Rostam (Mbunge) anawahadaa wananchi wa Igunga

kuongea ndani ya bunge sio kuwa ndio unafanya kazi ya ubunge.
kuwa mbunge siku hizi ni kujishibisha tumbo lako binafsi hasa hawa wabunge wa ccm, kwa mfano mbunge wangu karibu nitamsahau jina lake kwani haongei bungeni achilia mbali kutatua matatizo mbalimbali yanayotukabili, hebu fikiria sehemu wanayoita wilaya inapata umeme kwa muda wa masaa 6 kwa siku kweli hii ni haki? je huko vijijini ni lini utafika umeme kama mbunge hafanyi kitu chochote kile bungeni kwake zaidi ya kutoka kitambi na kuwasomesha watoto wake nje ya nchi katika shule ambazo zina'cost a milions of shilling?
 
Ubunge ni uwakilishi, hivyo kama mbunge zipo anafanya kazi tatu muhimu za uwakilishi:
1.kuwa sauti ya wananchi wa jimbo lake bungeni kwa mema au mabaya,
2. kusemea chama chake bungeni,
3. kushiriki kutunga sheria za nchi.

Kulingana na kazi hizo tatu kwa vyovyote vile inavyokuwa lazima mbunge aseme tu! akiwa bungeni hata kama ni kuunga mkono hoja zinazotolewa na wawakilishi wengine kama tu yanayosemwa yapo pia jimboni anakowakilisha.

Kwa mbunge Kutokusema chochote bungeni tafsiri yake ni kwamba jimboni kwake mambo yote ni murua kabisa,hivyo wabunge wengine waende jimboni kwake kujifunza!

Wilaya ya Igunga ambalo ndilo jimbo la RA ni ya mwisho kabisa kitaifa kwa ulinganisho wa vigezo mbali mbali vya elimu!!!!kwa miaka takriban sita sasa.

Kwa hali namna hiyo, ni halali mbunge wa jimbo hili kutokusema lolote juu ya elimu kuishauri serikali?????

Hizo fedha zinazosemwa RA anatoa zinafanya kazi gani?? ikiwa tu hata vipaumbele kutatua matatizo ya wananchi wake havijui!!!

Kwa kutokusema bungeni juu ya matatizo ya wananchi wa Igunga, RA anapoteza sifa ya uwakilishi! hafai tena kuwa mbunge.

Muwakilishi wa dhati wa wananchi hawezi kukosa cha kusema bungeni,sio bla bla!!kama wanavyofanya wengine, lakini mambo muhimu yanayohusu jimbo lake.

Lakini pia kama mbunge huhudhuria vikao vya baraza la madiwani jimboni ambako ndio matatizo yote ya wananchi jimboni huongelewa na kupatiwa ufumbuzi lazima atakuwa na la kusema bungeni!!!

Ukiwauliza watu wa Igunga watakuambia RA si muhudhuriaji kabisa wa vikao vya baraza la madiwani wilayani kwake!!ndio maana hana lolote la kuongea bungeni!!!!
 
Mwanasiasa,
Roho nzuri unayosema ikoje??? kualika watu na kuwapikia pilau wale??? au kugawa fedha elfu tano tano kwa wale wenye shida kila wanapokuja kwako.

Wananchi wa Igunga wanahitaji kupata mwakilishi mwingine sasa!!
kama rostam ana roho nzuri bado anayo nafasi kuwasaidia watu na si lazima akiwa mbunge!!

Lakini kazi ya ubunge haiwezi tena, kwanza sifa zake ni sub-standard, hazieleweki!!!

Ni mwoga kukutana na watu hata wa jimbo lake, unaweza kumtafuta mwezi usimuone!!! ofisi yake haileweki!

Anapenda kumaintain low-profile kuficha mapungufu aliyo nayo.
 
Mwanasiasa,
Roho nzuri unayosema ikoje??? kualika watu na kuwapikia pilau wale??? au kugawa fedha elfu tano tano kwa wale wenye shida kila wanapokuja kwako.

Wananchi wa Igunga wanahitaji kupata mwakilishi mwingine sasa!!
kama rostam ana roho nzuri bado anayo nafasi kuwasaidia watu na si lazima akiwa mbunge!!

Lakini kazi ya ubunge haiwezi tena, kwanza sifa zake ni sub-standard, hazieleweki!!!

Ni mwoga kukutana na watu hata wa jimbo lake, unaweza kumtafuta mwezi usimuone!!! ofisi yake haileweki!

Anapenda kumaintain low-profile kuficha mapungufu aliyo nayo.

Kaka/Dada

Naomba unipe mapungufu ya Mbunge Rostam Aziz! naomba unipe shida za wananchi wa Igunga unazotaka aziongelee bungeni. Ombi tu.
 
Mbunge Wa Igunga Ingefaa Aondolewe Safari Hii


Ng'wana Ngosha (raia mwema)
(ninafahamu nguvu ya fedha)

Hiyo kazi ya kumuondoa ni kazi ya watu wawili, moja ni TAKUKURU na wananchi waliomchagua sisi huku tuna kazi moja tu kupiga kelele wana-Igunga waamke na kusikia hilo.
 
Hiyo kazi ya kumuondoa ni kazi ya watu wawili, moja ni TAKUKURU na wananchi waliomchagua sisi huku tuna kazi moja tu kupiga kelele wana-Igunga waamke na kusikia hilo.

Bubu,

Naomba unipe makosa ya Rostam, unajua so far sijaona hasa tunachokiongelea. Mlianza na haongei bungeni, mkaambiwa sio hoja, kaangalie maendeleo jimboni kwake, mkamnukuu kuwa anasema angalia Barabara, hospitali, maji etc .."nimeleta mimi". Mkaambiwa ni kweli amezileta tena bila "KUONGEA" KAMA MLIVYOZOEA.

Naomba basi unipe makosa yake!
 
Kosa la Rostam ni kwa sababu haongei bungeni na haombi misaada serikalini yeye kila kitu anafanya mwenyewe kwa pesa zake.
 
Kosa la Rostam ni kwa sababu haongei bungeni na haombi misaada serikalini yeye kila kitu anafanya mwenyewe kwa pesa zake.

Hapo umenena. Na mimi natambua hilo kosa lake!

Lazima upayuke ndio uonekane mbunge safi. Kuna watu humu wamezidi uzushi, ukiwauliza niambie kosa kimya; wanaingia mitini, kazi yetu humu inakuwa kama kazi ya magazeti ya udaku!
 
Mimi ni mwanachama na mpenzi wa Chama Cha Mapindizi, tena waweza kuniiita wa siasa kali. Nadhani, nionavyo ni kwamba chama chetu kinahitaji kuteua wagombea makini katika hatua za mwamzo kwa kudhibiti mbinu chafu-chafu.

Nadhani sasa wakati umefika tuanze kuwakana hawa wana jf wanaojiita sisiem, mtu anatoa hoja ya mafisadi halafu anamention kuwa nae yumo ndani ya Chukua Chako Mapema anakuwa na maana gani? Nafikiri wana jf wengine ni watoto hawajui la kuzungumza na nafikiri kati ya wapambe wa huyo R basi na wewe ni mmojawapo. Nothing U can tell us as JF members. Watch out!!!!!
 
Hapo umenena. Na mimi natambua hilo kosa lake!

Lazima upayuke ndio uonekane mbunge safi. Kuna watu humu wamezidi uzushi, ukiwauliza niambie kosa kimya; wanaingia mitini, kazi yetu humu inakuwa kama kazi ya magazeti ya udaku!

Kwanza mbunge haombi misaada serikalini! ni wajibu wa serikali kuwafanyia wananchi kila linalowezekana kuwaletea maendeleo! mbunge anakuwepo kuikumbusha serikali wajibu wake na kuainisha vipaumbele vya maendeleo jimboni kwake!

Watu hawachagui mbunge ili eti yeye ndiye ajenge barabara, ajenge mashule, aajiri walimu na kuwalipa, ajenge zahanati na mengine ya jinsi hiyo.Fikiria kama nchi yote iwe na wabunge wanaotoa fedha zao kwa kazi zote za maendeleo, kuna haja ya kuwa na serikali hapo???wala mfumo wa uwakilishi haulekezi wabunge kutoa fedha zao kugharimia maendeleo!!ni kazi ya serikali ya Tanzania.

Takwimu zimetolewa hapa, kwamba wilaya ya igunga ni ya mwisho kwa ubora wa elimu nchini, hili si tatizo? inasaidia nini hata kama unajenga barabara nzr ya lami, lakini watu hawana elimu!!kila mwaka wilaya ya igunga ina upungufu wa chakula licha ya kuwa na eneo kubwa lenye ardhi nzr kwa kilimo!! matatizo ni mengi.

RA amefanya nini kutatua matatizo haya ya msingi?? kwa mfano ingekuwa jambo jema na la kujivunia sana kama hizo fedha zinazosemwa RA anatoa zingetumika kusomesha watoto wa igunga!!! kama wanavyofanya wabunge wegine majimboni kwao, hata mwalimu Nyerere alisema, ukitaka kumkomboa maskini msomeshee watoto wake tu!!!! tuache kufanya utetezi usiokuwa na maana hapa, watu wa igunga ndio wanaojua kama RA anafaa au hafai!!

Hapa JF si mahali pa kufanya utetezi kwa kuuliza maswali ambayo majibu yake yapo tyr, tena kwa takwimu.

Mahitaji ya watu wa igunga si fedha za rostam!!!Igunga itajengwa na wanaigunga wenyewe.
 
Mtu mpya,

Safi sana. Lete takwimu. Tatizo la Elimu Tanzania linaeleweka. Waalimu wengi hawapendi kwenda vijijini, wewe unapenda kwenda kuishi Mwanerumango?, Mishahara ya waalimu ni midogo. Hilo sio Tatizo la Rostam, ni la serikali.

Mzee Kjon,

Asante ndugu yangu ila I beg to differ. Sio wana CCM wote wameoza, wengi wanaosema mafisadi wajibu tuhuma ni wana CCM, Rais mstaafu Mwinyi ni mwana CCM naye katoa kauli yake.
Yes samaki mmoja akioza ni wote, lakini sio ktk hili.

Mimi ni mwana CCM pia!
 
Huyu Mheshimiwa mbunge wa Igunga Rostam Aziz huwa anasikika japo kwa nadra... hii nimeitoa google, shughuli nzima iko kwenye tovuti ya bunge ila ufungukaji wake mbinde:

Juzi wakati wa semina Mheshimiwa Rostam Aziz alizungumzia mamlaka mbali mbali katika nchi kuhusiana na masuala ya kisera ya kiuchumi akazungumzia kwa Wizara ...
parliament.go.tz/bunge/ContrLst.asp?Menu=Contr&PTerm=2005-2010&vpkey=1403&page=31 - 34k - Cached - Similar pages

Nionavyo mimi: Wabunge wengi hawagombei ubunge ili wakawakilishe wananchi, wengi hufanya hivyo wakiwa na malengo ya kujinufaisha binafsi, kumwandama Rostam Aziz pekee na mapungufu/makosa yake ni kudhoofisha hoja ambayo ningeiona ya msingi; kwamba wabunge wengi hawapo bungeni kwa maslahi ya majimbo yao bali kwa ajili yao wenyewe binafsi.
 
Mwakilishi,

Positive thinking! hawa ma spin doctors watakimbia tu mjadala, mbio za sakafuni mwisho wake ni uvunguni.

Tunaendelea
 
Mkuu FD,

Humu JF wengi kama sio wote tuna machungu na nchi yetu na tunataka kuona maendeleo sasa tukiwa katika kuwakosoa viongozi wetu wakati mwingine tunaweza kuelemea upande mmoja na kupoteza kile kinachoitwa kwa kikristu objectivity
 
Kama huyu mnasema kuwa anatoa pesa zake mfukoni kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Igunga ..kama yapo any way?
Hafai kuwa mbunge kwani kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananvhi na sio kukaa kimya hata wakati wa kupitisha bajeti ambayo itawaathiri wananchi katika kufanya manunuzi ya viberiti, mafuta ya taa , chumvi,sukari n.k.

Huyu ama hayaongelei hayo kwa sababu hayamhusu ila wananchi walimtuma ili aende kuyaongea hayo kwa niaba yake na sio kukaa kimya na kupewa posho za wabunge.

Ukifuatilia pia kwenye record zake za kukaa bungeni huyu huwa anaingia siku tatu za mwanzo wa kikao na kurudi wiki ya mwisho je?wana Igunga tunamuhitaji mbunge wa aina hii?
 
OK so far toka 2005 hajachangia

http://www.parliament.go.tz/bunge/MP_LS3.asp?Menu=Qns&MPStatus=&PTerm=2005-2010&page=3

Lakini hii inamaana ni mbunge mmbaya? kama maendeleo yapo?

Nimeona niwasaidie kuleta data maana mnajibu hoja bila back up.

Tusaidie kutaja hayo maendeleo unayoshabikia, na ni katika sehemu gani ya igunga!

Kuendelea kujadili hoja na watu wa aina yako, ni kupoteza muda tu, unavyojibu inadhihirisha hata huko igunga hukujui, unasoma na kusikia tu kwenye vyombo vya habari!

Kuwepo kwa wabunge wengine waliogombea kwa maslahi binafsi hakuhalalishi RA aendelee kuwa mbunge wa igunga.

Kama walimu hapendi kwenda kufundisha vijijini, tunategemea yeye kama mwakilishi anayo majibu!!! au achangie kutoa majibu ya matatizo ya watu wake kwa serikali, ndio maana tunahoji kwa nini hasemi wkt hali ya elimu jimboni kwake ni mbaya kiasi hicho!

Nyie si mmesema anazo fedha, alipe nyongeza ya mishahara midogo kwa walimu wanaopenda kenda igunga, labda itasaidia.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom