Rugemalila aitaka Benki Kuu iwataje watu wote waliopata mgawo wa Escrow. Gavana asita, aomba ruhusa ya Mahakama awataje

Vp nchi kama Rwnda, Burundi etc ambazo zinabadilisha katiba kukidhi matakwa ya wachache? Kama una katiba nzuri, itakufaa nini kama itabadilishwa kukidhi matakwa ya wachache?

Me nadhani tatizo la nchi za Africa ni Waafrika wenyewe

KATIBA ikiwa poa ata raisi/mahakama/bunge lazima ziwe na woga.
 
Umuofia kwenyu,

Sote tunajua sakata zima la Tegeta Escrow, wizi Wa mabilion yaliyofanywa na IPTL na PAP ambayo yaliumiza wananchi sana kuona rais mstaafu akibabaika sana pale Karimjee mbele ya wazee kushindwa kutaja kama Pesa ni za wananchi au ni za wale waliozichota kwa usiri mkubwa pale Stanbic Kinondoni.

Wiki iliyopita tumemwona Rugemalira akiiomba mahakama kuilazimisha BoT kuwataja waliochota pesa kwa usiri ambao hata Rais Mstaafu hawajui. Ni jambo la kijasiri sana la Rugemalira kuondoa uwoga kwamba anaweza kuangamizwa huko aliko, lakini kwa kuwa yupo mikono salama basi serikali itende haki kwa kuwataja watu hawa hata wasipochukuliwa hatua Watanzania kwa ujinga wetu tutawaacha tu kama tulivyowaacha wa Rada.

Pengine mtuumiwa mwenzake, Sigh Binder naye hawajui kwani huenda alijawa na mihemuko ya kuchota pesa kwa masandarusi hivyo kwa kuwataja hawa kunaweza kumsaidia kuwa jua hili wasaidie kuzirudisha kama ilivyo sera yetu ya sasa ya kutapika pesa za umma ilivyo.

Serikali kupitia BoT, kama lengo lenu ni kurudisha kilichochotwa basi msaidieni huyu manager wa PAP atapike hizi pesa na wenzake ili tununue nguzo na nyaya angalau tufaidi umeme. Tutapunguza machungu ya IPTL iliyotuingiza.

Seth na Ruge ni marafiki maadui wanaoishi gerezani kwa kesi moja, Rugememalila anadai kuguwa pesa zake kihalali na account yake ya Mkombozi inasomeka vizuri kwa wanufaika. Walionufaika walitenguliwa na Rais Mstaafu asiyejua kama Pesa zilikuwa zake kisahihi. Wanufaika wakina Chenge na Ngereja wapo Bungeni wanaongezewa vyeo tu. Hapo serikali kuwa transparent maana yake nini? Au nalo hili litapita kama litavyopita la Kangi Lugola.

 

Mtuhumiwa wa uhujumu uchumi mzee Rugemalira amesema yeye hajalipwa fedha yoyote kutoka account ya Escrow bali alilipwa na PAP.

Rugemalira amesema amemuandikia barua Gavana wa benki kuu Prof. Luoga kumtaka awataje hadharani wanufaika wote wa Escrow ili taifa liwajue. Gavana amesema atawataja watu hao pindi atakapopata ruhusa ya mahakama na si vinginevyo.

Aidha mzee Rugemalira ameshangazwa na kitendo cha upelelezi wa kesi yake kudaiwa haujakamilika wakati washtakiwa wenzake wameshakiri makosa.

======

RUGEMALIRA AOMBA ORODHA WALIOPOKEA MGAO ESCROW

MFANYABIASHARA maarufu nchini, James Rugemalira ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa amemuandikia barua Gavana wa Benki Kuu (BoT), akimuomba amuorodheshee watu wote, waliopokea fedha kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow ili ajisafishe.

Aidha, alidai ameandika notisi kwa taasisi tisa za serikali ikiwemo Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga akiomba mahakama hiyo, imuondoe katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili.

Taasisi nyingine zilizoandikiwa notisi hiyo ni Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Diwani Athumani, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Gavana wa BoT, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kamishna wa Magereza, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Clement Mashamba na Msajili wa Mahakama, ambapo alidai taasisi zote zimepokea taarifa hiyo.

Rugemalira alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshitakiwa huyo wa pili, alinyoosha mkono na kuieleza mahakama kuwa aliandika barua kwenda BoT akisema yeye hajapatiwa hata senti moja kutoka kwenye akaunti ya Escrow na kwamba fedha alizopewa yeye ni zile zilizotolewa kwa amri ya mahakama kwa Kampuni ya Power African Power (T) Limited (PAP).

“Nimemuomba Gavana kuorodhesha watu wote waliopokea fedha kutoka akaunti ya Escrow ili nijisafishe kwa sababu sikupokea hata senti moja. Majibu ya Gavana aliniambia atatoa orodha hiyo mpaka pale atakapopata amri halali ya mahakama ya kufanya hivyo,”alidai Rugemalira.

Awali, Rugemalira alidai alileta maombi mahakamani hapo kwamba aliandika barua kwenda kwa Kamishna wa TRA, akieleza namna Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong walivyokua wakikwepa kodi na ushuru wa forodha wa Sh bilioni 1.5. Alidai ameandika barua ya nyongeza na kuikabidhi Takukuru ili watakapotoa majibu watoe kwa usahihi.

“Februari 11 mwaka huu nilitoa notisi inayoelezea matatizo hata yalivyokuwa na kwamba kuna vipengele vya sheria havitekelezwi. Katika notisi hii nimeeleza ikiwa hawataniondoa kwenye kesi hii, hawataweza kukamilisha upelelezi na filimbi nilizopiga, zitasaidia kukamata wezi,” alidai.

Mshitakiwa huyo aliomba kukutana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kabla ya kwenda mahabusu kwa ajili ya kumpa ufafanuzi kuhusu kesi hiyo.

Kwamba kama hawatamtoa katika kesi hiyo, ataleta maombi maalum ya kutaka kuondolewa kwenye kesi hiyo. Baada ya kusikiliza maelezo hayo, Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 27, mwaka huu kwa kutajwa.

Mbali na Rugemalira, washitakiwa wengine ni Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power (IPTL) na Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege.

Chanzo: Habari leo

Zaidi soma: Dar: Mahakama yaruhusu Rugemarila kuleta hoja za kutaka aachiwe huru
Keep it up a prisoner lawyer you will win this case with flying colours!
 
Back
Top Bottom