Rubani Kapteni Mapunda aliyetunukiwa na Rais Magufuli afunguka

Bila shaka tumesikia maelezo ya kapteni Mapunda ukweli umefahamika,
Tatizo sio kizazi cha sasa, ila ni hao watoa tuzo, same story mtu mwingine pia alipewa tuzo, so mmojawapo anaongopa. I hope sio huyu ila ni yule mmpewatuzo mwingine, Tanzania ya kizazi hiki every thing is a play!!!!
 
Kwani Makinda wakati anapewa tuzo ,Magazeti hayakuandika
Enzi hizo gazeti la Daily News liliandika na picha ya black and white ilipigwa pale ikulu.
Mimi bado sijaelewa kwanini Mapunda hakuhahikisha Rais anapewa taarifa sahihi, hii ya DC9 Rais aliipata wapi? Utafutwe ukweli.
 
Mapunda alikubali vipi sifa ambazo sio zake na anajua kabisa yeye hakufanya hayo?

Ikulu hawana kumbukumbu za kilichotokea?
Mapunda inabidi atueleze kwanini alikubali sifa za kugushi ili apate zawadi mono na kwanini siku zote alikaa kimya huku watu wakibishana.
 
Hiki kizazi cha sasa kina laana
yaani mtu alijitoa muhanga hivyo bado anaonekana Hajafanya lolote!!
Kazi ipo
Yule mzee aliyemhifadhi Nyerere nyumbani kwake kipindi cha mapinduzi ya wanajeshi alipewa baadae zawadi ya kujengewa nyumba na serikali akaikataa akasema alifanya vile kwa mapenzi yake yote mwishowe akaishia kupewa baiskeli tu.

Ila ingekua sasa hivi huyo mzee ange-demand wamjengee hekalu maana tunaambiwa tuwe wazalendo wkt wenzetu viongozi wanatembelea Vx v8,M/benz S class,Bmw 7 series mishahara minono,hatariiiiii.
 
Kapteni Mapunda ambaye ni Rubani mstaafu aliyetunukiwa na Rais Magufuli katika siku za hivi karibuni kutokana na uzalendo wake kwa taifa alioufanya kwa kutorosha ndege ya Tanzania baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyotokea baada ya kuripotiwa kenan Tomy Makinda alitunukiwa Nishani ya Mwenge wa uhuru daraja la nne.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mapunda siku ilipotangazwa kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki imevunjika , alikuwa zamu na rating yake ya kazi siku hiyo ilikuwa kurusha ndege kutoka Nairobi kwenda Mombasa, halafu Tanga na mwisho Dar es salaam. Alipofika Mombasa, taarifa zilimfikia kwamba jumuiya imevunjika hivyo ameagizwa awashushe abiria wote Mombasa, kisha airudishe ndege hy Nairobi.

Ndege hiyo ilikuwa aina ya Fokker Friendship F27 anaeleza alikataa kushusha abiria kwa sababu abiria wengi kweny ndege hiyo walikuwa wanakwenda Dar es salaam akawaomba wamuongezee mafuta ya kumfikisha Dar na kuahidi kwamba akishawafikisha atairejesha ndege Nairobi hata hivyo wahusika walikataa kumpa mafuta kwa kigezo kuwa mafuta ya ndege yameisha. Ndipo alipopiga hesabu yake na kuona kwamba mafuta aliyokuwa nayo yalimtosha kufika Tanga. Akaendelea na safari yake hadi Tanga na alipofika Tanga aliongeza mafuta na kwenda Dar na mara baada ya kufika dar alishusha abiria wote aliyokuwa nao na kuikabidhi ndege kwa wahusika pale uwanja wa ndege wa Dar es salaam - terminal 1.

Kwa ufafanuzi huo uliotolewa na mhusika mwenyewe mzee Mapunda bila shaka minong'ono, utata, mjadala na sintofahamu ya uhusika wake katika kuleta ndege yetu nchini baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki itkuwa imeisha. Kinachobaki sasa ni kelele za watu wasiopenda kutambua Michango ya kipekee na ujasiri ya Watanzania kwa taifa Lao.View attachment 989828
Kumbe ni ndege ndogo ain ya Fokker friendship, nilijua ilikua Boeing 737 kubwa kama dreamliner ivi.

Na kwa ufisadi wa ccm naamini kajindwge hako waliishakauza kwa mafisadi wrnzao wa kihindi akina Patel na Rostam aziz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu akisema "nimepanda basi kwenda Moshi Jumatatu iliyopita saa tatu", na mwingine akasema ""nimepanda basi kwenda Moshi jumatatu iliyopita saa tatu".. ina maana wote wamepanda basi hilo hilo au kuna uwezekano wamepanda mabasi tofauti? Ili kuweza kujua kama wanazungumzia basi lile lile na wakielekea safari ile ile mtu mwenye hekima atataka kujua taarifa zaidi (more details). Niliposikia habari za marubani wote wawili sikuona kujipinga kwa Kikwete au Magufuli; nilijua kuna haja ya kupata taarifa zaidi. Shida hapa mara nyingi inatokea kwa watu wa serikali ambao wanafikiria wakitoa taarifa za kutosheleza wataharibu sanaaaa.. Hili lingefafanuliwa mapema isingekuwa shida; kwa mfano kwanini Kikwete alitoa tuzo kwa mmoja lakini si kwa mwingine? Je, ni hawa wawili peke yao waliofanikisha kurusha zile ndege na hakuna wengine walioshirikiana nao na ambao na wao wanahitaji kukumbukwa kwa uzalendo ule ule? Au wazalendo walikuwa ni marubani tu? Kama ni shukrani na tuzo basi itolewe kwa wote waliohusika moja kwa moja kufanikisha hili.. na labda yapo mengine tusiyoyajua..
Mzee soma vizuri uelewe kisha toa hoja zako, usahihi alioutoa Mapunda ni yeye alitorosha Fokker toka Mombasa kwenda Dar na siyo DC9 toka Nairobi kama ilivyosemwa wakati wa kumtunuku. Makinda alitorosha DC9 toka Nairobi kwenda Dar na ndiyo iliyotumika kuanzisha ATC kama Rais alivyosema. Kwanini Mapunda alikubali sifa isiyo yake?
 
Back
Top Bottom