peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 12,830
- 21,460
Moshi. Kesi ya uhujumu uchumi ambayo inawakabili waliokuwa wafanyakazi watatu wa benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL), upelelezi wake umekamilika huku upande wa mashitaka ukiwasilisha mahakamani vielelezo 471 na mashahidi 29.
Kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2023 ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Salome Mshasha huku upande wa mashitaka ukiongozwa na Mawakili wa Serikali Donasian Chuwa, Samwel Kaaya, Henry Kasiano Daudi na Bora Msafiri Mfinanga.
Octoba 2019, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa iliwafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, aliyekuwa Meneja Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo, Joseph Kingazi, na aliyekuwa Meneja Mkuu wa benki, Elizabeth Makwabe, wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi.