Rubani Kapteni Mapunda aliyetunukiwa na Rais Magufuli afunguka

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Kapteni Mapunda ambaye ni Rubani mstaafu aliyetunukiwa na Rais Magufuli katika siku za hivi karibuni kutokana na uzalendo wake kwa taifa alioufanya kwa kutorosha ndege ya Tanzania baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyotokea baada ya kuripotiwa kenan Tomy Makinda alitunukiwa Nishani ya Mwenge wa uhuru daraja la nne.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mapunda siku ilipotangazwa kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki imevunjika , alikuwa zamu na rating yake ya kazi siku hiyo ilikuwa kurusha ndege kutoka Nairobi kwenda Mombasa, halafu Tanga na mwisho Dar es salaam. Alipofika Mombasa, taarifa zilimfikia kwamba jumuiya imevunjika hivyo ameagizwa awashushe abiria wote Mombasa, kisha airudishe ndege hy Nairobi.

Ndege hiyo ilikuwa aina ya Fokker Friendship F27 anaeleza alikataa kushusha abiria kwa sababu abiria wengi kweny ndege hiyo walikuwa wanakwenda Dar es salaam akawaomba wamuongezee mafuta ya kumfikisha Dar na kuahidi kwamba akishawafikisha atairejesha ndege Nairobi hata hivyo wahusika walikataa kumpa mafuta kwa kigezo kuwa mafuta ya ndege yameisha. Ndipo alipopiga hesabu yake na kuona kwamba mafuta aliyokuwa nayo yalimtosha kufika Tanga. Akaendelea na safari yake hadi Tanga na alipofika Tanga aliongeza mafuta na kwenda Dar na mara baada ya kufika dar alishusha abiria wote aliyokuwa nao na kuikabidhi ndege kwa wahusika pale uwanja wa ndege wa Dar es salaam - terminal 1.

Kwa ufafanuzi huo uliotolewa na mhusika mwenyewe mzee Mapunda bila shaka minong'ono, utata, mjadala na sintofahamu ya uhusika wake katika kuleta ndege yetu nchini baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki itkuwa imeisha. Kinachobaki sasa ni kelele za watu wasiopenda kutambua Michango ya kipekee na ujasiri ya Watanzania kwa taifa Lao.

IMG_1315.JPG
 
Mtu akisema "nimepanda basi kwenda Moshi Jumatatu iliyopita saa tatu", na mwingine akasema ""nimepanda basi kwenda Moshi jumatatu iliyopita saa tatu".. ina maana wote wamepanda basi hilo hilo au kuna uwezekano wamepanda mabasi tofauti? Ili kuweza kujua kama wanazungumzia basi lile lile na wakielekea safari ile ile mtu mwenye hekima atataka kujua taarifa zaidi (more details).

Niliposikia habari za marubani wote wawili sikuona kujipinga kwa Kikwete au Magufuli; nilijua kuna haja ya kupata taarifa zaidi. Shida hapa mara nyingi inatokea kwa watu wa serikali ambao wanafikiria wakitoa taarifa za kutosheleza wataharibu sanaaaa. Hili lingefafanuliwa mapema isingekuwa shida; kwa mfano kwanini Kikwete alitoa tuzo kwa mmoja lakini si kwa mwingine?

Je, ni hawa wawili peke yao waliofanikisha kurusha zile ndege na hakuna wengine walioshirikiana nao na ambao na wao wanahitaji kukumbukwa kwa uzalendo ule ule? Au wazalendo walikuwa ni marubani tu?

Kama ni shukrani na tuzo basi itolewe kwa wote waliohusika moja kwa moja kufanikisha hili.. na labda yapo mengine tusiyoyajua..
 
Uzalendo ukiwekwa kisiasa unapoteza radha halisi na ukweli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo ndege zilizorudishwa Bongo toka Kenya baada ya EAC kuvunjika ni mbili, yake na ya Makinda?

Mimi binafsi ningependa kupata taarifa sahihi ili kuweka rekodi zangu kichwani sawa.

Makinda na Mapunda ni mtu na mtani wake, mwingine ni bird na mwingine ni animal
mwingine kwao Njombe mwingine Songea na wote majina yanaanza na Ma yanaishia na nda kwahiyo hakijaharibika kitu
 
Mtu akisema "nimepanda basi kwenda Moshi Jumatatu iliyopita saa tatu", na mwingine akasema ""nimepanda basi kwenda Moshi jumatatu iliyopita saa tatu".. ina maana wote wamepanda basi hilo hilo au kuna uwezekano wamepanda mabasi tofauti? Ili kuweza kujua kama wanazungumzia basi lile lile na wakielekea safari ile ile mtu mwenye hekima atataka kujua taarifa zaidi (more details).

Niliposikia habari za marubani wote wawili sikuona kujipinga kwa Kikwete au Magufuli; nilijua kuna haja ya kupata taarifa zaidi. Shida hapa mara nyingi inatokea kwa watu wa serikali ambao wanafikiria wakitoa taarifa za kutosheleza wataharibu sanaaaa. Hili lingefafanuliwa mapema isingekuwa shida; kwa mfano kwanini Kikwete alitoa tuzo kwa mmoja lakini si kwa mwingine?

Je, ni hawa wawili peke yao waliofanikisha kurusha zile ndege na hakuna wengine walioshirikiana nao na ambao na wao wanahitaji kukumbukwa kwa uzalendo ule ule? Au wazalendo walikuwa ni marubani tu?

Kama ni shukrani na tuzo basi itolewe kwa wote waliohusika moja kwa moja kufanikisha hili.. na labda yapo mengine tusiyoyajua..
We mzee upo😊?

Salamu zako za mwaka mpya
 
Kapteni Mapunda ambaye ni Rubani mstaafu aliyetunukiwa na Rais Magufuli katika siku za hivi karibuni kutokana na uzalendo wake kwa taifa alioufanya kwa kutorosha ndege ya Tanzania baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyotokea baada ya kuripotiwa kenan Tomy Makinda alitunukiwa Nishani ya Mwenge wa uhuru daraja la nne.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mapunda siku ilipotangazwa kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki imevunjika , alikuwa zamu na rating yake ya kazi siku hiyo ilikuwa kurusha ndege kutoka Nairobi kwenda Mombasa, halafu Tanga na mwisho Dar es salaam. Alipofika Mombasa, taarifa zilimfikia kwamba jumuiya imevunjika hivyo ameagizwa awashushe abiria wote Mombasa, kisha airudishe ndege hy Nairobi.

Ndege hiyo ilikuwa aina ya Fokker Friendship F27 anaeleza alikataa kushusha abiria kwa sababu abiria wengi kweny ndege hiyo walikuwa wanakwenda Dar es salaam akawaomba wamuongezee mafuta ya kumfikisha Dar na kuahidi kwamba akishawafikisha atairejesha ndege Nairobi hata hivyo wahusika walikataa kumpa mafuta kwa kigezo kuwa mafuta ya ndege yameisha. Ndipo alipopiga hesabu yake na kuona kwamba mafuta aliyokuwa nayo yalimtosha kufika Tanga. Akaendelea na safari yake hadi Tanga na alipofika Tanga aliongeza mafuta na kwenda Dar na mara baada ya kufika dar alishusha abiria wote aliyokuwa nao na kuikabidhi ndege kwa wahusika pale uwanja wa ndege wa Dar es salaam - terminal 1.

Kwa ufafanuzi huo uliotolewa na mhusika mwenyewe mzee Mapunda bila shaka minong'ono, utata, mjadala na sintofahamu ya uhusika wake katika kuleta ndege yetu nchini baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki itkuwa imeisha. Kinachobaki sasa ni kelele za watu wasiopenda kutambua Michango ya kipekee na ujasiri ya Watanzania kwa taifa Lao.View attachment 989828
Salamu...... Salamu!
 
Tumemuelewa, ila tumeshakuwa Paranoid kuhusu haya mambo tunayolishwa,kama lile la Dr. Shika kuwa ni jasusi la Kimarekani kumbe ni mgojwa wa Akili.
 
Tumemuelewa,ila tumeshakuwa Paranoid kuhusu haya mambo tunayolishwa,kama lile la Dr.Shika kuwa ni jasusi la Kimarekani kumbe ni mgojwa wa Akili.
Bado hili jambo halijakaa sawa. Nini kinafichwa? Jee Focker F27 inakuwa na marubani Wawili? Kwa nini JK alimtambua Makinda pekee akaachwa Mapunda? Kwa nini Magu alipomwelezea Mapunda alikwepa kabisa habari za Makinda?

Kuna upotoshaji mkubwa sana katika hili, lakini watu hawataki JPM akisema kitu kihojiwe ndio maana hata aliposema makinikia watatulipa Trilioni kadhaa walio pinga kuwa sio kweli waliitwa majina yote kasoro mbwa.

Tupewe ukweli ili uingie vitabuni bila kupotosha.
 
Shida sio kwa Mapunda, shida ni aliyempa Heshima. Wao jambo lolote litakalo fanywa na jpm ni lzm lipingwe kwa nguvu zote.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
Shida kuu ni viongozi wakuu wawili kutoa nishani kwa tukio lilelile kwa watu wawili tofauti.lakini pia kwa wahusika wa serikali kutotolea ufanunuzi sitofahamu hiyo.Hata hili gazeti limeandika bila weledi hawakuoji upande wa pili ama Makinda au waliomtunuku nishani tuelewe.Bado tupo njia panda.
Makinda tokelezea kama ulisistahili nishani au la

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu akisema "nimepanda basi kwenda Moshi Jumatatu iliyopita saa tatu", na mwingine akasema ""nimepanda basi kwenda Moshi jumatatu iliyopita saa tatu".. ina maana wote wamepanda basi hilo hilo au kuna uwezekano wamepanda mabasi tofauti? Ili kuweza kujua kama wanazungumzia basi lile lile na wakielekea safari ile ile mtu mwenye hekima atataka kujua taarifa zaidi (more details).

Niliposikia habari za marubani wote wawili sikuona kujipinga kwa Kikwete au Magufuli; nilijua kuna haja ya kupata taarifa zaidi. Shida hapa mara nyingi inatokea kwa watu wa serikali ambao wanafikiria wakitoa taarifa za kutosheleza wataharibu sanaaaa. Hili lingefafanuliwa mapema isingekuwa shida; kwa mfano kwanini Kikwete alitoa tuzo kwa mmoja lakini si kwa mwingine?

Je, ni hawa wawili peke yao waliofanikisha kurusha zile ndege na hakuna wengine walioshirikiana nao na ambao na wao wanahitaji kukumbukwa kwa uzalendo ule ule? Au wazalendo walikuwa ni marubani tu?

Kama ni shukrani na tuzo basi itolewe kwa wote waliohusika moja kwa moja kufanikisha hili.. na labda yapo mengine tusiyoyajua..
Tatizo mkuu wetu anataka kuvunja rekodi ya waliomtangulia, usijeshangaa ukasikia kuna siku atachanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar
 
Kapteni Mapunda ambaye ni Rubani mstaafu aliyetunukiwa na Rais Magufuli katika siku za hivi karibuni kutokana na uzalendo wake kwa taifa alioufanya kwa kutorosha ndege ya Tanzania baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyotokea baada ya kuripotiwa kenan Tomy Makinda alitunukiwa Nishani ya Mwenge wa uhuru daraja la nne.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mapunda siku ilipotangazwa kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki imevunjika , alikuwa zamu na rating yake ya kazi siku hiyo ilikuwa kurusha ndege kutoka Nairobi kwenda Mombasa, halafu Tanga na mwisho Dar es salaam. Alipofika Mombasa, taarifa zilimfikia kwamba jumuiya imevunjika hivyo ameagizwa awashushe abiria wote Mombasa, kisha airudishe ndege hy Nairobi.

Ndege hiyo ilikuwa aina ya Fokker Friendship F27 anaeleza alikataa kushusha abiria kwa sababu abiria wengi kweny ndege hiyo walikuwa wanakwenda Dar es salaam akawaomba wamuongezee mafuta ya kumfikisha Dar na kuahidi kwamba akishawafikisha atairejesha ndege Nairobi hata hivyo wahusika walikataa kumpa mafuta kwa kigezo kuwa mafuta ya ndege yameisha. Ndipo alipopiga hesabu yake na kuona kwamba mafuta aliyokuwa nayo yalimtosha kufika Tanga. Akaendelea na safari yake hadi Tanga na alipofika Tanga aliongeza mafuta na kwenda Dar na mara baada ya kufika dar alishusha abiria wote aliyokuwa nao na kuikabidhi ndege kwa wahusika pale uwanja wa ndege wa Dar es salaam - terminal 1.

Kwa ufafanuzi huo uliotolewa na mhusika mwenyewe mzee Mapunda bila shaka minong'ono, utata, mjadala na sintofahamu ya uhusika wake katika kuleta ndege yetu nchini baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki itkuwa imeisha. Kinachobaki sasa ni kelele za watu wasiopenda kutambua Michango ya kipekee na ujasiri ya Watanzania kwa taifa Lao.View attachment 989828
sawa tumekusikia Bambo lakini tunajua kwenye hili hauko "hero" peke yako.
tunasubiri "heroes" wengine wajitokeze na stori zao ili kila mmoja apatiwe haki yake!
 
Bado hili jambo halijakaa sawa. Nini kinafichwa? Jee Focker F27 inakuwa na marubani Wawili? Kwa nini JK alimtambua Makinda pekee akaachwa Mapunda? Kwa nini Magu alipomwelezea Mapunda alikwepa kabisa habari za Makinda?

Kuna upotoshaji mkubwa sana katika hili, lakini watu hawataki JPM akisema kitu kihojiwe ndio maana hata aliposema makinikia watatulipa Trilioni kadhaa walio pinga kuwa sio kweli waliitwa majina yote kasoro mbwa.

Tupewe ukweli ili uingie vitabuni bila kupotosha.

Na pia ujiulize kwa nn JPM alimtambua mapunda akamwacha makinda. Think both.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom