Rubani Kapteni Mapunda aliyetunukiwa na Rais Magufuli afunguka

Makinda na Mapunda ni mtu na mtani wake, mwingine ni bird na mwingine ni animal
mwingine kwao Njombe mwingine Songea na wote majina yanaanza na Ma yanaishia na nda kwahiyo hakijaharibika kitu
Duh
 
Kapteni Mapunda ambaye ni Rubani mstaafu aliyetunukiwa na Rais Magufuli katika siku za hivi karibuni kutokana na uzalendo wake kwa taifa alioufanya kwa kutorosha ndege ya Tanzania baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyotokea baada ya kuripotiwa kenan Tomy Makinda alitunukiwa Nishani ya Mwenge wa uhuru daraja la nne.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mapunda siku ilipotangazwa kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki imevunjika , alikuwa zamu na rating yake ya kazi siku hiyo ilikuwa kurusha ndege kutoka Nairobi kwenda Mombasa, halafu Tanga na mwisho Dar es salaam. Alipofika Mombasa, taarifa zilimfikia kwamba jumuiya imevunjika hivyo ameagizwa awashushe abiria wote Mombasa, kisha airudishe ndege hy Nairobi.

Ndege hiyo ilikuwa aina ya Fokker Friendship F27 anaeleza alikataa kushusha abiria kwa sababu abiria wengi kweny ndege hiyo walikuwa wanakwenda Dar es salaam akawaomba wamuongezee mafuta ya kumfikisha Dar na kuahidi kwamba akishawafikisha atairejesha ndege Nairobi hata hivyo wahusika walikataa kumpa mafuta kwa kigezo kuwa mafuta ya ndege yameisha. Ndipo alipopiga hesabu yake na kuona kwamba mafuta aliyokuwa nayo yalimtosha kufika Tanga. Akaendelea na safari yake hadi Tanga na alipofika Tanga aliongeza mafuta na kwenda Dar na mara baada ya kufika dar alishusha abiria wote aliyokuwa nao na kuikabidhi ndege kwa wahusika pale uwanja wa ndege wa Dar es salaam - terminal 1.

Kwa ufafanuzi huo uliotolewa na mhusika mwenyewe mzee Mapunda bila shaka minong'ono, utata, mjadala na sintofahamu ya uhusika wake katika kuleta ndege yetu nchini baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki itkuwa imeisha. Kinachobaki sasa ni kelele za watu wasiopenda kutambua Michango ya kipekee na ujasiri ya Watanzania kwa taifa Lao.View attachment 989828
Mbona gazeti halijabalance story? hakuna mtu anayekataa kwamba Mapunda alistahili hiyo heshima, swali ni.. je Yule Kapteni Makinda aliyetunukiwa nishani na Mh JK yeye pia alirusha ndege hiyo hiyo au ni nyingine au walikua wawili? Ni hilo tu
 
Mzalendo namba moja kachonga mzalendo wake wa ndege, yule aliyetunukiwa na Rais asiye mzalendo naye si mzalendo.

Mzalendo ni anayetambuliwa na mzalendo.
 
Na pia ujiulize kwa nn JPM alimtambua mapunda akamwacha makinda.think both.
Isijekuleta tafrani kama yule jamaa aliyebuni Nembo ya Taifa hahahahaa hii nchi mara nyingine utasema idara ya maji imeunganisha mtambo wa Balimi watu wanapata moja kwa moja.
 
Kapteni Mapunda ambaye ni Rubani mstaafu aliyetunukiwa na Rais Magufuli katika siku za hivi karibuni kutokana na uzalendo wake kwa taifa alioufanya kwa kutorosha ndege ya Tanzania baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyotokea baada ya kuripotiwa kenan Tomy Makinda alitunukiwa Nishani ya Mwenge wa uhuru daraja la nne.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mapunda siku ilipotangazwa kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki imevunjika , alikuwa zamu na rating yake ya kazi siku hiyo ilikuwa kurusha ndege kutoka Nairobi kwenda Mombasa, halafu Tanga na mwisho Dar es salaam. Alipofika Mombasa, taarifa zilimfikia kwamba jumuiya imevunjika hivyo ameagizwa awashushe abiria wote Mombasa, kisha airudishe ndege hy Nairobi.

Ndege hiyo ilikuwa aina ya Fokker Friendship F27 anaeleza alikataa kushusha abiria kwa sababu abiria wengi kweny ndege hiyo walikuwa wanakwenda Dar es salaam akawaomba wamuongezee mafuta ya kumfikisha Dar na kuahidi kwamba akishawafikisha atairejesha ndege Nairobi hata hivyo wahusika walikataa kumpa mafuta kwa kigezo kuwa mafuta ya ndege yameisha. Ndipo alipopiga hesabu yake na kuona kwamba mafuta aliyokuwa nayo yalimtosha kufika Tanga. Akaendelea na safari yake hadi Tanga na alipofika Tanga aliongeza mafuta na kwenda Dar na mara baada ya kufika dar alishusha abiria wote aliyokuwa nao na kuikabidhi ndege kwa wahusika pale uwanja wa ndege wa Dar es salaam - terminal 1.

Kwa ufafanuzi huo uliotolewa na mhusika mwenyewe mzee Mapunda bila shaka minong'ono, utata, mjadala na sintofahamu ya uhusika wake katika kuleta ndege yetu nchini baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki itkuwa imeisha. Kinachobaki sasa ni kelele za watu wasiopenda kutambua Michango ya kipekee na ujasiri ya Watanzania kwa taifa Lao.View attachment 989828
Hakuna asiyependa ila watu wanataka usahihi wa tukio, usitake kuwalazimisha watu wakubali kuwa yeye ndiye aliyeileta ndega DC 9 Tanzania, ndiyo maana mimi binafsi niliuliza inakuwaje ndege moja ikarushwa na marubani wawili tofauti kwenye tukio moja! Kauli yako uliyomalizia ni yakipuuzi nadhani ufafanuzi unajitosheleza bila ya wewe kuongeza neno.
 
Kwa hiyo ndege zilizorudishwa Bongo toka Kenya baada ya EAC kuvunjika ni mbili, yake na ya Makinda?

Mimi binafsi ningependa kupata taarifa sahihi ili kuweka rekodi zangu kichwani sawa.
DC 9 iliyotamkwa na Rais kuwa ilitoroshwa na Mapunda na ndiyo ilitumika kuanzisha ATC ilitoroshwa na Makinda ikitokea Nairobi, Mapunda yeye alitorosha ndege ndogo Fokker akitokea Mombasa siyo Nairobi.
Ni naamini Mapunda naye alikuwepo kwenye viwanja vya Ikulu siku Makinda akipewa nishani.
 
Mapunda alikubali vipi sifa ambazo sio zake na anajua kabisa yeye hakufanya hayo?

Ikulu hawana kumbukumbu za kilichotokea?
 
Shida sio kwa Mapunda, shida ni aliyempa Heshima. Wao jambo lolote litakalo fanywa na jpm ni lzm lipingwe kwa nguvu zote.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu

Acha upotoshaji, huyo Magu alitoa service charge ya umeme watu wengi walimsifia. Anatekeleza elimu bure watu wanamsifia. Kuna mengi anapatiia anasifiwa, na hata kama hasifiwi basi hapondwi. Anachokosea ni kusaka kick kisha anatumia hizo kick kupora nafasi ya wengine kukutana na wananchi.
 
Mbunge inatakiwa ufanye siasa kwenye jimbo lako we hutaki, unataka kugundua nini?

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Tumemuelewa,ila tumeshakuwa Paranoid kuhusu haya mambo tunayolishwa,kama lile la Dr.Shika kuwa ni jasusi la Kimarekani kumbe ni mgojwa wa Akili.
Mkuu kwani bado unabisha kuhusu ujasusi wa Dr shika?

Hapo mwenzio yuko kazini
 
Bado hili jambo halijakaa sawa. Nini kinafichwa? Jee Focker F27 inakuwa na marubani Wawili? Kwa nini JK alimtambua Makinda pekee akaachwa Mapunda? Kwa nini Magu alipomwelezea Mapunda alikwepa kabisa habari za Makinda?
Kuna upotoshaji mkubwa sana katika hili, lakini watu hawataki JPM akisema kitu kihojiwe ndio maana hata aliposema makinikia watatulipa Trilioni kadhaa walio pinga kuwa sio kweli waliitwa majina yote kasoro mbwa.
Tupewe ukweli ili uingie vitabuni bila kupotosha.
Unauliza maswali halafu unamaliza kwa hitimisho kuwa kuna upotoshaji! Ina maana una majibu ya maswali yako hapo juu. Share kwanza hayo majibu yako ili tuone conclusion yako imetoka wapi. Halafu unashangaa mnaohoji issues kubanwa. Tatizo mnahoji na preconceived bias, mfano ni wewe.
 
Mtu akisema "nimepanda basi kwenda Moshi Jumatatu iliyopita saa tatu", na mwingine akasema ""nimepanda basi kwenda Moshi jumatatu iliyopita saa tatu".. ina maana wote wamepanda basi hilo hilo au kuna uwezekano wamepanda mabasi tofauti? Ili kuweza kujua kama wanazungumzia basi lile lile na wakielekea safari ile ile mtu mwenye hekima atataka kujua taarifa zaidi (more details). Niliposikia habari za marubani wote wawili sikuona kujipinga kwa Kikwete au Magufuli; nilijua kuna haja ya kupata taarifa zaidi. Shida hapa mara nyingi inatokea kwa watu wa serikali ambao wanafikiria wakitoa taarifa za kutosheleza wataharibu sanaaaa.. Hili lingefafanuliwa mapema isingekuwa shida; kwa mfano kwanini Kikwete alitoa tuzo kwa mmoja lakini si kwa mwingine? Je, ni hawa wawili peke yao waliofanikisha kurusha zile ndege na hakuna wengine walioshirikiana nao na ambao na wao wanahitaji kukumbukwa kwa uzalendo ule ule? Au wazalendo walikuwa ni marubani tu? Kama ni shukrani na tuzo basi itolewe kwa wote waliohusika moja kwa moja kufanikisha hili.. na labda yapo mengine tusiyoyajua..

Tukiendelea kuwa hai tutashuhudia na hao wengine wakitunukiwa matuzo mbalimbali tena kwa mbwembwe ndani ya awamu zijazo!
Muhimu kujua ni kuwa mara zote siasa zetu ni za "kijinga" na zinapotosha sana uhalisia!
 
Hiki kizazi cha sasa kina laana
yaani mtu alijitoa muhanga hivyo bado anaonekana Hajafanya lolote!!
Kazi ipo
Tatizo sio kizazi cha sasa, ila ni hao watoa tuzo, same story mtu mwingine pia alipewa tuzo, so mmojawapo anaongopa. I hope sio huyu ila ni yule mmpewatuzo mwingine, Tanzania ya kizazi hiki every thing is a play!!!!
 
Back
Top Bottom