Rugemalila aitaka Benki Kuu iwataje watu wote waliopata mgawo wa Escrow. Gavana asita, aomba ruhusa ya Mahakama awataje

Mara ya kwanza watu wanaona aibu kutaja waizi? taja wote mdogo na mkubwa na kuwasaidia zaidi semeni rudisheni tumewasamehe hata kama hawatarudisha lakini waishi na aibu hii tusidhulumu watu kama hawana makosa.
 
Gavana ni mwanasheria anajua taratibu zilivyo,we tulia mahakama iruhusu uone kama anaficha
Haiwezekani Gavana wa BOT apate kigugumizi cha kuwataja waliopata mgawo wa Escrow ili hali wanajulikana na wananchi tunawajua halafu pale Yupo mahakani kwa hiyo kuwataja sio kosa..na wala hakuwaingizi hatiani....Je GAVANA HAJUI WALIOHUSIKA AMA NI UHUNI INA MAANA AMESHINDWA KUMTAJA HATA NGELEJA NA PROF ANNA NTIBAIJUKA...WALIOPEWA MKIMGAO KIDOGO...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wa kwenye account ndio hawa akina chenge,Tibaijuka,Ngeleja Nk!Sasa kuna wale waliochota mabilioni cash wakabeba kwenye sandarusi kutoka Bank na kutokomea zao!Hawa ndio mpaka leo wamefanywa siri!
Siri ya muda tu,lakini kuhamisha pesa kuna kumbukumbu nyingi kwa njia nyingi.Kama swala lilikuwa kulinda Vigogo wakati ule,sasa tunajiuliza kwanini Magu awakamate akina Ruge na hali asiwaguse wapokeaji wa fedha zilizojaa viroba?
 
sasa kwa nini gavana asiwataje tu hao watu maana mzee Ruge inaonekana kama anaonewa tu yeye hakujua kilichokuwa kinaendelea nyuma ya mapazia
 
Rugemalira Ni Muumini mzuri wa Kanisa moja, Takatifu na la mitume. Pia, anaamini katika ushirika wa watakatifu ambao wengi wao walikufa wakiwa wanatetea ukweli.

Naye ameamua kuusimamia ukweli katika Hili, ninamuombea kwa Mungu, amjaalie nguvu ya kustahimili mitihani anayopita na kama wakitokea watu wanataka kumdhuru, laana na mikosi ikafanyike juu yao na mpaka vizazi vyao vya tatu.
 
Gavana ni mwanasheria anajua taratibu zilivyo,we tulia mahakama iruhusu uone kama anaficha

Sent using Jamii Forums mobile app
Ktk nchi hii kwa sasa mambo yote ni kwa rais. Usitegemee huyo Gavana ataje hao watu kama asiporuhusiwa na rais.

Usitegemee kabisa, isingekuwa huyo rais hata akina Ruge wasingekuwa hapo walipo make kwenye awamu iliyopita kwani serikali haikuwepo au mahakama hazikuwepo.
 
Kila zama na kitabu chake bwashee!
 
Siri ya muda tu,lakini kuhamisha pesa kuna kumbukumbu nyingi kwa njia nyingi.Kama swala lilikuwa kulinda Vigogo wakati ule,sasa tunajiuliza kwanini Magu awakamate akina Ruge na hali asiwaguse wapokeaji wa fedha zilizojaa viroba?
Hapo sasa ndio tunaquestion dhamira ya Rais kupambana na ufisadi!
Kwanini majizi mpaka leo yako huru?
 
Back
Top Bottom