
Na thamani inaongezeka kadiri sarafu zinavyokuwa za zamani, si ajabu ukipata sarafu za enzi ya utawala wa Ming utaweza kupata malaki kama si mamilioni ya dola.Haya hayaishii kwenye sarafu tu, watu wanauza mpaka vinyago vya kale, wanajeshi wa Kimarekani waliiba sana artifacts za Babeli kutoka makumbusho za Iraki.

Hizi habari nyingine zinazoelekea kwenye ushirikina ni tetesi zisizo na msingi.

Kwamba kila mjerumani ni mtaalamu wa kutengeneza utajiri kwa rupia inachekesha.
Kuna cousin yangu mmoja alianza kutafuta hizi hela akiwa kijana sasa hivi ana 65 hakuna cha sarafu wala nini - anasema anatafuta mizimu ya kufukua eti kuna mashimo waliacha wajerumani - na wameweka nguvu za kiza. anadai bila kujua unganga huwezi kuzichukua sarafu, dhahabu na vito vya thamani kwenye haya mashimo.

Waliacha ardhini wakati walivyoambiwa waondoke nchini sasa eti kuna wajukuu na watukuu wanachukua hizo ramani wanakuja africa kufuatilia hizo thamani, sasa yeye na wenzake wanatumia unganga kuzitafuta na kuzichukua.

i never believe this.....crup....
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
39,851
Likes
12,507
Points
280

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
39,851 12,507 280
Kuna cousin yangu mmoja alianza kutafuta hizi hela akiwa kijana sasa hivi ana 65 hakuna cha sarafu wala nini - anasema anatafuta mizimu ya kufukua eti kuna mashimo waliacha wajerumani - na wameweka nguvu za kiza. anadai bila kujua unganga huwezi kuzichukua sarafu, dhahabu na vito vya thamani kwenye haya mashimo.

Waliacha ardhini wakati walivyoambiwa waondoke nchini sasa eti kuna wajukuu na watukuu wanachukua hizo ramani wanakuja africa kufuatilia hizo thamani

i never believe this.....crup....
Though I am highly doubtful, I will not be surprised at all if all of that is true, except for the mizimu part.
 
Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
Though I am highly doubtful, I will not be surprised at all if all of that is true, except for the mizimu part.
Katika mazingira tulimo tunaamini uchawi upo, labda suala ambalo ni tata ni pale ambapo mtu ana kuambia kwamba ana uwezo wa kukufanya ukawa tajiri wakati yeye mwenyewe hali yake ki uchumi sio nzuri. Ukiondoa utata huu, uchawi upo kwani tunaukuta hata kwenye maandiko mbali mbali ya zamani.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
39,851
Likes
12,507
Points
280

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
39,851 12,507 280
Katika mazingira tulimo tunaamini uchawi upo, labda suala ambalo ni tata ni pale ambapo mtu ana kuambia kwamba ana uwezo wa kukufanya ukawa tajiri wakati yeye mwenyewe hali yake ki uchumi sio nzuri. Ukiondoa utata huu, uchawi upo kwani tunaukuta hata kwenye maandiko mbali mbali ya zamani.
Ushawahi kuushuhudia uchawi wewe mwenyewe?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
39,851
Likes
12,507
Points
280

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
39,851 12,507 280
Kama ambavyo sijawahi kuuona umeme lakini naziona kazi zake, hata uchawi ni nguvu sio something touchable hivyo nasisitiza upo na unatenda!!
Sijasema "ushawahi kuuona uchawi" nimesema "ushawahi kuushuhudia uchawi", big difference.

Kwa hiyo swali linarudi pale pale, ushawahi kuona kazi za uchawi firsthand?

By the way, umeme unaonekana ukiwa na vifaa vya kuupima, uchawi unaupima kwa vifaa gani?

Wabongo kwa kuamini uchawi na ushirikina tu!
 
Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
Sijasema "ushawahi kuuona uchawi" nimesema "ushawahi kuushuhudia uchawi", big difference.

Kwa hiyo swali linarudi pale pale, ushawahi kuona kazi za uchawi firsthand?

By the way, umeme unaonekana ukiwa na vifaa vya kuupima, uchawi unaupima kwa vifaa gani?

Wabongo kwa kuamini uchawi na ushirikina tu!
Kwangu mimi ushuhuda kwa mujibu wa ufahamu ni kitendo cha kutumia milango ya fahamu (macho,masikio,pua, kuhisi,kugusa, nk) kufanya utambuzi hivyo unaposema kama nilivyo wekea wino mwekundu hapo juu kwamba kuna tofauti kati ya kuona na kushuhudia kama utakuwa na hoja za msingi za kunishawishi kwamba you are right than me nitalazimika back to school (swhili language). Vinginevyo hizo ni hoja za nguvu na si nguvu za hoja!!

Kuhusu kwamba umeme una meter za kupimia je uchawi tunaupima na nini? Jibu ni kwamba hata huo umeme ni something professional sio kila mtu anauwezo wa kupima umeme pengine hata wewe mwenyewe hujui kupima umeme kama sio fani yako. Hivyo hata uchawi una vipimo vyake ndio maana akina prof. Maji Marefu walikuwa wana kamata wachawi.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
39,851
Likes
12,507
Points
280

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
39,851 12,507 280
Kwangu mimi ushuhuda kwa mujibu wa ufahamu ni kitendo cha kutumia milango ya fahamu (macho,masikio,pua, kuhisi,kugusa, nk) kufanya utambuzi hivyo unaposema kama nilivyo wekea wino mwekundu hapo juu kwamba kuna tofauti kati ya kuona na kushuhudia kama utakuwa na hoja za msingi za kunishawishi kwamba you are right than me nitalazimika back to school (swhili language). Vinginevyo hizo ni hoja za nguvu na si nguvu za hoja!!
Kwa kutumia approach yako ya milango ya fahamu, unatumia macho kuona, lakini unaweza kupata ushuhuda kwa mlango wowote wa fahamu. Ni vigumu kuiona sauti, lakini unaweza kutumia masikio yako kupata ushahidi kwamba redio ni nzima na inatangaza habari. Kwa hiyo mwenyewe umerahisisha kuonyesha tofauti ya kuona na kushuhudia.Nimekupa uwanja mpana zaidi ya kuona, labda uliweza kuunusa, kuusikia, kuugusa uchawi, uje utuambie hapa.

Kuhusu kwamba umeme una meter za kupimia je uchawi tunaupima na nini? Jibu ni kwamba hata huo umeme ni something professional sio kila mtu anauwezo wa kupima umeme pengine hata wewe mwenyewe hujui kupima umeme kama sio fani yako. Hivyo hata uchawi una vipimo vyake ndio maana akina prof. Maji Marefu walikuwa wana kamata wachawi.
Basically hapa unachosema kina justify mtu yeyote kusema chochote.Mimi naweza kusema kuna dudu lina miguu milioni mbili linakaa juu ya mlima Kilimanjaro, ila huwezi kuliona mpaka uwe na elimu maalum. Utakubali au kukataa? Kwa principle yako hiyo itabidi ukubali kwa sababu si nishasema ili kuliona inabidi uwe na elimu maalum? Utakubali au utakataa?

Huwezi ku prove kitu kwa kushhindwa kuonyesha kitu. Unaweza ku prove kitu kwa kuonyesha kitu.

Nionyeshe uchawi unaupimaje? Kama hujui uchawi unaupimaje then kubali kwamba unaongelea kitu usichokifahamu.
 
Forum statistics

Threads 1,191,696
Members 451,730
Posts 27,717,962