Shigganza
Senior Member
- May 24, 2018
- 160
- 412
Kapteni Mapunda ambaye ni Rubani mstaafu aliyetunukiwa na Rais Magufuli katika siku za hivi karibuni kutokana na uzalendo wake kwa taifa alioufanya kwa kutorosha ndege ya Tanzania baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyotokea baada ya kuripotiwa kenan Tomy Makinda alitunukiwa Nishani ya Mwenge wa uhuru daraja la nne.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mapunda siku ilipotangazwa kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki imevunjika , alikuwa zamu na rating yake ya kazi siku hiyo ilikuwa kurusha ndege kutoka Nairobi kwenda Mombasa, halafu Tanga na mwisho Dar es salaam. Alipofika Mombasa, taarifa zilimfikia kwamba jumuiya imevunjika hivyo ameagizwa awashushe abiria wote Mombasa, kisha airudishe ndege hy Nairobi.
Ndege hiyo ilikuwa aina ya Fokker Friendship F27 anaeleza alikataa kushusha abiria kwa sababu abiria wengi kweny ndege hiyo walikuwa wanakwenda Dar es salaam akawaomba wamuongezee mafuta ya kumfikisha Dar na kuahidi kwamba akishawafikisha atairejesha ndege Nairobi hata hivyo wahusika walikataa kumpa mafuta kwa kigezo kuwa mafuta ya ndege yameisha. Ndipo alipopiga hesabu yake na kuona kwamba mafuta aliyokuwa nayo yalimtosha kufika Tanga. Akaendelea na safari yake hadi Tanga na alipofika Tanga aliongeza mafuta na kwenda Dar na mara baada ya kufika dar alishusha abiria wote aliyokuwa nao na kuikabidhi ndege kwa wahusika pale uwanja wa ndege wa Dar es salaam - terminal 1.
Kwa ufafanuzi huo uliotolewa na mhusika mwenyewe mzee Mapunda bila shaka minong'ono, utata, mjadala na sintofahamu ya uhusika wake katika kuleta ndege yetu nchini baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki itkuwa imeisha. Kinachobaki sasa ni kelele za watu wasiopenda kutambua Michango ya kipekee na ujasiri ya Watanzania kwa taifa Lao.