Rostam (Mbunge) anawahadaa wananchi wa Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam (Mbunge) anawahadaa wananchi wa Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MegaPyne, Oct 6, 2007.

 1. Mbunge Wa Igunga Ingefaa Aondolewe Safari Hii

  Ng'wana Ngosha (raia mwema)
  (ninafahamu nguvu ya fedha)
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145

  Kateuliwa na CCM au kachaguliwa na wananchi wa Igunga?

  Wananchi wenyewe inabidi kubeba msalaba kwa kukubali rushwa na kumchagua mtu ambaye hatetei maendeleo ya wilaya yao.
   
 3. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Kweli..........lakini ishu ya rushwa serikali kuu inawajibu wa kumchukulia hatua kama ushahidi upo!!!au unasemaje kaka?
   
 4. m

  mwana siasa Senior Member

  #4
  Oct 6, 2007
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  haya kazi ipo,mlidhani ile miaka 10 ya kujiandaa na kumfanyia kampeni ya kutosha kikwete ilikuwa bure?
   
 5. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2007
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Hajawahi hata siku moja kuzungumza ndani ya bunge, kuna haja ya kuwa na sheria za kuwafanya wananchi waweze kumngoa mbunge kama wakiona hana faida kwao.
   
 6. M

  Mshamba wa Kijijini Member

  #6
  Oct 6, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ni mwanaCCM tena eti wa siasa kali! acha uongo, tangu lini wanaCCM wakawa wa siasa kali? nyie ndio mnafaidi hii nchi kwa kukumbatia CCM, inakusaidia nini wewe binafsi na raia wenzako? nimekunukulu unasema eti CCM "chama makini" kimeanza lini kuwa makini? huu ndio tunaita upuuzi, unasifu usichokiamini! sijui una umri gani lakini nataka nikupe hukumu ya jumla tu, "umepitwa na wakati" nadhani wewe sio wa awamu yetu.

  unasifia mafanikio kwakuwa huna data za matatizo yaliyojitokeza. tangu lini katika matatizo 100 yakitatuliwa 30 useme umefanikiwa wakati umeshindwa 70? sio kila maendeleo ni ya maana bali ya maana maendeleo.

  unatuma hayo malalamiko TUT na sehemu zingine kufanyaje wakati CCM ni chama makini? kwanini unaishi katika nyumba usiyoipenda kama hiyo CCM? Rostam mbunge wa IGUNGA sio mwakilishi wa jimbo hilo la IGUNGA ni mwakilishi wa tumbo na biashara zake.

  kwa taarifa yako; Rostam ni bosi sana humo CCM mweka hazina Taifa na mmiliki mkubwa wa 'habari Corporation' wamiliki wa RAI,MTANZANIA,DIMBA,BINGWA na THE AFRICAN zaidi ya hapo ni mwana mtandao "number one" anasafiri kila mara kwenda ulaya na america unataka achangie nini bungeni wakati mlikwisha pewa bahasha ndio mlichostahili, vumilia hadi mtakapomaliza pesa hizo tshs 20,000 ndio ataanza kuchangia na kuwatetea huko bungeni!

  lakini mnataka shida wenyewe kweli watu wa Igunga mnamchagua ROSTAM ili awatetee bungeni kwa lipi? hana shida ya maji wala halali njaa na kamwe hawezi kujua kuna watu wanakosa hata shs 500 kununua vibaba vya unga!

  endelea kuwa mwana CCM utajua kwanini watu makini hawako huko CCM maana uamuzi wako ni wa maana kwa maisha yako Mungu akupe hekima ujue ubaya wa CCM.

  unamjua rais mwinyi? mwanae anaitwa husein mwinyi waziri ofisi ya makamu wa rais (muungano, 2010 anagombea urais zanzibar kupitia CCM upo hapo? makamba katibu mkuu wako, mwanae Januari makamba ni mshauri wa rais kikwete Ikulu, mke wake makamba ni kada CCM mkoa wa DSM, shemeji yake Dr.Ishengoma mkuu wa mkoa pwani, amemzawadia juzi ubunge viti maalum baada ya kifo cha Amina Chifupa wewe nani atakupa kitu huko CCM? labda hao mnaokula nao maana ndio maana unayo siasa kali. kwaheri nakutegemea uwe chachu ya wanaharakati sio chama, tunahitaji kuikomoa hii nchi sio vyama tena!
   
 7. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2007
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Babu endelea kumpasha huyo mufilisi maana anaonyesha jinsi asivyo jua mambo.Unamshitaki Rostam TUT?
  Pia naomba kujua mengi kuhusu hawa mafedhuli wanavyopeana madaraka na ulaji.

  Pia JK anafanya nini ufaransa,kama anaona aibu kujiachia basi na atangaze hukohuko kuwa hawezi kazi!!!!!!!!!!!11
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  I see, kumbe performance ya mbunge ni kuongea sana bungeni, kama hili ndilo mbunge wangu angekuwa madarakani milele!

  Hili waachieni wananchi wa Igunga, ndio demokrasia inayotakiwa, msijifanye mwaijua kumbe nanyi mtakuwa mafisadi wa demokrasia... ninyi lalamike upande mwingine!
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Watanzania amkeni, kazi ya mbunge si kupiga kelele bungeni. Mafanikio ya mbunge yatatokana na juhudi zake za wazi za kuendeleza jimbo lake.

  Wachangiaji wakubwa bungeni, ukienda kwenye majimbo yao hakuna kitu.

  Mambo mengi ambayo wabunge wanauliza bungeni au kuchangia wanaweza kupata majibu yake bila hata kusubiri kikao cha bunge.

  Ni rahisi kusema bungeni kuliko kufanya matendo kwernye jimbo lako.

  Simtetei Rostam lakini naona wananchi wake wamkabe koo kwa kushindwa kuiendeleza wilaya yake na sio kushindwa kuchangia bungeni.

  Wakati mwingine kuongea bungeni ni cheap politics ambazo zinawafanya wapate cha kuwaambia wananchi wao huku ukweli ni kwamba wameshindwa kufanya kazi ya msingi ambayo ni kusukuma maendeleo kwenye majimbo yao.

  Michango mingine ni pumba tupu wala haiongezi tija kwa mtu yeyote.
   
 10. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwani atawezaje kuwasilisha maoni na kero za wananchi kama haongei na wala hata swiku moja sijawahi kumsikia amechangia kwa maandishi jambo lolote kule Bungeni?

  Huyu anawakilishaje hoja za wananchi wa jimbo lake?

  Nani anawasemea wananchi wa Igunga kama mbunge mwenyewe ni bubu?

  Alienda kuwaomba kura za kazi gani kama hawezi kuwasemea?

  Anawakilisha watu gani huko na kwa njia gani?
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mawaziri hawachangii bungeni kwenye hoja zisizohusu wizara zao, je nani anawasemea wananchi wa wilaya zao?

  Binafsi sioni kwamba ni muhimu sana kuwa msemaji mkubwa bungeni, badala yake muhimu ni kule wilayani.

  Kwasasa wabinge wengi hawakai kwenye wilaya zao, hawatatui matatizo ya wananchi na wala hata hawahimizi maendeleo. Hilo ni tatizo kubwa kuliko kutokuongea bungeni.
   
 12. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hongera kwa kufikiri kwa makini!!! wapo wabunge wengi wasioongrs ni wachapakazi na wana-deliver...
   
 13. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Amka tu usingizini utajua kwamba kuna watanzania/wawakilishi wengi wanachapa mzigo, lakini hawapigi kelele!!!

  Tafakari, chunguza, kwa nini wananchi wameamua kuwapa hawo wabunge kura, kama ni kuongea tu ndio kigezo,,, du Mzindakaya asingepata taabu kurudi mbungeni kipindi hiki, au Jimbo lake lingekuwa zuri sana...

  Aidha ningeungana na wewe tu kwenye kusema wabunge wa kitaifa, wale wa kuteuliwa na wengineo wakitaifa angalau tuwasikie...
   
 14. m

  mTz JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2007
  Joined: Aug 20, 2006
  Messages: 283
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tafadhali naomba utufahamishe kuhusu huu ushemeji
   
 15. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2007
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  NCHI hii inaumizwa sana na huyu RA kwa kitendo cha kuwa kwake kule bungeni , aliwahinga wabunge wa ccm shilingi laki tano kila mmoja ili spika SITTA aweze kuchaguliwa kuwa spika.

  Kma huko ndio kuchapa kazi kwenyewe basi yuafaa aendelee kukaa ndani ya bunge ila kama ni kinyume chake basi yaafaa asiwepo ndani ya bunge.
   
 16. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2007
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa mimi ninavyo jua ROSTAM AZIZ ndio mfadhili wa CCM na inavyosemakana kampeni ya KIKWETE yote aligalamia yeye, hivyo basi huyu mheshimiwa kuondolea ni ngumu.... ROSTAM AZIZ ni kama ndio Rais wa Tanzania na KIKWETE ni mtekelezaji tu, Akae bungeni aongee nini wakati anajua pesa yake itaongea?????? nchi yetu ilishanunuliwa na wafanya biashara wenye pesa siku nyingi tu. hii si nchi yetu tena ni nchi ya wenye nazo tu.
   
 17. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2007
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kilitime na Mtanzania,

  Kama tukipewa madaraka hakika tutaivusha Tanzania, maana baadhi ya hizo thinking za wachangiaji hapo juu zinachekesha!

  Rostam amefanya mengi sana Igunga, unlike Mkono yeye haongei kwenye magazeti wala bungeni. The boy is simply smart!!!

  Kama ni shule kaenda, kama ni kuchzesha karata zake anajua, kama ni miradi anayo kibao kama ni wananchi wake anawasaidia sana!

  Mnataka akapayuke tu kule bungeni wakati hahitaji msaada wa serikali? what if yeye anasema nataka hiki kifanyike Igunga na kinafanyika?

  Duh! wabongo kweli ndio tulivyo!
   
 18. H

  Hume JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Mbunge kama huongei, basi bunge siyo sehemu yako.
  Mtu akisema kuongea hamaanishi tu kuomba mambo mbalimbali kwa ajili ya jimbo lake. Ni pamoja na kuboresha bajeti ili ikidhi mahitaji ya watu wake, kama huongei na kuna mapungufu yatarekebishwaje?

  Bila Zitto kuongea ungefahamuje habari za Buzwagi?
  Jifunze majukumu ya Mbunge kabla ya kutetea usichokijua.
   
 19. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  nakubaliana nawe Hume,
  kama wabunge hawaendi bungeni kuongea basi hamna haja ya kufanya vikao vya bunge!

  Na kazi ya mbunge ni zaidi ya kuendeleza miradi jimboni kwake kwa kutumia fedha zake, ni pamoja na kuwakilisha wananchi wake kuwasemea kwa serikali ili kuhakikisha gurudumu la nchi linaenda mbele! Kutunga sheria na kurekebisha, pamoja na mikataba ambayo ndo udikiteta wa serikali yetu unaifanya siri!

  Kama hawezi sema kwa maana ya kuwasemea wananchi wake waliomtuma awawakilishe, hafai kuwa Mbunge kwa mantiki hiyo!.
   
 20. H

  Hume JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Siyo kweli braza kuwa mawaziri hawachangii, nishasikia michango ya mawaziri na manaibu wao kwa MAANDISHI

  Ngoja tu nikupe kifungu kinachoeleza majukumu ya mbunge;

  Masharti ya kazi ya Mbunge kupitia Bunge yameelekezwa katika Ibara ya 63(2) kwamba Bunge litakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake na huo ndio uhusiano wa msingi kati ya Mbunge na kazi za Serikali.

  kama husemi huo ushauri UTAUTOLEA WAPI? Nyumbani kwa Mawaziri?
   
Loading...