Rostam (Mbunge) anawahadaa wananchi wa Igunga

Rostam (Mbunge) anawahadaa wananchi wa Igunga

  • Thread starter Thread starter MegaPyne
  • Start date Start date
Ukarabati wa Miradi ya Maji Vijijini

42. Mheshimiwa Spika, kama nilivyolieleza Bunge lako Tukufu mwaka jana, Wizara yangu, kwa kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya, ilifanya utambuzi wa miradi ambayo haijakamilika na haifanyi kazi. Jumla ya miradi 794 yenye kuhitaji shilingi bilioni 43 kuikamilisha, ilitambuliwa. Katika mwaka 2003/2004, Wizara ilitenga jumla ya shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kukarabati miradi 31. Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya ilifanya ukarabati wa miradi ya maji ya Migori na Kiponzelo (Iringa Vijijini), Lumeya (Sengerema), Misasi (Misungwi), Malya (Kwimba), Mugango-Kiabakari (Musoma Vijijini) Bunda mjini, Gabimori (Tarime), Hedaru (Same), Lotima (Rombo), Biharamulo na Chunya. Aidha, miradi mingine iliyofanyiwa ukarabati ni Mwamapuli/Bulenya (Igunga), Singida Vijijini, Mahenge Mjini, Shinyanga Vijijini, Kilulu (Bariadi), Magugu (Babati), Korogwe mjini, Nassa (Magu), Kitomondo (Lindi), Urambo mjini, Ndea (Mwanga), Majengo/Eslalei, Elerai/Longido na Mto wa Mbu (Monduli).

Bwana kaka siyo kila kinachofanyika jimboni kina mkono wa mbunge.
Angalia majukumu ya wote hapa chini, unadhani bila mbunge hakuna kinachofanyika cha maendeleo?

Pia ukiangalia vizuri, utagundua mbunge ana majukumu ya kuishauri serikali pale anapoona inapotoka kulingana na matakwa ya waliompa kura, kwani yeye ndo sauti yao bungeni.
Narudia tena, bila kuongea leo ungejua ya Buzwagi?

Bunge likiwa na jukumu la kutunga sheria, utazitunga huku umeuchapa usingizi bungeni?
Kuna haja gani ya kuhudhuria vikao vya bunge kama huna na wala hutarajii kuleta mchango wowote? Au unafata posho tu!

check out below!
.......................................................

c) Mheshimiwa Spika, kazi za Mbunge ni pamoja na uhamasishaji wa maendelo ya wananchi na uwakilishi wa wananchi Bungeni. Masharti ya kazi ya Mbunge kupitia Bunge yameelekezwa katika Ibara ya 63(2) kwamba Bunge litakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake na huo ndio uhusiano wa msingi kati ya Mbunge na kazi za Serikali.

Kwa mujibu wa Sheria Na. 19 ya mwaka 1997 baadhi ya majukumu ya Mkuu wa Wilaya, ni pamoja na kuwa mwakilishi mkuu wa Serikali Kuu Wilayani, msimamizi wa Ulinzi na Usalama, Miongozo na Kanuni za Maendeleo. Jukumu la kusimamia miongozo na Kanuni za Maendeleo linaendana na majukumu ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji ambaye anayo majukumu ya kisheria na kiutawala katika Halmashauri na pia ni Katibu wa vikao vya Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, Mbunge, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wote wanatumikia umma na wanatekeleza majukumu yao kwa lengo la kuleta maendeleo ya wananchi. Tofauti waliyonayo ni utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia tofauti za masharti ya kazi na mgawanyo wa madaraka uliozingatia mihimili ya dola.
 
Huyu Rostam hapaswi kupewa sifa ya kuwa mwakilishi wa wananchi kwani hawawakilishi.

Hivi kila mbunge akiwa bubu kama huyu fisadi unafikiri bungeni patakuwaje?
huu ni mtizamo tuu, think big.
 
Mtu Mpya, Hume na Mzee wa Msemo wa Chadema.

Nilipoleta yaliyosomwa na mawaziri bungeni, nilimaanisha kuwa kama tayari wizara husika zinafanya kazi zake vizuri kwenye jimbo la Igunga kutokana na bajeti iliyopo, na yeye kama mwananchi ameridhika kwanini akaulize maswali bungeni? so what ili mradi ajibiwe wakati majibu anayajua?. What if anauliza pembeni na kupewa jibu?

Ninachopinga ni dhana ya kusema kila mbunge akaulize maswali ili mradi aonekane anauliza hata kama anyouliza hayana maana au majibu anayajua. Hiyo ni cheap political popularity.

Ni aina hiyo ya vingozi ndio tunao wanaropoka ku buy u popularity. Thats not for Mbunge wangu Rostam Aziz.
 
Huyu Rostam hapaswi kupewa sifa ya kuwa mwakilishi wa wananchi kwani hawawakilishi.

Hivi kila mbunge akiwa bubu kama huyu fisadi unafikiri bungeni patakuwaje?
huu ni mtizamo tuu, think big.

Hivi kama ingekuwa serikali ina fanya kazi zake vizuri kungekuwa na haja gani wabunge kuulizia miradi ya maendeleo ya majimbo yao?
Wangechangia tu kwenye utungwaji wa sheria.

Labda RA is smart enough to realize that bunge ni rubber stamp tu ya upitishwaji sheria. They do NOTHING zaidi ya kusema Ndiooooo. Akajiamulia kukaa kimya!

What about that?
 
Mtu Mpya, Hume na Mzee wa Msemo wa Chadema.

Nilipoleta yaliyosomwa na mawaziri bungeni, nilimaanisha kuwa kama tayari wizara husika zinafanya kazi zake vizuri kwenye jimbo la Igunga kutokana na bajeti iliyopo, na yeye kama mwananchi ameridhika kwanini akaulize maswali bungeni? so what ili mradi ajibiwe wakati majibu anayajua?. What if anauliza pembeni na kupewa jibu?

Ninachopinga ni dhana ya kusema kila mbunge akaulize maswali ili mradi aonekane anauliza hata kama anyouliza hayana maana au majibu anayajua. Hiyo ni cheap political popularity.

Ni aina hiyo ya vingozi ndio tunao wanaropoka ku buy u popularity. Thats not for Mbunge wangu Rostam Aziz.

Hivi kuleta mradi wa maji kwenye kijiji kimoja katio ya vijiji zaidi ya 136, ndio wizara inafanya kazi yake vzr? wakati kwanza vipo vijiji vyenye shida ya maji zaidi ya hicho kimoja kilichopata mradi!

Halafu unajuaje wananchi wameridhika na majibu ya serikali, na kwamba yeye kama mbunge wao haoni haja ya kuuliza tatizo la maji katika vijiji vingine?

Halafu unasema anauliza pembeni, pembeni wapi?? wakati mambo yote yanaongelewa ndani ya bunge tena kwa uwazi ili umma wote usikie, na kwa nini aulize pembeni? anamwuliza nani pembeni, wakati fursa ya kuuliza ilikuwepo bungeni? je huo ndio utaratibu rasmi wa wabunge kuiuliza serikali?

Hayo unayosema kwamba hata kama anayouliza hayana maana, hayana maana kwa nani? mfano serikali imeona tatizo la maji igunga liko kijiji cha bulenya, je ni kweli haina maana mbunge kuiuliza serikali kwa nini imechagua kijiji cha bulenya wakati vipo vijiji vingine shida ya maji ni kubwa kuliko hata bulenya! na ina mpango gani kufanya miradi kama hiyo kwa vijiji vingine!kwa wananchi wa igunga maswali haya yana maana ili wajue serikali inasema nini kuhusu shida zao, hiyo ndio maana ya uwakilishi, sio sawa kusema haina maana kuuliza, mbunge lazima atimize wajibu wake!! kuiuliza serikali na kuishauri pale inapohitajika!!!ndio maana tunasema kama rostam hafanyi wajibu wake mkuu bungeni bora aondolewe!

Halafu hicho unachosema wabunge wanaropoka kuwin populatity si sawa, kama tu kile anachokisema mbunge kipo na kinahitaji majibu ya serikali!serikali ndio inachance ya kusema hayo unayosema, kama maswali yanayoulizwa yamelenga kuwin political populality.
 
Newman,

Mjadala mzuri. Vipi kama anaelewa mpango mzima wa serikali wa kutatua tatizo la maji jimboni kwake?, bado aulize tu ili mradi wananchi wamsikie nae kasema bungeni?

Kule nyuma niliulizwa kuhusu kufahamu Buzwagi kabla ya Bunge. Jibu ni Ndio nilikuwa nafahamu.
 
New man,

Sijajibiwa swali langu rahisi tu. Ni mgombea gani wa CCM alisimama na RA kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ubunge kwa ticket ya CCM 2005 hapo IGUNGA?

Ni mgombea gani alisimama na RA kwenye kugombea ubunge IGUNGA kutoka upinzani?

Naomba ujibu kisha tuendelee.

Asante
 
Walikuwepo wagombea kwenye kura za maoni kupitia ccm, namkumbuka mmoja dr. kafumu, lakini pia kotoka vyama vya upinzani walikuwepo, akiwemo mwanamke mmoja.
 
Newman,

Mjadala mzuri. Vipi kama anaelewa mpango mzima wa serikali wa kutatua tatizo la maji jimboni kwake?, bado aulize tu ili mradi wananchi wamsikie nae kasema bungeni?

Kule nyuma niliulizwa kuhusu kufahamu Buzwagi kabla ya Bunge. Jibu ni Ndio nilikuwa nafahamu.

Anaelewa kutoka wapi?? ni wapi pengine serikali inakutana na wawakilishi wa wananchi zaidi ya bungeni???

mipango yote ya serikali lazima isemwe bungeni tu!!ili ipate kibali cha utekelezaji. hakuna mahali pengine pa kusemea, labda kama unapafahamu tuambie.

Kwa nini wewe unacapitalize dhana ya kuwa mbunge anaposema bungeni anataka wananchi wake wasikie, na si kwamba hapo ndiyo jukwaa rasmi la wabunge kuiuliza serikali pia kuishauri! hiyo ni dhana mbovu kabisa!!! ni wajibu na haki ya kila mbunge kutumia jukwaa rasmi kuwasiliana na nguzo nyingine ya utawala, huo ndio mgawanyo wa madaraka! na si kufanya mambo kifichox2

Ni jukwaa gani hilo mbunge anaelezwa na serikali juu ya utendaji wake?
 
huyo mbunge kweli anakichaa yaani atoe hela zake mfukoni mwake aache kusaidia ndugu zake ? waache kutudanganya kihivyo sisis wenyewe tunaakili kama hizo, mill. 600 siyo mchezo wakati kwenye ubenge wao hata wamalize miaka 5 ya kukaa kwenye mjengo hawafikishi mill.100. waende zao hao wapo viti kibiashara zaidi.
 
Duh! Chasnadu,

Naona umeingia kichwa kichwa kwenye mjadala. Bwana RA tunaemzungumzia unamjua lakini?!?. Wengi humu watashangaa hiyo kauli ya kwenye sentesi yako ya kwanza.

Newman.

Dr Kafumu akajitoa ndio ilikuwa mwisho. Leo hii Dr Kafumu ndiye mkurugenzi wa Madini hapa Tanzania, ndie aliyeshiriki kuandaa mkataba wa Buzwagi na the likes......... Sasa think.

OK RA yumo kwenye Exec Commitee ya CCM, hao ndio wanatoa ilani ya chama, hao ndio wanaamua kwenye maendeleo kipaumbele ni wapi. Hao ni beyond ministers. Ministers wanatekeleza Ilani za CCM tu.

Umeshaelewa anapata wapi Information?

Tuendelee.
 
Angalau sasa naweza kutathmini mamna ulivyo! dr. kafumu hakujitoa kwenye kura za maoni, nimesema walikuwepo wengine na walishiriki hadi mwisho hakuna aliyejitoa, lakini baada ya kukuambia hivyo what do you want?

Lakini si kweli ulivyoeleza juu ya dr. kafumu, yeye ni kamishna wa madini, kuna tofauti kati ya mkurugenzi na kamishna!

Sielewi kwa nini unaingiza mambo ya buzwagi hapa!! tunaongelea utendaji wa rostam kama mbunge wa igunga, mbona unarukia mambo bila mpangilio?? ninapata wasi wasi juu ya yote unayosema kama kweli unayaelewa!!!labda kama uko hapa kuleta mabishano tu yasiyo na maana yoyote, kama ni hivyo pole sana!

kuwemo kwenye CC ya ccm, hakumfanyi yeye kama mbunge wa wananchi wote wenye itikadi tofauti asiulize maswali, hiyo ilani ya ccm pengine wanaoijua ni wana ccm tu! wengine hawaifamu. lakin jaribu kuelewa anapokuwa bungeni yuko kwa capacity nyingine, ni mbunge pale si mjumbe wa cc ya ccm, anauliza kama mbunge!!

Kwenye ilani ya ccm mambo yanaelezwa kwa jumla sana, its just a roadmap, and not a document for implentation at all!!

Hiyo ya wajumbe wa cc ya ccm kuwa beyond ministers unaijua wewe tu, unaleta mambo ya vijiweni hapa! but katiba yetu inatambua mfumo wa uongozi wa serikali kwamba ministers ni wasaidizi wa rais, katiba ya tanzania haiongelei mfumo wa uongozi wa ccm.

Hao wajumbe wa cc ya ccm wanaojua utendaji wao ni wana ccm tu! kikatiba hawawezi kuwa beyond ministers., tafuta shule ukasome!!!
 
Katika Mkutano Mkuu huo wa Julai 2005 (wilayani), mheshimiwa Rostam aligawa bahasha kwa wajumbe – na kila mmoja alipofungua alikuta TSH 20,000. Mungu ampe nini mjumbe huyu masikini? (na amchague nanikwa ajali ya kinyang'anyiro cha Oktoba mwaka 2005)?

Waliopokea bahasha ni miongoni mwenu, na wa kumtoa jamaa madarakani ni nyie. Mlilikoroga, mlinywe!
 
Newman

Sorry nilikosea. Ni Kamishna. You are right. Samahani sana.

Turudi kwenye topic.

Ninaposema NEC ya CCM ndio kila kitu na unapinga, naona tukubaliane kutokubaliana.

Sera za chama ndizo zinazotekelezwa na mawaziri (serikali). Hutaki unataka CCM kama chama bado kinashika HATAMU, chama kipo JUU ya serikali.

Mradi hilo umeliona ni la kijiweni naomba rasmi kuachia ngazi.

Alamsiki
 
Ulikuwa mjadala mzuri. Nimefurahi kujadiliana na wewe.

Thanks man!
 
Newman

Sorry nilikosea. Ni Kamishna. You are right. Samahani sana.

Turudi kwenye topic.

Ninaposema NEC ya CCM ndio kila kitu na unapinga, naona tukubaliane kutokubaliana.

Sera za chama ndizo zinazotekelezwa na mawaziri (serikali). Hutaki unataka CCM kama chama bado kinashika HATAMU, chama kipo JUU ya serikali.

Mradi hilo umeliona ni la kijiweni naomba rasmi kuachia ngazi.

Alamsiki

Nakupongeza FD uko muungwana!!
ccm kama chama cha siasa kilishapoteza ile nuru na umakini kiliokuwa nao miaka ya 70 na 80!! nionavyo mimi ccm ni mkusanyiko tu wa watu wengi kati yao wenye kulenga maslahi binafsi.

Kwa hivyo hata hiyo nec na cc za ccm ni kama magenge tu ya watu wengi kati yao hawana hata zile chembe ndogo kabisa za sifa ya kuwa kiongozi wa watu!!!!vyombo hivi vya ccm haviwezi kuja na kitu chochote kizuri kwa taifa ketu hili! hata wao wanajua, wakati wewe unawapa nafasi hiyo muhimu ya kutunga sera za kuongoza serikali, miongoni mwao wanakataa, kumbuka rais mstaafu na mwenyekiti wa ccm mstaafu mkapa aliwahi kusema ilani ya ccm haitekelezeki!!! anawezaje kuongoza vikao vya chama kuandaa ilani na mwisho aseme tena haitekelezeki!!!

Si hivyo tu, hata huyu wa sasa kikwete kaulizwa kwa nini tanzania ni maskini, yeye anasema hajui kwa nini tuko maskini!! lakini kwa pande mwingine yeye anaongoza vikao vya kutunga sera kujibu matatizo ya watanzania na umaskini ni moja ya tatizo kubwa miongoni mwetu toka tupate uhuru!!hivyo unaposema ccm iko juu ya serikali, wkati yenyewe hata mwelekeo haina si sahihi!!! wao wanataka sana tuamin hivyo, lakin hatukubaliani nao kabisa.ccm kushika hatamu its a ceremonial statement, practically NOT!!! ungesema brettonwoods institutions, hapo kiasi fulan ni sawa!! na ni kwa sababu wao ccm hawana agenda juu ya uongozi wa nchi yetu!!!kila kitu wanangoja wafundishwe ktk nje!!

Lakin tujifunze kitu kimoja hapa, siku zote ccm inaexploit ile hali ya ujinga wa watanzania kuwin madaraka!!!

Na kati ya mambo ambayo watanzania yamewasababishia hali hii duni ya maisha, kwanza ni UJINGA, pili kutanguliza sana
USHABIKI hata kwa mambo muhimu ya mustakabali wao, na tatu UPOFU wa kushindwa kuwatambua maadui wao ni nani!!

Kwa mfano tunapoongelea suala la kutokuwa makini kwa serikali na hata kwenye vyama vya siasa, tunataja sababu nyingine bila kutaja kuwa uwepo wa wazee wengi kwenye nafasi muhim za utendaji zinazohitaji nguvu kubwa ya akili na mwili ni tatizo , tena kubwa sana!!! pengine kuliko hata hayo mengine yote!!! nini maana ya ustaafu, ikiwa mtu anastaafu serikalin halafu anagombea uongozi kwenye chama au udiwan na ubunge!!tena bila hata kuwepo ukomo wa kuongoza???

Naamini tungekuwa na mfumo bora wa upatikanaji wa viongozi, nchi yetu ingepiga hatua haraka kabisa!!!fikiria watu kama malecela, kingunge, makamba na hata bungeni zaidi ya asilimia 90 ya wabunge ni retired officers unategemea nini hapo!!! na dunia ya leo tuko kwenye ushindani katika kila kitu, ni ubora wa mbinu na mikakati ya maendeleo ya nchi ndiyo inaleta mabadiliko na hatimaye ushindi, iwe ni kiuchumi, kisiasa, kijamii nk.

Ni bahati mbaya sana hata vyombo vyetu vya habari, ambavyo vingi kati ya hivyo vinaendeshwa na vijana, lakini hawajui kuwa wazee wetu nao sasa ni tatizo kwa maendeleo ya nchi hii!!! ni WABINAFSI! wakitambua kulipa kipaumbele suala hili, tayari tutakuwa tunajiandaa kubadilika kama taifa, tunayo mifano mingi nchi za jirani na sisi, rwanda,uganda,botswana nk.

Hayo tuyaache, nitajitahidi kuwaletea wana JF mapungufu ya RA.
tuombeane heri!
 
Newman,

Nilishaaaga, umenirudisha. Uliyosema hapo juu ni kweli kabisa isipokuwa la Chama kushika hatamu. Kweli IMF na World bank ndio wanaoongoza uchumi, unaweza kuona na ji contradict (mara chama mara Hizo Inst) ila nina maana kama hao jamaa wasipotia miguu yao sehemu basi CCM ndio inatoa mwelekeo.

Angalia Bungeni, wabunge wanaambiwa cha kufanya. Wanakuwa wawakilishi wa CCM na sio wananchi. Sioni tofauti yoyote kati ya RA asiyesema kuliko hao wanaongozwa na CCM na sio wananchi.

Mimi ni mwana CCM, bado naamini mabadiliko ya kweli yatatoka CCM na sio kwingine.

Asante sana
 
FD waongopee wasiojua Igunga, kwanza dr kafumu hakujitoa bali aliingia mitini baada ya kujazwa pochi na RA kwani ndiye pekee aliyekuwa tishio kwake, tukirudi kwenye mada ya kuongea na kutetea miradi ya Igunga huyo RA alipashwa aseme sana na aombe kwa sauti ya juu ili igunga ipate maendeleo, Igunga wakati wa masika haina mawasiliano na vijiji karibu nusu ya wilaya kwani kilometa chache kutoka mjini daraja la mto Mbutu lilisombwa na maji miaka mingi tu na hujiulizi familia ngapi zinakufa kwa kushindwa kupata matibabu ya Hospitali ya Igunga wakati wa masika? Hospitali ya Igunga ni duni na haitoi huduma zote na wagonjwa wengi hupelekwa Nkinga mission hospital sasa basi hiyo barabara ya Igunga to Nkinga inafaa kuitwa barabara ? au ya kutoka kwenu Ziba hadi Nkinga je inafaaa? Kuhusu maji ndio ballaa tupu kwani maji yapo Mwanzugi lakini ameshindwa kusimamia tu yaweze kufika Igunga acha kuyapeleka vijijini eg Sakamaliwa, Mbutu, Ibutamisuzi etc , vijiji hivyo enzi ya Mwalim Nyerere vilikuwa na maji ya bomba leo maisha bora kwa kila mtanzania ndio nyimbo wakati hakuna maji na Mbunge wako hawezi kuongea unatarajia nini kwa wananchi wa Igunga?
 
Wakubwa,

Nikiwa mwana Tabora Mzawa, nanyon'gonyezwa sana na habari za huyu RA kuhusu kupita kwake kwa kishindo kura za maoni kule Igunga kwa tiketi ya chama chake, kwa hesabu zangu za haraka haraka CCM hawana jeuri ya kumchukulia hatua kichama na kumkata jina, na kwa maana hiyo anaweza kurudi tena bungeni.

Napenda kutoa wito kwa CHADEMA, wakiunganisha nguvu zote kwa pamoja (zikiwemo na zangu) hatuwezi mn'goa huyu mtu bungeni? ningependa sana tuanze kumnyongonyeza taratibu kisiasa maana matendo yake yana walakini nyingi nyingi tu, hana nia ya dhati na taifa hili. Ni kweli ana nguvu kisiasa, ana pesa nyingi na ana ushawishi mkubwa kwa wana igunga - lakini kumngoa tunaweza wandugu.

Ningependa mno asirudi kwenye chombo chetu cha kutunga sheria abakie huko kwenye chama chao wanakomkumbatia.
 
Hawa jamaa lengo lao ni kuendelea kutufanya kuwa maskini kisha waendelee kututawala vyema, maana watakuwa na uhakika wa kutununua hata jimbo zima kwa bei ndogo tu.
 
Back
Top Bottom