Comrade 01
JF-Expert Member
- Feb 27, 2015
- 617
- 666
Ni kweli ndugu,kifupi afisa wa polisi mwenye nyota moja (sub inspector)ni sawa na WO2 ,na mwenye nyota mbili(inspector) ni sawa WO1.Hapana hapa nadhani hauko sahihi. Warrant Officer Class one, hana nyota, na ni cheo cha juu ngazi moja kutoka kwa Staff Sergeant. ACP ana madude yaliyo juu ya nyota tatu nadhani, vyeo vya polisi sivijui vizuri. Hivyo kicheo huwezi kumlinganisha ACP na RSM(Warrant Officer Class one); LAKINI:
RSM kiutawala ndani ya Kikosi, ni mkuu wa nidhamu kikosi kizima, na kwa hiyo huwa ana mamlaka ya karibu kabisa na Commanding Officer wa kikosi (yaani anawafuatia 2ic , CI na adjutant, kama sikosei). RSM kwenye kikosi akicharuka anaamuru fatiki halafu askari wote kikosini kuanzia nyota tatu (Captain na kurudi chini, ukiondoa adjutant ambaye anaye pia huwa ana nyota tatu) na kurudi chini, wanasomba matofali, hadi ma OC wa kombania ambao nao pia wana nyota tatu.
Kicheo ACP ni mkubwa kwa Warrant Officer Class one, ila kiutawala RSM ni mkubwa sana, na anateuliwa na Rais, na anakuwepo mmoja tu katika kila kikosi. Zaidi ni kuwa RSM akikutana na ACP, lazima atashusha saluti kwa ACP, ila yeye pamoja na kuwa na mamlaka makubwa kiutawala, huwa hapigiwi saluti kwa sababu hana nyota
Polisi wanapewa commission na Rais kuanzia nyota ya tatu(ASP).Huyu kiitifaki ni sawa na luteni usu wa JWTZ(nyota moja).
Na hawa ma ASP(nyota tatu) ndio huwa wanaanza kuteuliwa kuwa wakuu wa polisi wa wilaya(OCD).